Ripoti ya IMF (2025): Tanzania Miongoni Mwa Nchi 10 za Afrika Zenye Deni Kubwa la IMF

Just Dec 2020 tulikua hatudaiwi ht mia mbovu na IMF na ma miradi tulikua nayo kila kona...fast forward 5yrs tupo top 10 na vitu kwa ground ni vya kutafuta na tochi...we are truly li likichwa la mwendawazimu...
 
Sidhani kama dhamira ikiwepo,, kuna atakayekuwa maskini hapa Tanzania. Rasilimali lukuki, ila nia ikiwa sifuri hadi Yesu arudie hamna kitu. Ardhi, maji, misitu, utalii, madini, wanyama wote ama wa kufugwa au porini, nguvu kazi nk
Nakubaliana na wewe, mi issue najiuliza ni ile ya kuwaita watu mbumbumbu, wapunguze uoga waandamane, wagome, watumie nguvu. Halafu unacheki watarajiwa au wahamasishwaji aina ya maisha waliyo nayo wakafanye hivyo kweli?

Nadhani hata approach ya upinzani ingebadilika, sina pendekezo lakini hii ya migomo na maandamano kwa sasa haiwezi kufanya kazi.
 
Mama Abduli kasema Tanzania tuna deni dogo kuliko nchi zote afrika mashariki
 
Mbona la Kenya ni kubwa zaidi yetu? Basi bado tuko vizuri

Umeandika upuuzi ndugu yangu! Hivi Bakhresa akiwa na deni la shilingi bilioni 1, wewe ukawa na deni la milioni 600, utasema wewe una unafuu?

Kenya's nominal GDP is projected to be $131.67 billion in 2025, according to International Monetary Fund (IMF) data,
https://www.google.com/search?clien...2ahUKEwjRme_Vy7uPAxVg2wIHHTLcJQYQtKgLegQIDxAB
Tanzania's GDP in 2025 is projected to be around USD 85.98 billion.
 
Ukimtawala mtu asiye na uchungu na rasilimali zake, utachukua chochote akikuangalia na kukufurahia na kukuchekea tu.

Hii haipo duniani popote isipokuwa Tanzania tu.

Mpaka atokee mtu mwingine nje yetu atuonee huruma ya kutuendeleza, kitu ambacho hakitatokea asilani.

Aliishia Nyerere tu aliyejenga viwanda zaidi ya 400 Watanganyika wakaviuza na kubinafsisha kila shirika la umma kwa watu binafsi na wawezekezaji matapeli , hata yaliyokuwa yanazalisha faida kubwa na taasisi zote.
 
Consciousness ya jamii hailazimishwi, inakuja taratibu tu kwa wtu kuamshana, kuna time mambo yatabadilika ingawa kwa sasa hakuna dalili za moja kwa moja.
 


Kukopa ni ujasiri,kiafrika ukitaka mke,swali la kwanza,utaulizwa,una madeni?Ukisema huna madeni,hupewi mke,unaonekana utamlaza njaa mtoto wa watu.Ukiona mtu anapiga makelele kuhusu madeni ujuwe huyo sio mwanamme.
 
Dunia nzima wanakopa,ukiona mtu anaogopa madeni,ujuwe huyo ni.mwehu
 
Kukopa lazima,ukiona mtu hakopi,huyo ni mwendawazimu,mkichaa peke yake,duniani ndio hana madeni
 
Dunia nzima wanakopa,ukiona mtu anaogopa madeni,ujuwe huyo ni.mwehu
Hiyo dunia nzima ndiyo gani
chalii.

Wanaolipa wangekuwa wa Kikwajuni, Mchambawima, Chake chake sawa.

Maana ndiyo waliyokopa na ndiko zinakojenga.

Ukope wewe nilipe mimi, huo ni utumwa na ubabe broo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…