Riwaya: I died to save my President

Riwaya: I died to save my President

Mkuu Kulubule, huruma yako tafadhali, Tumosa hayupo Leo, na hivi weekend imeanza.
 
I DIED TO SAVE PRESIDANT

Season 7

Sehemu 62

Usiogope Graca nimekwisha
kuahidi kukupa kila
unachokihitaji.Nimekudhihirishia hilo
mchana wa leo na tutaendelea
kufurahi kila siku kila pale
utakapohitaji" akasema Elvis
"Ahsante sana Elvis.Ninakupenda
mno zaidi ya ninavyoweza
kukueleza.Naomba usiuvunje moyo
wangu" akasema Graca na kumbusu
Elvis
"It's time.Jiandae tuondoke"
akasema Elvis
Dakika tano baadae wote
walikuwa tayari na safari ikaanza.Ni
Graca pekee aliyefahamu mahala
walikokuwa wanaelekea


ENDELEA..............................Obi una hakika hakuna yeyote
aliyekuwa anamfuatilia huyu
msichana wakati unamleta hapa?
akauliza Frank baada ya kuwasili
mahala alipomuelekeza Obi ampeleke
Winnie
"Hakuna mkuu.Nimekuwa
makini sana kuhakikiha hakuna
yeyote anayemfuatilia.Nimechukua
kila aina ya tahadhari kabla ya kufika
hapa na kujiridhisha kuwa hakuna
hatari yoyote"akasema Obi
"Unamuonaje huyu msichana?
Anasema ukweli au ametumwa kama
mtego?kwa sababu simuamini tena
Vicky" akasema Frank
"Kwa namna nilivyomchunguza
anaonekana kweli ana shida ya
kuonana nawe.Sina hakika sana kama
ametumwa" akasema Obi "Kabla sijaenda kuzungumza
naye nataka ukahakikishe kwamba
hana kifaa chochote cha kuweza
kunasa au kurusha maongezi yangu
naye.Siku hizi teknolojia imekua
kubwa, nina wasi wasi yawezekana
amefungwa kifaa maalum cha kunasa
mazungumzo yetu.Nenda
kamchunguze umuhakiki kama hana
kifaa chochote.Hata simu yake pia
ichukue na uizime kabisa hadi
nitakapomaliza mazungumzo naye"
akasema Frank na Obi akarejea
sebuleni aliko Winnie.
"Frank yuko wapi? akauliza
Winnie
"Inuka! akaamuru Obi
"Unataka kunipeleka wapi?
akauliza Winnie
"Stand up!! akasema Obi kwa
ukali na Winnie akasimama na Obi
akaanza kumpapasa kuona kama kuna kifaa chochote amekivaa kinachoweza
kunasa maongezi yake na
Frank.Winnie hakupendezwa na
kitendo kile akamsukuma Obi
"Sikiliza we msichana,ukitaka
mambo yako yafanikiwe usiwe na
kiburi.Niache nifanye kazi yangu ama
sivyo hautapata unachokitaka"
akasema Obi na kuendelea kumkagua
Winnie.Alipohakikisha hakuna kifaa
chochote alichokuwa nacho
akaichukua simu yake halafu
akamfuata Frank
"She's clean.Hana kitu chochote
kibaya na simu yake hii hapa
nimeichukua" akasema Obi na
kumkabidhi Frank simu ya Winnie
"Thanks.Hakikisha eneo hili ni
salama wakati ninakwenda
kuzungumza na huyu msichana"
akasema Frank na kuingia
ndani.Winnie alipomuona Frank akiingia mle ndani akaogopa na
kusimama
"Winfrida tafadhali keti"
akasema Frank
"Shikamoo" akasema Winnie kwa
uoga
"Marahaba.Hujambo Winnie?
"Sijambo"
"Winnie nina mambo mengi ya
kufanya hivyo fanya haraka nieleze
kile unachotaka kunieleza" akasema
Frank
"Wewe ndiye Frank?
"Ndiye mimi.Una wasi wasi?
"Hapana umefanana na mwanao
Graca"
"Haya nieleze kilichokuleta hapa"
akasema Frank ambaye alionekana
kutokutaka mazungumzo marefu
"Mzee kama nilivyojitambulisha
simuni kuwa ninaitwa Winnie mimi ni
mdogo wake Vicky.Nimelazimika kuja kukuona kwa ajili ya kuzungumza
nawe mambo mawili makubwa"
akanyamaza akamtazama Frank
aliyekuwa amemkazia macho
akimtazama kwa makini sana halafu
akaendelea
"Jambo la kwanza ni kuhusiana
na dada yangu Vicky.Kabla sijasema
lolote nataka kufahamu kitu
kimoja.Huyu jamaa aliyenileta hapa
alituvamia asubuhi nyumbani,wewe
ndiye uliyemtuma?
