Ripoti ya Jaji Chande, Bado Haijaweza Kutibu Chuki ya October 29!, Chuki Hii Inaendelea Kulitafuna Taifa Kimya Kimya!, Tuitibu Haraka Vinginevyo...!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
59,804
Reaction score
134,593
Wanabodi,
Hii ni makala yangu kwenye gazeti la Mwananchi la leo. Hakuna ubishi kuwa kilichotokea October 29, kimesababishwa na chuki iliyopitiliza!. Japo Ripoti ya Jaji Chande, imepunguza kidogo kiu ya taarifa kwa kuitaja idadi ya vifo, lakini bado haijapunguza machungu ya October 29 na kupooza chuki dhidi ya kilichotokea!. Chuki hii inaendelea kututafuna taifa, kimya kimya, chini chini, mdogo mdogo na kidogo kidogo kidogo kwa mtindo wa panafuka moshi. Chuki hii ni ugonjwa, ambao unakuwa na kuambukiza kwa kasi, usipotibiwa kikamilifu, hautakuwa na mwisho mwema!. Andamana nami jinsi ya kuutibu.
Makala ya Tiba Chuki Gazeti la Mwananchi.jpg

Je ni wangapi miongoni mwetu, wajua kuwa chuki ikizidi ni ugonjwa?.

Chuki ni ugonjwa hatari na unaua!, tena unaoambukiza haraka kwa kasi ya kidigitali, hata kwa simu, sms, whatsapp, TV, Redio, magazeti au mitandao ya kijamii!. Natoa wito kwa Watanzania tuacheni chuki iliyopitiliza!.

Tiba ya ugonjwa huu wa chuki,ni kuwa na upendo,kwanza kwa kujipenda wewe mwenyewe,kisha kumpenda na jirani yako kama unavyo jipenda mwenyewe na hata ikitokea kuna mtu ni adui yako amekutenda visivyo,usimjibu kwa kumlipizia au kumtenda,bali mjibu kwa upendo, Adui Mpende!.

Kwa wale za zamani, tulioshuhudia ile Genocide ya Rwanda ya 1994, ilisababishwa na chuki tuu ya kikabila!, tena ni kabila moja hilo hilo , Watutsi na Wahutu, wote ni Wanyarwanda!. Waliuana kwa kuchinjana mpaka!. Kiwango hicho cha chuki kwa hapa nchini kwetu, kilifikia kikomo, October 29.

Naomba kueleza kisa kidogo cha kweli, wakati nikiwa Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, UDSM, nikiishi Block F, Mabibo, kunatokea visa vya wizi wa vitu vidogo vidogo, simu, vitabu, nguo, etc, kama kawaida, kwenye wengi kuna mengi,watu wakaanza kujenga chuki na wizi.

Kuna siku kuna mwanafunzi wa kike, alimpigia mtu yowe la mwizi, huyo kijana alivamiwa na wanafunzi wenye hasira za chuki ya kuibiwa, kijana yule alipigwa na alikufa papo hapo, na watu waliendelea kuupiga mwili wa marehemu, kumaliza hasira na chuki zao licha ya kujua ameishakufa!.

Polisi chuo walipokuja kuubeba, mwili, na kuuliza, aliyeibiwa ni nani, hakuna jibu, marehemu ameiba nini, hakuna jibu kumbe yule kijana ni mwanafunzi wa chuo, alikuwa amekwenda kwa rafiki yake wa kike, binti akapiga yowe la mwizi, kikatokea kilichotokea!. Mtu ukiwa na chuki iliyopitiliza, unarukwa na akili, unaweza kufanya jambo lolote hata kuua!.

Kufuatia kilichotokea ile October 29, ugonjwa huu wa chuki umeongezeka kwa Watanzanzia kwa kasi ya ajabu, huko mitandaoni ni hakufai, imefikia kiwango, mtu anakufa, badala ya watu kuhuzunika,ndio kwanza wanashangilia!.

