RIWAYA; URITHI WA GAIDI
NA; BAHATI MWAMBA
SIMU; 0758573660
SEHEMU YA ISHIRINI NA MOJA
***
Akiwa njiani; Sajenti Kobelo aliamua kupita kwenye vibanda vya kutengeneza simu, na alipofika aliomba wamtolee mfumo wa kudai neno la siri kwenye kioo kabla hujaendelea kufanya mengine kwenye simu.
Alilipa na kuahidiwa dakika chache kila kitu kitakuwa sawa.
Haikupita hata dakika ishirini, tayari fundi alimkabidhi simu janja aliopora mfukoni mwa marehemu J Malao.
Akaondoka huku akiwa na lengo la kuelekea kituoni kwake kuripoti mchana ule kama zamu yake ilivyohitaji kwa siku hiyo.
Njiani mawazo lukuki yalikuwa yanampitia hasa alipokumbuka kauli ya baunsa kwenda kwa Kenge.
Aliirejea "Fanya yanayokuhusu"
Aliguna!
Inamaana Kenge kuna kitu anajua kuhusu sakata hili sasa vije tena aonekane kushupalia suala hili, na kama baunsa aliamua kumuonya tu ili ujumbe umfikie kwa nini sasa alitaka kumlipua?
Yalikuwa ni maswali bila majibu na kulikuwa hakuna wa kumjibu zaidi ya yeye mwenyewe kulitafuta jibu.
Kenge kuna kitu anajua bwana" Kobelo alijisemea peke yake.
Kobelo aliingia kwenye maegesho ya utawala na kupaki gari lake kisha akashuka na kuelekea kituoni.
"Sajenti; kuna ujumbe wako hapa" Aliseme WP Mengi ambae alikuwa anatoa huduma mapokezi.
Kobelo alisogea karibu yake.
"Unahitajika kwa OCD tafadhali" Alisema WP Mengi.
"Nashukuru" Alisema Kobelo na kupiga hatua kuelekea mlango wa ofisi za mkuu wa kituo kile kidogo.
Alisukuma mlango na kuingia ndani baada ya kuruhusiwa kuingia.
Ndani alikuatana na Mzee wa makamo ambae umri wake ulikuwa bado unaruhusu kuendelea kufanya kazi kwa miaka kadhaa badae.
"Sajenti; unaweza kunambia ni kitu gani kimekuweka bize siku mbili hizi" alisema OCD huku akiwa amefumbata mikono pamoja na kuegemea juu ya meza iliokuwa karibu yake.
"Afande nipo tu nashuguli zangu za kila siku hasa baada ya kutoka kazini" Kobelo alijibu.
.
Mzee alitabasamu.
"Umri unanienda ila bado sijafikia kudanganywa namna hiyo bwana mdogo" OCD alisema huku macho yake yakiwa usoni mwa Kobelo.
Kobelo alitizama pembeni kwa aibu ya kugundulika.
"Umefikia wapi na kesi unayofuatilia?" OCD alihoji.
Kobelo alishituka licha ya kutoonesha mshituko wake hadharani.
"Najua umejipa kesi ambayo hutakiwi kuifuatilia na ipo mikononi mwa askari mwingine, huko ni kukosa nidhamu na pia ni viashiria vya rushwa kwa sababu hadi sasa umesababisha mauaji ya mhariri J Malao" Alieleza mzee.
Ohoo!!
Ilikuwa ni ngumu kumeza; Kobelo alitumbua macho mithili ya jogoo aliekosa kitoweo. Amesababisha vipi mauaji wakati hajui hata namna alivyokufa huyo mtu na ni nani mhusika kati ya Kenge na yule baunsa.
Ebenaee!
Kobelo aligwaya kwa muda na alijua msala umemwangukia jumla jumla.
"Ni kweli ila sijahusika na mauaji yake afande" Alijitetea Kobelo.
"Hata kama hujahusika na vipi unahusika katika kesi isiokuhusu? Au hujui huko ni kuharibu upelelezi? Na kwanini waenda kinyume na maadili ya kazi yako?" OCD aling'aka.
Kobelo alipiga kimya.
OCD alibinua droo na kutoa bahasha na kumkabidhi Kobelo.