Frank akatabasamu kidogo
halafu akasema
"Winnie tafadhali naomba
usipoteze wakati wangu.Nieleze kile
ambacho umeniitia hapa.Huruhusiwi
kuuliza chochote! akasema Frank
aliyeonekana kukasirishwa na swali
lile la Winnie
"Samahani mzee.Kitu cha kwanza
ambacho kimenileta hapa ni kuhusiana na dada yangu
Vicky.Amenieleza kwamba
unamtafuta umuue na baada ya
kumuona huyu jamaa aliyetuvamia
asubuhi yuko hapa ninaamini ni kweli
unamtafuta dada umuue.Kwa nini
unataka kumuua dada yangu?akauliza
Winnie
"Nani kakwambia ninamtafuta
dada yako? Frank akauliza
"Dada mwenyewe amenieleza
hivyo"
"Amekudanganya.Vicky ni rafiki
na mtu wangu wa karibu sana kwa
nini nimtafute au nitume mtu
akamteke? akauliza Frank
"Kwa nini hutaki kunileza ukweli
Frank?Ninafahamu kila kitu
kinachoendelea kati yako na dada na
ndiyo maana niko hapa kutafuta
suluhu" akasema Winnie na Frank
akatabasamu Nimeupenda ujasiri wako.Nini
unakifahamu kuhusu mimi na dada
yako?
"Everything" akajibu Winnie na
Frank akavuta pumzi ndefu
"Ok tell me everything you know"
akasema Frank
"Nitakwambia kila kitu ila na
mimi kuna sharti moja nataka
litekelezwe"
"Winnie nadhani haufahamu
unazungumza na nani.Unazungumza
na mtu mkubwa na si mwanafunzi
mwenzako hivyo jaribu kuwa na
adabu na ueleze kile kilichokuleta
hapa.Wewe si wa kunipa mimi sharti
lolote.Dada yako mwenyewe
ananifahamu vyema mimi ni nani na
ananiheshimu.Nakupa nafasi ya
mwisho uweze kueleza kile
kilichokuleta hapa"akasema Frank Frank nimesema hivyo kwa
sababu ninayo mambo ambayo
hutaamini nikikueleza na ambayo
yatakuwa na msaada mkubwa sana
kwako.Siwezi kukueleza mambo hayo
muhimu bila na mimi kutimiziwa kile
ninachokitaka"
"Unahitaji nini? akauliza Frank
baada ya kufikiri kidogo
"Ninahitaji umuache dada
yangu.Acha kumfuata na umuache
afanye shughuli zake kwa amani.Leave
her alone! akasema Winnie na Frank
akaangua kicheko
"Umenifanya nicheke Winnie ila
naomba nikufahamishe kitu
kimoja"akanyamaza na kumtazama
"Vicky ni rafiki yangu na mtu
wangu wa karibu sana lakini kuna
jambo amelifanya ambalo limeniudhi
na kunifanya nimsake kila kona ili
anieleze kwa nini amefanya vile,hivyo basi siwezi kumuacha hivi hivi hadi
atakaponieleza ukweli"akasema Frank
"Nafahamu unachomtafutia dada
ni kuhusiana na kifo cha Pascal"
akasema Winnie na Frank
akamtazama kwa makini akashindwa
aseme nini.Baada ya muda akauliza
"Unamfahamu
Pascal?Umefahamuje kuhusu kifo
chake?
"Nilikwambia kwamba nina
fahamu kila kitu hivyo tulia
nisikilize"akasema Winnie na
kunyamaza kidogo kisha akaendelea
"Unamuhusisha dada na kifo cha
Pascal.Ni kweli yeye ndiye aliyemuita
pale hotelini"akanyamaza tena na
kumtazama Frank ambaye alikaa
vizuri ili kumsikiliza Winnie kwa
makini
"Endelea Winnie" akasema Frank "Dada hakufanya vile kwa
kupenda bali alilazimishwa kufanya
vile.Alitekwa na watu fulani ambao
walimlazimisha afanye wanavyotaka
na kama angekataa basi
wangenidhuru mimi.Nadhani
unafahamu kuwa dada anajihusisha
na mambo ya ukahaba hivyo mmoja
wa watu hao alijifanya kumtaka
kimapenzi na ndipo walipomteka na
kumlazimisha amuite Pascal pale
hotelini.Kwa kutumia simu ya dada
walinipigia simu na kunidanganya
kuwa dada amepata ajali na anahitaji
kuniona nikawaelekeza nyumbani
mahala nilipo akaja mmoja wao
kunichukua na kumbe hakukuwa na
ajali yoyote aliyoipata dada bali
walitaka kunitumia kumlazimisha
dada afanye vile watakavyo.Kwa kuwa
dada yangu ananipenda sana hakuwa
na na njia nyingine zaidi ya kukubali matakwa ya wale jamaa ambao kitu
kikubwa walichokuwa wanakihitaji ni
kumpata Pascal.Walifahamu kuwa
Pascal na dada ni marafiki hivyo
wakamtaka dada ampigie simu na
kumtaka afike pale hotelini na dada
akafanya hivyo akawasiliana na Pascal
na kumtaka afike pale hotelini"
akanyamaza na kumtazama tena
Frank halafu akaendelea
"Pascal alifika pale hotelini na
wakafanikiwa kumuweka chini ya
ulinzi lakini kabla hawajamfanya
chochote dada akataka kupambana
nao wale jamaa na Pascal naye
