Ripoti ya Upambanaji wa rushwa na Ufisadi kimataifa - Tanzania yang'ara

Ripoti ya Upambanaji wa rushwa na Ufisadi kimataifa - Tanzania yang'ara

Mwananchi Huru

JF-Expert Member
Joined
Nov 20, 2021
Posts
2,128
Reaction score
1,896
IMG-20220125-WA0002.jpg

=====
Taasisi inayojishughulisha na harakati za kusimamia uwazi na mapambano dhidi ya rushwa na Ufisadi duniani ya " Transparency International " tayari imetoa ripoti yake ya mwaka,

Taasisi hii iliyofanya kazi ya kuchunguza kiasi cha rushwa na Ufisadi kwenye nchi zipatazo 180 duniani kwa kutumia kipimo cha Corruption Perceptions Index ( CPI ) huku Tanzania nayo ikiwemo mwaka 2020|21.

Ripoti iliyotolewa na taasisi hiyo inayoheshimika zaidi duniani kwa kuwa na taarifa za kweli ya Transparency International inaonesha nchi ya Tanzania rushwa na Ufisadi vimepungua kwa kasi hasa kwenye Uongozi huu wa Rais Samia Suluhu Hassan,

Mtakumbuka Tanzania ilipata alama 36 kati ya alama 100 zilizotolewa na taasisi hiyo mwaka 2019|20 huku Tanzania tukishika nafasi ya 94 kati ya nchi 180 zilizochunguzwa mwaka huo,

Kwamujibu wa ripoti iliyotolewa hivi majuzi Tanzania imepanda kwa nafasi saba ( 7 ) toka ile ya 94/180 mwaka 2019|20 hadi kufikia nafasi ya 87/180 huku ikijizolea alama 39 kati ya alama 100 zilizotolewa,

Point to note,
Rushwa duniani kote inazuiwa kwa watu kuwa huru kupitia asasi mbalimbali za kiraia kuweza kupaza sauti kama ilivyo sasa,

Rushwa kamwe huwezi kuipinga kwa kutumia vitisho na tumbuatumbua kwenye hili hata Hayati Dkt John Joseph Pombe Magufuli alichemka sana,
 
Utafiti huwa unapingwa kwa utafiti. Tuleteeni ripoti yenu inayopinga ripoti hii.

Mengine yote ni uzushi na majungu.
 
Hiyo ripoti ilianza mwezi wa ngapi 2020 na ikaishia mwezi wa ngapi 2021?
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Nadhani hukumwelewa Rais kabisa,

Kweli Rais ahamasishe Rushwa?

kuwa makini kidogo mkuu,

Malawi iliwahi kuwa na Rais ambae alirithi kiti hicho baada ya kifo cha incumbent , baada ya kumaliza muhula wake Rais Banda alikumbwa na kashfa ya ufisadi wa mamilioni ya $$$ zilizoibiwa wakati wa utawala wake!!! Nadhani umeelewa na swali lako kujibiwa!!
 
Back
Top Bottom