Riwaya: I died to save my President

Riwaya: I died to save my President

Nafasi anayo so lazima akabe, kwanza Patricia kashaniudhi mimi
 
Jaman mumuonee huruma kwanza kachepuka maramoja tu tena alikuwa na stress
Mkuu ukiona mwanamke anaanza kuchepuka kabla ya mume wake ujue huyo ni bure kabisa. Atakuja kumgawia tena Godson
 
Dokta atajipigia sana Patricia kipindi hiki cha maombolezo ya kifo cha Elvis....
 
Kulubule kama upo tupia season 4 wengine tupo lindo hatulali hadi majogoo😂😂😂
 
I DIED TO SAVE PRESDANT

Season 4

Sehemu 37

ILIPOISHIA SEHEMU
ILIYOPITA
Steven na Dr Philip
walisaidiana kumuingiza Elvis
garini halafu wakaondoka .Safari
ilikuwa ya kimya kimya hadi
walipowasili nyumbani.Taratibu
Elvis akatembea kuingia
ndani.Doreen aliyekuwa
amesimama mlangoni
akamkimbilia kutaka
kumkumbatia lakini Steven
akamzuia na kumuingiza ndani,
akampeleka chumbani
kwake.Graca alibaki anashangaa
kumuona Elvis akiwa katika hali
ile.
“Dada Doreen kitu gani
kinaendelea?Elvis amepatwa na nini hadi akawa katika hali
ile?Mbona anaonekana mgonjwa
sana? Graca akamuuliza Doreen
ambaye alikuwa ameegemea ukuta
“Relax Graca.He’s fine”
akajibu Doreen
“Relax ?!! Graca akahamaki
“Something is wrong with him
and I know you know what’s going
on but you don’t tell me.Toka
asubuhi nimekuwa nikikuuliza
alipo Elvis umekuwa unanipa
majibu ya mkato.Nataka
kufahamu Elvis ana matatizo
gani?Nijibu tafadhali kwani Elvis
ndiye pekee ninayemtegemea sasa
hivi.Usalama wangu unamtegemea
yeye”
Doreen akamfuata akamshika
mkono na kumketisha sofani Ni kweli Graca kuna jambo
linaendelea hapa lakini Elvis
amenizuia nisikueleze
chochote.Atakueleza yeye
mwenyewe nini kinaendelea”
Doreen akasema.Graca
akamtazama kwa wasi wasi
mkubwa
“Usiwe na wasi wasi
Graca.Elvis yuko sawa”
“Dada Doreen nashindwa
kujizuia kutokuwa na wasiwasi
kwa sababu yeye ndiye kila kitu
kwangu.Usalama wa maisha
yangu unamtegemea yeye kwa
kiasi kikubwa”
“Nalifahamu hilo Graca na
ndiyo maana ninakuhakikishia
kwamba Elvis yuko sawa” Na hawa jamaa alioongozana
nao ni akina nani? Unawafahamu?
Akauliza Graca
“Wale ni wafanyakazi
wenzake.Usiwe na shaka nao hata
kidogo” Akasema Doreen na mara
Steven akaingia pale sebuleni
akastuka alipokutanisha macho
na Graca
“Mhh !! Elvis anawatoa wapi
watoto wazuri kama hawa? Nahisi
huyu ndiye yulebinti aliyeniambia
alienda kumchukua afrika
kusini.She’s amazing” akawaza
Steve halafu akakohoa kidogo na
kusema
“Doreen tunahitaji chakula
chepesi kwa ajili ya Elvis”
Kwa haraka Doreen akainuka
na kuelekea jikoni akawaacha
Steven na Graca pale sebuleni Naitwa Steven” Akasema
Steven huku akimtazama Graca
“Naitwa Graca”
“Nafurahi kukufahamu
Graca.Mimi ni rafiki wa
Elvis.Tunafanya kazi pamoja kwa
hiyo tutaendelea kuonana kwani
nitakuwa nikikaa hapa kwa siku
kadhaa.Usihofu kuhusu Elvis.He’s
fine” akasema Steven kwa sauti ya
upole halafu akaondoka kuelekea
chumbani kwa Elvis
Wakati Elvis akiendelea
kulishwa taratibu na Doreen
Steven akampigia simu
MeshackJumbo akampa taarifa za
Elvis na kumuelekeza mahala
walipo
******************* MeshackJumbo aliwasili
mahala wanakoishi akina
Elvis,akapokewa na Steven
ambaye alimtambulisha kwa akina
Doreen na Graca halafu
akampeleka moja kwa moja
chumbani kwa Elvis
“Welcome back to the world”
MeshackJumbo akamtania Elvis
aliyekuwa amekaa sofani.Elvis
akatabasamu
Dr Philip akatoa maelezo ya
maendeleo ya Elvis halafu
MeshackJumbo akataka kusema
kitu lakini Elvis akamzuia
“Mzee nataka kwanza
kufahamu mke wangu
anaendeleaje?
“Usihofu Elvis nitakueleza kila
kitu” akasema MeshackJumbo na
kumueleza Elvis kila kitu kilivyoenda .Michirizi ya machozi
ikaonekana mashavuni mwa Elvis
“Elvis huu si wakati wa wewe
kuangusha chozi.Ni wakati ambao
unahitaji ujasiri wa aina yake
kuliko wakati mwingine wowote
katika maisha yako”akasema
Meshack
“Mzee naumia sana nikifikiria
mateso anayoyapata mke wangu
sasa hivi “
“Elvis ili tufanikiwe mpango
wetu lazima uyasahau hayo yote
kwa sasa na tuelekeze akili zetu
zote katika suala hili” akasema
MeshackJumbo na Elvis akafuta
machozi
“Hatua ya kwanza
imemalizika na Elvis tayari
amefariki.Nini hatua ya pili?