Kufuatia kueneo kwa kasi kwa gonjwa hili la chuki miongoni mwa Watanzania, taasisi ya Family Vibes Foundation (Family Vibes) ambayo ni shirika lisilo la kiserikali la Tanzania linalojihusisha na kuhamasisha na kuimarisha afya ya akili katika jamii nchini Tanzania, waliandaa semina maalum ya waandishi wa habari kuhusu Tiba ya Chuki iliandaliwa kama jukwaa la kitaifa la kuanzisha mjadala wa kijamii na kisera kuhusu namna bora ya kushughulikia changamoto za chuki, migogoro na upungufu wa mshikamano na upendo katika jamii.

Semina hiyo, ilihutubiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Family Vibes, Dkt. Mayrose Majinge ambaye alijenga msingi wa kitaaluma wa dhana ya Tiba ya Chuki kwa kuunganisha afya ya mwili, akili na jamii Semina hii ilihudhuriwa na waandishi wa habari zaidi ya 150 kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini, ikiwemo vikiwemo TV, Redio, Magazeti na mitandao ya kijamii.

Ushiriki huu mpana unaonesha nafasi ya kimkakati ya sekta ya habari kama “behavior change communication platform” katika kueneza elimu ya tiba ya gonjwa hili kwa jamii yetu, kwasababu vyombo vya habari vimebeba jukumu la kuwa daraja kati ya wataalamu, serikali na wananchi katika kueneza elimu ya afya ya akili na ustawi wa kijamii.

Dr. Majinge, alieleza katika mazingira ya sasa ya maisha yenye mabadiliko ya haraka, kutokuwa na uhakika na changamoto mbalimbali za kijamii na kiuchumi, kumekuwa na ongezeko la matatizo ya afya ya akili. Matatizo hayo yanajitokeza katika maeneo mbalimbali ikiwemo migogoro ya mahusiano (mtu na nafsi yake, marafiki na wenza), majeraha ya utotoni, msongo wa mawazo wa muda mrefu, kuvunjika kwa familia pamoja na changamoto zinazohusiana na masuala ya kijinsia na mahusiano.

Shirika linafanya kazi kwa kutumia mbinu bunifu zinazolenga kushughulikia changamoto za kijamii, kiuchumi na kitamaduni zinazoathiri afya ya akili. Katika utekelezaji wake, linatumia dhana ya Akili ya Kihisia (Emotional Intelligence – EI) pamoja na mbinu nyingine zinazokubalika na zinazoweza kutekelezwa kwa urahisi katika jamii.

Huduma hizi hutolewa kupitia programu yake ya Mahusiano & Family Clinic ambayo ni mfumo wa huduma unaolenga kusaidia na kuimarisha ustawi wa familia, taasisi, jamii na taifa kwa ujumla kupitia huduma za afya ya akili na msaada wa kisaikolojia na kijamii (Mental Health and Psychosocial Support – MHPSS).

Tafiti za kijamii na uchambuzi wa mwenendo wa kijamii zinaonesha kuwa, mivutano ya kihisia na kisaikolojia imeanza kujitokeza kwa uwazi zaidi katika jamii, hali inayohitaji mbinu mpya za elimu, uelimishaji wa umma na uimarishaji wa afya ya akili, changamoto hizi kwa Tanzania zilifikia kiwango cha juu tarehe 29 October, kwa vijana wenye chuki, kufanya uharibifu wa mali, na miundombinu ya umma, bila wao kujijua kuwa ni wagonjwa na vyombo vya dola navyo bila kujua vina deal na wagonjwa wa afya ya akiki,vikajibu mapigo kwa risasi za moto,na matokeo yake watu 518 wakipoteza maisha!

Vijana walioshikwa, walifikishwa mahakamani na kushitakiwa kwa uhaini, hata hivyo, Rais wa JMT, Dr. Samia Suluhu Hassan, aliwasamehe kwasababu wengi wao walifuata mkumbo kwa kuambukizwa na ugonjwa huo wa chuki, bila wao kujua watendalo.

Baada ya Tume ya Uchunguzi wa Vurugu za Tarehe 29 October, 2025 kuwasilisha ripoti yake kwa rais Samia, kilichofuatia kwenye mitandao ya kijamii, ni watu wenye ugonjwa huu wa chuki, walifungulia matusi kwa kutukana, na Tume ilipokea simu zaidi ya 300 zikiwatukana matusi!. Kitendo tuu cha mtu kupiga simu na kutukana matusi,ni uthibitisho wa changamoto ya afya ya akili ya ugonjwa wa chuki.