"Unasimamishwa kazi kwa muda usiojulikana hadi uchunguzi juu yako utakapokamilika na wakati wote huu usijaribu kufanya jambo lolote la kijinga, hatutakuwa na huruma na wewe tena zaidi tutakusekweka ndani" Aliunguruma Mzee huku akiwa amemtolea jicho Kobelo.
Kobelo alinywea gafla na kushindwa kuamini, hakupata kauli japo ya kujitetea na hatimae alibeba barua ile na kusaluti kisha akatoka nje akiwa mnyonge kupitiliza.
Kobelo alitupwa nje ya kazi kwa muda usiojulikana.
***
Upande mwingine alikuwepo Kenge akiwa amefungwa bandeji karibu uso mzima na kubakiza sehemu ndogo tu ya uso wake.
Licha ya kupachikwa bandeji hizo ila bado alionekana uso umemvimba na pia majeraha mengine yalikuwa yamejitokeza kwenye mikono yake..
Vioo vya kabati vilimuumiza sana ila uso uliumizwa na kofi alilopigwa na baunsa.
Licha ya kuwa na bandeji usoni bado miwani yake haikumtoka usoni ila wakati huu aliivaa juu ya bandeji na kufunika macho kwa juu juu tu.
Alikuwa ameshika kalamu na karatasi, ambazo alikuwa anazisoma kwa kuzinyayua juu mana kutazama mezani asingeweza kwa kuwa bandeji ilifungwa kuanzia shingoni.
Alizungusha shingo yake na kumtazama afande mwenye cheo cha koplo aliekuwa amesimama peke kando yake ndani ya ofisi ile.
"Nenda uniletee yule mwanamke" Aliagiza kibabe.
Koplo alitoka kutekeleza amri na dakika chache badae alirudi akiwa ameongozana na Remi ambae kimuonekano alionekana kudhoofu sana.
Kenge alipomuona alinyanyuka kwa hasira ila alirudi gafla kwenye kiti huku akigugumia kwa maumivu, alijisahau ya kuwa mbavu zake na mguu mmoja navyo vilikuwa vimefungwa kwa bandeji kuzungushia pande zote baada ya kuonekana mbavu zilipata athari kidogo wakati wa makabiliano.
Ingelikuwa ni mtu mwingine basi wakati ule angekuwa nyumbani ama hospitali kama alivyoshauriwa na matabibu, ila sio Kenge ambae bado alisisitiziwa kupewa pesa endapo angefanikiwa kumsainisha karatasi zenye maelezo ya kukiri kuua na kuhusika kwa sakata lile msichana Remi.
Angelala vipi wakati ameahidiwa donge nono!
Hata!!
Lazima Remi asaini.
Kwa hasira alimsukumia karatasi na kumuamuru asaini.
Remi akazichukua na kuzisoma kisha akacheka.
"Hata kama ningekuwa nimeua kweli, bado nisingekubali kusaini maelezo ya mtu mwingine; Polisi ni sehemu ya kupata haki vije tena ionekane mwataka kukandamiza haki ya mtu asiehusika."
Remi akanyamaza kidogo na kuendelea.
"Sikia nikwambie wewe askari mabandeji, nifungeni mtakavyo ila sisaini, nipigeni muwezavyo ila sisaini." Akanyamaza tena na kumtazama Kenge.
"Afu aliekufanya hivyo, angeongeza kidogo hakika hata nguo ningemvulia, mbona kakupiga kidogo afande" Alimalizia kwa tabasamu.
Kenge huwa hapendi dharau, ila afanye nini sasa wakati anamaumivu kila sehemu, kuinuka tu ni tabu vipi kurusha mkono.
Kenge alijikuta akivimba tu bila kumfanya lolote mtuhumiwa wake.
"Afu ulisema unaitwa Kenge; wewe kweli ni askari Kenge; yani unashindwa kutafuta ukweli unakuja na maelezo feki na kwanini nipo humu muda wote bila kupewa karatasi niandike mwenyewe? Askari Kenge" Remi aliongea kwa uchungu na maneno yake yakazidi kumuumiza Inspekta Kenge..
Kenge chozi likamtoka.
Kwanini?.
