Riwaya: I died to save my President

Riwaya: I died to save my President

I DIED TO SAVE MY PRESDENT

Sehemu 19

Nitakwenda nyumbani kwa
Pascal na kuitafuta hiyo pochi
mahala alipoificha Eliza na
nikiipata nitajua kilichomo ndani
yake”
“ Elvis !!...pauline akastuka
“ Please don’t do that.Leave
this matter as it is,Huyu Pascal
huwezi kujua ni kwa nini alitaka
kumuua Elizabeth kwa sababu tu
ya pochi.Naomba usijihusishe na
suala hili hata kidogo.Huyu
msichana tutamrejesha kwao
Iringa.” Akasema Patricia kwa
uoga
“ Usihofu kitu Patricia,nataka
tu kufahamu kilichomo ndani ya
hiyo pochi na baada ya hapo
sintakuwa na tatizo tena na Pascal
” akasema Elvis
“ Sawa Elvis lakini mimi moyo
wangu hauafiki kabisa suala hili lakinikwa kuwa umenihakikishia
kwamba hakutakuwa na tatizo
lolote basi nakuruhusu ufanye
hivyo unavyotaka k ufanya”
“ Ahsante kwa kukubaliana
nami.Lengo langu ni kutaka tu
kufahamu kwa nini Pascal alitaka
kumuua Elizabeth kwa sababu tu
ya pochi? Kuna kitu gani
kikubwa ndani ya hioyo pochi?
“ Utafanya nini ukigundua
kwambandaoi ya hiyo pochi kuna
jambo kubwa? Akauliza Patricia
“ Naomba nisikujibu kwa sasa
mke wangu hadi hapo
nitakapokuwa nimeipata hiyo
pochi na kujua kilichomo ndani
yake.” Kazi zetu sisi huwa
zimetawaliwa na usiri
mkubwa.Tunatembea na siri
nyingi za taifa kwa hiyoyawezekana katika pochi hiyo
kuna siri kubwa”
“ Umepanga kwenda lini
huko kwa Pascal?
“ Tonight.Ninapafahamu
nyumbani kwake,nimewahi
kwenda sikumoja na mkurugenzi
wangu wa zamani.Ninachohitaji ni
huyu msichana anielekeze mahala
alikoificha hiyo pochi ili
nikaichukue” akasema Elvis
*******************
Saa mbili na nusu za usiku
,Elvis akasimamisha gari nje ya
Akwinabe Bar halafu akashuka na
kuingia ndani ya baa ile maarufu
hasa kutokana na idadi kubwa ya
wasichana wanaouza miili
yao.Alikwenda kaunta akanunua
chupa kubwa ya maji ya kunywa halafu akatoka.Watu walikuwa
wengi kama kawaida ya mahala
hapa.
Akiwa na chupa yake ya maji
mkononi Elvis akaangaza angaza
pande zote kama kuna mtu
anayemfuatilia halafu akaanza
kupiga hatua akaondoka na
kuishika barabara iliyokuwa
ikielekea ilipo nyumba ya
Pascal.Ni nyumba ya nne toka
Akwinabe bar. Kwa mujibu wa
maelekezo aliyopewa na Elizabeth
ni kwamba njia rahisi ya kuingia
ndani ni kwa kupitia mlango
mdogo ulio nyuma ya nyumba
ambao hufungwa saa tano za
usiku.Saa nne usiku mbwa
hufunguliwa na kutolewa n je
kujisadia na saa tano za usiku
huingizwa tena ndani na mlango
huo hufungwa Elvis akapita katika
uchochoro mdogo uliolitenganisha
jumba la Pascal na nyumba ya
jirani akazunguka hadi nyuma ya
nyumba hakukuwa na mtu yeyote
kule nyuma,akatoa glovu nyeusi
akavaa halafu akachukua na kitu
mfano wa soksi kubwa akaivaa
kichwa na kubakisha eneo la
macho tu kisha akaambaa ambaa
na ukuta hadi katika mlango ule
mdogo akajaribu kuusukuma
ukafunguka.Taratibu na kwa
tahadhari ya aiana yake akaingia
ndani bastora yake ilikuwa
mkononi tayari kukabiliana na
chochote ambacho
kingejitokeza.Hakukuwa na mtu
yeyote kule nyuma ya nyumba.Taa
za ndani zilikuwa zinawaka
kuashiria kwamba kuna watu
walikuwemo ndani Moja kwa moja akaelekea
katika mti alioelekezwa na
Elizabeth ambako ndiko alikoificha
ile pochi ya Pascal.Mwangaza
haukuwa mkali sana eneo hilo
kutokana na matawi ya miti na
hakuweza kuonekana kiurahisi
kutokana na mavazi meusi
aliyoyavaa.Akavua begi alilokuwa
amevaa mgongoni akatoa kitu
Fulani kigumu chenye ncha kali
na kuanza kuchimba.Wakati
akiendelea na zoezi lile la kufukua
,ghafla mlango ule mdogo
ukafunguliwa na kijana mmoja
akaingia na bila kuhisi kitu
chochote akaelekea moja kwa
moja ndani.Elvis aliyekuwa
amejibanza pembeni ya mti
akaendelea na zoezi lake la
kuchimba .Baada ya muda
akakutana na kitu kama mfuko wa nailoni na ndaniyake kulikuwa
na pochi.Kwa haraka haraka
akaiweka pochi ile katika begi
lake halafu akaishika bastora
yake akatazama usalama wa
eneo lile kisha akaondoka kwa
tahadhari kubwa.Akaufungua
mlango mdogo lakini kabla
hajatoka mlango wa kuingilia
ndani ukafunguliwa na kwa
haraka akajirusha nje.Mara
akasikia msichana akipiga kelele
akiwaita watu waliokuwemo ndani
akawafahamisha kwamba ameona
mtu akitpoka pale mlangoni .Elvis
akavua ile kofia aliyokuwa
ameivaa kichwani halafu akatoka
mbio hadi barabarani na kuelekea
moja kwa moja katika baa mahala
alikoacha gari lake akaingia garini
na kuondoka kwa kasi ******************
Saa tano na dakika tatu za usiku
Elvis akawasili nyumbani
kwake.Patricia mke wake ndiye
aliyemfungulia geti.
“ Thank you lord you are
back” akasema Patricia na
kumkumbatia mumewe.Elvis
akambusu mkewe na kumshika
mkono wakaingia sebuleni.
“ Nilikuwa na wasi wasi sana
na ndiyo maana nimeshindwa
hata kupata usingizi”akasema
Patricia
“ Samahani kwa kukuweka
roho juu mpenzi wangu lakini
hakukuwa na sababu yoyote ya
kuwa na wasi wasi.Ilikuwa ni kazi
ndogo sana”
“ Usiseme hivyo Elvis.Ilikuwa
kazi ndogo kwako lakini ya hatari kubwa kwangu.Kazi yako naiogopa
sana.Kila siku namuomba Mungu
watume malaika zake
wakutangulie kokote
uendako.Sitaki upatwe na tatizo
lolote .I love you so much Elvis,you
are my everything.” Akasema
Patrician na kukilaza kichwa
chake katika kifua cha
mumewe.Elvis akainama
akambusu na kusema
“ I love you too Patricia.I love
you so much ” wakakumbatiana
.Baada ya muda kidogo Patricia
akauliza
“ Umeipata pochi hiyo
uliyokwenda kuitafuta?
“ Ndiyo nimeipata” akasema
Elvis halafu akainuka na
kulifungua begi lake akatoa pochi
ndogo akaifungua.Ndani ya pochi ile kulikuwa na kila kitu
alichokisema Elizabeth
“Kila kitu ni kama
alichokisema Elizabeth. Hizi fedha
sina haja nazo,tutampatia
Elizabeth zitamsaidia katika
matatizo yake.Vitu ambavyo
vilipelekea Pascal afikie maamuzi
ya kumuua Elizabeth ni hivi viwili
tu .Hii flash disc na h ii memory
card.” Akasema Elvis
“ Kuna nini ndani yake
mpaka afikie hatua ya kutaka
kuutoa uhai wa mtu kwa ajili ya
vitu hivi?” akauliza Patricia
“ I don’t know yet.I’ll find out”
akasema Elvis
“ Elizabeth anaendeleaje?
“ Anaendelea
vizuri.Ninaendelea kumpa
dawa.Hali yake inazidi kuboreka” Good.Hali yake ikisha
boreka itabidi tumsafirishe
kumrejesha kwao Iringa akaanze
maisha mapya.Hapa mjini
hatakiwi kuonekana kabisa.Ni
hatari kubwa kwake”
“ Hilo ni wazo la msingi
sana.Tutampatia mtaji wa
biashara akaanze maisha yake
huko kijijini.Hatupaswi kuendelea
kumuweka hapa kwa muda
mrefu” Elvis akamshika mkono
mkewe wakaelekea
chumbani.Elvis akamtazama
mkewe kwa makini bila
kumsemesha.
“ Vipi mbona unanitazama
hivyo Elvis?akauliza Patricia.Elvis
akamsogelea akambusu na
kusema
“ You are blessed my love.You
are so beautifull than all women in this world.I want to remind you
again of how much I love you and
how important you are in my life”
akasema Elvis
Patricia akamkumbatia kwa
nguvu kisha wakaanza kupeana
mabusu mazito na haukupita
muda wakahamia katika
ulimwengu wa huba
*************************
Saa sita za usiku Pascal