akaitumia nafasi hiyo kupambana nao
lakini wakawazidi nguvu na katika
mapambano hayo Pascal akapigwa
risasi akafa.Tukachukuliwa mimi na
dada na kupelekwa sehemu fulani
wakaanza kumtesa dada wakimtaka
awaeleze mahala ulipo.Dada aligoma kusema chochote na ndipo wakatisihia
kunitesa endapo hatawaeleza.Bado
dada alikuwa mgumu kuwaeleza
chochote na ndipo walipoanza
kunitesa ili kumlazmisha dada afanye
wanavyotaka.Walinitesa sana kwa
kunichoma na umeme na walipoona
bado dada amekuwa mgumu
wakataka kuanza kunibandua kucha
za vidole ndipo dada akawaomba
wasifanye hivyo atawaeleza
wanachokitaka.Akawadanganya
kwamba atawasaidia ili waweze
kukupata.Akawaeleza kuwa anayo
namba maalum ambayo huwa
anawasiliana nawe na ambayo iko
chumbani kwake na kulipopambazuka
wakatupeleka nyumbani.Dada akiwa
katika harakati za kutafuta namna ya
kutoroka akatuvamia yule jamaa
ambaye naamini ulimtuma na hapo
yakatokea ,mapigano kati yake na m,moja wa wale jamaa anayeitwa
Steve na mtu wako aliposhindwa
akakimbia.Steve akaturejesha tena
kule katika nyumba yao na dada
akawaahidi kwamba atawapeleka
mahala ambako anaamini watakupata
na usiku huu wamemchukua kuelekea
huko.Kwa bahati nzuri walisahau
kufunga mlango na mimi nikatoroka"
akasema Winnie na Frank akavuta
pumzi ndefu akamtazama Winnie kwa
macho makali yaliyojaa hasira
"Nani amekutuma uje unieleze
mambo haya?! akauliza kwa ukali
"Nimekwisha kueleza kwamba
hakuna mtu yeyote aliyenituma bali
nimekuja mimi mwenyewe ili
kutafuta msaada kwa dada
yangu.Frank,dada yangu hana kosa
alitumiwa na hawa jamaa ili kumpata
Pascal na kwa sasa wamegeuka
wanakutafuta wewe.Hivi tuongeavyo wameelekea mahala ambako dada
amewapeleka ambako wanaamini
watakupata.Nimekuja kukueleza haya
yote ili kutafuta msaada.Kwanza
kumukoa dada yagu kutoka katika
mikono ya wale jamaa na pili
kuhakikisha wale jamaa
wanapatikana"
"Who are they? Unaweza
kuwaelezea muonekano wao?
"Watu hao wako wawili tu na
majina yao ni Steve na Elvis"
Mstuko alioupata Frank ulikuwa
mkubwa sana.Alihisi mwili
ukimtetemeka
"Rudia tena umesema majina yao
ni akina nani?
"Mmoja anaitwa Steve.Huyu
ndiye aliyekuja kunichukua
nyumbani.Mwingine anaitwa Elvis na
huyu ndiye aliyekuwa ananitesa
akimlazmisha dada afanye wanachokitaka.Ni mtu mkatili sana"
akasema Winnie
"No! it's not true.Haweze kuwa ni
Elvis yule ambaye tulimuua.Huyu
atakuwa ni Elvis mwingine kabisa"
akawaza Frank
"Frank" akaita Winnie baada ya
kumuona Frank amebadilika ghafla
"Ninahitaji sana msaada wako
kumuokoa dada kutoka katika mikono
ya wale jamaa ambao hawana mpango
wa kumuachia huru.Wataendelea
kumtumia ili kufanikisha mipango yao
mbali mbali na mwisho watamuua"
"Nni hasa ambacho hawa jamaa
wanakitafuta?Unaweza kufahamu ?
"Nilivyowasikia wale jamaa
walikuwa wanaongelea masuala ya
silaha lakini sikujua ni silaha zipi hizo
ila inaonekana wanachokitafuta ni
kuhusiana na masuala hayo ya
silaha.Kwa sasa wameelekeza nguvu zao katika kukusaka wewe" akasema
Winnie na kuzidi kumstua Frank
"Oh my God! akasema Frank kwa
sauti ndogo
"Winnie una uhakika mtu huyo
ambaye alikutesa anaitwa Elvis?
"Ndiyo anaitwa Elvis" akasema
Winnie na Frank akainuka na kuanza
kuzunguka zunguka mle sebuleni
akiwa ameinamisha kichwa chake
alionekana kuzama katika mawazo
mazito
"Najaribu kutaka kumuamini
huyu sichana lakini ninashindwa
kwani Elvis ni mfu.Tayari tumemzika
na hakuna namna yoyote anayoweza
kurudi.Lakini swali lingine ni je kama
Winnie hasemi kweli amefahamuje
masuala haya ya silaha?Hata Vicky
mwenyewe hafahamu chochote
kuhusiana na masuala ya biashara ya
silaha.Mtu pekee ambaye aligundua kuhusu biasharaya silaha ni Elvis
ambaye amekwisha fariki hawa
wengine ni akina nani ambao
wanaanza kunifuatilia?Yawezekana
wakawa ni washirika wa Elvis?I'm
confused na sijui niamini kipi"
akawaza Frank akionekana kweli
kuchanganyikiwa.Akamtazama
Winnie na kuuliza
"Kwenye simu ulisema
unamfahamu
Graca?Umemfahamuje?Unafahamu
mahala aliko?