Najua saa hizi Jeshi la polisi linaendelea na kamata kamata ya watukanaji hawa, bila kujua hawa ni wagonjwa wa afya ya akili, nashauri, kama wale waandamanaji wa October 29 walivyosamehewa kwa maana hawakujua watendalo, nashauri jeshi la Polisi, baada ya kuwashitaki ili kutoa funzo kwa wengine, Family Vibes waitwe, wakawatibu watu hao, na baada ya kupata tiba ya chuki, wasamehewe na kwenda kuieneza hiyo tiba kwa wengine, taifa liponywe na hili gonjwa la chuki iliyopitiliza.

Waandishi wamependekeza kuanzishwa kwa vipindi maalum vya kitaifa vya afya ya akili na mahusiano ya kijamii katika vyombo vya habari, na Makala elimishi kama hii kwenye magazeti na mitandao ya jamii ili kuliponya taifa letu na gonjwa hili la chuki.

Paskali
 
Wanabodi,
Hii ni makala yangu kwenye gazeti la Mwananchi la leo. Hakuna ubishi kuwa kilichotokea October 29, kimesababishwa na chuki iliyopitiliza!. Japo Ripoti ya Jaji Chande, imepunguza kidogo kiu ya taarifa kwa kuitaja idadi ya vifo, lakini bado haijapunguza machungu ya October 29 na kupooza chuki dhidi ya kilichotokea!. Chuki hii inaendelea kututafuna taifa, mdogo mdogo na kidogo kidogo kidogo kwa mtindo wa panafuka moshi. Chuki hii ni ugonjwa, usipotibiwa kikamilifu, hautakuwa na mwisho mwema!. Andamana nami jinsi ya kuutibu.
View attachment 3587941

Mwalimu Paskali,
ni kweli kabisa ipo chuki ya kupindukia nchini, na hiyo inajidhihirisha zaidi baada ya mipango ovu ya AZAKI zilizofadhili utekelezaji wa vurugu za Oct 2025, zilizotoa mafunzo ya namna ya kufanya fujo, kufanya uharibifu na kuleta maafa, kutoa mbinu za kuwatambua na kuwashughilikia waliojitokeza kupiga kura na wanaogoma kujiunga nao kufanya fujo kufeli.

So,
AZAKI na vyama vya siasa vilivyoshiriki kuchochea vurugu zile zilizoshindwa, kiukweli wamejawa hasira na chuki kupindukia baada ya malengo yao mauvu kubainika na kushindwa kufikia malengo ya uovu ule.

hata ingelikua wewe,
umetumia gharama, muda, vifaa, umetumia watu kufanikisha lengo lako fulani halafu linafeli. Lazima utajawa hasira na chuki tu hasa dhidi ya waliokwamisha mipango na malengo yako.
I think that's nature.
 
Mwalimu Paskali,
ni kweli kabisa ipo chuki ya kupindukia nchini, na hiyo inajidhihirisha zaidi baada ya mipango ovu ya AZAKI zilizofadhili utekelezaji wa vurugu za Oct 2025, zilizotoa mafunzo ya namna ya kufanya fujo, kufanya uharibifu na kuleta maafa, kutoa mbinu za kuwatambua na kuwashughilikia waliojitokeza kupiga kura na wanaogoma kujiunga nao kufanya fujo kufeli.

So,
AZAKI na vyama vya siasa vilivyoshiriki kuchochea vurugu zile zilizoshindwa, kiukweli wamejawa hasira na chuki kupindukia baada ya malengo yao mauvu kubainika na kushindwa kufikia malengo ya uovu ule.
Msomi mzima wa Udsm unaandika upuuzi kama huu? Azaki zilifadhili mafunzo na kulipa vijana waandamane!
 
Chanzo cha chuki kinafahamika na ndicho kinahitaji tiba.
 
Mwalimu Paskali,
ni kweli kabisa ipo chuki ya kupindukia nchini, na hiyo inajidhihirisha zaidi baada ya mipango ovu ya AZAKI zilizofadhili utekelezaji wa vurugu za Oct 2025, zilizotoa mafunzo ya namna ya kufanya fujo, kufanya uharibifu na kuleta maafa, kutoa mbinu za kuwatambua na kuwashughilikia waliojitokeza kupiga kura na wanaogoma kujiunga nao kufanya fujo kufeli.