alirejea nyumbani kwake kama
kawaida yake.Mida hii ndiyo huwa
anarejea nyumbani kila siku.
Arejeapo nyumbani usiku huu
familia yote huwa imelala na hivyo
hufungua geti kwa kutumia
remote control.Aliingiza gari katika
gereji halafu akaingia sebuleni na
kushangaa kuwakuta Salvatory mdogo wake pamoja na mtumisi
wa ndani wakiwa sebuleni jambo
ambalo halikuwa la kawaida.
“Bado hamjalala mpaka mida
hii? Akauliza Pascal
“ Kaka tumeogopa kulala
kuna shida kidogo imetokea”
“ Shida gani imetokea?
“ Prisca anasema kwamba
alimuona mtu akiwa na mavazi
meusi akitoka ndani kwa kupitia
mlango wa nyuma”
“ Mtu ? !!..Pascal akashangaa
“ Ndiyo kaka” akajibu Prisca
mtumishi wa ndani
“ Ulimuona mtu huyo
alikuaje?
“ sikumuona usoni.Nilimuona
kwa nyuma wakati
akitoka.Alikuwa amevaa mavazi
meusi pamoja na begi mgongoni” Mmejaribu kuangalia kama
kuna sehemu yoyote kumevunjwa
au kuna kitu chochote kimeibiwa?
“ Tumeangalia lakini hakuna
sehemu yoyote iliyovunjwa au kitu
chochote kilichoibiwa.” Akasema
Salvatory.Pascal akafikiri kidogo
na kusema
“ Ok msiogope. Yawezekana
wakawa ni vibaka waliokuta
mlango uko wazi wakaingia ili
kutafuta cha kuiba
wakakosa.Msiache mlango wazi
tena ,muwe mkiufunga muda
wote” akasema Pasca na
kuzunguka nyumba yote
kuchunguza na kuhakikisha
hakuna sehemu iliyovunjwa
halafu akaingia katika chumba
chake ambacho hukitumia
kuhifadhia vitu vyake vya siri lazima atakuwa ni kibaka
aliyekuwa akitafuta nafasi ya
kuiba.Sina hakika kama ni mtu
aliyekuwa na nia yoyote mbaya na
mimi.Kama angekuwa ni mtu
mwenye kutafuta chochote toka
kwangu basi angeingia ndani.Hata
hivyo kuna ulazima wa kufunga
kamera za ulinzi hapa
nyumbani.Toka yule msichana
alipoipoteza ile pochi yangu yenye
vitu vyangu vya muhimu nimekosa
amani kabisa.Nashukuru niliwahi
kummaliza na nina hakika siku ile
ile hakutoka kabisa nje ya
nyumba hii kwa hiyo kama kuna
mtu alimtuma basi hakupata
nafasi ya kuonana naye
tena.Lakini sina hakika sana
kama kuna mtu yeyote anayeweza
kumtumia msichana kama yule
kuniibia vitu vyangu,najua shida yake ilikuwa ni fedha tu na vitu
vingine vyote akavitupa.Kama
angenieleza ukweli ningemsamehe
lakini aligoma kuwa mkweli na
kunilazimisha nimkate pumzi”
Akawaza Pascal
********************
Kumepambazuka siku ya
jumatatu,wiki mpya imeanza.Saa
kumi na mbili za asubuhi Elvis na
Patricia waliamka na kuelekea
katika chumba cha mazoezi na
kufanya mazoezi mepesi ya
viuongo .Kisha maliza maozezi
wakaingia bafuni wakaoga na
kujiandaa kwa ajili ya kuelekea
makazini.Kabla ya kutoka
wakapata kwanza kifungua
kinywa My love,sintoungana nawe
mchana wa leo kwa chakula
.Nitakuwa na kazi nyingi leo
kutokana na ujio wa rais wa
Marekani hapo kesho.Ugeni huu
ni mkubwa na idara zote za
usalama wa nchi zinahusika
kikamilifu” akasema Elvis wakiwa
mezani wakipata kifungua kinywa
“ Usihofu darling.I’ll miss you
a lot today”akasema Patricia
“I’ll miss you too my
angel.Kama kutakuwa na tatizo
lolote hospitali kuhusiana na
Elizabeth nitaarifu mara moja ili
tujue namna ya kufanya”
“ Usihofu Elvis.Sina hakika
kama kutakuwa na tatizo lolote.No
body cares for her.Kwa muda wote
aliokuwa hospitali hana fahamu
hakuna hata mtu mmoja
aliyejitokeza kumtafuta .Kila mtu pale hospitali anafahamu kwamba
ana matatizo ya akili kwa hiyo
hakuna anayejali kupotea
kwake.Kama kutakuwa na tatizo
lolote basi nitalimaliza mwenyewe
huko huko.” Akasema
Patricia.Baada ya kumaliza kupata
kifungua kinywa kila mmoja
akaingia katika gari lake na
kuondoka kuelekea kazini
Saa mbili kasorobo Elvis
akawasili ofisini na moja kwa moja
akaiwasha kompyuta yake.Kabla
hajaanza kufanya kazi yoyote
akatokea Sabina mmoja kati ya
wafanyakazi wapya wa idara
hii.Sabina alikuwa ni mtaalamu
wa kutegemewa wa masuala ya
kompyuta
“ Hello handsome” akasema
Sabina.Elvis akageuka huku
akitabasamu na kusema Hello queen of Africa”
Akasema Elvis huku akicheka
.Yeye na Sabina ni watu
waliozoeana sana na mara nyingi
wamekuwa wakitaniana.
“ How was your weekend?
Utanisamehe Elvis nilishindwa
kabisa kufika katika birthday
party ya mkeo,niliitwa mara moja
Morogoro anakosoma mdogo
wangu.Sherehe ilikwendaje?
“ Ilikuwa nzuri sana.We had
fun.Watu wengi
walihudhuria,tukala na
kunywa.Kwa ujumla ilikuwa nzuri”
akajibu Elvis
“ Nafurahi kusikia hivyo .Its
timefor work Elvis.Tal k to you
later “akasema Sabina na
kuelekea katika meza yake.
“Now its time to find the
truth. “ akawaza Elvis halafu akaichukua ile flash disc
akaichomeka katika kompyuta
yake na kuifungua.Kulikuwa na
mafaili matatu ndani yake
.Akafungua faili la kwanza na la
pili na la tatu yakamstua sana
.Zilikuwa ni nyaraka za kijeshi
zilizohusiana na silaha mbali
mbali za kivita.Kulikuwa na picha
mbali mbali za silaha nzito za
kivita na maelezo yake.Kulikuwa
na ndege vita tatu,vifaru tisa vya
kisasa ,na aina mbali mbali za
bunduki zenye nguvu na
mabomu.Mwanzoni mwa kila faili
kulikuwa jina la Pascal kwa
kalamu..
“Nyaraka za jeshi.Pascal
anahuska vipi na nyaraka hizi
nyeti za jeshi? Ninavyofahamu
mimi mambo ya silaha hasa silaha
nzito na kivita kama hizi huwa ni mambo ya siri ya kijeshi.Kwa nini
basi Pascal ambaye si mwanajeshi
awe na nyaraka kama hizi? Kuna
kitu anakichunguza ndani ya
jeshi? Hapana sina hakika kama
kuna kitu anachokifanyia
uchunguzi ndani ya
jeshi.Ninavyofahamu mimi kama
kuna tatizo lolote ndaniya jeshi
basi wana taratibu zao za kufanya
uchunguzi na si kwa kuwatumia
watu wasio wanajeshi kama Pascal
.Kama ni hivyo , Pascal amezipata
wapi nyaraka nyeti kama hizi za
kijeshi? akawaza Elvis
“ Sasa ninaanza kupata picha
ni kwa nini Pascalalitaka kumuua
Elizabeth kwa kuificha pochi
yake.Hakutaka nyaraka hizi
zionekane kwa watu wengine.Kwa
ninialiogopa? Ngoja kwanza
nifahamu Pascal ana daraja gani katika idara yake hadi kuwa na
nyaraka nyeti kama hizi ambazo
wahusika wake ni viongozi wakuu
wa nchi na wa jeshi ” Akawaza
Elvis na kuzitafuta namba Fulani
akapiga
“ Hallow Elvis” Habari za
siku?ikajibu sauti ya mwanadada
upande wa pili
“ Nzuri Imelda,unaendeleaje?
Umepotea sana siku hizi”akasema
Elvis
“ Nipo Elvis wewe tu ndiye
umepotea kabisa hata simu siku
hizi hutaki kunipigia”
“ Ni kweli Imelda sijawasiliana
nawe kwa kipindi kirefu kidogo
lakini ni kutokana na kubanwa
sana na kazi”
“ sawa Elvis,unahitaji nini leo
? Kwa sababu ukinipigia simu ni
lazima utakuwa na shida na unahitaji msaada.” Akasema
Imelda halafu wote wakacheka
“ Mbona unacheka Elvis? Ni
kweli hayo ninayoyasema? Huwa
hunikumbuki hadi upatwe na
tatizo”
“ Kweli Imelda nina shida
kidogo naomba unisaidie”
“ Una tatizo gani?
“ Imelda nahitaji kufahamu
Pascal Situmwa ana daraja gani
katika idara yenu ya usalama wa
taifa?
“ Daraja la PascalSitumwa?
Imelda akauliza
“ Ndiyo .Nahitaji kufahamu
daraja lake ndani ya idara yenu”
akasema Elvis
“ Elvis siwezi kujua kwa sasa
Pascal ni daraja gani hadi niingie
katika kompyuta ya mkurugenZi kwani haya huwa ni mambo ya siri