"Ndiyo ninafahamu mahala aliko
Graca.Yuko na hawa jamaa wawili
anaishi nao ndani ya nyumba
yao.Nilimkuta humo na akanieleza
historia yake yote.Amenieleza kila kitu
kilichomtokea mateso uliyompatia
ukimtaka arejeshe begi lenye
kompyuta yako ambayo iliibwa ofisini
kwako.Kwa ujumla amenieleza kilakitu hadi alivyokutana na Elvis afrika
kusini akamtoa katika hospitali ya
magonjwa ya akili na hadi walivyofika
hapa Tanzania.Amenieleza mambo
mengi sana kuhusu yeye na hata
matarajio ya maisha yake.Ameahidiwa
mambo mengi na Elvis.Kingine cha
kusikitisha zaidi ni kwamba Elvis na
Graca wana mahusiano ya
kimapenzi.Graca anaishi ndani ya
nyumba ile kama mtumwa wa ngono"
Frank alipandwa na hasira kali
baada ya maelezo yale ya Winnie na
kuibinua meza.Winnie akaogopa na
kutetemeka baada ya Frank
kumsogelea.Macho yake yaliwaka
hasira
"Winnie haya unayonieleza
hakikisha ni ya kweli kwani endapo
unanieleza uongo naapa nitakukata
kichwa.Nitazame vizuri machoni mimi sina huruma hata kidogo kwa yeyote
anayenidanganya!! akasema Frank
"Frank nakueleza mambo ya
kweli kabisa na si uongo" akasema
Winnie na Frank akavuta pumzi ndefu
haraka haraka
"Nisikilize!! akasema
"Huyo Graca ni mwanangu lakini
amenifanyia mambo mabaya sana
yeye na mama yake kiasi kwamba
ninajuta kuwa na mtoto kama
yeye.Simuhesabu kama mwanangu
bali kama adui yangu kwa mambo
aliyonifanyia endapo nitampata
adhabu yake ni kifo! Kama una hakika
kweli umemuona nipeleka mahala
hapo alipo ninamuhitaji sana huyu
mtoto!! akasema Frank kwa hasira
akionekana kuchanganyikiwa
"Frank sikudanganyi.Ni kweli
Graca yupo nimemuona na ninaweza
kukupeleka mahala alipo.Unapaswa kumuondoa kutoka katika jumba lile
kwani wale jamaa si watu wazuri hata
kidogo.Mambo wanayomfanyia si
mazuri.Graca bado ni mwanao na
unapaswa kumsaidia japo
amekukosea..
"No!! Frank akamkatisha Winnie
"Graca siwezi kumsamehe hata
kidogo.Aliwahi kuwa mwanangu
lakini kwa sasa ni adui yangu,tena
adui mkubwa na nitamfanya kama vile
ninavyowafanya maadui zangu,I kill
them!! akasema Frank kwa hasira na
mara akahisi kama miguu inaisha
nguvu akaketi sofani na kuinamisha
kichwa
"Elvis !! akasema kwa sauti
ndogo
"Graca alitoroshwa hospitali na
Elvis na akampatia kompyuta yangu
na Elvis akafahamu kuhusu biashara
ya silaha na kuanza kutufuatilia.Tukafanikiwa kumuua na
amezikwa kaburini huyu Elvis ambaye
Winnie anamtaja ni Elvis yupi? I'm
totaly confused" akawaza Frank
"Suala hili si la kupuuzia hata
kidogo lazima nifanye uchunguzi wa
haraka sana.Kwanza ni kuhakikisha
ninampata Vicky yeye ndiye
atakayeweza kunipa majibu ya suala
hili.Anamfahamu Elvis vizuri kuliko
huyu Winnie.Yawezekana kuna mtu
amejipa jina la Elvis ili kumuenzi rafiki
yao" akawaza Frank na kumtazama
Winnie
"Winne nakushukuru sana kwa
taarifa hizi ulizonipa.Ni taarifa nyeti
mno na ambazo nilikuwa nazihitaji
sana hasa kuhusiana na Graca ambaye
sikujua ni wapi ningeweza
kumpata.Ninachokitaka ni kunipeleka
huko mahala waliko ili nikamuokoe
dada yako na Graca" akasema Frank Frank nitakupeleka huko ila
nataka kwanza unihakikishie kwamba
dada yangu atakuwa huru na
hautamfuatilia tena" akasema Winnie
"Kama nilivyokueleza Winnie
kwamba dada yako ni rafiki yangu
sana na sina atizo naye.Ni bahati
mbaya tu sikuwa nikifahamu
kilichojificha nyuma ya pazia.Maelezo
yako yamenipa picha ya nani hasa
ninayepaswa kumtafuta kuhusiana na
kifo cha Pascal hivyo sina shida tena
na Vicky.Atakuwa huru" akasema
Frank
"Nitashukuru kama ukitimiza
ahadi yako"akasema Winnie
"Mimi si mkatili hadi pale
unaponichokoza.Vicky ni rafiki yangu
and I don't hurt my friends.Naomba
tafadhali unisubiri hapa ili twende
huko mahala waliko akina Vicky"
