ÙKuna mambo mengi sana yanafikirisha kwenye hili sakata jipya la ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kuhusu kuibua madudu mengi ambayo serikali iliyokuwa chini ya hayati JPM yamejitokeza...
Ukweli ni kuwa katika awamu nne kati ya tano ukiondoa awamu ya Nyerere ambapo ilikuwepo rushwa ndogo ndogo tu, awamu zingine kulikuwa na ufisadi wa kutisha. Wakati wa mzee Ruksa ufisadi kama wa kuuza mashirika ya umma kwa bei ya kutupa, kutokusanya kodi kwa wafanyabiashara ambapo tabaka la wafanyabiashara mabilionea ndipo lilipotokea baada ya wengi wao kupiga madili ya kugawana mali za umma kwa kushirikiana na baadhi ya mawaziri na maafisa, ubadhifu na wizi wa fedha za umma nk.
Wakati wa awamu ya uwazi na ukweli wimbi la kuuza mashirika ya umma kwa bei ya kutupa, mikataba mibovu hasa kwenye madini ndipo ilipishamiri licha ya awamu hiyo kujenga mifumo ya kitaasisi na kuleta nidhamu katika makusanyo ya kodi na matumizi kiasi cha kurudisha imani ya wafadhili, IMF na World bank. Hadi ilifikia Nyerere kushutumu uuzaji wa mashirika hata yale yalikuwa yanatengeneza faida.
Wakati wa awamu ya nne ilikuwa ndiyo mama wa mikataba mibovu ya mabilioni na matrilioni tena mingine ikipitishwa kwa hati ya dharura . Miradi ya nadini, gesi, mafuta, uzalishaji umeme nk ambayo athari zake zitadumu hata baada ya kizazi chetu ndipo ilipopitishwa. Miradi hewa au iliyojengwa chini kabisa ya viwango huko halmashauri zote ilishaniri sana. Kipindi hicho ndicho anbapo wafanyabiashara mafisadi walicontrol sana serikali, kila mara walionekana katika viunga vywa maofisi ya wizara wakifuatilia madili. Kipindi hiki ndipo maafisa wengi wa serikali wakiwemo wakurugenzi, makatibu wakuu, mawaziri na maafisa wa kawaida walitengeneza ubilionea na umilionea. Ndipo kipindi mahekalu ya mamilioni yalichipuka huko pembezoni mwa miji, vijijini na wilayani yote yakimilikiwa na maafisa hao.
Kipindi hiki cha JK ndipo sheria ya uwazi jatika ripoti ya CAG ilipopitishwa na madudu mengi kuanza kuanikwa. Kwa kumbukumbu zangu toka ripiti za CAG zianze kuwekwa hadharani, hakuna hata ripoti moja ambayo haionyeshi madudu ndani yake.
Sasa awamu ya JPM ripoti ya CAG imeanika ubadhirifu katika baadhi ya maeneo kama ambavyo ripoti za nyuma wakati wa JK zikivyoanika madudu mbalimbali. Lakini sasa wabaya wa JPM wanamshutumu kana kwamba yeye binafsi ndiye aliyetenda. Kila sehemu iliyotajwa ina watendaji: mkurugenzi mkuu, mkkuu wa idara ambaye ndiye mtekelezaji wa kazi fulani iliyibadhiriwa, mkaguzi wa ndani, mhasibu mkuu, Afisa ugavi ambaye ndiye anafanya procurement sasa hawa ndio wa kuwajibishwa. Inatakiwa TAKUKURU au polisi waingie kufanya uchunguzi na ikionekana kuna watu wamehusika wapelekwe mahakamani, huo ndio mkondo wa kufuatwa.
Sasa wapinzani wa JPM, yale majizi ya awamu ilyopita ambayo yalikwamishwa kufanya ufisadi ndio wana exploit hiyo ripoti kumshambulia JPM kana kwamba yeye binafsi ndiye ameiba.
Pia kuna wale ambao baadhi yao walikuwa madarakani na wakimuunga mkono sana tena hadharani nao sasa wamegeuka na kumkosoa. Hawa wanafanya hivyo ili kulinda maslahi yao binafsi kwa Rais mpya ili waò wasiondolewe katika position zao. Kuna msemo kuwa: Yule anayemsaliti mtu mbele yako, pia anaweza kukusaliti wewe mbele ya mwingine.
Mimi maoni yangu binafsi Rais angewaondoa katika nafasi zao hao walioko madarakani ambao sasa wanamkosoa JPM wakati huko nyuma walimsifia sana na hata baadhi yao kupiga debe aongezewe muda. Rais awaondoe ili aweke timu yake itakayomsaidia kwa kumshauri kwa uadililifu pale inapobidi badala ya wanafiki hao ambao nao siku moja SSH akitoka madarakani wanaweza kurudia kukosoa utendaji wake kama wanavyofanya sasa kwa JPM.