Akauliza Steven kwa mujibu wa mpango
ulivyo,keshi tutaanza
kushughulikia jeneza pamoja na
kaburi atakamozikwa Elvis.Kila
kitu kiko tayari vifaa vimekwisha
andaliwa.Mazishi yatafanyika lini?
“Kesho kutwa.Kikao cha
familia kimekaa na mimi
nikawashauri mazishi yafanyike
kesho kutwa kama tulivyokuwa
tumepanga.Nimewaambia
washughulikie masuala mengine
yote lakini suala la jeneza na
kaburi watuachie sisi
tutashughulikia.Dr Philip
umejipangaje kuhusu jeneza?
Akauliza MeshackJumbo
“Kesho nitakuwa na kazi ya
kulishughulikia suala hilo na
mpaka jioni kila kitu kitakuwa
tayari” Vizuri.Mimi kesho
nitakutana na ndugu wa Elvis
tena kumalizia baadhi ya
maandalizi ya mazishi.Nataka
tulimalize jambo hili la msiba kwa
haraka ili Elvis aanze kuifanya
kazi yake haraka kwani hawa
maadui zetu hawalali wakipanga
mipango yao na sisi tunapaswa
twende nao sambamba” akasema
MeshackJumbo
Majadiliano yaliendelea hadi
ilipotimu saa saba za usiku
ambapo MeshackJumbo aliondoka
kurejea kwake na Dr Philip yeye
alibaki pale pale kwa Elvis kwani
kulikuwa na nafasi ya kutosha
Baada ya watu wote kutoka
mle chumbani Elvis akajilaza
kitandani huku akihisi kichwa
kizito sana.Aliwaza mambo mengi kuhusiana na mpango ule
unaoendelea lakini kubwa
lililomtesa kichwa chake ni mke
wake Patricia.Taratibu kijiusingizi
kikaanza kumnyemelea na mara
kwa mbali akasikia kama mlango
unafunguliwa taratibu.Akafumbua
macho na kukutana na Doreen
“Doreen badio hujalala hadi
mida hii? Akauliza Elvis kwa sauti
ya uchovu
Doreen hakujibu kitu
akamfuata Elvis pale kitandani
akamkumbatia
“Elvis unajisikiaje?
“Najisikia vizuri japo kichwa
kinaniuma sana”
“Pole sana Elvis” akasema
Doreen Ahsante sana.Ahsante kwa
kila kitu” akasema Elvis kikapita
kimya
“Graca
anaendeleaje?Nilimuona wakati
nikiingia namna alivyopatwa na
mshituko”
“Ni kweli Graca amekwisha
gundua kuna jambo linaendelea
na hatujamwambia.Toka asubuhi
amekuwa ananiuliza kama
ninafahamu kinachoendelea
nilimkatalia kwamba sijui
chochote.Usiku huu alipokuona
ukiingia wasiwasi wake
umeongezeka na akanifuata
tena.Safari hii nilishindwa
kukataa na nikamwambia
kwamba ni kweli kuna jambo
linaendelea lakini utamweleza
wewe mwenyewe.Ana wasi wasi mkubwa na usalama wa maisha
yake”
“Usijali kuhusu hilo,she’ll be
fine.Nitaongea naye kesho”
akasema Elvis halafu akazama
mawazoni.Doreen akamuangalia
na kusema
“Unamuwaza Patricia?
“Ndiyo.Nashindwa
kutomuwaza.Nimemsababishia
mateso makali kwa kitendo cha
kudanganya kuhusu kifo changu”
akasema Elvis
Doreen akajisogeza karibu
yake na kusema
“Elvis usimuwaze Patricia kwa
sasa.She’ll be ok.Huko mbeleni
atakusamehe baada ya kugundua
kwa nini ulifanya
hivi.Unachotakiwa ni kuelekeza
akili yako yote katika kazi nzito iliyoko mbele yako.Bila wewe
mtandao huu wa vigogo
wanaofanya biashara haramu ya
silaha hutakoma na raia wasio na
hatia wataendelea kupoteza
maisha kila uchao huko Congo”
Elvis akamtazama Doreen
akatabasamu na kusema
“Ahsante sana Doreen kwa
ushirikiano wako.Ni wakati wa
kupumzika kesho itakuwa siku
ndefu mno”akasema
Doreen akatabasamu na
kumbusu Elvis akajilaza pembeni

yakeENDELEA……………..
“Doreen!! Akasema Elvis”
Doreen hakujibu kitu
akamkumbatia zaidi Elvis
“Ouh Elvis !! akasema
Doreen.Baada ya dakika takribani
mbili za kukumbatiana Doreen
akajitoa mikononi mwa Elvis na
kumuangalia usoni
“Unajikiaje Elvis?
“Najisikia vizuri japo kichwa
kinaniuma sana” akasema Elvis
“Pole sana Elvis” akasema
Doreen Ahsante sana Doreen kwa
kila kitu.” Akasema Elvis na kimya
kifupi kikapita
“Graca anaendeleaje?