“ Ok do it for me Imelda”
akaomba Elvis
“ Ok naomba unipe dakika
tano nitakupigia” akasema Imelda
na kukata simu.Elvis akaendelea
kuziangalia silaha zile na baada ya
kama dakika nne Imelda akapiga
“ Elvis ,Pascal situmwa ni
mfanyakazi wa daraja la tatu yaani
daraja la kawaida sana na hana
cheo chochote ndani ya idara.”
“ Kama Pascal ni mtu wa
daraja la tatu na hana cheo
chochote ndani ya idara ya
usalama wa taifa,kwa ninibasi
awe na nyaraka nyeti kamahizi za
kijeshi? Akajiuliza Elvis
“ Elvis are you there ?
Akauliza Imelda baada ya kuona
kumekuwa kimya Nipo Imelda.Ahsante sana
kwa msaada wako lakini kuna
jambo lingine dogo nataka
unisaidie tena”
“ semaElvis ni jambo gani
unahitaji?
“ Naomba unisaidie namba ya
simu ya Pascal”
“ Elvis Pascal kafanya nini?
Kuna nini unataka kukifanya
kwake? Nakufahamu vizuri mpaka
umfanyie uchunguzi mtu lazima
kuna jambo” akauliza Imelda
“ usihofu kitu Imelda,hakuna
tatizo lolote.Kuna kitu kidogo
nilichohitaji kukifahamu
kuhusiana na Pascal”
Imelda akamtumia Elvis
namba za simu za pascal
“ Ninachotaka kukifahamu
mimi ,nyaraka hizi za kijeshi
zimefikaje mikononi mwa Pascal? Inaonekana nyaraka hizi zina
umuhimu mkubwa sana kwake na
ndiyo maana alikuwa tayari hata
kuutoa uhai wa mtu ili
kuhakikisha kwamba hazitui
katika mikono ya mtu
mwingine.Nahitaji kulifanyia
uchunguzi jambo hili.Nataka
kufahamu uhalali wa pascal kuwa
na nyaraka nyeti kama hizi.”
Akafikirikidogo halafu akainuka
na kuelekea katika ofisi ya Sabina
“ Sabina ninatoka kidogo
kuna mahala ninaelekea”
“Unaelekea wapi Elvis?
Mkurugenzi alisema kwamba
asubuhi ya leo tunatakiwa wote
katika kikao mumu cha kazi”
“ Please sweet baby,cover for
me.Ninakwenda sehemu Fulani
muhimu sana na sintakawia
kurudi ” akasema Elvis na kutoka akaingia garini .Kabla hajaondoka
akazitafuta namba za simu za
Doreen akampigia
“ hallo Elvis,habari za
asubuhi?” akasema Doreen baada
ya kupokea simu
“ habari nzuri sana
Doreen.Ukowapi mida hii?
“Niko ofisini .Kuna tatizo
lolote Elvis?
“ Ninahitaji kukuona
.Ninakuja huko ofisini kwako sasa
hivi”akasema Elvis na kumstua
sana Doreen
“ Kuna tatizo gani
Elvis?akauliza Doreen kwa wasi
wasi.Elvis akacheka kidogo na
kusema
“ Hakuna tatizo
Doreen.Nahitaji kukuona kuna
jambo nahitaji msaada wako”
 
Story ni nzuri, japo heading inamfanya mtu asiisome.

I died saving the president ni Kama mwandishi alishakufa. Sasa anadikaaje?

Tafuta heading nyingine ya kusisimua ili msomaji atamani kujua lakini iwe na mvuto wa uhalisia.
 
Story ni nzuri, japo heading inamfanya mtu asiisome.

I died saving the president ni Kama mwandishi alishakufa. Sasa anadikaaje?

Tafuta heading nyingine ya kusisimua ili msomaji atamani kujua lakini iwe na mvuto wa uhalisia.
Tulia usome hadi mwisho kwanza ndio season 1 na ziko season 7 so uwe mpole
 
Tulia usome hadi mwisho kwanza ndio season 1 na ziko season 7 so uwe mpole
Ukiwa mwandishi, jitahidi sana kuboreshwa na watu baki. Positive feedback ni muhimu. Inamjenga mtu.

Mara kibao nilishaisoma hii heading na nikaipotezea kwa kutokusoma content. Nitakupa mfano, kwenye movie ya " hiden tiger and crouching dragon" hakuna tiger wala dragon, lakini nadharia yake ipo hidden.

Ukitoa heading ya story moja kwa moja, sitapata hamasa ya kusoma, kwa sababu kichwa chenyewe kimeshaniambia Jamaa kafa kwa kumwokoa rais, nasoma nini tena wakati ushanipa story nzima kwenye kichwa cha habari.

Lakini wewe ndiye mhusika, unaweza ukauchukua ushauri au ukautupa. Kingine jaribu kuweka spacing ili iwe rahisi kusoma.

