Championship
JF-Expert Member
- Aug 7, 2019
- 5,500
- 10,616
Kila halmashauri hutenga angalau 100m kwa ajili ya auditing.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hivi serikali huwa inachukua hatua kupitia Takukuru au huwa tunasomeana inakuwa imetoka hiyo?Hii ndiyo ripoti kamili ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichere kwa Mwaka wa Fedha 2020/21, imewekwa hadharani Jumanne Aprili 12, 2022.
Baadhi ya mambo yaliyoguswa:
Mashirika ya Umma kutopeleka michango Sh bilioni 129.33
Mashirika ya umma manne mwaka 2020/21 hayakupeleka michango ya kisheria ya Sh. bilioni 129.33 kwenye mifuko ya pensheni, Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu, na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi kama inavyotakiwa. Hali hii ilichangiwa na ukosefu wa fedha.
Wanaume kupewa huduma za kujifungua
Nilipopitia taarifa za fedha za NHIF, nilibaini taarifa zinaonyesha wanaume wamepewa huduma ya kujifungua kwenye vituo vya afya.
TARURA kutelekeza miradi
Miradi ya barabara yenye thamani ya Sh. bilioni 1.9 imetelekezwa na TARURA.
Manunuzi nje ya mipango ya Serikali
Mamlaka za Serikali za Mitaa 24 zimefanya ununuzi wa bidhaa za Sh. bilioni 3.4 nje ya mpango wa ununuzi wa mwaka.
Mwingiliano majukumu TANROADS na TAA
Katika kufuatilia ujenzi na ukarabati wa viwanja vya ndege, nimebaini kuna mwingiliano wa majukumu kati ya TANROADS na TAA kutokana na TANROADS kupewa mamlaka na majukumu yale yale yanayotekelezwa na TAA.
Upungufu wa walimu 16,577 (41%)
Tathmini ya uwiano wa walimu na wanafunzi katika mamlaka 48 za serikali za mitaa, ilibainisha kati ya walimu 40,458 wanaohitajika kwa shule za msingi walikuwepo walimu 23,881 tu ikimaanisha upungufu wa walimu 16,577 sawa na asilimia 41.
Serikai kulipa fedha kwa marehemu, waliofukuzwa
Mamlaka za Serikali za Mitaa 25 zimelipa fedha Sh milioni 556.8 kwa watumishi waliofariki dunia, waliostaafu na wasiostahiki. Ninapendekeza TAMISEMI izisimamie ipasavyo.
ATCL hasara imepungua kutoka Sh bilioni 60 hadi 36
CAG Charles Kichere: Mwenendo wa uendeshaji wa ATCL umeimarika. Kampuni imepunguza hasara kutoka Sh. bilioni 60 mwaka 2019/20 hadi Sh. bilioni 36 katika mwaka wa ukaguzi (2020/21).
Tsh bilioni 7 zimetumika vibaya Benki ya Maendeleo
Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichere amesema fedha za Mfuko wa Dhamana kwa Wafanyabiashara Wadogo na wa Kati Sh bilioni 7 zilizopelekwa Benki ya Maendeleo ya Kilimo hazikutumika kwa malengo ya kutoa dhamana kwa wahusika, zilitumika kwa matumizi ya kibiashara ya kibenki
#RipotiCAG2022 ya CAG imeonesha Sh milioni 917.342 za Mfuko wa Kilimo Kwanza na Sh 226,758,800 za Mfuko wa Taifa wa Pembejeo zilitumika kwa madhumuni mengine tofauti na yaliyokusudiwa
Amesema mikopo kutumika nje ya malengo ilitokana na mifumo dhaifu ya ufuatiliaji wa matumizi ya mikopo na uchambuzi wa sifa za wateja
Kuna upungufu wa Mawakili wa Serikali kwa 89%
CAG katika #CAGReport2022 amesema Ofisi ya Taifa ya Mashtaka ambayo inahusika kusimamia, kudhibiti na kushtaki kesi za jinai Nchini kuna upungufu mkubwa wa idadi ya watumishi kwa asilimia 89, hiyo inachangia ucheleweshaji wa utoaji wa haki.
Kuna watumishi 661 tu badala ya 5890 sawa na upungufu wa asilimia 89 ya mawakili wa Serikali wanaohitajika, pia watumishi waliopo licha ya kuwa hawatoshi lakini hawakupangwa kulingana na uzito wa kazi katika Mahakama mahususi.
CAG: Miradi ya bilioni 7.68 imekamilika lakini haitumiki
Tathmini ya ufanisi wa utoaji wa huduma zilizokusudiwa kwa Miradi iliyokamilika imeonesha katika Halmashauri 30, miradi yenye thamani ya Tsh. Bilioni 7.68 ilikuwa imekamilika lakini haitumiki.
Hii imehusishwa na sababu kadhaa ikiwa ni pamoja na ukosefu wa umeme, kukosekana Wataalamu wa kuendesha Mifumo mbalimbali pamoja na idadi ndogo ya Watumishi.
