RIWAYA; URITHI WA GAIDI
NA; BAHATI MWAMBA
SIMU; 0758573660
SEHEMU YA KUMI NA NANE
Kobelo alibaki akiwa haamini kinachomtokea.
Akagwaya!
Aligwaya sababu hakujua mtu alienyuma yake alitumia kasi ya aina gani hadi kumfikia wakati yeye alijiridhisha kabisa na usalama wa eneo lile.
"nyoosha mikono juu" Aliamriwa na sauti kavu nyuma yake!
Alinyoosha.
Mtu yule pengine hakujua hila za Kobelo kunyayua mikono juu.
Mtu yule akaanza kumpapasa Kobelo ili kumpokonya silaha yoyote aliokuwa nayo.
Kobelo alijua kabisa mtu yule mkono alioshika silaha utakuwa hauna umakini wowote wa kufanya shambulizi na pia mwili wake hautakuwa na mhimili pindi tu akiwa ameinama kuendelea na ukaguzi.
Kweli hesabu zikatiki.
Mtu yule aliinama ili akague miguuni mwa mateka wake.
Likawa kosa.
Alishangaa akipaishwa juu na kisigino safi kilichompata kwenye kidevu na kumfanya ainuke juu na kuiacha silaha yake ikisambaa chini huku yeye akiishia kushika kinywa chake kilichogongana na meno.
Kabla hajakaa sawa, alishangaa akipigwa mateke mawili kwa mpigo yaliojaa vyema kifuani kwake na kumfanya atoe mguno mithili ya malaya aliebambiwa na njemba mbili.
Mtekaji akagwaya ila akajipanga na kumsubiri Kobelo.
Kobelo nae alihitaji kumaliza mchezo mapema.
Akafanya papara bila hesabu.
Kosa!!
Kobelo alijiachia kwa mapigo safi, ila alikutana na hewa kisha akapigwa ngumi safi iliojaa pembeni kidogo ya moyo.
Alihisi anataka kutapika na kutema nyongo kwa wakati mmoja.
Akajigeuza ili amkabili adui yake ambae wakati huo alikuwa amenesa kumzunguka.
Napo akakutana na teke lilikosa uzito wa kutosha na kumyumbisha kidogo.
Mtekaji akaona ushindi u karibu.
Nae akatia mbwembwe kwa kuchezesha miguu kama mcheza dansi za asili ya mdundiko.
Kobelo alimsoma.
Mvamizi akaachia teke safi kwa kutanua msamba hewani, ila Kobelo alitanua msamba wa chini na kuachia ngumi maridadi ilioenda kuzipasua korodani za mtekaji na kumwacha mtekaji akiruka juu kama mtoto alieng'atwa na siafu kalioni huku mikono akiwa ameifumbata kumziba mkojolea uke ambae alikuwa hana mawasiliano tena na korodani zake.
Mtekaji alilia kama kabwela aliedhulumiwa kiwanja katikati ya stendi ya mabasi.
Kobelo hakutaka kuchelewesha akamdaka shingo mithili ya Simba na windo lake kisha akatumia nguvu kidogo kuivunja na kumwacha mtekaji akijibwaga chini kama teja aliekosa unga.
Hakuwa na uhai.
Kobelo alitumia vidole vya miguu yake kutembea kuelekea kwenye nyumba ile ambayo ilikuwa kimya.
Uani aliona gari alilokuwa analifuatilia tangu posta.
Akasukuma mlango na kuingia ndani kwa tahadhari kubwa.
Ila aligundua mle ndani hakukuwa na mtu.
Aliamua kukagua hapa na pale ili kuona lolote linaloweza kumsaidia, aliambualia patupu.
Alikata tamaa na ile nyumba ambayo aligundua ilikuwa na mlango wa dharura na ambao alihisi ulitumika kumtoa bwana kitambi ndani ya ile nyumba.
Akapiga hatua ili atoke.
Simu ikaita!!
Ilikuwa ni simu ya mezani.
Akaifuata na kupokea!
"Ukimalizana nae njoo Temba hotel kuna maagizo yako" Iliongea sauti ya upande wa pili kisha kukatwa simu.
Ndio ni Temba hotel; chumba gani sasa.
Alijiuliza bila kupata majibu.