So,
AZAKI na vyama vya siasa vilivyoshiriki kuchochea vurugu zile zilizoshindwa, kiukweli wamejawa hasira na chuki kupindukia baada ya malengo yao mauvu kubainika na kushindwa kufikia malengo ya uovu ule.

Hakuna raia mwema angetaka kile kilichokuwa kimeanza kisambae bila kudhibitiwa.

Chuki inakuzwa na gharama ya udhibiti, namna ghasia zilivyodhibitiwa na kutokuwepo na aliyewajibika kwa madhaifu wakati wa udhibiti.,

Ujue hakuna hata mtu mmoja, si mkuu wa wilaya au katibu wa wizara, hata hawa wa serikali za mitaa aliyewajibika au kujiwajibisha.

Kama kuna watu 100 waliuwawa bila hatia wana ndugu, rafiki, wazazi unadhani hawatabeba chuki?

Kama kweli tuna nia ya kusafisha kilichotokea, tuache kusifiana, kunahitajika uwajibikaji, lazima kuna askari alivuka mipaka ya utendaji, atafutwe awajibishwe, kuna kiongozi alifanya makosa ya kiusimamizi, awajibishwe. Huo ndo ustaarabu na angalau ndugu, jamaa na marafiki wa waliouwawa wanaweza pata sababu ya kuwa na amani ndani mwao.
 
UNCLE T
Wewe kazi yako na michezo unayofanyiwa inajulikana
 
Wanabodi,
Hii ni makala yangu kwenye gazeti la Mwananchi la leo. Hakuna ubishi kuwa kilichotokea October 29, kimesababishwa na chuki iliyopitiliza!. Japo Ripoti ya Jaji Chande, imepunguza kidogo kiu ya taarifa kwa kuitaja idadi ya vifo, lakini bado haijapunguza machungu ya October 29 na kupooza chuki dhidi ya kilichotokea!. Chuki hii inaendelea kututafuna taifa, mdogo mdogo na kidogo kidogo kidogo kwa mtindo wa panafuka moshi. Chuki hii ni ugonjwa, usipotibiwa kikamilifu, hautakuwa na mwisho mwema!. Andamana nami jinsi ya kuutibu.
View attachment 3587941
Je ni wangapi miongoni mwetu, wajua kuwa chuki ikizidi ni ugonjwa?.

Chuki ni ugonjwa hatari na unaua!, tena unaoambukiza haraka kwa kasi ya kidigitali, hata kwa simu, sms, whatsapp, TV, Redio, magazeti au mitandao ya kijamii!. Natoa wito kwa Watanzania tuacheni chuki iliyopitiliza!.

Tiba ya ugonjwa huu wa chuki,ni kuwa na upendo,kwanza kwa kujipenda wewe mwenyewe,kisha kumpenda na jirani yako kama unavyo jipenda mwenyewe na hata ikitokea kuna mtu ni adui yako amekutenda visivyo,usimjibu kwa kumlipizia au kumtenda,bali mjibu kwa upendo, Adui Mpende!.

Kwa wale za zamani, tulioshuhudia ile Genocide ya Rwanda ya 1994, ilisababishwa na chuki tuu ya kikabila!, tena ni kabila moja hilo hilo , Watutsi na Wahutu, wote ni Wanyarwanda!. Waliuana kwa kuchinjana mpaka!. Kiwango hicho cha chuki kwa hapa nchini kwetu, kilifikia kikomo, October 29.

Naomba kueleza kisa kidogo cha kweli, wakati nikiwa Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, UDSM, nikiishi Block F, Mabibo, kunatokea visa vya wizi wa vitu vidogo vidogo, simu, vitabu, nguo, etc, kama kawaida, kwenye wengi kuna mengi,watu wakaanza kujenga chuki na wizi.

Kuna siku kuna mwanafunzi wa kike, alimpigia mtu yowe la mwizi, huyo kijana alivamiwa na wanafunzi wenye hasira za chuki ya kuibiwa, kijana yule alipigwa na alikufa papo hapo, na watu waliendelea kuupiga mwili wa marehemu, kumaliza hasira na chuki zao licha ya kujua ameishakufa!.

