Ripoti ya CAG Ina mapungufu makubwa ya kimantiki; "non-compliance" imetumika kama ubadhirifu kufurahisha umma

Ripoti ya CAG Ina mapungufu makubwa ya kimantiki; "non-compliance" imetumika kama ubadhirifu kufurahisha umma

Watanzania wengi wanaweza kujiuliza kwanini riport ya CAG Ina madudu mengi lakini Mhe. Rais na serikali Kwa ujumla awachukui hatua? Wanajiuliza awamu ya sita inafumbia macho wizi na ubadhirifu tofauti na awamu ya Tano? Lakini wapo wanaohoji kama madudu hayayamefanyika wakati wa JPM je mbona alikuwa anatuadaa kwamba hakuna wizi?

Ripoti ya CAG wetu imejikita zaidi kuona kama sheria zilifuatwa? Hata kama hakuna Fedha iliyokwapuliwa lakini akabaini sheria imekiukwa basi yeye anachokuja nacho nikuonyesha serikali imepata hasara Jambo amabalo naamini limekuwa likipotosha umma wa Watanzania.

Mfano Kuna hoja unaona anasema mfumo ulipata itilafu na mifumo Mingine ikatumika kutoa Huduma,Kwake yeye anataka kusema tayari ni ubadhirifu wakati miundombinu Yetu inafahamika wazi kwamba Taifa halina reliable network,electricity nk. Sasa yeye badala ya kuibua ubovu wa miundombinu anakwenda kuangalia waliohudumiwa nje ya mfumo anasema serikali imepata hasara. Hoja za Haina hii haziwezi kumwajibisga mtu maana hazina evidence ni mtumishi Gani au Watumishi Gani walikwapua hizo Fedha?

Mfano mwingine kwenye ujenzi naona anacholeza nikukiukwa Kwa sheria ya manunuzi ambayo sheria Hiyo imepigiwa kelele Sana; ripoti yake inaonekana inawahukumu wale ambao waliona sheria unaleta urasimu wakaamua kufanya kazi speed nje ya sheria kurahisisha ujenzi au manunuzi.

Kwa aina hii ya riport ambayo imeandikwa ikiwa na dhima ya non compliance lakini ikahitimishwa na kiasi Cha ubadhirifu ni dhahiri kila mwaka tutaona anasema Kuna wizi wa mabilioni lakini hakuna wakuchukuliwa hatua Kwa sababu inashindwa kutofautisha wizi ( fedha kuingia mifukoni) na non compliance ( kutumia fedha Kwa KAZI iliyopangwa au kubadili matumizi bila kuweka fedha mfukoni).

Hii ripoti Kila mmoja serikalini ataipuuza Kwa sababu imechafua taasisi Kwa kuonyesha Kuna wizi kumbe ukweli ni watendaji kutozingatia sheria.

Maeneo mengi hakuna wizi Kuna ukiukwaji wa sheria.
Namm nlishangaa pale aliposema kuwa kuna POS 86 (idadi sikumbuki vizuri) za polisi hazijawahi kurekodi muamala hata mmoja sasa nikajiuliza mbona sabbu ya kutokutumika hazikutajwa... kwa mfano ni mbovu, au ziliwekwa tu ofisin, alipewa askari na hakutumia kwa maksudi au aliyepewa hakujua namna ya kutumia. Maswal ni meng bila majibu. Lakini pia je ni lazima kila poss irekodi mumala njiani ndo ionekane hakuna shida. Je kama kulikuwa hamna kosa kwa kipind chote hicho...??? Kiukwel kuna wakat napata waswas lengo la hizi ripot n nn... Mungu atusaidie, Tanzania yetu izidi kuwa na amani.
 
Kweli kwa mara ya kwanza natofautiana na Ripoti ya CAG hasa pale anaposema eti NHIf wanaume walijifungua na kulipiwa fedha.

Personally nina uzoefu kwenye industry ya Bima za Afya nje na NHIF, huwa kuna minor errors kwny fomu za Claims ambapo unakuta baada ya Female formu imetikiwa male.. Narudia very minor errors tena kwenye normal operations katika ujazaji wa fomu... ila duh CAG kaifanya kuwa ishu kubwa sana kiukweli jamaa inabidi achunguzwe
Wanaume wamejifungua na kulipiwa fedha[emoji23][emoji23]
 
mkuu nitoe tongotongo,weka facts kutoka kwenye report badala ya maneno matupu
Nitakupa mfano ingawa siyo kutoka kwenye report moja kwa moja. Idara ya serikali inaweza kuwa na magari kadha na bahati nzuri pia madereva wa magari hayo wanaweza kuwa na taaluma ya ufundi mechanical, sasa muda wa service ukifika magari yanatakiwa kwenda TEMESA kwa service na merekebisho madogo na bahati mbaya idara inaweza kuwa haina fedha za kutosha kwa matengenezo.

