Ripoti ya Richmond Bungeni (FULL TEXT) na yatokanayo

Ripoti ya Richmond Bungeni (FULL TEXT) na yatokanayo

Mimi nina swali moja:

1. Hivi Dr. Mwakyembe amesema ataomba bunge livunje kanuni/sheria ipi? Ile ya kujadili upya issue ambayo imeshajadiliwa na kumalizwa(in this case Richmond) au livunje sheria ya kulinda "heshima ya serikali"(whatever that means) ili aweze kusema mengine ambayo hakuyasema?
 
Mbona "ushujaa" wenyewe anapewa Mh. Mwakyembe peke yake? Kuna Wabunge wengine MAKINI sana kwenye KAMATI hii!
 
Ili kuweka huu mjadala katika context inabidi kwanza tukumbushane ni kwa nini hasa watanzania tukiwemo sisi hapa JF tulishangilia report ya Mwakyembe na kumuingiza Mwakyembe katika orodha ya mashujaa wa taifa letu. Kwa maoni yangu ni kwamba tulimshangilia sana Mwakyembe na kamati yake kwa kufanya kile ambacho kamati nyingi huko nyuma zilishindwa kukifanya. Kamati nyingi zilizoundwa huko nyuma zilitumika kuwasafisha wakubwa na kufunika ukweli badala ya kuufunua. Kwa hiyo utaona kwamba tulimshangilia Mwakyembe kwa sababu alithubutu kufunua ukweli bila kuwaangalia wakubwa usoni kama ilivyozoeleka katika siasa za Tanzania.

Kwa kawaida kazi ya kamati ya uchunguzi kama ilivyokuwa ile ya Mwakyembe ni kutafuta, kujua na kuanika ukweli na ukweli wote. Sasa swali linakuja, je Kamati ya Mwakyembe ilitafuta, kujua na kuanika ukweli wote kama tulivyoambiwa awali? Binafsi nilishatoa maoni yangu tangu awali kwamba kitendo cha kamati ya Mwakyembe kutokumhoji mhusika mkuu wa saga la Richmond Ndugu Edward Lowasa ilikuwa ni mapungufu makubwa yaliyotia dosari ya kutisha credibility ya report. Mpaka hapo kwangu mie report ya Mwakyembe ilikuwa shwari na nzuri sana ukiacha hii methodological fault.

Sasa hii ya kauli ya Mwakyembe ya kwamba wapewe nafasi ingine ili waseme yale ambayo hawakusema kuhusu uchunguzi wao ni tatizo la pili kwenye report yao ambalo kusema kweli ni kubwa. Tatizo lenyewe ni kwamba kumbe after all kamati ya ndugu yetu Mwakyembe haikutuambia ukweli wote kama tulivyodhani!! Again, this a serious flaw that further waters down the credibility of the report and, unfortunately, strongly strengths the arguments of those alleged in the report that the committee was more intrumental politically than a significant step towards addressing the problem of corruption and public resources vandalisation in our country. Kwa hiyo kwa maoni yangu tukubaliane kwamba kuna makosa ya msingi katika uandaji na yaliyomo katika report ya Mwakyembe.

Je, makosa haya yanamtoa ndugu Mwakyembe kwenye orodha yetu ya "mashujaa" wa taifa? Mimi nasema hapana. Hata hivyo natoa wito kwamba tunapoendelea na mijadala hii ya ufisadi na tunapowaunga mkono na kuwatia moyo wenzetu waliopo katika mstari wa mbele wa mapambano tusijefika mahala tukawaona kwamba wao hawawezi kukosea. Kufumbia macho makosa ya "mashujaa" wetu hakuwasaidii wao katika kuongoza vita tuliyoianzisha. Tuwakosoe constructively kwa lengo la kuwajenga ili waimarike zaidi. Sisis pia tujitahidi kujua ukweli wote hata ule ambao pengine hatuupendi au ni mchungu kwetu lakini ni mtamu kwa maadui zetu, yaani mafisadi. Haya makosa mawili niliyoyataja hapo juu ni wazi kwamba ni machungu sana kwetu tunaowaunga mkono ndugu zetu wapambanaji, lakini pia ni wazi kwamba makosa haya yanatoa mwanya wa kutosha kwa mafisadi wa Richomond kujitetea na kuisambaratisha report ya Mwakyembe.
 