Polisi chuo walipokuja kuubeba, mwili, na kuuliza, aliyeibiwa ni nani, hakuna jibu, marehemu ameiba nini, hakuna jibu kumbe yule kijana ni mwanafunzi wa chuo, alikuwa amekwenda kwa rafiki yake wa kike, binti akapiga yowe la mwizi, kikatokea kilichotokea!. Mtu ukiwa na chuki iliyopitiliza, unarukwa na akili, unaweza kufanya jambo lolote hata kuua!.

Kufuatia kilichotokea ile October 29, ugonjwa huu wa chuki umeongezeka kwa Watanzanzia kwa kasi ya ajabu, huko mitandaoni ni hakufai, imefikia kiwango, mtu anakufa, badala ya watu kuhuzunika,ndio kwanza wanashangilia!.

Kufuatia kueneo kwa kasi kwa gonjwa hili la chuki miongoni mwa Watanzania, taasisi ya Family Vibes Foundation (Family Vibes) ambayo ni shirika lisilo la kiserikali la Tanzania linalojihusisha na kuhamasisha na kuimarisha afya ya akili katika jamii nchini Tanzania, waliandaa semina maalum ya waandishi wa habari kuhusu Tiba ya Chuki iliandaliwa kama jukwaa la kitaifa la kuanzisha mjadala wa kijamii na kisera kuhusu namna bora ya kushughulikia changamoto za chuki, migogoro na upungufu wa mshikamano na upendo katika jamii.

Semina hiyo, ilihutubiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Family Vibes, Dkt. Mayrose Majinge ambaye alijenga msingi wa kitaaluma wa dhana ya Tiba ya Chuki kwa kuunganisha afya ya mwili, akili na jamii Semina hii ilihudhuriwa na waandishi wa habari zaidi ya 150 kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini, ikiwemo vikiwemo TV, Redio, Magazeti na mitandao ya kijamii.

Ushiriki huu mpana unaonesha nafasi ya kimkakati ya sekta ya habari kama “behavior change communication platform” katika kueneza elimu ya tiba ya gonjwa hili kwa jamii yetu, kwasababu vyombo vya habari vimebeba jukumu la kuwa daraja kati ya wataalamu, serikali na wananchi katika kueneza elimu ya afya ya akili na ustawi wa kijamii.

Dr. Majinge, alieleza katika mazingira ya sasa ya maisha yenye mabadiliko ya haraka, kutokuwa na uhakika na changamoto mbalimbali za kijamii na kiuchumi, kumekuwa na ongezeko la matatizo ya afya ya akili. Matatizo hayo yanajitokeza katika maeneo mbalimbali ikiwemo migogoro ya mahusiano (mtu na nafsi yake, marafiki na wenza), majeraha ya utotoni, msongo wa mawazo wa muda mrefu, kuvunjika kwa familia pamoja na changamoto zinazohusiana na masuala ya kijinsia na mahusiano.

Shirika linafanya kazi kwa kutumia mbinu bunifu zinazolenga kushughulikia changamoto za kijamii, kiuchumi na kitamaduni zinazoathiri afya ya akili. Katika utekelezaji wake, linatumia dhana ya Akili ya Kihisia (Emotional Intelligence – EI) pamoja na mbinu nyingine zinazokubalika na zinazoweza kutekelezwa kwa urahisi katika jamii.

Huduma hizi hutolewa kupitia programu yake ya Mahusiano & Family Clinic ambayo ni mfumo wa huduma unaolenga kusaidia na kuimarisha ustawi wa familia, taasisi, jamii na taifa kwa ujumla kupitia huduma za afya ya akili na msaada wa kisaikolojia na kijamii (Mental Health and Psychosocial Support – MHPSS).

Tafiti za kijamii na uchambuzi wa mwenendo wa kijamii zinaonesha kuwa, mivutano ya kihisia na kisaikolojia imeanza kujitokeza kwa uwazi zaidi katika jamii, hali inayohitaji mbinu mpya za elimu, uelimishaji wa umma na uimarishaji wa afya ya akili, changamoto hizi kwa Tanzania zilifikia kiwango cha juu tarehe 29 October, kwa vijana wenye chuki, kufanya uharibifu wa mali, na miundombinu ya umma, bila wao kujijua kuwa ni wagonjwa na vyombo vya dola navyo bila kujua vina deal na wagonjwa wa afya ya akiki,vikajibu mapigo kwa risasi za moto,na matokeo yake watu 518 wakipoteza maisha!

