ili Kuweka Huu Mjadala Katika Context Inabidi Kwanza Tukumbushane Ni Kwa Nini Hasa Watanzania Tukiwemo Sisi Hapa Jf Tulishangilia Report Ya Mwakyembe Na Kumuingiza Mwakyembe Katika Orodha Ya Mashujaa Wa Taifa Letu. Kwa Maoni Yangu Ni Kwamba Tulimshangilia Sana Mwakyembe Na Kamati Yake Kwa Kufanya Kile Ambacho Kamati Nyingi Huko Nyuma Zilishindwa Kukifanya. Kamati Nyingi Zilizoundwa Huko Nyuma Zilitumika Kuwasafisha Wakubwa Na Kufunika Ukweli Badala Ya Kuufunua. Kwa Hiyo Utaona Kwamba Tulimshangilia Mwakyembe Kwa Sababu Alithubutu Kufunua Ukweli Bila Kuwaangalia Wakubwa Usoni Kama Ilivyozoeleka Katika Siasa Za Tanzania.
Kwa Kawaida Kazi Ya Kamati Ya Uchunguzi Kama Ilivyokuwa Ile Ya Mwakyembe Ni Kutafuta, Kujua Na Kuanika Ukweli Na Ukweli Wote. Sasa Swali Linakuja, Je Kamati Ya Mwakyembe Ilitafuta, Kujua Na Kuanika Ukweli Wote Kama Tulivyoambiwa Awali? Binafsi Nilishatoa Maoni Yangu Tangu Awali Kwamba Kitendo Cha Kamati Ya Mwakyembe Kutokumhoji Mhusika Mkuu Wa Saga La Richmond Ndugu Edward Lowasa Ilikuwa Ni Mapungufu Makubwa Yaliyotia Dosari Ya Kutisha Credibility Ya Report. Mpaka Hapo Kwangu Mie Report Ya Mwakyembe Ilikuwa Shwari Na Nzuri Sana Ukiacha Hii Methodological Fault.
Sasa Hii Ya Kauli Ya Mwakyembe Ya Kwamba Wapewe Nafasi Ingine Ili Waseme Yale Ambayo Hawakusema Kuhusu Uchunguzi Wao Ni Tatizo La Pili Kwenye Report Yao Ambalo Kusema Kweli Ni Kubwa. Tatizo Lenyewe Ni Kwamba Kumbe After All Kamati Ya Ndugu Yetu Mwakyembe Haikutuambia Ukweli Wote Kama Tulivyodhani!! Again, This A Serious Flaw That Further Waters Down The Credibility Of The Report And, Unfortunately, Strongly Strengths The Arguments Of Those Alleged In The Report That The Committee Was More Intrumental Politically Than A Significant Step Towards Addressing The Problem Of Corruption And Public Resources Vandalisation In Our Country. Kwa Hiyo Kwa Maoni Yangu Tukubaliane Kwamba Kuna Makosa Ya Msingi Katika Uandaji Na Yaliyomo Katika Report Ya Mwakyembe.
Je, Makosa Haya Yanamtoa Ndugu Mwakyembe Kwenye Orodha Yetu Ya "mashujaa" Wa Taifa? Mimi Nasema Hapana. Hata Hivyo Natoa Wito Kwamba Tunapoendelea Na Mijadala Hii Ya Ufisadi Na Tunapowaunga Mkono Na Kuwatia Moyo Wenzetu Waliopo Katika Mstari Wa Mbele Wa Mapambano Tusijefika Mahala Tukawaona Kwamba Wao Hawawezi Kukosea. Kufumbia Macho Makosa Ya "mashujaa" Wetu Hakuwasaidii Wao Katika Kuongoza Vita Tuliyoianzisha. Tuwakosoe Constructively Kwa Lengo La Kuwajenga Ili Waimarike Zaidi. Sisis Pia Tujitahidi Kujua Ukweli Wote Hata Ule Ambao Pengine Hatuupendi Au Ni Mchungu Kwetu Lakini Ni Mtamu Kwa Maadui Zetu, Yaani Mafisadi. Haya Makosa Mawili Niliyoyataja Hapo Juu Ni Wazi Kwamba Ni Machungu Sana Kwetu Tunaowaunga Mkono Ndugu Zetu Wapambanaji, Lakini Pia Ni Wazi Kwamba Makosa Haya Yanatoa Mwanya Wa Kutosha Kwa Mafisadi Wa Richomond Kujitetea Na Kuisambaratisha Report Ya Mwakyembe.