Asante sana Kitila

sijui nikuite na wewe shujaa hapa!!!! kwi kwi kwiiii
 
For the third time nakuomba usiniite mkuu, mkuu ni wewe mzee wa dataz ili kuona unaheshimiwa kwazo.

Nashukuru sana kwa kukubali kuwa hakusema yote. On top of that your hero does not say all - your hero ni muoga. So the type of your hero is not mine, unless i miss the meaning of the word hero.

Kimasai ukamdunga simba na mkiku halafu akakimbia na usimwone tena wewe sio shujaa, shujaa ni yule anayeleta ukucha wa simba kumaanisha amemuua na akahakikisha kuwa kafa. Kwangu huyu pia ndiye shujaa, sio shujaa nusu nusu.

Kwangu huyu ni mtu (mwakyembe) anatimiza wajibu wake kazini, analipwa kwa kuwa bungeni na amelipwa kwa kukaa kama kamati. So he has to be responsible kwa chochote kile hata uficha ukweli, amemess step kwani hakutimiza wajibu wake efficiently, he did it in pieces.

In the sense of kutukana labda Rais Kikwete ndio hajatukanwa kwenye hii forum, lakini mbunge wa kyela katukanwa sana.

Thank you God! My pints worked me wonder, now I can understand why "mkuu Mama" is absolutely negative to Mwakyembe regardless of the facts! (see bold)
 
Mama you're the hero of the day! Com' on, what have you done to your country so far, hero?
 
Mama you're the hero of the day! Com' on, what have you done to your country so far, hero?

nimezaa na kuongeza idadi ya watanzania, thats all! Kuhusu uhero wa kimasai usijesema ya lowassa as am dreaming of where you are going! ukabila na nchi hii! am not into it. However, whoever calls me mkuu/hero is bogus and insane, or may be eating own shit.
 
Nimesoma makala ya mwandishi mmoja nikakutana na hili kwa kweli Mwakyembe kama ni kukosea hapa ulikosea sana. Inakuwaje anasema kuwa 'walificha baadhi ya mambo kulinda 'heshima' ya serikali?'. Naomba nieleweshwe kidogo hapa. Ni heshima gani hii serikali inayo kama siyo ujinga. Angesema wanaficha baadhi ya mambo 'kulinda usalama wa taifa' hapo angeeleweka japo kidogo.

Ni bora mheshimiwa huyu ambaye siku za karibuni amejizolea sifa kemkem kama shujaa wetu yeye na kamati yake kufafanua hii kauli tete.

Hivyo basi hatutashangaa hata pale mmoja wa 'majeruhi' mmoja wa kisiasa kudai kulikuwa na uwezo wa 'kuchomekea' baadhi ya mambo ili kuhalalisha makosa ya baadhi ya waheshimiwa waliotuhumiwa na kamati hiyo?

Mheshimiwa kwa niaba ya wakereketwa wengi tunakuomba utoe ufafanuzi wa ziada kuhusu kauli yako.

Ni kweli, umehitimisha kutokana na maoni ya mwandishi uliyemsoma na siyo kutokana na yale Dr Mwakyembe aliyosema ingawa kwa kufanya hivyo unaona ni haki yako ya kutoa mawazo. Ingekuwa vizuri kama ungemsikiliza Dr Mwakyembe wewe mwenyewe na kufanya uamuzi wako. Kwa kweli hakusema "alificha au wameficha" habari fulani. Ila alisema kuna mambo hawakuyasema kwa ajili ya kulinda hadhi ya serikali.

Ujue katika kusema kitu lazima kupima matokeo na kama wewe mwenyewe utaona kama hayo utakayoyasema yataleta madhara zaidi kuliko suluhu, ni afadhali kutosema kabisa. Lakini pamoja na hayo, Dr Mwakyembe alisema kama itahitajika, hiyo hoja ya Richmond ijadiliwe upya bungeni na wako tayari kusema yote kama watatakiwa kufanya hivyo (for public interest) na pia kama itagundulika yeye na kamati yake hawakutenda haki, wako tayari kujiuzuru. Ila kama itagundulika walichosema ni kweli basi wahusika wote waachie nyadhifa zao. Hivyo ndivyo nilivyosikia na kuelewa.

