Ripoti ya CAG Ina mapungufu makubwa ya kimantiki; "non-compliance" imetumika kama ubadhirifu kufurahisha umma

Mfano unaotoa ni irrelavant kabisa. Kinachozungumzwa hapo ni wewe uache kutoa huduma badala yake umuachie Abood na kampuni yake wewe uingie mitini.Tuliingia mkataba na wewe au Abood? Muwe mnasoma vizuri ripoti sio kukaza shingo tu.

CAG ni mtu makini sana. Unachosema wewe ni sawa na huyo mkandarasi angepungukiwa mitambo akaenda kukodi kwa wenzie ili apige kazi,kitu ambacho sio issue
 
Broo soma sheria ya manunuzi imeweka wazi ndio maana unaskia wanatangaza tenda sio kwamba unaenda tuu wakishakuhoji wanakuambia uanze kubeba wafanyakazi na hapo ndio tatizo linaanzia kwa ufupi lazma watakagua ubora wa vitu ulivyo navyo ikiwemo magari na ufanisi wa kazi yako kwa kipindi cha muda waliokupa kuhakikisha kwamba unakidhi vigezo na masharti mliyokubaliana ,moja wapo ni kulinda mkataba mlioingia huwezi kuingia mkataba alafu ukaenda kinyume na makubaliano ukienda kinyume ni ubadhirifu.....kwa maana hiyo inawezekana umekusanya tuu magari ili upewe iyo kazi (mchongo)kumbe huna vigezo kwa hiyo sheria itakubana ili taasisi nyingine zisiingie makubaliano ya kidalali namna iyo
 
Kubishana na wewe ni kupoteza muda kwani huna unachojua na hujawahi hata kuongoza timu ndani ya serikali!
 
Hata majizi huwa kama wewe usemavyo,wanadai wamepoteza docs. Huyu CAG alikuwa na wewe wakati unanunua tofali? Yeye anaaminishwa na nyaraka na UHALISIA WA KAZI.
Mtu kama wewe hata kwenye hiyo nafasi hutoshi. Unatakiwa kuwekwa pembeni

Sasa anataka uhalisia upi zaidi ya tofali alilokuta site na akauliza bei kwenye soko akakuta ipo sawasawa au juu kidogo ya bei nilimwambia nimenunua tofali?
Nakubali wapo wengi sana wanasingizia kupoteza risit kuficha wizi lakini since auditing inafanywa na binadam na sio mashine, they must be able to tell the difference.
Hivi hata yeye tukikagua matumizi ya ofisi yake tutakuta kila kitu kipo sawa?
 
Hilo nalo litapita na hakuna mtu atakaye chukuliwa hatua. Sana sana ni mtu mmoja kiongozi katika taasisi kutumbuliwa lakini watendaji wanabaki
 

Hapo tuko pamoja, siyo kila audit query ni wizi. Zingine ni kutofuata utaratibu tu. Pia zinaweza kujibika.
 
Mkuu kwani kazi ya risit ni nini? tuanzie hapo. Kuhusu kukaguliwa CAG anakaguliwa kila mwaka ripoti wanayo PAC. Kama hawakukuta risit hawajasema unamlalamikia CAG? Zingatia taratibu za fedha na manunuzi hutogombana na mtu tofauti na hapo wale wabwana watakuandika sana tu.
 
Magufuli alikuwa analazimisha watu watii sheria na kufuata utaratibu, iweje yeye asifuate huo utaratibu kama alikuwa na nia njema? Kwa hiyo wale aliowatumbua alikuwa anatumia grounds zipi wakati sio lazima kufuata utaratibu?

Ni kweli, nyakati nyingine hakufuata sheria, kanuni na taratibu, licha ya kuwa alifanya kupisha urasimu ili jambo lifanyike kwa haraka.
 
Hata majizi huwa kama wewe usemavyo,wanadai wamepoteza docs. Huyu CAG alikuwa na wewe wakati unanunua tofali? Yeye anaaminishwa na nyaraka na uhalisia wa kazi.
Mtu kama wewe hata kwenye hiyo nafasi hutoshi. Unatakiwa kuwekwa pembeni

Wewe unaishi kwenye UTOPIA au unataka vyovyote vile tafsiri ya hii ripoti iwe ni inayomshusha JPM so kubishana na wewe naona ni kupoteza muda.
 
Ni kweli, nyakati nyingine hakufuata sheria, kanuni na taratibu, licha ya kuwa alifanya kupisha urasimu ili jambo lifanyike kwa haraka.
kama angeona sheria inaleta urasimu angeiboresha kama sio kuibadilisha. unajenga mradi wa mabilioni bila kufanya upembuzi yakinifu halafu unasema unapisha urasimu?
 
Acha story, TOR za audit ya CAG unazijua? Kama huna empirical evidence ya malipo ambayo ni risiti unataka mtu aamini vipi kama legal transaction zilifanyika? Hii nchi tunapenda kuongea ongea kila kitu, mambo ya kitaalamu tuache yafanywe na gurus husika!

Wengine tunadhani audit ya CAG ni kama ukaguzi wa mauzo ya sigara na soda dukani, tuwe na heshima na vitu tusivyojua!
 

WIzi mkubwa huwa una risiti.
 

Ungeonekana msomi kama ungeweka page au sehemu ya ripoti yenye kasoro!

Lasivyo utaonekana kama wanawake wa pwani wakisutana saluni.
 
Ungeonekana msomi kama ungeweka page au sehemu ya ripoti yenye kasoro!

Lasivyo utaonekana kama wanawake wa pwani wakisutana saluni.
Wapumbavu wasiokua na hoja ndo hua wanajibu hoja kwa personal attacks.
Grow up.
 
Kubishana na wewe ni kupoteza muda kwani huna unachojua na hujawahi hata kuongoza timu ndani ya serikali!
Umenyosha mikopo kiutu uzima,sio?! siku nikiongoza timu ndani ya serikali watu kama wewe lazima niwazingue tu. Najiuliza serikali imewezaje kuwa na watu hovyo kama wewe, badala ya kupeleka gari temesa au fundi aliyesajiliwa unapeleka kwa dereva. Dereva amesomea kutengeneza magari au kuendesha? Gari lako mpe dereva atengeneze,la serikali peleka kwa wahusika. Umenisikia broo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…