Akatoka na kumwendea mtakaji wake ambae wakati huo alikuwa mbali na dunia hii.
Alimkagua na kuchukua simu yake ndogo mana kubwa ilikuwa na pini na asingeweza kuifungua.
Akakagua jumbe fupi zilizoingia na hazikufutwa.
Bahati ilikuwa kwake!
Alikutana na ujumbe uliomtaka afike Temba hotel chumba namba tisa na aliposoma tarehe ya ujumbe ule ilikuwa ni siku tano nyuma.
Akaijaribu bahati yake.
Akaelekea huko Temba Hotel.
***
Kabla ya saa tano na nusu usiku; Sajenti Kobelo alikuwa anaegesha gari karibu na Temba hotel. Alishuka na kumlipa mmlinzi ili amwangalizie usalama wa gari lake.
Alipiga hatua za uhakika na kuelekea mapokezi kama wageni wengine.
Alipofika mapokezi alikadibishwa kwa tabasamu mwanana na mwanamke wa makamo aliekuwa mapokezi pale.
"Nahitaji kuelekea chumba namba 9" alisema Kobelo.
Yule dada alistuka kiasi ambacho kilimpa mashaka Kobelo.
"una wenyeji na hicho chumba au umekosea kutaja?" Aliuliza mhudumu.
Kobelo alitabasamu.
"Kuna jamaa angu amehitaji tuonane hapo" Alisema Kobelo.
.
Mhudumu aliguna.
"Kwani hicho chumba kina kitu gani labda" Kobelo alidadisi.
Mhudumu alijichekesha na kujibu...
" Hamna kitu, ila hakina wapangaji zaidi ya mwaka mzima sasa na ndio mana nimeshangaa unapokiulizia"
Eeh!!
Kobelo alibaki akiwa anamtazama yule mhudumu ambae alikuwa anaendelea na shuguli zake baada ya wageni wengine kuwasili kwenye kaunta aliopo.
Kobelo alisubiri hadi wakati ambao mhudumu yule alipoinama kuchukua funguo ndipo na yeye alipochepuka haraka na kuishia kwenye korido iliokuwa na ngazi kuelekea vyumba vya juu.
Alipanda ngazi kwa haraka kidogo na alifika kwenye varanda iliotenganisha vyumba upande wake wa kushoto na kulia.
Alipishana na watu wawili watatu ambao walikuwa wanatokea vyumbani mwao.
Alitupia macho kwenye namba za vyumba bila kuona hicho chumba.
Hadi anamaliza varanda ile,hakuwa ameona chumba hicho.
Mwisho wa varanda ile kulikuwa kuna korido pweke na alipoifuata alikutana na kibao kilichokuwa kimeandikwa maelekezo ya kuonesha ili ufike vyumba vya juu panda ngazi na pia ukiendelea kuifuata korido ile unaelekea kwenye vyumba vya ofisi za meneja wa hotel.
Hata yeye hakujua kwa nini aliamua kutokupanda juu na kujikuta akielekea kule kuliko na ofisi za utawala.
Maajabu!!
Kabla hajafikia ofisi ya utawala alikutana na chumba kilichokuwa kimeandikwa namba 9.
Akatazama kushoto na kulia na kuona hakuna aliekuwa anamuona.
Akajaribu kusukuma.
Kikafunguka.
Akajitosa ndani kwa umakini wa hali ya juu.
Ajabu nyingine!!
Chumba kile kilikuwa kidogo tofauti na matarajio yake na mbele yake kulikuwa kuna mlango uliokuwa na kibao kilichosomeka
"Only members"
Aliguna!!
Mwili ukamsisimka na hamu ya kuelekea huko ikamvaa.
Akausukuma mlango ule.
Akajikuta anazama kwenye korido tulivu iliokuwa inataa za rangi rangi na chini kulikuwa kuna zulia la bei mbaya.
Akaifuata korido ile na kitambo kifupi alikuta mlango mwingine kushoto mwa korido na kuufungua.
E bana ee!!
Alikutana na Dunia nyingine kule na hakuwa amedhania kama katika hotel ile kuna Club kubwa namna ile na watu wanafanya anasa mbele za watu bila kujali.
Alipoingia hakuna mtu ambae alionekana kumjali na alichogundua kwa haraka ni kuwa watu waliokuwa mle ndani wengi walikuwa ni wenye asili ya uarabuni.