Na kutokana na haya, binafsi sioni kama Dr Mwakyembe hatufai ila naona kama ametumia busara sana katika kusema kama alivyosema. Ambao hawatufai ni wale wanaojaribu kupotosha mambo yaliyowazi na kutuchanganya!

Dr Mwakyembe (na kamati yake) hawakutunga ripoti. Walifanya mahojiano na watu mbalimbali na wana vielelezo kimaandishi na ripoti yao imetokana na hayo. Au hivyo vielelezo na mahojiano waliyofanya ndiyo siyo kweli? On face value, nadhani kuna uthibitisho wa kutosha kuwa kuna matatizo makubwa 'issue' ya Richmond.
 
nimezaa na kuongeza idadi ya watanzania, thats all! Kuhusu uhero wa kimasai usijesema ya lowassa as am dreaming of where you are going! ukabila na nchi hii! am not into it. However calls me mkuu is bogus and insane, or may be eating own shit.


Congratualtion for worsening the population burden we have!
 
nimezaa na kuongeza idadi ya watanzania, thats all! Kuhusu uhero wa kimasai usijesema ya lowassa as am dreaming of where you are going! ukabila na nchi hii! am not into it. However calls me mkuu is bogus and insane, or may be eating own shit.

I just hope haujatuongezea mafisadi nchini.
 
Congratualtion for worsening the population burden we have!

I just hope haujatuongezea mafisadi nchini.

kwi kwi kwi, i brought ufisadi-free Tanzanians, to make matter worse, ni member wazuri tu humu JF na unawapa asante zako na hata ukiona hawakusupport huondi ile asante. Nataka kukwambia kuwa ni watu unaowasupport.
 
kwi kwi kwi, i brought ufisadi-free Tanzanians, to make matter worse, ni member wazuri tu humu JF na unawapa asante zako na hata ukiona hawakusupport huondi ile asante. Nataka kukwambia kuwa ni watu unaowasupport.

Cheers for that! (bold)
Lakini, sina muda wa kuondoa my thnx kwa sababu tu mtu huyo hanisupport! What I value the most is his/her contribution and not his pay-back thnx! Hili halinisumbui kabisa, waambie nitaendelea kuwapa thnx wanapofanya mamboz!
Just curious question: umetuongezea wangapi Mama?
Keep good spirit!
 
Cheers for that! (bold)
Lakini, sina muda wa kuondoa my thnx kwa sababu tu mtu huyo hanisupport! What I value the most is his/her contribution and not his pay-back thnx! Hili halinisumbui kabisa, waambie nitaendelea kuwapa thnx wanapofanya mamboz!
Just curious question: umetuongezea wangapi Mama?
Keep good spirit!

the bolded statement remain vague, unamaanisha nini?
 
Hapana alisema atamuomba Spika ili kusudi avunje kanuni ndio aweze kusoma ripoti yote, angeyaanika iwapo Spika angevunja kanuni na sio anything else!



Huu hapa sio ukweli mkuu kabisaa!

Wakuu, naona kama tunachanganya mambo hapa. Kanuni ambayo Mwakyembe alisema atamuomba Spika aivunje ni ile inayotaka "Jambo ambalo limeishajadiliwa bungeni na kumalizika, lizizungumzwe tena labda tu Spika avunje kanuni (nadhani, sorry sina uhakika!) ya 51/54 ili mjadala huo urudishwe tena bungeni!!!!
Maana yake ni kwamba kwa vile mjadala wa Richmond uliishafungwa Bungeni na unasubiri kufanyiwa kazi na serikali, basi ili urudishwe tena Bungeni ili watu wasafishwe na pia Mheshimiwa Mwakyembe aseme kile alichokuwa ameficha kwa ajili ya heshima ya Serikali basi wabunge, akiwemo mheshimiwa Mwakyembe na majeruhi wa kashfa hiyo, wamuombe mheshimiwa Spika avunje hiyo kanuni namba deshdeshi ili mambo yaaze upya!!