Kumbuka mtu hujengwa kwa kupokea positive feedback, ila kama ulivyosema, ngoja nitulie. Usijidefend kuwa huru kurekebiswa.
 
I DIED TO SAVE MY PRESDENT

Sehemu 20

Elvis alifika katika ofisi za
kampuni ya Tanzacom anakofanya
kazi Doreen.Aliegesha gari na
kushuka akaelekea moja kwa moja
ofisini kwa Doreen ambaye kwa
wakati huo alikuwa ana mteja
ndani akimuhudumia hivyo
kumlazimu Elvis kusubiri nje
hadi mteja yule alipotoka ndipo
alipoingia
“ Hallow Elvis!! Doreen
akasema huku akisimama na
kumpa mkono Elvis halafu
akaufunga mlango wa ofisi yake
hakutaka watu wasikie maongezi
yake na Elvis
“ karibu sana Elvis,habari za
toka juzi?
“ habari nzuri sana
Doreen.Unaendelaje? Ninaendelea vizuri sana
Elvis.” Akasema Doreen halafu
kimya kifupi kikapita wote wawili
wakiangaliana
“ uhhm Elvis ulisema una
tatizo.Ni tatizo gani nikusaidie?
Akauliza Doreen
“ Doreen nimekuja nina tatizo
na ninahitaji msaada
wako”akasema Elvis
“ I can do anything for you
Elvis.Hata vile ambavyo unafikiri
kwamba siwezi ninaweza.”
akasema Doreen huku
akitabasamu.Elvis naye
akatabasamu na kusema
“ Nafurahi kusikia hivyo
Doreen.Ahsante kwa kuwa tayari
kunisaidia kwa jambo
lolote.Kilichonileta hapa muda
huu ni hiki”akaingiza mkonomfukoni na kutoa kijikaratasi
akampata Doreen
“ Nahitaji kupata mawasiliano
ya namba hizi ya mwezi mmoja
ulipita.”Doreen akaegemea kiti na
kumtazama Elvis kwa makini
“ Umenipa mtihani mgumu
sana Elvis but let me see what I
can do for you” akasema Doreen
na kutoka.Baada ya kama dakika
kumi hivi akarejea akiwa na flashi
disc mkononi akampatia Elvis
“ Kila kitu unachokihitaji kiko
humu ndani” akasema Doreen na
kumpatia Elvis ile flash disc
iliyokuwa na taarifa za
mawasiliano ya Pascal kwa muda
wa mwezi mmoja uliopita
“ ahsante sana
Doreen.Ahsante kwa msaada wako
huu mkubwa” usijali Elvis,niko tayari
muda wowote kukusaidia.Kwa
sababu yako niko tayari kufanya
jambo lolote hata lile la
hatari”akasema Doreen na
kumfanya Elvis atabasamu
“ Ahsante sana
Doreen.Tutaonana
baadae”akasema Elvis huku
akitoka na kumuacha Doreen
akiwa bado amesimama
“ Sikuwa nimepanga kuja
kuonana na Doreen kwa sababu
kila ninapomuona mwili wangu
hunisismka sana na
kunikumbusha usiku ule.Hili ni
jaribu zito katika ndoa yangu
ambalo sina budi
kulishinda.Ngoja kwanza
nishughulike na suala hili la
msingi ndipo niligeukie suala hili la Doreen” akawaza Elvis wakati
akiingia garini
“Baada ya kuondoka katika
ofisi za Tanzacom,moja kwa moja
akaelekea nyumbani
kwake.Akaichomeka flash disc
aliyopewa na Doreen katika
kompyuta yake na kuanza kuipitia
taarifa Iile lenye mawasiliano ya
pascal.Ilikuwa ni taarifa ndefu
iliyomchukua zaidi ya nusa saa
kulipitia.Katika orodha ya simu
zote ambazo Pascal alipiga na
kupigiwa kuna namba mbili
ambazo zilionekana kuwasiliana
naye mara nyingi zaidi.Hakujua
namba zile ni za akina nani kwani
zilikuwa ni za mtandao tofauti na
ule wa Pascal.Bila kuchelewa
akachukua tena simu na kumpigia
Doreen akampatia zile namba
mbili na kumuomba amsaidie kufahamu ni za akina nani.Baada
ya dakika mbili Doreen akampigia
simu
“ Elvis,namba ya kwanza ni ya
Edna jumbe na ya pili ni Franck
kwaju”
Elvis akastuka baada ya
kulisikia jina la pili la Frank
Kwaju
“ Umesema Frank kwaju?
“ Ndiyo .kwani kuna tatizo
gani? Akauliza Doreen
“ Doreen ahsante sana kwa
msaada wako” akasema Elvis na
kukata simu.Akaegesha kiti chake
halafu akainuka na kwenda
kuchungulia nje
“ Brigedia jenerali Frank
kwaju !! akasema Elvis huku
akizunguka zunguka mle
chumbani Sasa nimeanza kupata picha
kwa nini nyaraka zile za kijeshi
zimemfikia Pascal.Lazima kuna
kitu kinachoendelea kati ya Pascal
na Brigedia jenerali Frank
Kwaju.kwa mujibu wa taarifa hii
ya mawasiliano ya
Pascal,inaonekana kwamba pascal
na Frank wamekuwa wakiwasliana
mara nyingi zaidi.Hata katika
orodha ya simu alizopokea
inaonyesha kwamba amepokea
simu nyingi zaidi toka kwa Frank
kwaju…Something is going on
here.I need to find out.” Akawaza
Elvis
“ Nakumbuka wakati nikiwa
jeshini kabla ya kwenda masomoni
nje ya nchi kuna kijana mmoja
namkumbuka kwa jina la David
Elifariji ambaye alituhumiwa
kumbaka mtoto wa Frank.Wakati naondoka kueleka Marekani
nliacha bado kesi ile ikiunguruma
na sikuwahi kufuatilia tena ili
kujua nini ilikuwa hatima
yake.Ninavyokumbuka kesi ile
ilijaa utata mkubwa.Natakiwa
kufahamu nini kilitokea katika
kesi ile.Nahisi kuna kitu Fulani
hakikuwa sawa na ambacho
natakiwa kukifahamu.” Akawaza
Elvis halafu akatoka na moja kwa
moja akaelekea ofisini kwao mara
tu baada ya kluegesha gari
akashuka na kuelekea moja kwa
moja katika ofisi ya mkurugenzi
wake ambaye alishangaa
kumuona Elvis mida ile
“ Elvis,what are you doing
here? Akauliza mkurugenzi
“ Mkurugenzi nina shida
kidogo ya dharura na ndiyo maana
niko hapa “ Shida gani Elvis? Akauliza
mkurugenzi
“ Mzee ,wakati nikwia jeshini
kuna mwanajeshi mmoja
aliyejulikana kwa jina la David
Elifariji ambaye alikuwa na kesi ya
kumbaka mtoto wa Brigedia
jenerali Frank kwaju.Niliondoka
na kuelekea Marekani na kuiacha
kesi ile ikiendelea kuungurma na
sikuifuatilia tena.Nahitaji
kufahamu hatima ya kesi ile na
maamuzi yaliyotolewa”
“ Elvis kwa sasa rais wa
Marekani yuko angani akija
Tanzania na jukumu letu ni
kushirikiana na vyombo vingine
vya usalama kuimarisha ulinzi na
sina wakati wa kufuatilia kesi
zilizokwishapita miaka mingi.Timu
yote iko kazini muda huu ni wewe tu ambaye uko hapa” akasema
mkurugenzi
“ Mzee,jambo hili ni la
muhimu sana na ndiyo maana
niko hapa ninahitaji msaada
wako”
Mkurugenzi akamtazama
Elvis kwa makini na kusema
“ Unafuatilia jambo gani?
“ Kwa sasa ni mapema mno
kukueleza ninachokifuatilia mzee
lakini naomba unipe muda kidogo
,kuna mambo nayakamilisha
halafu nitarudi kwako na kukupa
taarifa kamili.Ili kuikamilisha
taarifa hiyo nahitaji msaada wako
na ndiyo maana niko hapa”
Mkurugenzi akaendelea
kumkazia macho Elvis halafu
akasema
“ Unataka nikusaidie nini
Elvis? Nataka unipatie barua
ambayo itaniwezesha kulipata faili
la keshi ya ubakaji iliyomkabili
David”
“ Elvis kitu unachokiomba ni
kigumu sana.Inawekana tu
kufanya hivyo endapo kuna jambo
zito ambalo tunalifuatilia”
“ Naelewa hivyo mkurugenzi
na nisingeweza kuja hapa kwako
kukuomba kitu hicho kwa jambo
ambalo si la muhimu”
“ Unataka kuona nini katika
faili hilo? Akauliza Mkurugenzi
“Kuna kitu nahitaji
kukiangalia “
Mkurugenzi akafikiri kwa
muda na kusema
‘ Ok ! Nitakuandikia hiyo
barua kwa sababu ninakuamini
na ninaamini kuna jambo la
muhimu unalolifuatilia.Naomba taarifa mara moja ya jambo hilo
unalolifuatilia mara tu umalizapo
uchunguzi wako.Mara nyingi
sipendi mtu afanye uchunguzi wa
jambo nisililolifahamu lakini kwa
vile ninakuamini ninakuruhusu
uendelee na uchunguzi wako .Vile
vile nataka ufuatilie suala hili la
faili kwa muda wako lakini kwa
sasa nataka ukaungane na
wenzako katika kuimarisha
ulinzi.”akasema Mkurugenzi na
kumuandikia Elvis barua
itakayomuwezesha kulipata faili
analolihitaji
“ Tafadhali Elvis naomba
uelekee moja kwa moja uwanja wa
ndege”akasisitiza mkurugenzi
wakati akimpatia Elvis barua
“ Usijali mzee wangu
,ninaelekea huko “akasema Elvis
na kutoka ,akapanda gari lake na kuondoka kuelekea uwanja wa
ndege kuungana na wenzake
“ Sifahamu ni kitu gani
ninachotaka kukiangalia katika