akasema Frank Yule mtu wako alichukua simu
yangu.Naweza kuipata? akauliza
Winnie na Frank akatoa simu mfukoni
mwake akampa
"Dada yako au mtu mwngine
yeyote akikupigia simu usipokee hadi
uniulize.Umenielewa?" akasema Frank
"Nimekuelewa Frank" akasema
Winnie na Frank akatoka akamfuata
Obi
"Obi kuna kazi kubwa
imejitokeza.Nahitaji vijana sita au
kumi kwa haraka kuna kazi ya
kufanya usiku huu"
"Kazi gani mkuu? akauliza Obi
"Yule mwanamke niliyekutuma
ukamteke asubuhi tayari nimefahamu
mahala alipo.Winnie amenielekeza
mahala alipo na si yeye peke yake bali
pia mwanangu Graca naye yuko
hapo.Nahitaji kwenda kuwachukua
kutoka mahala wanaposhikiliwa" "Nani wanawashikilia?akauliza
Obi
"Winnie anasema kuna watu
wawili wanawashikilia Vicky na Graca
hivyo andaa kikosi ili tukavamie
mahala hapo na kuwachukua Vicky na
Graca haraka sana" akasema Frank
lakini Obi akaonyesha shaka kidogo na
kuuliza
"Mkuu unamuamini huyu
msichana?
"Ninamuamini.Kuna mambo
amenieleza ambayo yamenifanya
nimuamini"
"Nina wasiwasi asiwe anatumiwa
kama mtego"
"Tutajua huko huko kama
anatumiwa au vipi ila lazima
tukavamie mahala hapo na
kuwachukua akina Vicky.Tafadhali
andaa vijana wanaoweza kazi kwani
sitaki uzembe kama uliofanyika asubuhi.Safari hii hata mimi
mwenyewe nitakuwepo kuhakikisha
kila ktu kinakwenda vyema" akasema
Frank na kurejea ndani
"Ninaandaa vijana kwa ajili ya
kwenda huko aliko Vicky.Wakati
wanajiandaa nataka uniambie kuhusu
Elvis.Yukoje?akauliza Frank.Winnie
akafikiri kidogo na
"Elvis ukimtazama amefanana
sana na yule mcheza mpira wa kikapu
mahiri wa timu ya Golden state
warriors ya marekani anaitwa
Stephen Curry.He's very handsome
sipati namna ya kumuelezea vizuri ila
ukiipata pcha ya Stephe utakuwa
umepata picha halisi ya Elvis kwani
wamefanana sana" akasema Winnie
na Frank akahisi kibaridi kinapenya
mwilini mwake
"This cant be!! akasema kwa
sauti Unasemaje Frank? akauliza
Winnie na Frank hakumjibu kitu
akainuka akatoka
"Winnie anachokiongea ni cha
kweli kabisa.Elvis amefanana sana na
yule mchezaji mpira wa kikapu wa
Marekani.Lakini mbona Elvis tayari
amefariki dunia?Huyu Elvis gani
aliyejitokeza tena?Ni
mzimu?akajiuliza Frank na kusimama
akaegemea ukuta
"Siamini sana katika mambo haya
ya imani za mizimu lakini yawezekana
kuna mambo yanaongelewa yakawa
kweli kuhusu mzimu wa mtu
kurudi.Inawezekana Elvis huyo
anayeonekana sasa hivi akawa ni
mzimu umerudi kututafuta.Jibu
nitalipata usiku wa leo kama ni
binadamu au ni mzimu " akawaza na
kumfuata Obi
"Obi vijana wako tayari? Ndiyo mkuu nimepata vijana
saba na wote wako tayari.Tutawapitia
sehemu fulani.Wewe uko tayari?
"Niko tayari lakini itanilazimu
kupita kwanza nyumbani kwangu
kuchukua silaha kisha tuelekee huko
ambako naamini kutakuwa na
mapambano" akasema Frank
akamfuata Winnie na kumtaka
waondoke.
"Wale mashetani leo ndiyo
mwisho wao.Nashukuru Frank
ameniamini kwa namna picha
nilivyoipanga.Kwa sasa dada yuko
huru kwani nimemuondoa katika
sakata lile la mauaji ya Pascal na
mzigo wote nimewatupia wale
jamaa.Nina hasira nao sana na roho
yangu itakuwa na amani
nitakapowaona nao wakiteseka kwa
unyama walionifanyia.Siwezi kusahau
nilivyochomwa na umeme bila kosa lolote.Dada naye huu ni mwisho wake
kufanya kazi hizi za
upelelezi.Anatakiwa ajikite zaidi
katika biashara na kuachana na
shughuli hizi hatarishi ambazo
zinatufanya sote kuishi maisha
magumu" akawaza Winnie wakiwa
garini wakielekea nyumbani kwa
Frank kwenda kuchukua silaha
akijiandaa kuelekea kwa akina
Elvis.Bado picha ya Elvis iliendelea
kuzunguka kichwani kwake


**************

"Simu ya Winnie imezimwa"
Omola akawataarifu akina Elvis
wakiwa garini.