Kuna upungufu wa mawakili wa Serikali kwa 89%
CAG katika #RipotiCAG2022 amesema Ofisi ya Taifa ya Mashtaka ambayo inahusika kusimamia, kudhibiti na kushtaki kesi za jinai Nchini kuna upungufu mkubwa wa idadi ya watumishi kwa asilimia 89, hiyo inachangia ucheleweshaji wa utoaji wa haki.
Kuna watumishi 661 tu badala ya 5890 sawa na upungufu wa asilimia 89 ya mawakili wa Serikali wanaohitajika, pia watumishi waliopo licha ya kuwa hawatoshi lakini hawakupangwa kulingana na uzito wa kazi katika Mahakama mahususi.
CAG: Mtu mmoja apimwa damu mara 30 kwa siku
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichere amesema alipokagua taarifa za Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kwa mwaka 2020/21 alibaini kuna mtu mmoja imeonekana katika Nyaraka zake za Hospitali kuwa amefanyiwa vipimo vya damu (Full Blood Picture) mara 30 kwa siku moja.
CAG: Iliyokuwa Manispaa ya Ilala haikupeleka bilioni 10.13 benki
Katika kaguzi maalumu 37 katika Halmashauri 36 Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali alibaini kuwa jumla ya shilingi bilioni 19.72 zilikusanywa kutoka vyanzo mbalimbali lakini hazikupelekwa benki.
Kati ya fedha hizo , kiasi cha shilingi bilioni 10.13 ( asilimia 51) zinahusiana na iliyokuwa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala ambapo shilingi bilioni 4.64 hakikupelekwa benki na mawakala 20 wakati kiasi cha shilingi bilioni 5.49 hakikupelekwa benki na watumishi 19 waliokuwa wakikusanya mapato.
😁😄😃😃😀Kila halmashauri hutenga angalau 100m kwa ajili ya auditing.
Umelogwa wewe sio bureRipoti ya CAG kuanzia Mwaka 2018 kuja mpaka leo haina tija kwa Watanzania. Baada ya CAG Prof Assad kudhalilishwa na Spika Job Ndugai kisha Magufuli kumfuta kazi hakuna kinachoendelea. Kimsingi hata National Audit Office imeteremka hadhi kwa vile yale madudu wanayoibua hayachukuliwi hatua. Kusoma Ripoti ya CAG kwenye wiki ya kwanza ya kikao cha Bunge imekuwa sawa tu na kufunga mwezi wa Ramadhani kwa waislamu au kupaka majivu siku ya Jumatano ya majivu kwa wakristu.
Ili CAG report ifikie hadhi ya kipindi cha Prof Assad au Luis Uttoh miaka hiyo inabidi Bunge lichukue hatua kwanza kwa uozo wa ukaguzi uliyopita yaani 2019/20. Hapo wanapitia na kuwawajibisha mawaziri juu ya hatua zilizochukuliwa dhidi ya wabadhirifu. Kisha ndiyo waangalie mahesabu ya 2020/21.
Otherwise TUNAPOTEZEANA MUDA tu kwa kufuatilia CAG Report
Ndugu pambana tu na maisha yako. Utapasuka bure. Hii dunia si ya malaika.Hao wakaguzi wanaotumwa na CAG wanayoonesha tu maovu Kama ma 3 hivi Kati ya 100, Wana maisha mazuri kwa kupokea Rushwa wakati wa ukaguzi, madudu mengi wanaficha kwakuwa wanapewaga pesa huko wanapoenda kukagua , na pesa wanazolipwa ni hizo hizo Kodi za Wananchi. Hakuna kitu,
Hizo riport Zinazotolewa ni the best you can have, zoezi la ukaguzi ni zoezi la kupiga hela. Nyie mnapagawa na riport , je wakifanya kwa uwazi , wote mtaandamana hayo madudu
Nimemaliza.
Ripoti ya CAG kuanzia Mwaka 2018 kuja mpaka leo haina tija kwa Watanzania. Baada ya CAG Prof Assad kudhalilishwa na Spika Job Ndugai kisha Magufuli kumfuta kazi hakuna kinachoendelea. Kimsingi hata National Audit Office imeteremka hadhi kwa vile yale madudu wanayoibua hayachukuliwi hatua. Kusoma Ripoti ya CAG kwenye wiki ya kwanza ya kikao cha Bunge imekuwa sawa tu na kufunga mwezi wa Ramadhani kwa waislamu au kupaka majivu siku ya Jumatano ya majivu kwa wakristu.
Ili CAG report ifikie hadhi ya kipindi cha Prof Assad au Luis Uttoh miaka hiyo inabidi Bunge lichukue hatua kwanza kwa uozo wa ukaguzi uliyopita yaani 2019/20. Hapo wanapitia na kuwawajibisha mawaziri juu ya hatua zilizochukuliwa dhidi ya wabadhirifu. Kisha ndiyo waangalie mahesabu ya 2020/21.
Otherwise TUNAPOTEZEANA MUDA tu kwa kufuatilia CAG Report
Lena,mbowe,lissu hawawezi!!?
Ni huzuniWizi ni Mkubwa sana,pole kwa asiyekua na Kitengo.
Dangerous sanaMkaguzi anakula mlungula, yaani mbwa anakula mbwa....