Vijana walioshikwa, walifikishwa mahakamani na kushitakiwa kwa uhaini, hata hivyo, Rais wa JMT, Dr. Samia Suluhu Hassan, aliwasamehe kwasababu wengi wao walifuata mkumbo kwa kuambukizwa na ugonjwa huo wa chuki, bila wao kujua watendalo.

Baada ya Tume ya Uchunguzi wa Vurugu za Tarehe 29 October, 2025 kuwasilisha ripoti yake kwa rais Samia, kilichofuatia kwenye mitandao ya kijamii, ni watu wenye ugonjwa huu wa chuki, walifungulia matusi kwa kutukana, na Tume ilipokea simu zaidi ya 300 zikiwatukana matusi!. Kitendo tuu cha mtu kupiga simu na kutukana matusi,ni uthibitisho wa changamoto ya afya ya akili ya ugonjwa wa chuki.

Najua saa hizi Jeshi la polisi linaendelea na kamata kamata ya watukanaji hawa, bila kujua hawa ni wagonjwa wa afya ya akili, nashauri, kama wale waandamanaji wa October 29 walivyosamehewa kwa maana hawakujua watendalo, nashauri jeshi la Polisi, baada ya kuwashitaki ili kutoa funzo kwa wengine, Family Vibes waitwe, wakawatibu watu hao, na baada ya kupata tiba ya chuki, wasamehewe na kwenda kuieneza hiyo tiba kwa wengine, taifa liponywe na hili gonjwa la chuki iliyopitiliza.

Waandishi wamependekeza kuanzishwa kwa vipindi maalum vya kitaifa vya afya ya akili na mahusiano ya kijamii katika vyombo vya habari, na Makala elimishi kama hii kwenye magazeti na mitandao ya jamii ili kuliponya taifa letu na gonjwa hili la chuki.

Paskali
Hiyo chuki ipo kwa viongozi baadhi chadema,wanaharakati na viongozi baadhi wa kanisa katoliki
Moravian Jana wamempa tuzo rais,walutheri wapo na rais, waislam wapo na rais,95% ya nchi Iko pamoja na rais na wanalaani waliochoma miundombinu,mali za watu na kuiba
 
Hakuna raia mwema angetaka kile kilichokuwa kimeanza kisambae bila kudhibitiwa.

Chuki inakuzwa na gharama ya udhibiti, namna ghasia zilivyodhibitiwa na kutokuwepo na aliyewajibika kwa madhaifu wakati wa udhibiti.,

Ujue hakuna hata mtu mmoja, si mkuu wa wilaya au katibu wa wizara, hata hawa wa serikali za mitaa aliyewajibika au kujiwajibisha.

Kama kuna watu 100 waliuwawa bila hatia wana ndugu, rafiki, wazazi unadhani hawatabeba chuki?

Kama kweli tuna nia ya kusafisha kilichotokea, tuache kusifiana, kunahitajika uwajibikaji, lazima kuna askari alivuka mipaka ya utendaji, atafutwe awajibishwe, kuna kiongozi alifanya makosa ya kiusimamizi, awajibishwe. Huo ndo ustaarabu na angalau ndugu, jamaa na marafiki wa waliouwawa wanaweza pata sababu ya kuwa na amani ndani mwao.
Of course,
ambao hawakutaka wala kutamani uovu na vurugu zile kudhibitiwa ni pamoja na AZAKI na vyama vya siasa vilivyoshiriki kupanga, kuchochea na kufadhili magaidi waliofanya vurugu, uharibifu na kusababisha maafa yaliyotokea kuendelea kufanya hivyo kote nchini.