Kwa sababu alilia hana uwezo wa kumwadabisha Remi na alishaonywa na wakubwa zake kuhusu kuruhusu mtu mwingine kumwadhibu mtuhumiwa aliemikononi mwake hadi viongozi wajiridhishe na uhitaji huo, lakini pia alilia kuona Remi katia ngumu kusaini ili yeye apate pesa na kukabidhi kesi mahakamani.
Ilitia uchungu hakika.
"Wewe mwanamke nikipona utalipa maneno yako yote ya leo fisi wewe" Alijitutumua Kenge..
"Ukiona askari anaependa kutukana watuhumiwa, basi huyo kichwa chake kinawalakini. Mimi ni mtuhumiwa tu wala sio muuaji na nipo kwenye mikono salama hivi sasa, sasa kwanini mnataka nionekane nipo jehanamu" Remi alisema kwa uchungu.
"Najua uonaongea hayo kwa kuwa waniona nipo hivi afu..." Kenge hakumalizia kauli yake, akaingia mtu mwingine ndani ya ofisi zile.
Kenge alishituka kuona mtu mwenye cheo kikubwa na anaefanya kazi makao makuu akiingia mle ofisini kwake.
Kenge akapaparika kutoka saluti ila kajikuta hawezi na kuishia kupiga mweleka huku akitoa mguno wa maumivu.
Ofisa alieingia akatabasamu kwa tukio lile kisha kwa madaha alikaa kwenye kiti alichokuwa amekalia Kenge.
"Inspekta Kibe nadhani unahitaji kupumzika lau siku mbili hivi, nitaongea na mkubwa wako akuache upumzike na hongera kwa kuipenda kazi yako" Ofisa alisema.
Kenge akajichekesha huku akifanya juhudi za kusimama na kisha kutoka mle ndani baada ya kupewa ishara atoke.
Alikuwa ni Naibu Kamishina P. Kagoshima.
"Najua hupendi kuwa humu Remi; ila hakuna namna ni lazima uwepo humu kwa usalama wako" Alisema Kagoshima.
Remi hakumjibu.
"Nimekuja hapa kukusalimia na pia kuweka mambo fulani sawa" Kagoshima alisema tena.
Remi kimywa.
"Uwezo wa kujisaidia unao, ila hutaki tu Remi"
"Vipi unataka nijisaidie kwa kukiri kuuwa? Au najisaidia vipi sasa ikiwa nipo selo?" Remi alisema..
Kagoshima alitabasamu.
"Remi sio kukiri, ila ombi langu tu linaweza kukutoa humu" Kagoshima alisema.
"Lionee haya vazi tukufu ulilovaa, mbona walidhalilisha namna hiyo? Unawezaje Ofisa mkubwa kutega kwa kutumia matatizo yangu?" Alijitutumua Remi.
Kagoshima alikunja uso.
"U jeuri sana, ila jeuri yako si lolote, kumbuka upo mikononi mwa dola na unatuhumiwa kuua, mumeo anatuhumiwa ugaidi, vipi kuhusu mwanao Pius?" Kagoshima alitupa karata makini sana.
Remi alistuka kukumbushwa mwanae ambae alikuwa shule wakati huo na hajui maendeleo yake. Ni vipi kama ataendelea kushikiliwa na mwanae afunge shule nani atampokea ama nani atampa pesa aende kwa ndugu zake Zanzibar alikozaliwa baba yake?
Ebana eeh!!
Ubaridi ulimtambaa mwili mzima. Alimtizama Kagoshima kwa huruma na Kagoshima akainua mabega juu bila kusema neno.
Ilimaanisha maamuzi yapo kwa Remi mwenyewe,abaki selo mwanae ahangaike ama akubali kuwa mpango wa kando kwa Kagoshima ili ajue namna ya kumweka sawa mwanae.
Utata!!..
NB; KUNA WATU HAWAPENDI ALOSTO, HIVYO BASI ILI UWATANGULIE WENGINE, UNAPASWA KUNUNUA KWA TSH 2000/=
UNATUMIWA KWA NJIA YA WHATSAPP NA EMAIL.
NAMBA ZA MALIPO NI 0758573660 NA 0658564341 NA 0624155629.
Namba zote jina ni Bahati Mwamba.