Ripoti ya Richmond Bungeni (FULL TEXT) na yatokanayo

Ripoti ya Richmond Bungeni (FULL TEXT) na yatokanayo

Mwanakijiji pia kuna taarifa zaidi juu ya ripoti hiyo kuna ambayo inaonyesha mikataba iliyoingiwa na TANESCO na ipo sita hiyo ngoja ntakutumia kwenye mail yako ya jf muda huu.
 
kwanini tunajiuliza kuhusu kuachia ngazi na sio kufikishwa kwenye mikono ya sheria au kuchukuliwa hatua? have we lost our minds?
 
Baada ya kupitia thread mbalimbali ndani ya JF na kurejea makabrasha yangu LUNYUNGU nakuamini kabisa kuwa ujumbe ulioleta ni kweli; Mzee Mzima toka Mvumi ndiye asimamia mambo. Twaamini busara zitatumika kwa kuzingatia ukweli uliofukuliwa na kufunuliwa!!!

Kwa maneno yako mwenyewe means ulikurupuka kunishutumu kwa kuomba ushahidi.Kumbuka mimi huwa siokotezi hadithi za mitaani huwa naleta issues hapa .Kwa kuwa u mgeni basi nakuomba chukua muda kujifunza JF iko vipi .Na kwa kuonuesha ustaarabu basi niombe msamaha kwa kunituhumu.
 
Thanks MKJJ

Hii report in deep kuliko nilivyotegemea...Yaani Dr na Timu yake wamefanya kazi kwenye ndani ya mwezi mmoja...kwa mara ya kwanza narithika na kazi ya Mbunge yoyote wa CCM
 
MOST WANTED

View attachment 1079

WATAJWA HAPO JUU NI WATUHUMIWA WA UFUJAJI WA MABILIONI YA PESA ZA WATANZANIA KWA KUTUMIA KAMPUNI HEWA.YEYOTE MWENYE TAARIFA ZITAKAZO SAIDIA KUKAMATWA KWAO ANAOMBWA KUTOA TAAFIRA MARA MOJA KWA WATANZANIA
 
Asante Mwanakijiji, hii CD uliyotuma ina miziki mingi zaidi ya ile iliyotumwa mapema. Wacha niendelee kucheza.

Mukiweza unganisheni hii na ile ya Mnyika ili kuweka mtiririko msafi.

Leo JF imevunja record yake kwa kuwa na wasomaji wengi zaidi kuliko siku nyingine yoyote.

Hapa ndio wale wanaopiga madongo JF wanapoabika! This baby is the ultimate place to be kwenye siku kama hizi. Nafurahi pia kuwa hata server ilibeba wageni wote hao (ingawa kulikuwa na tatizo kidogo kwenye speed) lakini all was best.

Hongera Invisible na wenzako kwa kazi nzuri!
 
Thanks MKJJ

Hii report in deep kuliko nilivyotegemea...Yaani Dr na Timu yake wamefanya kazi kwenye ndani ya mwezi mmoja...kwa mara ya kwanza narithika na kazi ya Mbunge yoyote wa CCM

Yeboyebo,

Wakitaka wanaweza, ni UCCM wao ndio unawaua na kuua nchi.
 
Ogah,

Kikwete sasa ataunda tume ya kuchunguza kamati ya Mwakyembe....

Watch this space..............
God forbid this Mwafrika wa Kike! Kamati kuchunguza kamati- no way. Naelewa kwa nini wafikiri hivyo, and deep in my heart i have a similar fear too. Ila kwa hatua aliyochukua Mheshimiwa Mwakyembe na kamati yake ya kuwa wazi kiasi hiki, ninaimani kubwa kuwa zile zama za kamati kuchunguza kamati-kuchunguza kamati etc zimefika ukingoni. Nijumuike nanyi wote kumpongeza Mh. Mwakyembe na kamati yake, na bila kumsahau JK kwa kuweza mazingira ya haya yote kuwezekana. Kama ninyi nyote, am all ears waiting to see action. The RIGHT action kwa manufaa ya taifa letu. JK, usitiangushe. God Bless Tanzania.
 
Wewe subiri tu uone kitakachotokea, usanii utakaofanyika hapa hadi watu watashangaa. Kamati inaundwa sasa hivi ni majina tu ndiyo yamebakia kutajwa. Kikwete anasubiria watu wajiuzulu wakati Lowasa na wenzake wanasema hatoki mtu hapo!

tik tak tik tak............
 
Mwanakijiji tayari nimeshakutumia hiyo ripoti na soma nilichokushauri please.
 
Kwa kweli nilipoanza kusoma summary hiyo sikuamini kama DR.Mwakyembe na kamati yake angediriki kuandika kwa uwazi namna hii. Nawapa pongezi saana.
Naomba pia huu uwe mfano kwa wabunge wengine wa CCM kuwajali watanzania wanaoumia ili wao wapate posho nene na kutembelea magari ya kifahari huku watu waliowatuma wakikosa hata kandambili. Nyinyi Wabunge hamna budi kujiuliza ni nchi gani mnayoitumikia.Matumbo yenu au Tanzania. Atleast Mwakyembe na Kamati yake wameonyesha kuwa wanawajali zaidi watu waliowatuma.
 
Kinachosubiriwa sasa hivi ni utekelezaji wa haya yote... walking the talk..... Kuna kawaida ya viongozi kuja na maneno makali na matamu..... maisha bora kwa kila mtanzania na kadhalika.....

subiri uone usanii unaofuatia hapa...

tik tak tik tak tik tak...............
 
Jamani hapa kuna kitabu kikubwa sana cha ushahidi ambacho kina kurasa zaidi ya 1000 kama nikiweza kukipata kwa kesho kwenye soft copy nitawafurahisha humu kaeni mkao wa kula ili kujua jinsi wajamaa walivyokuwa wanatumia nguvu kuipitisha hii tenda.
 
Mwakyembe For Presidency 2015!

Je Mwakyembe ana beef na EL? Je hawpatani? Je ndani aya CCM kuna mgawanyiko?

Au simply watu wamechoshwa na skandali za kila siku wakaona waseme ukweli?

Je Mwakyembe ni mwadilifu nae? Rekodi yake ikoje?
 
Back
Top Bottom