Sio kwamba kanuni hii inamzuia mheshimiwa Mwakyembe kusema aliyotishia kuyasema,NOOOOO! inazuia tu kujadili suala ambalo tayari liliishajadiliwa Bungeni!! All in All, kama nimewaelewa wachangiaji wengi humu, hakuna anayehoji kazi NZURI sana aliyofanya Mheshimiwa Mwakyembe. LAKINI, hili lisituzuie kujiuliza: Ni nini alichoficha?? alitumwa na nani kukificha?? alikuwa na kigezo gani alichotumia kuamua kuwa hiki tufiche na hiki tuseme?? ni maswali ya kawaida kabisa ambayo si lazima mtu anayeyauliza awe adui wa mheshimiwa Mwakyembe na kazi yake nzuri aliyotenda.period
.
 
Mzamivu Mwakyembe hapa ameingia ktk trap ya aliowachunguza wakuu, kuna game ambayo nadhani mzamivu hakuing'amua. Kuna tatizo kwetu wanadamu hasa pale unapokuwa mbele ya hadhira iliyoduwaa au sikivu pindi unapotoa maelezo yako. Hufikia mahala wewe msemaji unatambua sasa tune na tone zimeafikiana na hatimaye taratibu hadhira inazipokea kwa utulivu wa hamasa au woga unaotokana na mrindimo wa hoja zako kwao, kuna tatizo ktk mazingira hayo, ukishafikia stage hiyo ktk uwasilishaji wa hoja zako kwa hadhira daima ari,kasi na nguvu hukuaminisha ktk mamlaka iliyo juu sana kuliko ulivyo na hapo ndipo ile hali ya uroopokaji huanzia.

Mzamivu alisukumwa na hoja + utulivu wa hadhira + mamlaka na akasahau kuwa kila analolitamka lina wajibu mbele ya hadhira husika na jamii nzima. Naamini wote waliolizungumzia jambo hili kabla ya Mwakyembe wengi wao walilenga kuichokoza kamati yake na Spika ambaye April alimzuia Rostam kuja na hoja kama hiyo bungeni, strategically Mzamivu alijenga msingi mzuri kulisaidia Bunge kusimama ktk kanuni zake lakini baada kuona sasa waheshimiwa wenzake wameridhia akasonga mbele kuipa hadhira doze ya kimamlaka hapo sasa amejikuta ametumbukia mtegoni. Ni nani aliyebakia baada EL,Kara,Msaba wa kuzitema nyadhifa zao ambazo kama Mzamivu na kamati yake wangelidiriki kuziweka wazi habari zao basi nchi yetu isingelikuwa salama???

Siku Nyerere alipokuwa anamshinikiza Mwinyi amng'oe Malecela alitamka haya" Waziri mkuu ni nani ? Ni nani ktk nchi yetu? Wananchi wana haki ya kumkataa mpishi wako hata kama wewe unaamini huyo ndiye aliye bora. Nchi itayumba kama Rais wa nchi ataingia matatani, nchi itatikisika lakini Waziri mkuu! Hata kidogo ,tunasema amuondoe ili asije akasababisha nchi kutikisika. hayo nimemwambia ndg Rais Ally"

Ndio maana watu wanjiuliza Mzamivu amekusudia nini? Na kwanini sasa? Tuendelee kujiuliza wakuu.

JF tukubali kuwa Mzamivu Mwakyembe ameteleza na sasa tuangalie hekima ya Spika dhidi ya hoja ya Karamagi.

Ninakumbuka nilikuwa wa kwanza kuhoji umakini wa Mzamivu Mwakyembe hususani kwa ile kauli ambayo Chesi Mpilipili ameaindikia makala. Acheni hoja ijichuje yenyewe na hakuna haja ya vita kwa sisi kwa sisi wakuu,tuelimashane tu.

Kazi bado ipo hapo wakuu
 
ili Kuweka Huu Mjadala Katika Context Inabidi Kwanza Tukumbushane Ni Kwa Nini Hasa Watanzania Tukiwemo Sisi Hapa Jf Tulishangilia Report Ya Mwakyembe Na Kumuingiza Mwakyembe Katika Orodha Ya Mashujaa Wa Taifa Letu. Kwa Maoni Yangu Ni Kwamba Tulimshangilia Sana Mwakyembe Na Kamati Yake Kwa Kufanya Kile Ambacho Kamati Nyingi Huko Nyuma Zilishindwa Kukifanya. Kamati Nyingi Zilizoundwa Huko Nyuma Zilitumika Kuwasafisha Wakubwa Na Kufunika Ukweli Badala Ya Kuufunua. Kwa Hiyo Utaona Kwamba Tulimshangilia Mwakyembe Kwa Sababu Alithubutu Kufunua Ukweli Bila Kuwaangalia Wakubwa Usoni Kama Ilivyozoeleka Katika Siasa Za Tanzania.