"Vicky mahala hapo alipo mdogo
wako unapafahamu? akauliza Elvis Hapana sipafahamu na wala
sijawahi fika"
"Sawa.Omola endelea kumfuatilia
endapo atawasha simu yake ili
tukimaliza huku tujue mahala aliko
tumfuate" akasema Elvis na safari
ikaendelea kimya kimya.Graca
aliyekuwa amekaa mbele na Steve
alikuwa akitoa maelekezo ya sehemu
ya kwenda.
"Graca una hakika na huku
tunakoelekea? akauliza Steve baada ya
kuona wanazidi kuelekea nje ya mji
"Ndiyo nina uhakika.Japo ni
muda mrefu sijafika huku lakini
napakumbuka sana"akasema Graca
"Huku ni wapi?Frank ana
nyumba huku?akauliza Elvis
"Huku ni shambani kwake.Kuna
nyumba kubwa sana huku ameijenga
na chini ya nyumba hiyo kuna ofisi
yake ya siri na vile vile kuna ghala ambalo huhifadhi vitu vyake mbali
mbali"
"Umefahamuje kuhusu nyumba
hiyo ya siri aliyoijenga chini?Umewahi
kuingia?akauliza Elvis
"Wakati ule ananitesa na
kunitaka nirejeshe kompyuta yake
aliwahi kunileta huku akanifungia
huko chini na kuniacha kwa siku
mbili.Nilihisi upweke mkubwa sana na
woga mwingi kwani ni sehemu yenye
kiza kikubwa.Aliniacha bila chakula
wala maji kwa siku mbili na akaja
kunifungulia akanitaka nimueleze
ilipo kompyuta yake lakini bado
sikuwa tayari kumueleza mahala
ilipo.Alipokuja aliwasha taa na ndipo
nikafanikiwa kuona ofisi yake ya
siri.Ndani ya ofisi hiyo kuna mlango
ambao ukiufungua unaingia katika
ghala kubwa ambalo huhifadhi vitu
vyake" akasema Graca Dah! Pole sana Graca.Sikujua
kama Frank ni mkatili kiasi hiki.Hata
hivyo wewe ni jasiri sana" akasema
Vicky
"Ahsante sana Vicky.Unanionaje
ninaweza kufaa kuwa mpelelezi?
akauliza Graca
"Unafaa sana kwani kazi hii
inahitaji mtu jasiri asiyekata tamaa
wala kulegea hata akiteswa vipi.Kama
unapenda kuifanya kazi hii utafaa
sana"akasema Vicky
"Graca ana maisha mengine
mazuri baada ya operesheni hii
kumalizika na si kuingia katika kazi
hizi za hatari" akasema Elvis na Graca
akatabasamu
"Graca tupe picha pana zaidi ya
mahala hapo.Je pana walinzi? akauliza
Elvis Walinzi wapo.Kuna nyumba tatu
amejenga wanazoishi walinzi
wanaolinda nyumba kubwa"
"Tutawezaje kuingia humo ndani
hadi katika ofisi yake ya siri?
"Tutayaacha magari kijijini
halafu tutatembea kwa miguu si
umbali mrefu sana kutoka hapo
kijijini.Tutazunguka upande wa
mashariki ambako kuna bwawa la
samaki na mashine ya kufua umeme
wa maji kwani kuna mto unapita hapo
karibu.Tukipita huko ni njia rahisi
kidogo ya kukwepa kupita karibu na
nyumba za walinzi" akasema Graca
"Nimepata wazo.Kama kuna
umeme wa nguvu za maji basi
tutazima umeme kwa muda ili tuweze
kupata nafasi ya kuingia ndani.Mimi
na Steve,tutatangulia ndani,Vicky na
Omola mtabaki pale katika mashine ya
maji kulinda usalama.Baada ya sisi kuingia ndani tutawajulisha na
mtawasha umeme.Nina uhakika
mkubwa kuwa umeme utakapozima
lazima walinzi watakuja kuangalia
kama kuna tatizo.Yeyote atakayefika
eneo hilo mzimisheni haraka
sana.Endapo mtaona kuna hatari
yoyote basi mtujulishe haraka sana"
akasema Elvis
"Graca unahakika baba yako
huhifadhi nyaraka zake za siri huku?