faili hilo lakini nahitaji tu
kuliona.Kuliona jina la Frank
Kwaju katika orodha ya watu
waliowasiliana na Pascal mara
nyingi kumenitia shaka kidogo na
kunilazimisha nianze kumfanyia
uchunguzi “akawaza Elvis akiwa
njiani kuelekea uwanja wa ndege
*******************
Kwa mara ya kwanza katika
historia ya Tanzania ulinzi mkali
na wa aina yake ulishuhudiwa
katika uwanja wa ndege wa
kimataifa wa Julius Nyerere .Hii
ilitokana na ujio wa rais wa
Marekani anayefanya ziara ya siku nne nchini Tanzania.Ulinzi huu wa
aina yake ulihusisha vikosi
maalum vya ulinzi toka Marekani
,makachero toka shirika la ujasusi
la marekani C.I.A na wale wa
F.B.I bila kusahau vikosi mbali
mbali vya ulinzi vya hapa nchini
Tayari rais wa jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dr
Samweli Mhamba alikwisha wasili
uwanjani kumlaki mgeni wake
.Pamoja naye alikuwepo pia rais
wa serikali ya mapinduzi ya
Zanzibar Dr Makame Abdallah
,makamu w a rais wa
Tanzania,waziri mkuu pamoja na
viongozi wengine wakubwa wa
serikali.Tayari viongozi wote
walikwisha jipanga mstari ishara
kwamba mgeni wanayemtegemea
yuko karibu kuwasiliEneo la uwanja lilijawa na
heka heka za walinda usalama
waliokuwa makini wakizunguka
huku na kule kuhakikisha
kwamba hali ya amani na usalama
inaimarika kabla na baada ya
mgeni kuwasili.Hali ya uwanjani
hapo ilikuwa tulivu na mandhari
nzima ilivutia sana .Bendera za
Tanzania na Marekani zilipepea
katika kila kona ya uwanja
huu.Vikundi mbali mbali vya
ngoma za kiutamaduni viliendelea
kutumbuiza wakati mgeni
akisubiriwa. Vilikuwepo pia
vikundi mbali mbali vya akina
mama na vijana waliokuwa
wamevalia sare maalum zenye
picha ya Kiongozi huyu wa taifa
kubwa duniani huku wakiwa
wameshika bendera za taifa la
marekani na Tanzania mikononi kwa jumla hali ya uwanjani hapo
ilikuwa ni ya kupendeza mno.
Saa tano na dakika arobaini
juu ya alama dege maarufu sana
duniani lijulikanalo kama Air
force one likaonekana
angani.Uwanja wote ukalipuka
kwa shangwe .Kila mtu
aliyekuwapo pale uwanjani
alijikuta akiwa na furaha kubwa
ya kutaka kumshuhudia kiongozi
huyu mashuhuri duniani.
Hatimaye dege lililombeba
rais wa marekani likaigusa ardhi
ya Tanzania na kwenda umbali
mrefu kisha likaanza kurudi pole
pole na mwishowe
likasimama.Mlango ukafunguliwa
na baadhi ya maofisa wa usalama
wakaingia ndani ya ndege
Baada ya dakika kama
ishirini toka dege lile lisimame uwanja ukarindima kwa shangwe
na nderemo baada ya mgeni
aliyekuwa akisubiriwa kwa hamu
kujitokeza katika mlango wa
ndege na kupunga mkono.Alikuwa
ameambatana na mkewe na binti
yao Shanon
Dr samweli Mhamba
akampokea mwenyeji wake
wakasalimiana kisha akaanza
kumtambulisha kwa viongozi
wengine wa kitaifa waliokuwepo
pale uwanjani.Baada ya
utambulisho ule ,rais wa Tanzania
na mgeni wake wakaelekea katika
jukwaa lililoandaliwa wakasimama
na nyimbo mbili za taifa za mataifa
haya mawali zikapigwa na baada
ya hapo rais wa Marekani
akakagua gwaride maalum
lililoandaliwa kwa ajili
yake.Alipomaliza akaongozwa na mwenyeji wake katika kukagua
vikundi mbali mbali vya ngoma na
burudani vilivyokuwapo pale
uwanjani.Rais wa Marekani na
ujumbe wake walionekana kujawa
na furaha sana kwa burudani
iliyokuwepo pale uwanjani.Kisha
kagua vikundi vile vya ngoma na
burudani misafara ya marais
ikaondoak pale uwanjani na
shughuli za uwanjani hapo zikawa
zimemalizika .Elvis na timu yake
nao hawakuwa na cha kufanya
tena pale uwanjani
“ Ni muda sasa wa kwenda
kulifuatilia lile faili.” Akawaza
Elvis akawaaga wenzake na
kuondoka
********************** Saa mbili za usiku Elvis
akarejea nyumbani .Tayari Patricia
alikwisha rejea muda mrefu na
alikuwa asebuleni akimsubiri ili
wale wote chakula cha usiku
“ Hallow my love umeshindaje
leo? Akauliza Patricia huku
akimkumbatia mumewe na
kumbusu
“ Nimeshinda salama
Patricia.Tulikuwa na shughuli
nzito leo ya ulinzi lakini
nashukuru Mungu imekwenda
salama”
“ Pole sana mume wangu.I
missed you so much.” Akasema
Patricia na kumsaidia Elvis kuvua
koti halafu akamuongoza hadi
chumbani na kisha wakaingia
bafuni kuoga.Kisha oga wakapata
chakula cha usiku halafu
wakaingia tena chumbani kwao.Waliongea mambo mengi
kuhusiana na siku ilivyokuwa
hadi pale Patricia alipopitiwa na
usingizi.Elvis alihakikisha mkewe
amepitiwa kabisa na usingizi
halafu akainuka taratibu akatoka
na kuelekea katika ofisi yake ya
nyumbani.Akaufungua mkoba
wake na kutoa faili moja
akalifungua na kuanza kulipitia
taratibu.Hili ni falili la kesi
iliyokuwa ikimkabiili Private David
Elifariji
Muda wa masaa mawili sasa
Elvis aliendelea kulipitia falili lile
kwa umakini mkubwa,na
alipomaliza akaegemea kiti
“ David Elifariji alikutwa na
hatia ya kumbaka Graca mtoto wa
Frank na akafungwa miaka
thelathini gerezani.Ninapata
mashaka makubwa kuhusiana na namna kesi hii ilivyoendeshwa.Ni
kweli David alimbaka huyu mtoto
wa Brigedia Frank? Akajiuliza
Elvis halafu akasimama na kukaa
juu ya meza
“ Natakiwa kumuona David
gerezani na kumuhoji kuhusiana
na jambo hili.Nataka niufahamu
ukweli.Hii ni sehemu nzuri sana
kuanzia kumfahamu Frank
Kwaju.Kuna kitu lazima nitakipata
baada ya kuonana na
David”akawaza Elvis halafu
akarejea chumbani kwake na
kulala
Saa mbili za asubuhi siku
iliyofuata Elvis tayari alikuwa
katika ofisi ya mkurugenzi wake
.Alikuwa ni mtu wa kwanza
kuonana na mkurugenzi
“ Habari za toka jana
Elvis”akauliza Mkurugenzi Habari nzuri mzee.”
“ Elvis nashukuru kwa kazi
mliyoifanya jana.Mpaka hivi sasa
hakuna tishio lolote la usalama na
kila kitu kinakwenda
vizuri.Pamoja na hayo lazima
tuendelee kushirikiana na vikosi
vingine vya usalama kuhakikisha
hali inaendelea hivi hadi mgeni
atakapoondoka.Hatutakuwa na
muda wa kupumua kwani ugeni
huu ni mkubwa na kama
unavyojua nchi ya Marekani ina
maadui wengi duniani.Ulifanikiwa
kulipata lile faili ulilokuwa
ukilihitaji ? ” akauliza
mkurugenzi
“ Ndiyo mzee nilifanikiwa
lakini nina shida nyingine naomba
msaada wako”
“ Shida gani tena Elvis? Mtuhumiwa mwenye faili
lile alihukumiwa miaka thelathini
gerezani kwa kosa la
ubakaji,nahitaji kuonana
naye.Kuna mambo ambayo
nahitaji kuyafahamu toka kwake.”
akasema Elvis
“ Elvis ni kitu gani
kinaendelea? Unachunguza jambo
gani?
“ mzee kuna jambo
ninalolifuatilia .Ni jambo kubwa
na sitaki kuliweka wazi kwa sasa
mpaka hapo nitakapokuwa na
taarifa za kutosha.”
“ Elvis unachokifanya ni
kinyume kabisa na taratibu za
idara yetu.Kila kitu
kinachofanyika hapa katika idara
hii ninapaswa kukifahamu hata
kama ni cha hatari kiasi gani ili
niweze kuona kama kinafaa kuchunguza ama vipi.lakini wewe
unajifanyia uchunguzi wako kimya
kimya bila kumshirikisha mtu
yeyote na bado unahitaji msaad
wangu.Ninakusaidia kwa vile
ninakuamini tu lakini naomba
haraka iwezekanavyo unitaarifu ni
kitu gani hasa unachokichunguza”
akasema Mkurugenzi
“ Mzee kwanza nashukuru
kwa kuniamini na kunisaidia
japokuwa nimetoka nje ya taratbu
zetu za kazi.Ninakuahidi mara tu
baada ya kumaliza uchunguzi huu
nitakuja kwako na kukueleza kila
kitu” akasema Elvis
Mkurugenzi akainama
akatafakari kidogo kisha akasema
“ Ok nitawasiliana na uongozi
wa gereza alilofungwa na
watakuruhusu uonane na mtu
unayemuhitaji” Bila kupoteza muda Elvis
akaingia garini na kuondoka
kuelekea gereza la Uwangwa
kuonana na Private David Elifariji