Nilimuona namna alivyopatwa na
mstuko wakati nikiingia”
“Graca tayari amekwisha
gundua kwamba kuna kitu
kinaendelea na
hatujamueleza.Toka asubuhi
amekuwa akiniuliza kama
ninafahamu
kinachoendelea.Nilimkatalia
kwamba sifahamu chochote lakini
alipokuona usiku huu amenifuata
tena na nikashindwa
kukataa.Nilimweleza kwamba
kuna jambo linaendelea lakini
utamweleza wewe mwenyewe.Ana wasi wasi mkubwa na usalama
wako na maisha yake kwa ujumla”
“Usijali kuhusu hilo,she”ll be
fine.Nitaongea naye kesho”
akasema Elvis halafu akazama
mawazoni.Doreen akamuangalia
na kusema
“You are thinking of her?
“Ndiyo Doreen.Nashindwa
kuacha kumuwaza
Patrica.Nimemsababishia mateso
makali kwa kitendo hiki cha
kudanganya kuhusu kifo changu”
Doreen akakisogeza kichwa
karibu na sikio la Elvis na
kunong’ona
“Elvis usimuwaze Patricia kwa
sasa.She’ll be ok and she’ll forgive
you for that.Unachotakiwa kufanya ni kufikiria kazi nzito iliyoko
mbele yako.Bila wewe biashara hii
ya silaha haitakoma na raia wasio
na hatia wataendelea kuuawa
huko mashariki ya Congo”
Elvis akamtazama
Doreen,akatabasamu
“Thank you Doreen.I
appreciate your support”
Doreen akainama na kumbusu
halafu akakilaza kichwa chake
kifuani kwa Elvis
******************
Ni asubuhi nyingine na kijua
tayari kimekwisha
chomoza.Steven Kinke na Dr Philip
tayari walikuwa barabarani wakielekea sehemu mbalimbali
kila mmoja kushughulikia jukumu
alilopewa.Dr Philip alielekea
kwanza nyumbani kwake
kujiandaa kabla ya kuanza
kushughulikia jeneza
atakamozikiwa Elvis
Saa mbili na nusu za asubuhi
mlango wa chumba cha Elvis
ukagongwa,Elvis ambaye asubuhi
hii alikuwa katika hali yake ya
kawaida akainuka na kwenda
kufungua mlango akakutana na
Graca
“Graca ! akasema Elvis na
kumshika mkono akamkaribisha
ndani
“Unaendeleaje Elvis? Akauliza
Graca baada ya kuketi sofani Ninaendelea vizuri.Wewe je
unaendeleaje?
“Naendelea vizuri pia
japokuwa bado mwili hauna nguvu
za kutosha hasa baada ya kuacha
kutumia zile dawa za wagonjwa wa
akili nilizokuwa napewa.I know
it’ll take sometime to be ok but I’ll
be fine” akasema Graca huku
akitabasamu kwa mbali
“You’ll be fine Graca” akasema
Elvis kimya cha sekunde kadhaa
kikapita,Graca akasema
“Elvis,jana nilistushwa kidogo
na hali uliyokuwa nayo
uliporejea.Nilimuuliza Doreen
kama unaumwa akanihakikishia
kwamba huumwi ila kuna jambo
linaendelea.Alikataa kunieleza akasema kwamba utanieleza wewe
mwenyewe.What’s going on Elvis?
Akauliza Graca
Elvis akanyamaza kidogo
akamtazama Graca halafu
akamueleza kila kitu
kinachoendelea
“Hiyo ndiyo hali halisi Graca
ila nakuomba usiwe na wasiwasi
hata kidogo kuhusiana na usalama
wako.Nilikuahidi kukulinda na
kuhakikisha unakuwa salama na
ndivyo itakavyokuwa.Niwe mzima
au nimekufa usiwe na hofu kabisa
utakuwa salama” akasema Elvis na
Graca ambaye alikuwa ameuweka
mkono wake mahala ulipo moyo
alionekana kuwa na wasi wasi
mwingi “Elvis ninakuamini sana kwa
kila unachonieleza lakini kwa
jambo hili unalotaka kulifanya
nafsi yangu inakataa
kabisa.Hakuna namna nyingine ya
kufanya? I’m so worried.Ni vipi
kama mambo hayatakwenda kama
mlivyopanga na ukawa ndiyo
mwisho wako? Hofu yangu ni
kwamba sisi ni wanadamu na kuna
kukosea hivyo kunaweza
kukafanyika makosa madogo na
mambo yakaharibika.Elvis please
don’t do this” akasema Graca huku
akilengwa na machozi.Mathew
akainuka akamfuata pale sofani
akaketi pembeni yake
“Graca nakuomba usiwe na
wasiwasi hata kidogo.Watu nilio nao ni zaidi ya wataalamu na
mambo kama haya wanayafahamu
kwa undani hiyo nakuomba usiwe
na hofu hata kidgo.Nakubaliana
nawe kwamba makosa yapo lakini
endapo kutatokea kosa lolote
ambalo linaweza kusababisha uhai
wangu kutoka basi itakuwa ni ajali
kama ajali nyingine lakini
sitegemei kabisa kwa watu wangu
kufanya makosa.Wako makini
sana kuhakikisha kwamba
operesheni hii inafanikiwa.Graca
hii ni kazi ambayo unapoifanya
huwazi kuhusu kufa bali
unayaweka mbele maisha ya watu
na nchi yako hivyo mawazo ya kufa
hayapo kichwani kwangu ila kama
ikitokea ikawa hivyo basi watakaobaki watakuhudumia na
watahakikisha unakuwa
salama.Tafadhali naomba
uniamini” akasema Mathew na
Graca akatikisa kichwa kuonyesha
kukubaliana na kile alichokisema
Elvis.