akauliza Steve
"Toka mama alipoinia katika ofisi
yake na kuiba kompyuta baba
hakutaka tena kuhifadhi vitu vake vya
siri katika ofisi yake iliyopo nyumbani
akahamishia kila kitu huku
shambani.Nina uhakika lazima kuna
kitu kitapatikana kuhusiana na
biashara zake au mtandao wake"
akasema Graca na safari ikaendelea
hadi walipofika kijiji chaMsolali.Walikipita kijiji kidogo halafu
Graca akaelekeza kuwa waache gari
hapo na watembee kwa miguu.Gari
likaegeshwa chini ya mkorosho halafu
wakaanza kutembea kwa miguu.Kiza
kilikuwa kinene na kwa mbali taa
zilionekana na Graca akawaeleza
mahala pale panapowaka taa ndipo
shambani kwa baba yake.Walitembea
kwa dakika kumi na tano wakipita
katika majani marefu na hatimaye
wakafika katika uzio wa seng'enge
"Huu ndio uzio wa shamba letu "
akasema Graca na kwa kutumia mkasi
mgumu seng'enge ikakatwa wakaingia
shambani.Kila mmoja alikuwa na
bastora mkononi tayari kukabiliana na
lolote isipokuwa Graca.Walitembea
kwa tahadhari na baada ya dakika sita
wakatokeza katika bwawa kubwa la
samaki Hapa ni bwawani na ukishuka
kule chini kuna mashine ya umeme"
akasema Graca akiwaelekeza akina
Elvis
"Ninakwenda kuchunguza kama
kuna mtu yeyote kule halafu
nitawajulisha" akasema Steve na
kuanza kutembea kwa tahadhari
kubwa akishuka mahala iliko mashine
ya kufua umeme wa maji.Baada ya
dakika nne akarejea na kuwajulisha
kuwa hakukuwa na mtu yeyote
mahala pale.Wote wakashuka
kuelekea katika mashine ile.Mlango
haukuwa umefungwa Elvis
akausukuma wakaingia ndani.Steve
pekee ndiye aliyebaki nje akilinda
usalama.
"Kazi inaanza" akasema Elvis na
kuzima mashine ya umeme.Eneo lote
kukawa giza na kwa haraka
wakiongozwa na Graca wakaanza kutembea kuelekea katika jumba
kubwa.Mbwa walisikika
wakibweka.Mara ghafla wakasikika
watu wakizungumza wakielekea kule
katika mashine wakiwa wamewasha
tochi za simu zao.Haraka akina Elvis
wakarukia ndani ya mtaro wa maji
wakajificha
"Hii mashine tumueleze bosi
alete mafundi waitazame ina matatizo
gani.kwani ni mara ya pili sasa
inazima" akasema mmoja wao
wakitembea kwa kasi kueleka katika
mashine ya umeme.Walipopita akina
Elvis wakatoka mtaroni.Elvis akapiga
piga sikioni alikoweka kifaa cha
kuwawezesha kuwasiliana halafu
akasema kwa sauti ndogo
"Vicky,Vicky do you copy"
"Nakupata Elvis"
"Kuna watu wawili wanakuja
huko katika mashineUsijali Elvis watakutana nasi"
"Wangejua wanachokwenda
kukutana nacho huko waendako
wangegeuza na kurejea walikotoka"
akasema Elvis huku wakitembea
taratibu kwa tahadhari kuelekea
katika nyumba wakiongozwa na
Graca.Walifika katika bustani
iliyokuwa na miti mingi ya maua na
sanamu kadhaa za wanyama
"Kuna mlango wa kuigilia ndani
uko upande huu wa nyuma" akasema
Graca.
"Steve ninakwenda kuufungua
mlango.Cover me" akasema Elvis na
kutoka kwa tahadhari katika ile
bustani akatembea kwa kunyata huku
Steve akiwa makini kuhakikisha
hakuna hatari yoyote eneo lile.Elvis
akafuata maelekezo ya Graca na
kutokea katika kibaraza cha
nyuma.Akaangaza angaza kama kuna mtu yeyote maeneo yale lakini
kulikuwa kimya kabisa.Akatoa pochi
ndogo katika begi alilobeba iliyokuwa
na vifaa fulani vidogo na kuanza
kuufungua mlango.Kwa sekunde
chache akafanikiwa kuufungua halafu
akamtaarifu Steve ambaye naye akiwa
na Graca wakamfuata na wote
wakaingia ndani.Bado eneo lote
lilikuwa giza.
"Vicky unanisikia? akauliza Elvis
baada ya kufanikiwa kuingia ndani
"Ninakupata Elvis,huku kila kitu
inakwenda vyema na wale jamaa
wawili tumekwisha walaza usingizi
wa muda.Tayari mko ndani?
"We're in.Washeni mashine"
akasema Elvis na baada ya dakika
mbili umeme ukawaka.Ndani
hakukuwa na taa iliyowashwa ila
kulikuwa na mwanga mdogo kutokana
na taa zilizokuwa zikiwaka nje Graca tuelekeze tunaelekea
wapi?akauliza Elvis
"Tunaelekea katika chumba cha
kulala cha baba na humo kuna mlango
wa kuingilia katika chumba cha chini"
akasema Graca na kuwaongoza akina
Elvis kuelekea sebuleni halafu
wakaelekea katika chumba cha baba
yake cha kulala.Elvis akatumia funguo
bandia na kuufungua mlango
wakaingia katika chumba cha
kulala.Kulikuwa giza.Elvis akatoa tochi
ndogo katika begi lake na kuiwasha.