***************
Taarifa za ujio wake tayari
zilikwisha fika katika ofisi ya
mkuu wa gereza la Uwangwa hivyo
baada tu ya kufika Elvis alipelekea
moja kwa moja katika sehemu
ambayo angekutana na David
Elifariji.Kilikuw ani chumba
chenye ukubwa wa wastani
chenye meza na viti viwili
Baada ya dakika kadhaa
mlango ukafunguliwa na David
Elifariji akaingizwa mle ndani
“ Ouh my God !.....Elvis
akasema kwa sauti ndogo ya
mstuko baada ya kumuona David.Alikuwa amekonda sana na
kupauka
“ Afisa ,mtu uliyemuhitaji
huyu hapa.Uko huru kuongea
naye.Kamera za ulinzi za chumba
hiki zimezimwa kutokana na
maelekezo ya mkuu wa
gereza.Mkishamaliza maongezi
yenu utagonga mlango
nitakuwepo hapo nje”akasema
askari magereza aliyemleta David
mle ndani
“ Ahsante sana
Afande.”akajibu Elvis na yule
askari akatoka akawaacha yeye na
David pekee
“ Hallow david”akasema Elvis
huku akimpa mkono david
“ “halow “ akajibu David
“ Pole sana david” “ahsante sana kaka” akajibu
David .Kimya cha sekunde kadhaa
kikapita kisha Elvis akasema
“ David sina hakika kama
unanikumbuka kwa sababu ni
muda mrefu umepita.Ninaitwa
Elvis ninatoka katika idara ya
ujasusi ya taifa kitengo kipya cha
kuzuia na kupambana na
ugaidi.Mimi na wewe tulimaliza
wote mafunzo ya kijeshi na
niliondoka kuelekea marekani kwa
mafunzo zaidi ya ujasusi na
namna ya kupambana
ugaidi.Wakati ninaondoka niliacha
bado kesi yako ikiendelea na
sikujua nini kilitokea huku
nyuma.Jana nililazimika kulipitia
tena faili la kesi yako na leo
nimelazimika kuja
kukuona.Nimekuja hapa ili
kuongea nawe kuhusiana na kilichotokea na kupelekea
ukafungwa gerezani kifungo
kirefu.Tafadhali nieleze kila kitu
unachokifahamu bila
kunificha.Nini hasa kilitokea? Ni
kweli ulimbaka mtoto wa Frank
Kwaju? Kuwa huru kuniambia kile
unachokifahamu.Kwa pamoja
tunaweza kupata kitu ambacho
kinaweza kukusaidia na kukutoa
humu .I’m here to help you””
Akasema Elvis.David akamtazama
Elvis kwa macho ya huruma na
kutoa machozi
“Jikaze Elvis.Niambie ukweli”
akasema Elvis
“ Elvis nakosa hata sehemu
ya kuanzia lakini nakushukuru
sana kwa kuja kwako.Japokuwa
ni muda umepita lakini bado sura
yao naikumbuka.Ahsante sana
kwa kuja ndugu yangu.Nimefarijika mno moyoni
kwani toka nimefungwa hajawahi
kutokea mtu yeyote ambaye
ametaka kufahamu nini
kilichotokea.Wewe nimtu wa
kwanza kutaka kuufahamu ukweli
na nitakueleza kila kitu” akasema
David halafu akanyamaza kimya
akafikiri kwa muda na kusema
Ilianza oale tu tulpomaliza
mafunzo ya kijeshi na kupangiwa
kituo cja kazi.Siku ya kwanza
tu,niliporipoti kambini nikiwa
katikalindo la jioni ndipo
nilipokutana naGraca Frank
ambaye baadae nilikuwa
kumfahamu kwamba ni mtoto wa
brigedia jenerali Frank kwaju.Siku
hiyo alikuwa akitaka
shuleni.Aklijuwa na mabegi mawili
mazito nikamsaidia moja na siku
hiyondipo uradfiki wetu ulipoanza.Nilijikuta nikimpenda
Graca halikadhalika naye
akatokea knipenda.Tukajikuta
tukianzisha mahusiano ya
kmapenzi .Graca bado alikuwa ni
mwanafunzi kwahiyo mahusiano
yetu yalikuwa ni ya siri sana” Daid
akanyamaza akainama kana
kwamba kuna kitu anakumbuka
halafu akainua kichwa na
kuendelea.
“ Siku moja Graca alinipigia
simu na kuniomba nionane
naye.Siku hiyo alionekana kuwa
muoga na mwenye wasiwasi
mwingi.Mkononi alikuwa
ameshika begi dogo.Alinipa begi
na kuniamba kwamba nikalifiche
lile na nisimuonyeshe mtu yeyote
na wala nisijaribu kufungua na
kuangalia kilichomo
ndani.Nilichukua begi lile na kwenda kulificha kwangu na
sikuwahi kulifungua kuangalia
ndani yake kulikuwa na nini”
David akanyamaza kidogo
kishaakendelea
“ Baada ya wiki mbili toka
unipatie lile begi,akanipigia simu
usiku na kuniuliza kama begi lile
ninalo,nikamjibu kwamba
badoninalo akakata
simu.Nilistushwa na sauti yake
usiku ule.Haikuwa sautile
niliyoifahamu
“ Ilikuaje sautiyake? Akauliza
Elvis
“ Ilionekana kana kwamba
alikuwa analia.Sikutaka
kumuuliza kilichomsibu lakini
nilistuka sana.Saa kumi na mbili
siku ilifuata Graca alinifuata saa
kumi na moja alfajiri.Nilistuka
sana kwa hali aliyokuwanayo.Macho yake yalikuwa
mekundu na yamevimba kwa
kulia.Mwili wake ulikuwa
umemvimba ilionekana alikuwa
amepigwa.Nilijaribu kumuuliza
kilichompelekea awe katika hali ile
lakini hakunijibu zaidi ya
kulia.Aliniomba nimpatie lile begi
alilinipa nimuhifadhie.Nilimuuliza
kilichokuwamo ndani ya lile begi
akasema kwamba itakuwa vyema
kwa usalama wangu endapo
nisingefahamu katika begi ile
kulikuwa na kitu gani.Nilimpatia
lile begi akaondoka” David
akanyamaza kidogo kisha
akaendelea
Saa kumi na mbili za asubuhi
nilikamatwa na kuwekwa katika
mahabusu ya kambi.Nilituhumiwa
kwa kosa la ubakaji.Niliambiwa
kwamba nilimbaka Graca.Nilistushwa mno na jambo
hilo na nikajieleza vya kutosha
kwamba sikufanya kitendo kile
lakini hakuna aliyeonekana
kuniamini.Nilifunguliwa
mashitaka ya kijeshi nikakutwa na
hatia hivyo nikafukuzwa kazi na
kufunguliwa mashitaka
mahakamani.Mpaka leo hii sielewi
nini kwa nini nilibambikiwa kesi
ile lakini ukweli ni kwamba
sikumbaka Graca na hata
mwenyewe anajua
hilo.Nimefungwa sina hatia
ninaozea gerezani kwa kosa
ambalo sikulitenda.Mpaka leo
sielewani kitu gani niliwafanyia
Brigedia Frank na mwanae Graca
kiasi cha kuniadhibu namna hii.”
Akasema David kwa
uchungu.Elvis akamtazama akamuonea huruma sana na
kusema