“Elvis ninakubaliana nawe
kwa shingo upande bado moyo
wangu unakataa kabisa.Sina
namna ya kukuzuia usifanye hivyo
kwani kama ulivyosema ndiyo njia
pekee ya kuweza kuufumua
mtandao wa baba na kuokoa
ndugu zetu wanaokufa huko nchini
Cong😵nly God Knows how I feel
inside but I’ll be fine” akasema
Graca na kutoka mle chumbani kwa Elvis huku macho yake yakiwa
yamejaa machozi
*****************
Steven alisimamisha gari nje
ya jumba moja kubwa la ghorofa
mbili,akashuka garini na
kubonyeza kengele ya geti na
haukupta muda kijana mmoja
akafungua geti.
“Habari yako ndgu yangu”
akasema yule kijana
“Habari nzuri”akajibu Steven
“Nikusaidie nini? Akauliza
yule kijana
“Nataka kuonana na Benard
Amuma.Mwambie ni Steven Kinko”
akasema Steven na yule kijana akarejea ndani baada ya dakika
mbili akarejea na kufungua geti na
kumkaribisha Steven ndani
“Karibu sana” akasema yule
kijana na kumuongoza Steven
kueleka sebuleni.Kabla
hawajaufikia mlango wa kuingilia
sebuleni akatokea jamaa mmoja
mnene aliyekuwa tumbo wazi na
kifuani akiwa amevaa mikufu
mitatu mikubwa ya dhahabu.
“The devil is back !! akasema
yule jamaa na kumkumbatia
Steven kwa furaha
“Welcome back Steven”
akasema
“Thanks Ben” akajibu Steven
wakaeleka sebuleni.Ben akamuagiza mtumishi wake
awaandalie mvinyo
“Bado siamini macho yangu
kama kweli ni wewe umerudi tena
uraiani.Nimefurahi sana kukuona
tena Steve”akasema Ben
“Its me.I’m back Ben” akajibu
Steven
“Imekuaje ukatoka? Yale
mambo yako yamemalizika?
“Ben tutazungumza baadae
kuhusu suala hilo lakini kwa sasa
naomba tuzungumze jambo la
msingi lililonileta hapa
kwako.Nimekuja kuomba msaada
wako Ben”
“Usihofu Steven.Ni msaada
gani unahitaji kaka? Kwanza kabisa nipe taarifa
kuhusu Samira.Anaendeleaje yule
malaika? Unaonana naye? Nina
hamu sana ya kuonana naye
tena.Nikiwa kifungoni niliteseka
sana kwa mawazo juu
yake.Anautesa mno moyo
wangu.Japo yeye ndiye sababu ya
mimi kufikwa na masahibu yale
lakini katu sintoacha
kumpenda.Nipe taarifa zake”
akasema Steven.Ben akachukua
sekunde kadhaa na kusema
“Steven wewe ni mtu wangu
wa karibu sana na ni zaidi ya
rafiki.Wewe ni ndugu yangu kabisa
na kwa sababu hiyo basi siwezi
kukushauri urejeane na
Samira.Naomba niwe wazi kwako kwamba yule mwanamke hakufai
kabisa.Amekuingiza katika
matatizo makubwa na umetoka
huko ulikokuwa kwa kudra za
Mungu kwa hiyo si wakati wa
kurejesha tena mahusiano naye”
akasema Ben
“Ben naomba nikuweke wazi
ndugu yangu kwamba linapokuja
suala la Samira ninashindwa
kufanya maamuzi.Ameniingia
katika kila mshipa uliomo mwilini
mwangu.Tafadhali nisaidie niweze
kuonana naye.Hilo ndilo jambo
kubwa la kwanza lililonileta hapa
kwako asubuhi hii.Hapa nilipo
moyo wangu ni kama umekufa
ganzi na dawa yake ni pale nitakapoiona sura ya yule malaika
Samira” akasema Steve
“Steven kama nilivyokwambia
kwamba wewe ni rafiki yangu na
ulipopatwa na matatizo na kwa
taarifa yako nimehangaika sana
kupata sehemu ulikokuwa
umefungwa lakini sikuweza
kufanikiwa.Ninamshukuru Mungu
kwamba ametenda muujiza na
sasa uko huru na huu ni wakati
wako wa kujipanga kwa maisha
mapya na kumsahau kabisa
mwanamke yule ambaye
amekuweka katika matatizo
makubwa na wala haumii kwa
wewe kufikwa na masahibu kama
yale”akasema Ben “Ben mimi na Samira
tunapendana sana na sina hakika
kama yupo mwanamke
atakayeweza kuchukua nafasi yake
katika moyo wangu.Tafadhali
naomba unipe taarifa zake na wapi
ninaweza kumpata” Steven
akaendelea kusisitiza.Ben
akamtazama kwa muda na kusema
“Kwa kuwa umesisitiza
nitakueleza.Yule kigogo aliyekuwa
naye wakati ule ambaye ndiye
aliyekufanyia unyama huu wote na
kutaka kukupoteza alifariki kwa
ajali ya gari na kwa sasa Samira
ana kigogo mwingine mzito zaidi
ya yule na ndiyo maana
ninakushauri ndugu yangu
uachane naye kabisa kwani anaweza akakuweka katika
matatizo makubwa zaidi”
“Ahsante kwa ushauri Ben
lakini uamuzi wangu ni kwamba
nitaendelea na Samira.Nisaidie
niweze kuonana naye” akasema
Steven.Ben akamtazama na
kugundua kwamba Steven alikuwa
anamaanisha anachokisema.