Kupeleka magari TEMESA ni gharama kubwa na wakati mwingine TEMESA hawana mafundi wa kutosha hivyo nao wanapeleka magari hayo katika garage binafsi ambazo zimeteuliwa na wao. Kwa hiyo bill inapokuja itajumuisha:

1. inspection charges za TEMESA

2. inspectioncharges za garage binafsi

3. gharama za spares

4. labour charges za TEMESA

5. labour charges za garage binafsi na

6. labour charges za TEMESA.

Kwa hiyo gharama ya service ya gari moja TEMESA inaweza kuwa zaidi ya Tsh. milioni moja mpaka mbili kwa gari moja ambapo kama ofisi ingetumia madereva wake kufanya service na kununua spares gharama isingezidi Tshs laki tano kwa gari moja.

Hapa ni kweli taratibu zimekiukwa kwa idara kujitengenezea magari yenyewe lakini imeokoa fedha nyingi sana. Auditor akija ataandika query na mwishowe itakuja hoja kuna fedha zimetumika vibaya au kupotea hata kama idara itaonyesha risiti za spares, kwa sababu Auditor atataka risiti kutoka TEMESA.

Kumbuka wakati mwingi idara hazipati au kupelekewa fedha kwa wakati na hata zikipelekewa fedha unakuta haitoshi kufanya kazi zilizopangwa kwa hiyo wakuu wa idara wanajitoa muhanga kufanya baadhi ya vitu bila kufuata utaratibu ili baadhi ya kazi zisilale.
 
Ripoti ya CAG wetu imejikita zaidi kuona kama sheria zilifuatwa? Hata kama hakuna Fedha iliyokwapuliwa lakini akabaini sheria imekiukwa basi yeye anachokuja nacho nikuonyesha serikali imepata hasara Jambo amabalo naamini limekuwa likipotosha umma wa Watanzania.
Naamini hakuna taasisi isiyolindwa na sheria,pengine hii imekuathiri mojakwamoja ila unaelewa majukumu ya CAG? Na yeye kama mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali kuna katiba inayoratibu ukaguzi huo na unachotaka kusema ni kwamba anakagua bila kufuata sheria huku ukijua kuwa hiyo ni report na nyuma yake wako wakaguzi mbalimbali ,ni sawa nakusema ni sawa kwa mkandarasi kuchkua bilion 164 nae akatoa tenda kazi ifanyike kwa bil 40 hata kama kazi itaisha ila hakuna sheria inaruhusu icho kitu,elewa tuu kwamba hiyo report inatoka kulingana na sheria ya manunuzi na matumizi ya taasisi husika,sioni mantiki ya mada yako
 
Aisee hongera Mkuu umeongea kama mtu professional na mwenye vast experience kuhusu auditors.. Bila kuwapa treatment nzuri mfano hotel, vyakula vzuri, luxuries na kitu kidogo jamaa wanakuchafulia ripoti.

Hata mimi nishafanya nao kazi sana ndo nikaja kupata mtazamo tofauti kuhusu wakaguzi..

Kifupi ma auditor especially wa Tanzania hawana maana.
 
Hivi wewe watu wasipofuata sheria ya manunuzi na wakanunua kitu cha mabilioni bila stakabadhi wewe utawaweka kundi gani!...??

ukiwaweka kundi la wezi moja kwa moja bila kusikiliza unakua kama robot sio binadam, though sikatai baadhi ya watu wanatumia upande huo kufanya upigaji.
 
Mfano nimenunua tofali moja kwa sh. 900 na risiti ikapotea lakini umekuja site umelikuta tofali na katika kuulizia bei za matofali unagundua bei zinachezea sh. 900-1100?
Wewe kama auditor utapeleka ripoti kwa public kwamba pana ubadhirifu wa sh.900 sio?
Mkuu unategemea huo mfano kila mtu akiamua kupoteza ricept itakuaje? Unajua maana ya sheria ya manunuzi na matumizi!,chukulia huo ni mradi wa serikali pengine unahitaji tofali milioni moja wewe kama mnunuzi ukanunua tofali hafifu laki 6 kwa mia6,mia6 then ukanunua laki 4 mia 9,mia9 huku ukaguzi unaanza unasema una recept ya tofali laki4 kwa kuwa ndio bei inayojulikana......wewe kama mkaguzi mkuu utabaini nini???
 