“ Katika faili lile la kesi yako
kuna cheti kinaonyesha kwamba
Graca ana matatizo ya akili.Katika
kipindi hicho ulichokuwa na
mahusiano naye ulimuonaje?
Kweli ana matatizo ya akili?
“ Hapana.Sikubaliani na mtu
yeyote anayesema kwambaGraca
alikuwa na matatiozo ya
akili.Jambo hilo nimelisikia baada
ya kesi yangu
kuanza.Ninachofahamu mimi
Graca alikuwa mzima kabisa na
sikumuona kama ana tatizo lolote
la kiakili kama inavyodaiwa.Kuna
mtu aliniambia kwamba baada tu
ya mimi kuhukumiwa kwenda jela
miaka thelathini ,Graca alipelekwa
nchini afrika kusini katika
hospitali ya magonjwa ya akili iitwayo Nxhasa mental hospital.”
akasema David
“ Unahisi ni kitu gani hasa
kilichomfanya Brigedia frank
akubambikie kesi ile ya ubakaji na
kukusababishia kifungo hiki?
Akauliza Elvis
“ Sifahamu kaka.Nimejaribu
sana kujiuliza ni kitu gani hasa
kilichosababisha hadi nikafungwa
gerezani kwa kosa ambalo
sikulitenda lakini nimekosa
jibu.Nimeamuachia Mungu yote
yeye ndiye anayeufahamu ukweli”
akasema Davis .Elvis akaendelea
kumtazama kwa makini na
kumuuliza
“ Unahisi ndani ya lile begi
alilokupa Graca kulikuwa na nini?
“ Sina hakika kulikuwa na
nini lakini kwa namna lilivyokuwa ilionyesha ndani yake kulikuwa na
kompyuta ndogo.”
“ unahisi kilichokuwamo
ndani ya hilo begi ndicho
kilichopelekea wewe kufikwa na
tatizo hili?
“ Sina hakika sana lakini
ninahisi inawezekana ikawa
hivyo.Graca alinisisitiza sana
kwamba nisifungue ndani
kuangalia kuna nini .Inaonekana
kulikuwa na kitu cha muhimu
mno ambacho alikuwa anakificha
watu wasikione.Hata siku ya
mwisho alipokuja kulichukua begi
lile nilijaribu kumuuliza kuna nini
ndani lakini hakuwa tayari
kuniambia.Ninahisi
kilichokuwamo ndani ya mkoba
ule kina uhusiano wa moja kwa
moja na Brigedia Frank.Ninahisi
huenda Frank alifahamu kwamba begi lile liko kwangu na kwamba
tayari ninafahamu kilichomo
ndani yake na ndiyo maana
akanifanyia hivi.” Akasema David
“ David ahsante sana kwa
maelezo yako.Umenipa mwanga
mkubwa sana”
“ Ndugu yangu nimekueleza
ukweli wote bila kukuficha hata
kitu kimoja kwa sababu
ninakuamini.Tafadhali naomba
unisidie kama utaweza ili niweze
kutoka humu gerezani.Sina hatia
yoyote na mateso ninayopata
humu ni makubwa” akasema
David
“ Pole sana
David.Nitakusaidia.Nitafanya kila
ninaloweza kuhakikiksha kwamba
unatoka humu
gerezani.Nimeumizwa sana na
kitendo alichokufanyia Frank.Nitakuja kukuona tena
baada ya siku chache zijazo lakini
kwa sasa naomba usimweleze mtu
yeyote kile ulichonieleza.” akasema
Elvis halafu akaagana na David
akaondoka.
“ David amefungwa bila
hatia.Nimemtazama machoni.He’s
telling the truth.Kwa nini Frank
amfanyie hivi? Akawaza Elvis
akiwa garini
“ Katika faili lile la kesi kuna
uthibitisho toka hospitali
ukithibitisha kwamba ni kweli
Graca alibakwa na David.Dr
Herman Mapunda ndiye aliyefanya
uchunguzi huo na kuthibitisha
kwamba Graca alibakwa.Natakiwa
kumtafuta daktari huyu niongee
naye” akawaza Elvis na kuongeza
mwendo wa gari huku maneno aliyoambiwa na David yakizidi
kujirudia kichwani
“ Kwa mujibu wa David ni
kwamba Graca hakuwa na
matatizo yoyote ya kiakili katika
kipindi chote cha mahusiano
yao.David anadai kwamba baada
tu ya kesi yake kuanza ndipo
ugonjwa wa Graca
ulipoanza.Ninapatwa na wasi wasi
mkubwa kuhusiana na jambo
hili.Ngoja kwanza nikaonane na Dr
Herman halafu nitajua nini
kitafuata”
Elvis alifika katika hospitali
ambako ndiko iliandikwa kwamba
Graca alifanyiwa uchunguzi na
kubainika kwamba
alibakwa.Akashuka na kuelekea
ndani ya hospitali.Kulikuwa na
wagonjwa wengi na mara
akamuona muuguzi mmoja aliyekuwa anongea na simu
akamsogelea na kumsubiri hadi
alipomaliza kuzungumza na simu
akamsabahi
“samahani dada yangu.”
akasemaElvis.Muuguzi yule
aliyevaa vazi lililomkaa vyema
akatabasamu na kusema
“ Bila samahani kaka
yangu,nikusaidie nini?
“ Ninahitaji kuonana na Dr
Herman Mapunda.Unaweza
ukanielekeza mahala ninakoweza
kumpata? Akasema Elvis na
kumstua yule muuguzi
“ Dr Herman?!! Yule dada
akashangaa
“ Ndiyo .Mbona
umeshangaa.Humfahamu?
“ Kwani kaka wewe umetokea
wapi? Akauliza yule muuguzi “ Nimetokea nje ya nchi .Kuna
wakati niliwahi kuwasiliana naye
na akaniambia kwambanikija
tanzania nije nimtafute hapa”
akasema Elvis
“ Dah pole sana kaka
yangu.Dr DrHerman unayemtafuta
hayupo tena katika hospitali hii.”
“ Yuko wapi? Amehama kituo
cha kazi? Akauliza Elvis
“ Dr Herman alikwisha fariki
dunia muda mrefu”
“Amefariki dunia?..Elvis
akashangaa
“ Ndiyo amefariki dunia”
“ Nini sababu ya kifo chake?
“ alianguka ghafla na
kufariki.Uchunguzi unaonyesha
kwamba moyo wake ulipasuka
lakini kuna tetesi kwamba alipewa
sumu”
Elvis akavuta pumzi ndefu Ahsante sana dada yangu
kwa kunipa taarifa hii“akasema
Elvis na kuondoka huku yule
muuguzi akiendelea kumshangaa
“ Dah ! Dr Herman naye
amekufa.Ninaanza kuwa na
uhakika na hisia zangu kwamba
kuna kitu hapa
kinachoendelea.Yeye ndiye
anayedaiwa kumfanyia uchunguzi
Graca na kuthibitisha kwamba ni
kweli amebakwa na
David.Inawezekana akawa
ameuawaa ili kuendelea kuuficha
ukweli kuhusiana na kubakwa
kwa Graca.Ili kuupata ukweli wa
jambo hili natakiwa kuonana na
Graca.Yeye ndiye mwenye majibu
kuhusiana na kizungumkuti hiki”
akawaza Elvis halafu akawasha
gari na kuondoka na moja kwa
moja kwa akelekea ofisini kwao
 