Na ngozi nyeusi walikuwa ni wadada ambao wengi walikuwa watupu wakichezea nyeti zao na kushangiliwa na waarabu wale.
Kila mtu alionekana kujali zaidi raha zake kuliko kitu kingine.
Kwa hesabu za haraka haraka Kobelo alihisi waarabu wale hawakuwa pungufu ama zaidi ya thelathini.
Nae akatafuta meza moja na kukaa!
Macho yake yalitembea kila kona ya ukumbi ule na hatimae aliona kile alichokuwa anahisi na kukitafuta.
Alimuona kitambi.
Na aliona kitambi akiongea na njemba moja huku wakimtupia jicho la wizi.
Hatimae wote walinyanyuka na kuelekea upande mwingine wa ukumbi ule na kuingia kwenye mlango uliokuwa umeandikwa "Toilet"
Kobelo nae alifuata!.
Tofauti na alivyodhani kuwa kule ni sehemu ya vyoo; alikutana na korido ambapo alijua ni ya kutokea ndani ya ukumbi ule.
Alipofuata zaidi alikuta inamfikisha kwenye vyumba vya juu kabisa.
Akazidi kuwa makini, mara mbele yake alikutana na njemba iliokuwa inapiga soga na Kitambi..
"Anga hizi zina wenyewe na hupaswai kukatiza" Alifoka yule jamaa na bila kusubiri jibu la Kobelo; akamvamia..
Wakapiga mweleka chini na kila mmoja alipiga ukelele wa uwezo wake.
Bila kupoteza muda walisimama wote kwa pamoja kwa kuruka sarakasi safi.
Wakategana!.
Mchezo wa kuviziana ukafika ukomo.
Kobelo akazuga kutisha.
Njemba ikatishika!!.
Kobelo akaenda juu na kukanyaga ukuta kisha akarudi kwa kasi na kuachia ngumi nzito iliotua sawia kwenye taya ya njemba na kumwacha akilia kama mwanamke alieshikwa makalio bahati mbaya.
Kobelo hakutaka kumpa nafasi.
Akaruka tena na kumpiga double kick zilizomsambaratisha chini jamaa yule aliekuwa na mwili mkubwa nguvu kisoda.
Jamaa akataka kuamka akajikuta akijaa kwenye kabali matata ya Kobelo.
"Sema nyie ni kina nani" Aliuliza Kobelo.
Ikawa kimya!
Na alisikia mpinzani wake akianza kulegea.
Akamwachia!!
Njemba ikaenda chini bila pingamizi.
Akawahi kuitazama na alipigwa na butwaa.
Njemba ilijing'ata ulimi.
"Duh hawa jamaa ni hatari" Alisema Kobelo na aliposimama alikuta hayuko peke yake kwenye korido.
Watu wengi walijaa huku wengine wakiwa na vyupi tu na walikuwa wanatazama sinema ile kutokea kwenye milango ya vyumba vyao.
Mara yakaanza makelele baada ya kuhisi Kobelo ameua mpinzani wake.
Kobelo hakutaka makuu akatokomea.
***
Kobelo alifika chini yalipo mapokezi, lengo lake ni kutaka kuzungumza na mhudumu yule aliempokea, alihisi kuna mengi anayajua.
Alipotokeza tu, alikutana na umati wa watu wakishangaa kule mapokezi huku wengine wakipiga picha na wengine wenye roho nyepesi walikuwa wanalia.
Nae akaenda kutazama!
Shiit nimewahiwa tena!
Alijisemea peke yake baada ya kuona mwanamke yule mzuri akiwa amelala sakafuni na tundu kubwa kichwani.
Alipigwa risasi.
Kobelo alitoka huku roho yake ikimuuma sana na pasi na shaka alijua yeye ndie chanzo cha kuuliwa mwanamke yule.
Akapanda gari yake huku akiwa hana hata nusu ya lolote aliloangua kwenye mkasa ule.
Usiku nao ulikuwa unaelekea kuukaribisha mwanga wa ahsubuhi.
Na alihitaji kupata lepe la usingizi huku ahsubuh akiwa na lengo moja tu.
Kitu ambacho hakujua ni kuwa lengo lake lilizidi kuzua balaa na utata mkubwa.