Kwa Kawaida Kazi Ya Kamati Ya Uchunguzi Kama Ilivyokuwa Ile Ya Mwakyembe Ni Kutafuta, Kujua Na Kuanika Ukweli Na Ukweli Wote. Sasa Swali Linakuja, Je Kamati Ya Mwakyembe Ilitafuta, Kujua Na Kuanika Ukweli Wote Kama Tulivyoambiwa Awali? Binafsi Nilishatoa Maoni Yangu Tangu Awali Kwamba Kitendo Cha Kamati Ya Mwakyembe Kutokumhoji Mhusika Mkuu Wa Saga La Richmond Ndugu Edward Lowasa Ilikuwa Ni Mapungufu Makubwa Yaliyotia Dosari Ya Kutisha Credibility Ya Report. Mpaka Hapo Kwangu Mie Report Ya Mwakyembe Ilikuwa Shwari Na Nzuri Sana Ukiacha Hii Methodological Fault.

Sasa Hii Ya Kauli Ya Mwakyembe Ya Kwamba Wapewe Nafasi Ingine Ili Waseme Yale Ambayo Hawakusema Kuhusu Uchunguzi Wao Ni Tatizo La Pili Kwenye Report Yao Ambalo Kusema Kweli Ni Kubwa. Tatizo Lenyewe Ni Kwamba Kumbe After All Kamati Ya Ndugu Yetu Mwakyembe Haikutuambia Ukweli Wote Kama Tulivyodhani!! Again, This A Serious Flaw That Further Waters Down The Credibility Of The Report And, Unfortunately, Strongly Strengths The Arguments Of Those Alleged In The Report That The Committee Was More Intrumental Politically Than A Significant Step Towards Addressing The Problem Of Corruption And Public Resources Vandalisation In Our Country. Kwa Hiyo Kwa Maoni Yangu Tukubaliane Kwamba Kuna Makosa Ya Msingi Katika Uandaji Na Yaliyomo Katika Report Ya Mwakyembe.

Je, Makosa Haya Yanamtoa Ndugu Mwakyembe Kwenye Orodha Yetu Ya "mashujaa" Wa Taifa? Mimi Nasema Hapana. Hata Hivyo Natoa Wito Kwamba Tunapoendelea Na Mijadala Hii Ya Ufisadi Na Tunapowaunga Mkono Na Kuwatia Moyo Wenzetu Waliopo Katika Mstari Wa Mbele Wa Mapambano Tusijefika Mahala Tukawaona Kwamba Wao Hawawezi Kukosea. Kufumbia Macho Makosa Ya "mashujaa" Wetu Hakuwasaidii Wao Katika Kuongoza Vita Tuliyoianzisha. Tuwakosoe Constructively Kwa Lengo La Kuwajenga Ili Waimarike Zaidi. Sisis Pia Tujitahidi Kujua Ukweli Wote Hata Ule Ambao Pengine Hatuupendi Au Ni Mchungu Kwetu Lakini Ni Mtamu Kwa Maadui Zetu, Yaani Mafisadi. Haya Makosa Mawili Niliyoyataja Hapo Juu Ni Wazi Kwamba Ni Machungu Sana Kwetu Tunaowaunga Mkono Ndugu Zetu Wapambanaji, Lakini Pia Ni Wazi Kwamba Makosa Haya Yanatoa Mwanya Wa Kutosha Kwa Mafisadi Wa Richomond Kujitetea Na Kuisambaratisha Report Ya Mwakyembe.

need We Say More?? Take Five, Mkumbo.....:d
 
wawili, and still expecting!


KUDOS!!
Lakini nenda ado ado kwa Mh. Mwakyembe basi, funika kombe mwanaharamu apite! Tusijewapa mafisadi nafasi ya kupumulia, we need to suffocate them now by any means!
 
Back
Top Bottom