In fact,
lengo la AZAKI zile ilikua ni kuona maafa zaidi yakitokea na uharibifu zaidi ukitokea ili hatimae wajihakikishie pesa nyingi zaidi kutoka kwa mabwenyenye ya magharibi yaliyokusudia kupenyeza ushoga Tanzania kwa lazima na kwa mgongo wa kisiasa kwa kutumia AZAKI na baadhi ya vyama vya siasa.

baadhi ya AZAKI na baadhi ya vyama vya siasa ndivyo haswa vimejawa chuki na kujaribu kuisambaza kwa wengine ambao kwa kweli wengi wamekataa kuuziwa ujinga huo humu nchini. 🐒
 
Of course,
ambao hawakutaka wala kutamani uovu na vurugu zile kudhibitiwa ni pamoja na AZAKI na vyama vya siasa vilivyoshiriki kupanga, kuchochea na kufadhili magaidi waliofanya vurugu, uharibifu na kusababisha maafa yaliyotokea kuendelea kufanya hivyo kote nchini.

In fact,
lengo la AZAKI zile ilikua ni kuona maafa zaidi yakitokea na uharibifu zaidi ukitokea ili hatimae wajihakikishie pesa nyingi zaidi kutoka kwa mabwenyenye ya magharibi yaliyokusudia kupenyeza ushoga Tanzania kwa lazima na kwa mgongo wa kisiasa kwa kutumia AZAKI na baadhi ya vyama vya siasa.

baadhi ya AZAKI na baadhi ya vyama vya siasa ndivyo haswa vimejawa chuki na kujaribu kuisambaza kwa wengine ambao kwa kweli wengi wamekataa kuuziwa ujinga huo 🐒
AZAKi walihusika na kutuliza ghasia? Hoja yangu ni udhaifu uliotokea wakati wa kutuliza ghasia na uwajibikaji.
 
Hiyo chuki ipo kwa viongozi baadhi chadema,wanaharakati na viongozi baadhi wa kanisa katoliki
Moravian Jana wamempa tuzo rais,walutheri wapo na rais, waislam wapo na rais,95% ya nchi Iko pamoja na rais na wanalaani waliochoma miundombinu,mali za watu na kuiba
Boss, Kama 5% inaweza sababisha gharama kubwa namna ile basi 5% si ya kuitamka kiwepesi.

Hiyo 5% ambayo sijui usahihi wake si ya kupuuzwa. Hapo unaongelea watu karibu M3.

Kinachotakiwa ni hiyo 5% unayoisema isipuuzwe kwa kiwango cha kuamua kuwa liwalo na liwe. Umeshajionea mwenyewe liwalo na liwe inaweza sababisha nini.

Kutokukubaliana hakuleti chuki ya kiwango cha liwalo na liwe, Tanzania bara tumekuwa tukiishi kwa mitazamo tofauti kwa muda mrefu sana na serikali haijawahi kufikia hatua ya kulazimika kutuliza ghasia ya liwalo na liwe.

Kuna maswali lazima tujiulize na tuulizane ili hili jambo lisijirudie. Huu si muda wa kusifiana ni muda wa kuulizana maswali. Jaribu kujiuliza maswali badala ya kusifia pekee. Kila jambo kwa kiasi.
 
AZAKi walihusika na kutuliza ghasia? Hoja yangu ni udhaifu uliotokea wakati wa kutuliza ghasia na uwajibikaji.
AZAKI hawakuhusika kutuliza ghasi bali kuchochea na kufadhili uharibifu zaidi na maafa zaidi kwasababu hilo ndio haswaa lilikua lengo lao.

hapakua na udhifu hata kidogo katika kudhibiti ugaidi uliopangwa kiustadi sana na kufadhiliwa na baadhi ya AZAKI na vyama vya siasa vilivyo kua na chuki na waTanzania zaidi ya million 30 waliojitokeza kutumia haki yao ya msingi ya kupiga kura, chuki ambayo inaendelea mpaka hivi leo.

Heko kwa vyombo vyetu vya ulinzi na usalama kwa ustadi na umahiri wa kimataifa katika kudhibiti na kuisambaratisha kabisa mipango ovu ya kigaidi iliyofadhiliwa na AZAKI kuiharibu nchi yetu.🐒
 
Mimi ninachofahamu hizi danadana, porojo, vitisho, uonevu, dhuluma, utekaji, mauaji, uminywaji wa haki, wizi wa kura, ukosefu mkubwa ajira kwa vijana, ufisadi uliokithiri, na umasikini wa kipato kuongezeka! basi siku zijazo kitanuka tena.
 
Back
Top Bottom