“Mimi na Samira
tunawasiliana na apatapo nafasi
huwa ananitafuta
tunazungumza.Mara ya mwisho
tulionana mwezi uliopita
alinitafuta alikuwa anahitaji
kuagiziwa gari nikamfanyia
mpango akapata gari alilokuwa
analihitaji.Ni gari la kifahari sana lenye thamani kubwa zaidi ya
shilingi milioni mia mbili”
“Wow ! Inaonekana mambo
yake mazuri sana siku
hizi.Mlipokutana aliniulizia?
“Wakati wote ninapokutana
naye ana kwa ana au kuwasiliana
katika simu hajawahi kuacha
kukuulizia.Amekuwa akinisisitiza
pindi nikifahamu mahala ulipo
nimjulishe mara moja aje
akutazame lakini hii haimaanishi
kwamba ni mwanamke mwenye
mapenzi ya kweli kwako bali
anahisi hatia moyoni mwake kwa
haya yaliyokufika.Maisha yake ni
mazuri siku hizi kwani anatembea
na waziri mkuu mstaafu David
Sichoma” Taarifa ile ikamstua sana
Steven
“Samira wangu ni kimada wa
waziri mkuu mstaafu? akauliza
“Ndiyo maana nakushauri
ndugu yangu uachane kabisa na
Samira atakuweka katika matatizo
makubwa.Mtu aliye naye sasa ni
kigogo mkubwa japokuwa hayuko
katika madaraka lakini bado ana
nguvu ya kuweza kukufanya
chochote.Wanawake ni wengi sana
katika hii dunia na ukitulia
ukamuomba Mungu utampata
mwanamke bora kabisa kuliko
wote ambaye atakufaa katika
maisha yako na si hawa wapenda
pesa kama Samira” akasema Ben.Steven akainamisha kichwa
akatafakari kidogo na kusema
“Usemayo ni ya kweli kabisa
Ben lakini ninampenda Samira na
nitapambana na yeyote hadi
nimpate.Naomba namba yake ya
simu tafadhali” akasema Steven na
Ben akampa namba ya Samira
“Ahsante sana Ben.Hilo
lilikuwa ni la kwanza.La pili kubwa
lililonileta kwako ni kuomba
msaada wako.Nimetolewa
kifungoni kwa ajili ya kusaidia
katika operesheni fulani muhimu
sana.Mtu aliyesaidia nikatoka
amewaacha watu wengine wote na
akanichagua mimi kwa kuwa
ananiamini sana na mimi nahitaji kumuonyesha kwamba hakukosea
kunichagua”
“Huna hata muda wa
kupumzika?Ben akauliza
“hakuna muda wa kupumzika
kaka.Sisi nikazi kazi”akajibu Steve
“Ni operesheni gani hiyo? You
want to kill someone? Ben akauliza
“It is more than killing”
akajibu Steven na kupiga funda la
mvinyo
“Kuna mtu anahitaji kughushi
kifo”
Kauli ile ya Steven ikamfanya
Ben atoe kicheko
“Anataka kughushi kifo?
Akauliza
“C’mon Ben mbona unajifanya
huyafahamu mambo haya? Nimekuwa nikiyaona mambo
haya yakifanyika sana katika
filamu na sikuota kama siku moja
nitasikia kwa masikio yangu mtu
akighushi kifo chake mwenyewe”
“Iko hivi” akasema Steve
“Huyo jamaa ni mwenzangu
tunafanya naye kazi na ndiye
aliyenitoa kifungoni.Kuna jambo
amelinusa mahala na baada ya
kugundulika anatafutwa auawe
hivyo ili aweze kulishughulikia
kikamilifu hilo jambo anatakiwa
aghushi kifo chake ili wale jamaa
wanaotaka kumuua waamini
kwamba amekufa na waendelee na
mambo yao.Hili ni jambo zito na
ndiyo maana nimekuja hapa
kwako kuomba msaada wako.Wewe ni ndugu yangu na
huwezi kunitupa naamini
utanisaidia” akasema Steven.Ben
akafikiri kwa muda na kuuliza
“Unahitaji nikusaidie nini
Steven?
Steven akatumia nafasi hiyo
kumueleza Ben kila kitu namna
mpango wote utakavyokuwa
“Kwa hiyo Ben nimekuja
kwako kuomba msaada.Wewe ni
mhandisi nataka utusaidie
kuandaa kaburi atakamozikwa
Elvis.Kwa upande wa jeneza yupo
mtaalamu wetu anashughulikia na
mpaka jioni ya leo litakuwa
tayari.Litakuwa ni jeneza la aina
yake ambalo litawekwa kifaa
maalum ndani yake kumuwezesha Elvis kupata hewa hata pale
litakapokuwa limefungwa.Kwa
upande wako kuna aina ya kaburi
tunalotaka ututengenezee ambalo
litaruhusu hewa kuingia ndani
kwa muda mfupi ambao Elvis
atakaa humo kaburini”
“Huu ni mpango wa wa hatari
kubwa.Sikujua kama kazi zenu
kuna nyakati zinakuwa za hatari
namna hii.Ni vipi endapo kuna
jambo litakosewa na kupelekea
kifo cha huyo jamaa? Ninaogopa
sana”
“Usiogope Ben.Kila kitu
kinafanyika kitaalamu sana na hii
si mara ya kwanza kwa jambo
kama hili kufanyika.Endapo
kutatokea la kutokea basi ni ajali kazini lakini kwa namna suala
lenyewe lilivyoandaliwa tuna
uhakika tutafanikiwa.Tafadhali
sana Ben naomba unisaidie jambo
hili.Tunahitaji sana mtu wa
kutujengea kaburi lakini tunahitaji
mtu ambaye ataitunza siri.Kiasi
chochote cha fedha utakachohitaji
utalipwa.Jambo kama hili ni la siri
kubwa na hatuwezi tukamueleza
mtu yeyote lakini wewe ni zaidi ya
ndugu na ndiyo maana
nimekueleza kwa kuwa
ninakuamini sana na ninaamini
siri yetu itakuwa salama” akasema
Steven.Ben akafikiri kidogo na
kusema Umesema mnaye mtaalamu
wenu ambaye ameandaa mpango
huu?