Huo uongo wa huyo mzee asitoe tena

Kama kweli anasali na anamfahamu Mungu aache mara moja.
 
Nitakupa mfano ingawa siyo kutoka kwenye report moja kwa moja. Idara ya serikali inaweza kuwa na magari kadha na bahati nzuri pia madereva wa magari hayo wanaweza kuwa na taaluma ya ufundi mechanical, sasa muda wa service ukifika magari yanatakiwa kwenda TEMESA kwa service na merekebisho madogo.

Kupeleka magari TEMESA ni gharama kubwa na wakati mwingine TEMESA hawana mafundi wa kutosha hivyo nao wanapeleka magari hayo katika garage binafsi ambazo zimeteuliwa na wao. Kwa hiyo bill inapokuja itajumuisha:

1. inspection charges za TEMESA

2. inspectioncharges za garage binafsi

3. gharama za spares

4. labour charges za TEMESA

5. labour charges za garage binafsi na

6. labour charges za TEMESA.

Kwa hiyo gharama ya service ya gari moja TEMESA inaweza kuwa zaidi ya Tsh. milioni moja mpaka mbili kwa gari moja ambapo kama ofisi ingetumia madereva wake kufanya service na kununua spares gharama isingezidi Tshs laki tano kwa gari moja.

Hapa ni kweli taratibu zimekiukwa kwa idara kujitengenezea magari yenyewe lakini imeokoa fedha nyingi sana. Auditor akija ataandika query na mwishowe itakuja hoja kuna fedha zimetumika vibaya au kupotea hata kama idara itaonyesha risiti za spares, kwa sababu Auditor atataka risiti kutoka TEMESA.

Kumbuka wakati mwingi idara hazipati au kupelekewa fedha kwa wakati na hata zikipelekewa fedha unakuta haitoshi kufanya kazi zilizopangwa kwa hiyo wakuu wa idara wanajitoa muhanga kufanya baadhi ya vitu bila kufuata utaratibu ili baadhi ya kazi zisilale.
naweza sema umetunga hadithi ili kusindikiza hoja yako na ndiyo maana umesema mwenyewe haipo kwenye ripoti. tujadili facts za kwenye ripoti sio kuleta hadithi. hata mimi hapa nikija naweza kusema CAG nilimpa nyaraka zote akaficha halafu akaandika kuna ubathirifu.

Kuhusu hoja yako
Serikali imeweka sheria magari yake yote yatengenezwe Temesa au kampuni iliyosajiliwa. Sasa wewe unampa dereva atengeneze,hiyo sio kazi ya dereva. Tunapimaje performance na ufanisi wa dereva? Akibumba matengenezo je. Ndio haya magari mengi ya serikali yamechoka kwa sababu ya service za kihuni.

Halafu ukiruhusiwa kila mtu anafanya anavyojisikia nje ya utaratibu,hiyo ni serikali au pori la manyani?

CAG sio mwehu akute gari imetengenezwa na dereva na docs za manunuzi ya vifaa zote zipo, vifaa vilikaguliwa, vimeingizwa kwenye reja na service yako imekaguliwa kama kweli imefanyika,halafu aseme kuna wizi. Nachojua ataonyesha utaratibu uliokiukwa.

Kama umeruka stage nilizotaja hapo watakuletea noma tu,kitu ambacho ni sahihi. Nyinyi mnajinunulia tu bidhaa bila kufuata utaratibu halafu mnalaumu wakaguzi. Kibaya zaidi mnafanya makusudi kuficha nia ovu
 
Sijawahi kukuunga mkono mleta mada ila kwa hii mada nakuunga mkono mia kwa mia
Umechambua ki great thinker
 
Kutofuata taratibu au sheria kunaweza kuwa ni kiashiria cha wizi, uzembe au taratibu ngumu.

Kwa mfano sheria ya manunuzi inasema kuwa manunuzi yote ni lazima kuwe na stakabadhi. Kutokuwepo stakabadhi kunaweza kuashiria wizi, kwa sababu hatujui kilichotajwa kununuliwa kama kilinunuliwa, na kama kilinunuliwa, hakuna uthibitisho wa bei na kiasi kilichonunuliwa. Aliyefanya manunuzi hayo yasiyo na uthibitisho atachukuliwa hatua kama mwizi maana ameshindwa kuthibitisha kama kulikuwa na manunuzi kwa utaratibu uliowekwa.

