Ripoti ya Jaji Chande, Bado Haijaweza Kutibu Chuki ya October 29!, Chuki Hii Inaendelea Kulitafuna Taifa Kimya Kimya!, Tuitibu Haraka Vinginevyo...!

Ripoti ya Jaji Chande, Bado Haijaweza Kutibu Chuki ya October 29!, Chuki Hii Inaendelea Kulitafuna Taifa Kimya Kimya!, Tuitibu Haraka Vinginevyo...!

Wanabodi,

Baada ya Tume ya Uchunguzi wa Vurugu za Tarehe 29 October, 2025 kuwasilisha ripoti yake kwa rais Samia, kilichofuatia kwenye mitandao ya kijamii, ni watu wenye ugonjwa huu wa chuki, walifungulia matusi kwa kutukana, na Tume ilipokea simu zaidi ya 300 zikiwatukana matusi!. Kitendo tuu cha mtu kupiga simu na kutukana matusi,ni uthibitisho wa changamoto ya afya ya akili ya ugonjwa wa chuki.

Najua saa hizi Jeshi la polisi linaendelea na kamata kamata ya watukanaji hawa, bila kujua hawa ni wagonjwa wa afya ya akili, nashauri, kama wale waandamanaji wa October 29 walivyosamehewa kwa maana hawakujua watendalo, nashauri jeshi la Polisi, baada ya kuwashitaki ili kutoa funzo kwa wengine, Family Vibes waitwe, wakawatibu watu hao, na baada ya kupata tiba ya chuki, wasamehewe na kwenda kuieneza hiyo tiba kwa wengine, taifa liponywe na hili gonjwa la chuki iliyopitiliza.

Waandishi wamependekeza kuanzishwa kwa vipindi maalum vya kitaifa vya afya ya akili na mahusiano ya kijamii katika vyombo vya habari, na Makala elimishi kama hii kwenye magazeti na mitandao ya jamii ili kuliponya taifa letu na gonjwa hili la chuki.

Paskali
Leo tarehe 29 October, 2026 ni kumbukumbu ya mwaka mmoja wa kilichotokea October 29, 2025. Mimi naiadhimisha siku hii kwa kutafakari kwa kuyatembelea mabandiko yangu, ya post October 29, 2025.

Ila Watanzania tuendelee kupeana pole, kwa kilichotokea, mwaka mmoja ni kipindi kirefu, kuna badhi ya wenzetu wame heal kutokana na muda mrefu kupita, katika kumbukizi ya kilichotokea, tukumbuke kwa kiasi, tusije kujikuta tunapitiliza na kufumua makovu, na kutonesha tena kile kidonda na kuleta machungu upya, tujifunze kusamehe hata bila kuombwa msamaha, ili maisha yaendelee.

Mungu Ibariki Tanzania.

Mzee Pasco.
 
Back
Top Bottom