“Ndiyo tunaye Dr Philip.Yeye
ni daktari lakini ni jasusi pia”
“Nitahitaji kumuona huyo Dr
Philip ili nizungumze naye
masuala ya kitaalamu kuhusiana
na jambo hili”
“Ahsante sana Ben” akasema
Steven kwa furaha
“Nisubiri nijiandae halafu
tuongozane wote tukaonane na Dr
Philip” akasema Ben akaelekea
ndani na kujiandaa halafu akatoka
wakaingia katika gari la Steven na
kuondoka
“Mambo yako mazuri siku
hizi” akasema Steven wakiwa garini.Ben akatabasamu na
kusema
“Siwezi kukataa Steven.Ni
kweli mambo yangu yanakwenda
vizuri.Kampuni yangu ya ujenzi
imepanuka sana siku hizi na
ninapata kazi nyingi hadi nje ya
nchi.Nimewekeza pia katika
miradi mingine mikubwa.Kwa
ujumla mambo ni mazuri.Vipi
wewe una mpango gani kuhusu
maisha yako baada ya kutoka
kifungoni?Bado unataka
kuendelea na kazi yako ya awali?
“Mpaka sasa bado sijafanya
maamuzi yoyote kuhusu maisha
yangu ya usoni.Baada ya
operesheni hii kumalizika nitajua
nini cha kufanya” Steven sikushauri uendele na
kazi hizi za hatari.Ona matatizo
yaliyokupata na kusababisha
mwelekeo mzima wa maisha yako
kuharibika.Mimi nitakupa mtaji
wa biashara na utaweza
kuyabadili maisha yako ndani ya
kipindi kifupi sana.Nataka
uyafurahie maisha ndugu yangu”
akasema Ben
“Ahsante Ben kwa wema wako
na kwa kujitoa kutaka kunisaidia
lakini siwezi kukupa jibu kwa sasa
kuhusu nini ninakipanga kwa
maisha yangu hadi pale
nitakapotafakari kwa kina .Ninalo
deni kwa Elvis na baada ya hapo
nitaamua maisha yangu yawaje”
akasema StevenMuda wowote utakapofanya
maamuzi utanijulisha,mimi niko
tayari kukusaidia”
“Ahsante sana” akajibu Steven
Walifika katika duka
yanakouzwa majeneza ambako
walipanga kukutana na Dr
Philip.Steven akamjulisha Dk
Philip kwamba tayari wamekwisha
fika mahala walikopanga
wakutane na hazikupita dakika
kumi Dr Philip naye akatokea
akiwa na gari aina ya Noah.Steven
akamtambulisha Ben kwa Dr
Philip na wote wakaingia ndani ya
jengo lile wakaanza kuzunguka
kutafuta jeneza ambalo lingefaa
kwa shughuli yao.Hatimaye Dr
Philip akafanikiwa kupata aina ya jeneza alilokuwa analitafuta
akalipa wakalipakia garini na
moja kwa moja wakaelekea
nyumbani kwa Elvis ambako ndiko
shughuli yote ya uandaaji wa
jeneza ilikuwa inafanyika.Jeneza
likashushwa na kuingiza
ndani.Haraka haraka Doreen
akamchukua Graca ambaye
alipatwa na mtuko baada ya
kuliona jeneza lile likiingia
sebuleni na kumpeleka chumbani
kwake
“Graca unapaswa kuwa jasiri
sana hasa katika kipindi hiki.Hili si
jambo jepesi kwa Elvis kulifanya
lakini amejitolea kulifanya kwa
ajili ya kuokoa maisha ya ndugu
zetu wanaouawa bila hatia huko Congo.Ni watu wachache sana
wanaoweza kufanya jambo kama
hili kwa ajili ya watu wengine
hivyo anachohitaji Elvis ni
ushirikiano wetu.Tumpe
nguvu.Tusimame naye katika
wakati huu mgumu kwake”
akasema Doreen
“Dada Doreen ninaogopa sana
kwa hiki anachotaka kukifanya
Elvis.Ni vipi endapo watakosea
na……..” Graca akashindwa
kuongea akainamisha kichwa
“Naifahamu hofu yako Graca
kwamba endapo kuna jambo
halitakwenda sawa Elvis anaweza
akapoteza maisha.Nikutoe hofu
kwamba wale watu anaoshirikiana
nao wamebobea katika mambo haya na hawawezi
kukosea.Nakuomba usionyeshe
mbele ya Elvis kwamba una
hofu.Muda wote jitahidi
kutabasamu na onyesha
kumuunga mkono na hiyo itampa
nguvu sana.Tumeelewana Graca?