Ukiwa mwandishi, jitahidi sana kuboreshwa na watu baki. Positive feedback ni muhimu. Inamjenga mtu.

Mara kibao nilishaisoma hii heading na nikaipotezea kwa kutokusoma content. Nitakupa mfano, kwenye movie ya " hiden tiger and crouching dragon" hakuna tiger wala dragon, lakini nadharia yake ipo hidden.

Ukitoa heading ya story moja kwa moja, sitapata hamasa ya kusoma, kwa sababu kichwa chenyewe kimeshaniambia Jamaa kafa kwa kumwokoa rais, nasoma nini tena wakati ushanipa story nzima kwenye kichwa cha habari.

Lakini wewe ndiye mhusika, unaweza ukauchukua ushauri au ukautupa. Kingine jaribu kuweka spacing ili iwe rahisi kusoma.

Kumbuka mtu hujengwa kwa kupokea positive feedback, ila kama ulivyosema, ngoja nitulie. Usijidefend kuwa huru kurekebiswa.
Wewe soma utajua kwanini inakichwa hicho
 
I DIED TO SAVE MY PRESDENT

Sehemu 21

Mtunzi Patrick co

akabisha hodi katika ofisi ya
mkurugenzi wake
“ Elvis unafanya nini hapa
mida hii?Unatakiwa uungane na
timu ya wenzako” akasema
mkurugenzi
“ Samahani sana
mzee.Nimelazimika kuja kukuona
kuna jambo nataka kuongea
nawe.Nahitaji tena msaada wako”
Mkurugenzi akamtazama kwa
makini na kusema
“ Evis kuna kitu gani
unachokifuatilia?Kitu gani
kinachoendelea ambacho hutaki
kuniambia?
Elvis akavuta kiti na kuketi
halafu akasema
“ Mzee najua unahitaji sana
kujua kitu
ninachokichunguza.Nahitaji sana
kukueleza ni kitu gani lakini inaniwia ugumu kwa sababu hata
mimi mwenyewe bado sijapata
undani hasa wa kile
ninachokifuatilia.Nahitaji
uchunguzi zaidi ili niweze kupata
taarifa zenye kutosheleza na ndipo
nitakapokuja kwako kukueleza ”
akasema Elvis.Mkurugenzi
akamtazama na kusema
“ Elvis ninakuamini sana
kijana wangu na niko tayari
kukusaida msaada wowote
unaouhitaji lakini nimeanza
kuingiwa na shaka kuhusiana na
usiri wako katika jambo hilo
unalolichunguza”
“ Mzee nafahamu kwamba
ninakwenda kinyume na taratibu
kwa kuchunguza jambo bila
kukushirikisha kwanza
wewe.Jambo ninalolichunguza ni
jambo kubwa na ninahitaji bado kufahamu mambo kadhaa ili
niweze kulileta mezani kwako
likiwa limekamilika .Naomba
muda kidogo ili niweze
kukamilisha uchunguzi
wangu”akaomba Elvis.Meshack
Jumbo akasema
“ What do you need this time?
“Nahitaji kwenda Afrika ya
kusini”akasemaElvis
“ Afrika ya kusini?
“ Ndiyo mzee
“Kufanya nini?
“ Kuna mtu ambaye nahitaji
kwenda kumuhoji.Nina uhakika
yeye ndiye mwenye majibu yote ya
kile ninachokichunguza”akasema
Elvis
“ Kwa hiyo unahitaji nini?
“ nahitaji ruhusa ya kwenda
huko na endapo nitahitaji msaada
wowote nikiwa huko basi nitakufahamisha.Mzee suala hili
ni muhimu sana.Utimilifu wa
jambo zima ninalolichunguza
unategemea sana safari hii”
akasema Elvis .Mkurugenzi
akafikiri kidogo na kusema
“ Umeniacha nikiwa sina
uamuzi mwinginezaidi ya
kukuruhusu uende huko afrika ya
kusini.Pamoja na hayo ukumbuke
siku zote kwamba ninakuamini
kila unachoniambia kwa niyo
pindi ukamilishapo uchunguzi
wako ujekwangu mara moja
kunieleza”
“ Mzee ahsante sana kwa
kuniamini .Nakuahidi
nitakaporejea nitakuwa na kitu
muhimu cha kuweka mezani
kwako” Akasema Elvis
“ Elvis Kitu kingine
ninachotaka kukufahamisha ni kwamba safari hii ni ya siri kati
yangu nawe na haitakuwepo
katika orodha ya kazi za ofisi kwa
hiyo jitahidi asifahamu mtu
mwingine yeyote..” akasema
mkurugenzi
“ Ahsante sana
mzee.Ninategemea kuondoka
kesho asubuhi na baada ya siku
mbili nitarejea.”
“ sawa Elvis.Nakutakia kila la
heli. Nitaongea na Bongani
Makath ambaye ni mtu wetu kule
afrika kusini na atakupatia kila
aina ya msaada unaouhitaji ukiwa
kule”
“ Ahsante sana
mzee.Tutaonana nitakaporejea”
akasema Elvis na kuondoka ili
kuanza maandalizi ya safari yake
ya kuelekea afrika kusini.

ELVIS ATAFANIKIWA KUPATA
KILE ANACHOENDA KUKITAFUTA
AFRIKA KUSINI? USIKOSE PART 2
YA SIMULIZI HII
 
Back
Top Bottom