Ripoti ya CAG imefichua madudu mengi ya awamu ya tano, kulikuwa na ufisadi wa kutisha

Niliwahi kusema kitu cha kuhusu ndege tena nikiwa kigoma hotelini jamaa wakataka kunila nyama kisa namseba vibaya mkuu.
Kuna mturuki alishawahi kufukuzwa baada ya kuwahoji ukweli viongozi wa TRC Juu ya kwanini tunajenga baadhi ya matanuri ya kupitisha reli badala ya kuipitisha njia ya nnje ambayo gharama yake sio kubwa sana?
Muda ni kitu chaajabu sana kwakweli.
 
AHSANTENI KWA KUJA


 
mama D mwaka huu yamezidi. Hata ukiangalia mh angekuwepo yasingewekwa hadharani kama hivi inavyofanyika sasa. Mwaka jana tu alituambia ATCL imefanya faida ya bil 28. Mwaka huu angekubali CAG aseme hasara ni 60bil kwa miaka 5?
Ngoja tupate report zilizopita ndio tuone yaliyozidi maana kila report ina madudu
 
Jamii ifanye nini ? Hatuna mamlaka yeyote kwenye hii nchi hata kumtoa mbunge.
Ingia barabarani ukutane na form four wanaolipwa posho ya nyumba, usafiri, chakula, umeme wakutandike virungu ufe.
 
Hata aongoze nani ufisadi hauwezi kuisha, upigaji utaendelea kuwepo tu
 
Ngoja tupate report zilizopita ndio tuone yaliyozidi maana kila report ina madudu
Labda utafute ya mwaka 2015 au kabla yake. Zote kuanzia 2016 zinaonesha mambo ni shwari. Mamiradi tu yanatekelezwa masgr, JNHP, n.k si unajua tena serikali ya kiongozi wa Malaika😂😂😂
 
Ni hatari sana ukiona kiongozi sio muwazi na anafichaficha mambo au ni mbabe sana jua hapo kuna kitu na wateule wake walijua anapenda kusifiwa hivo akisifiwa hawezi kuchukia na wakatumia njia hiyo kupiga pesa nyingi
 
Tuliowapa mamlaka au dhamana ya kukomesha hili wanatuangusha, hatuwezi kunyanyuka jamii nzima na kupigana na mafisadi au wabadhirifu, kuna sheria kwa ajili ya kuwawajibisha, tuna mamlaka za juu zenye kuweza kutoa tamko juu ya hawa wanaotumia ofisi za umma kwa manufaa yao, katiba yetu haijatupa wananchi mamlaka ya kuwawajibisha hawa kwa sababu hata kwenye masanduku ya kura wanatufanyia ubadhirifu, simply katiba isipobadilishwa basi haya mambo hayatakwisha, ni muda muafaka hizi ofisi ziwe na watendaji proffesional na sio wanasiasa wa kuteuliwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…