Akauliza Doreen
“Ndiyo dada” akajibu Graca
“Good.Endelea kupumzika
humu chumbani hadi
watakapomaliza mambo yao”
akasema Doreen na kutoka mle
chumbani akasimama mlangoni na
kushika kiuno
“Najaribu kumpa moyo Graca
wakati mimi mwenyewe miguu
yote imeisha nguvu.Nimeingiwa na
woga mkubwa sana baada ya kuliona lile jeneza.Nahisi kama
vile Elvis hataamka tena akiingia
ndani ya lile jeneza.Sijawahi kuwa
na wakati mgumu kama huu katika
maisha yangu.Tunachopaswa
kukifanya ni kumuomba Mungu
atusaidie jambo hili limalizike kwa
salama na Elvis awe mzima kwani
sijui nini kitatokea endapo Elvis
atapoteza maisha.Nimetokea
kumpenda mno Elvis kuliko
nilivyokuwa nikimpenda awali na
kwa sasa tayari amekwisha tua
katika mikono yangu siwezi tena
kumuacha akaondoka” akawaza
Doreen na kuelekea jikoni na
kuwaandalia wageni chai.
“Ahsante sana Doreen kwa
ukarimu wako.Mungu akubariki wewe na uzao wako” akasema
Steven na uso wa Doreen ukajenga
tabasamu pana,hakujibu kitu
akaondoka.Elvis akawaacha akina
Steven wakiendelea kupata chai
akamfuata Doreen chumbani
kwake na kumkuta amejikunyata
kitandani
“Elvis nimeogopa sana baada
ya kuliona lile jeneza.Hapa nilipo
mwili wote unanitetemeka kwa
ndani” akasema Doreen
“Nilimuona Graca alipatwa na
mstuko mkubwa
pia.Anaendeleaje? Umejaribu
kumtuliza?
“Ndiyo nimejitahidi kumtuliza
ila bado ana wasiwasi mwingi
sana” Tafadhali nawaomba msihofu
hata kidogo.Hakuna tatizo lolote
litakalotokea.I’ll be fine” akasema
Elvis
“Nalifahamu hilo Elvis lakini
hili ni jambo gumu sana kwetu”
“Tuachane na hayo.Kuna
jambo ambalo nataka ulifanye kwa
siku ya leo.Nataka uende kwenye
msiba ukawe karibu na
Patricia.Yule ni rafiki yako
mkubwa sana na unapaswa kuwa
naye karibu mno kwa wakati
huu.Usiondoke pale hadi pale
msiba utakapomalizika.Ukiwa pale
jaribu kuwa makini katika
kuangalia namna mambo
yanavyokwenda na ukiona kuna
jambo lolote ambalo si la kawaidia nitakupa namba za Steven au
Meshack Jumbo yule mkurugenzi
wangu utamjulisha mmoja wao
mara moja.Baada ya mazishi
kumalizika ndipo utakaporejea
hapa.Jitahidi sana kumpa moyo
Patricia lakini kwa namna yoyote
ile usithubutu kumueleza kwamba
niko hai.Utaharibu kila kitu kfanya
hivyo” akasema Elvis na kurejea
sebuleni kuungana na wenzake
wakaanza kujadiliana kuhusiana
na namna kaburi
litakavyokuwa.Yalikuwa ni
majadiliano ya kina na ya
kitaalamu sana mwishowe
wakakubaliana namna kaburi
litakavyokuwa.Ben na Steven
wakaondoka kwenda kuanza maandalizi ya kaburi.Dr Philip na
Elvis wakaanza kuandaa
jeneza.Elvis akalitazama jeneza lile
akavuta pumzi ndefu na taratibu
akaingia ndani yake akajilaza.Dr
Philip akachukua vipimo
alivyovihitaji na kumtaka Elvis
atoke.Uso ulikuwa umeloa
jasho.Dr Philip akampiga piga
mgongoni
“Relax Elvis .You’ll be
fine.You’ll visit hell for few hours
and come back to earth” akatania
Dr Philip.
“Dr Philip this is not a joke”
akasema Elvis akionekana
kutokuyafurahia maneno yale ya
Dr Philip “I’m sorry brother.Najaribu
kutafuta namna ya kukufanya
ufurahi utabasamu kwani sura
yako inaonyesha uoga ndani yake”
“Philip hili si suala rahisi
kwangu hata kidogo.Ninajitahidi
sana kulifanya liwe la kawaida
lakini inaniwia ugumu.Ukibahatika
kufika eneo la msiba na kuona
namna watu walivyoumizwa na
kifo changu,namna wanavyolia na
wengine kupoteza fahamu utaona
ukubwa wa jambo hili.Sikuwahi
kuhisi kama siku moja ningeweza
kufanya jambo kubwa kama
hili.Kuwadanganya watu
ninaowapenda kuwa
nimekufa.Uchungu alionao mke
wangu Patricia hivi sasa hakuna anayeweza
kuuelezea.Nimemsababishia
donda kubwa ambalo haliwezi
kupona.Unadhani itakuaje pale
atakapofahamu kuwa nilitunga
uongo huu mkubwa? Maisha yangu
tayari yameharibika I’ll never be
the same Elvis.I’m dead! Akasema
Elvis kwa uchungu
“Elvis” akasema Dr Philip na
Elvis akainua kichwa akamtazama
“Nafahamu hili si jambo
dogo,kuna athari nyingi sana
zitakazosababishwa na jambo
hili.Maisha yako tayari
yamebadilika na hayatakluwa
kama awali.Katika vinywa vya
watu jina lako limebadilika na sasa
unaitwa marehemu Elvis.Lakini pamoja na haya yote bado
nasimama na kukwambia kwamba
umefanya jambo sahihi na kwa
wakati sahihi.Hakuna namna
tunayoweza kuwasaidia ndugu
zetu wanaoteseka na kuuawa kila
uchao huko Congo bila wewe kufa
kwanza.Ni wewe ambaye Mungu
amekuelekeza macho yako na
ukalifahamu jambo hili lililojificha
kwa hiyo ni wakati wako wa
kumaliza taabu na mateso
wanayoyapata watu wake huko
Congo.Ndugu jamaa na marafiki na
hata mkeo wanaweza wasikuelewe
kwa nini umefanya hivi lakini tupo
watu wachache tunaelewa uzito wa
jambo hili na tutasimama nawe
katika jambo hili hadi mwisho.Naomba usiangalie sana
athari bali angalia zaidi faida
zitakazopatikana kwa kuufyeka
mtandao huu wa kuuza silaha kwa
waasi wanaoua watu.Utaokoa
maisha ya watu wengi unaweza
kuwa chanzo cha kupatikana kwa
amani ya kudumu Congo pale
waasi watakapokosa silaha na
kushindwa kuendeleza
mapambano na serikali.Elvis wewe
ni mtu muhimu sana na hupaswi
kujilaumu kwa hili unalotaka
kulifanya” akasema Dr
Philip.Maneno yale yalionyesha
kumuingia Elvis.