Kwa taratibu za manunuzi, kama hakuma risiti ina maana hakuna manunuzi, na kama hakuna manunuzi, hela iliyotajwa kwamba imefanya manunuzi maana yake imeibiwa. Japo yawezekana haikuibiwa, lakini ndiyo taratibu zilizowekwa na kukubalika.
Huelewi hata maana ya Receipt ni nini?
Receipt sio tu kile kikaratasi unachopewa ukinunua kitu waweza printiwa hicho kikaratasi ukapewa kumbe bidhaa hukupewa !

Receipt ni kama bidhaa au huduma zilikuwa received!! Mleta mada ndio kajikita hapo wewe unajikita kwenye kikaratasi kinachoitwa receipt!!.kuwa compliance unataka receipt kikaratasi aiseeee!!
 
Receipt ni kama bidhaa au huduma zilikuwa received!! Mleta mada ndio kajikita hapo wewe unajikita kwenye kikaratasi kinachoitwa receipt!!.kuwa compliance unataka receipt kikaratasi aiseeee!!
mnatia uongo kumtetea Hayati. Risit ni nyaraka kuonyesha hela iliyolipwa imepokelewa na uliyemlipa. Mtoa huduma anakiri kupokea pesa yako, wengine hutoa EFD receipts. Sasa wewe umechukua imprest kujenga choo,risit hakuna halafu unataka CAG aamini ulilipa sawa sawa na unachosema. Mind you mali za serikali zinatumika kwa nyaraka.

Baba yako mwenyewe alikuwa akisisitiza ukilipa dai risit,leo hii hutaki CAG akomalie risit.

Humo mitaani TRA kibao wanafukuzana na wanaonunua vitu bila risit. hujiulizi kwa nini? 😆😆😆😆
 
Naamini hakuna taasisi isiyolindwa na sheria,pengine hii imekuathiri mojakwamoja ila unaelewa majukumu ya CAG? Na yeye kama mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali kuna katiba inayoratibu ukaguzi huo na unachotaka kusema ni kwamba anakagua bila kufuata sheria huku ukijua kuwa hiyo ni report na nyuma yake wako wakaguzi mbalimbali ,ni sawa nakusema ni sawa kwa mkandarasi kuchkua bilion 164 nae akatoa tenda kazi ifanyike kwa bil 40 hata kama kazi itaisha ila hakuna sheria inaruhusu icho kitu,elewa tuu kwamba hiyo report inatoka kulingana na sheria ya manunuzi na matumizi ya taasisi husika,sioni mantiki ya mada yako
Ok mimi umenipa kazi ya kupeleka wafanyakazi ofisini na kurudi umenilipa kwa mwaka mzima

Mabasi yangu nikaona yana shida kidogo nikaenda kuchukua mabasi kwa Aboud bus service mazuri kuliko hata yangu wafanye kazi hiyo ili nisivunje uaminifu wafanyakazi waende na kurudi kazini bila shida kipindi chote cha mkataba na ikawa hivyo wewe shida yako nini hata kama ulinilipa bilioni moja Aboud.nikamlipa milioni mia lakini huduma ulipewa kinsmuuma nini? Mkataba mimi na wewe nimeuvunja wapi? Ulinitaka nikuletee mabasi nimepita kwa bilioni moja sasa huyo third party unamtakia nini? Kazi ikiwa mbovu nilaumu mimi sio huyo third party lakini issue ya kuwa huyo third party nimemlipa kiasi gani non of your business
 
Mfano nimenunua tofali moja kwa sh. 900 na risiti ikapotea lakini umekuja site umelikuta tofali na katika kuulizia bei za matofali unagundua bei zinachezea sh. 900-1100?
Wewe kama auditor utapeleka ripoti kwa public kwamba pana ubadhirifu wa sh.900 sio?
Hata majizi huwa kama wewe usemavyo,wanadai wamepoteza docs. Huyu CAG alikuwa na wewe wakati unanunua tofali? Yeye anaaminishwa na nyaraka na uhalisia wa kazi.
Mtu kama wewe hata kwenye hiyo nafasi hutoshi. Unatakiwa kuwekwa pembeni
 
Back
Top Bottom