“Dr Philip sijilaumu wala
kujutia hiki nilichokifanya lakini
kuna mtu mmoja anayeniumiza sana ambaye ni mke wangu
Patricia.Mwanamke huyu
hakupaswa kuumizwa kiasi
hiki.Sikupaswa kumuumiza na
niliapa kutokufanya hivyo.Mimi na
yeye tuna historia ndefu hata hivyo
naanza kuhisi kwamba huu
utakuwa ni mwisho wetu”
akasema Elvis na kuinama
akatafakari
“Dr Philip endelea na kazi
yako mimi najipumzisha ndani”
akasema Elvis na kuinuka akaenda
chumbani kupumzika
“Patricia ananiumiza mno
moyo wangu.Sijui atakuwa katika
hali gani hivi sasa.Sifahamu atalia
kilio gani.Sifahamu itachukua
miaka mingapi machozi kumkauka.Mimi ndiye niliyekuwa
kila kitu kwake.Mimi ndiye baba
na mama yake.Mimi ndiye nguzo
yake,mlinzi wake ,furaha
yake.Sipati picha namna
atakavyonyanyaswa na ndugu
zangu kwa kuwa tu mimi na yeye
hatujabahatika kuwa na
mtoto.Mali zote tulizochuma naye
watazinyang’anya na kumuacha
hana kitu.Kama waliweza
kumnyanyapaa wakati niko
hai,tena wakiongozwa na mama
yangu mzazi,nini kitatokea wakati
sipo? Hili jambo linaniumiza
sana..” akaendelea kuwaza.
“Kuna swali lingine ambalo
bado sijalipatia jibu kwamba
baada ya operesheni kukamilika nini kitatokea?Nitajitokeza na
kudai kwamba sikuwa
nimekufa?Hapana! Hakuna
atakayenielewa na……” Elvis
akatolewa mawazoni na mlango
uliogongwa akainuka akaenda
kuufungua na kukutana na Graca
“Graca ! akasema Elvis
akionekana kushangazwa na
mwonekano alionao Graca
“Nini kimetokea? Unaumwa ?
“Sina tatizo Elvis bali ni
mstuko nilioupata baada ya
kuliona jeneza likiingizwa ndani”
akasema Graca huku akilengwa na
machozi
“C’mon Graca tafadhali
usiumizwe na jambo
hili.Nimekwisha kueleza kwamba I’ll be fine.Nitakaa ndani ya jeneza
lile kwa saa chache tu kisha
nitatoka na nitarejea”
“Hakuna namna nyingine ya
kulitatua jambo hili zaidi ya
kufanya hivi unavyotaka kufanya?
“Kwa ajili ya kuusafisha
mtandao wa baba yako,hakuna
namna nyingine ya kufanya.Tayari
wamekwisha fahamu kwamba
nimewagundua na ninawafuatilia
hivyo wanataka nife ili waweze
kufanya mambo yao kwa
uhuru.Hivyo basi ili kuwakabili
inabidi kuwapa kwanza uhuru wa
kufanya mambo na uhuru huo
wataupata pale nitakapokuwa
nimekufa.Hawatakuwa tena na
hofu kwamba kuna mtu anawafuatilia na hiyo itanipa mimi
na wenzangu fursa nzuri ya
kuufahamu mtandao wao wote na
kuufagia kabisa.Kwa hiyo Graca
hiyo ndiyo njia pekee ya
kufanya.Nakuhakikishia kwa mara
nyingine tena kwamba nitakuwa
salama.Nafahamu hofu yako ni
kuhusu usalama na hatima ya
maisha yako endapo nitakuwa
nimepoteza maisha.Nakuomba
usiwe na hofu hata kidogo kwani
hata kama nikipoteza maisha
katika jambo hili wapo watu
ambao watakuangalia na
kuhakikisha unakuwa salama”
akasema Elvis.Graca akamtazama
kwa sekunde kadhaa na kusema
“Elvis can…ca..can I hug you?
 
Jaman mumuonee huruma kwanza kachepuka maramoja tu tena alikuwa na stress
Kwangu mm tokea alipompa nyuchi yule mwana godson kwa mazingira yale tu nilijua ni vile videmu ukivibana kwny kona tu havinaga ujanja wa kukubania
 
Back
Top Bottom