"Tunapita huku katika chumba
cha nguo" akasema Graca na
wakaingia katika chumba cha
kuadilishia nguo kilichosheheni nguo
nyingi.
"Nyuma ya kabati kubwa kuna
mlango.Sukumeni hili kabati" akasema
Graca.Elvis na Steven wakalisukuma kabati na kweli wakakuta kuna
mlango nyuma yake
"Huo ndio mlango wa kuingilia
katika chumba cha chini" akasema
Graca.Elvis akaumulika na kugundua
ulikuwa unafunguliwa kwa namba .
"Tumekwama.Mlango huu
unafunguliwa kwa namba
maalum.Unaweza kuzikumbuka
namba za kufungulia mlango?Elvis
akauliza
"Hapana sizifahamu.Wakati ule
baba aliponileta hakukuwa na huu
mlango wenye namba" akasema
Graca.Elvis akafikiri kwa muda halafu
akapiga sikioni
"Vicky ,Vicky unanipata?
"Ninakupata Elvis"
"Good.Tumefanikiwa kuupata
mlango wa kuingilia ndani lakini kuna
tatizo limejitokeza.Mlango huu
unafunguliwa kwa namba kabati na kweli wakakuta kuna
mlango nyuma yake
"Huo ndio mlango wa kuingilia
katika chumba cha chini" akasema
Graca.Elvis akaumulika na kugundua
ulikuwa unafunguliwa kwa namba .
"Tumekwama.Mlango huu
unafunguliwa kwa namba
maalum.Unaweza kuzikumbuka
namba za kufungulia mlango?Elvis
akauliza
"Hapana sizifahamu.Wakati ule
baba aliponileta hakukuwa na huu
mlango wenye namba" akasema
Graca.Elvis akafikiri kwa muda halafu
akapiga sikioni
"Vicky ,Vicky unanipata?
"Ninakupata Elvis"
"Good.Tumefanikiwa kuupata
mlango wa kuingilia ndani lakini kuna
tatizo limejitokeza.Mlango huu
unafunguliwa kwa namba maalum.Nitahitaji kumtumia Omola
katika kuufungua mlango huu kwani
uliniambia kuwa ni mtaalamu wa
mambo haya.Steve anakuja huko
kumchukua wewe utabaki hapo
ukihakiki usalama,hivyo zimeni
umeme" akasema Elvis na kisha Steve
akatoka kwenda kumchukua Omola
"Baba yako amejihami
sana.Naamini kuna mambo mengi ya
muhimu anayaficha huku na ndiyo
maana akaweka mlango wa namna
hii" akasema Elvis wakati wakimsubiri
Steve na Omola
"Baba naweza kumfananisha na
gaidi kutokana na roho yake ya
kikatili.Kwake kutoa roho ya mtu ni
kitu kidogo sana" akasema Graca
"Usihofu haya yote yanakwenda
kumalizika muda si mrefu.Utakuwa na
amani tena" akasema Elvis Naomba iwe hivyo.Nimechoka
kuishi maisha ya ndege" akasema
Graca.Zilipita dakika kumi na mbili na
Steve akarejea akiwa na Omola
"Huko nje salama? akauliza Elvis
"Usihofu.Huko nje ni salama
kabisa.Hakuna mtu yeyote
anayezunguka maeneo haya na
inaonekana watu wa hapa hawaelewi
kinachoendelea.Hawajui kama
wamevamiwa"
"Good." akasema Elvis na
kumgeukia Omola
"Omola imekuwa vizuri
umeongozana nasi.Tunahitaji msaada
wako katika kuufungua huu mlango"
akasema Elvis na Omola akachukua
tochi ndogo akaumulika halafu
akatafuta katika kompyuta yake aina
ya kitasa kile na kuanza kutafuta
namba za siri.Baada ya dakika mbili
kompyuta ikamonyesha namna ya kubadili namba za siri za kufungulia
mlango ule.Akaanza kufuata taratibu
za kufungua mlango ule na baada ya
kumaliza kuingiza namba
alizoelekezwa na kompyuta yake taa
ndogo ya kijani ikawaka na mlango
ukafunguka
"Ahsante sana Omola" akasema
Elvis akiwa wa kwanza kuingia ndani
na kumulika akaziona ngazi za
kushuka na wote wakashuka kuelekea
chini
"Vicky,tayari tumeingia
tunaelekea chini" akasema Elvis
akimjulisha Vicky
"Elvis mawasiliano si mazuri
baada ya kuingia huko chini.Sikupati
vizuri" akasema Vicky lakini Elvis
naye hakuweza kumpata sawa sawa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wow! What a sweet page! Shikamoo Kulubule. Asante sana Boss. Ongeza nyingine kiongozi.
 
Ngoma inogile,frank ameshakusanya team ya vijana wake na wanaenda kuchukua silaha kwanza,nahisi hizo silaha wanaenda kuzichukulia palepale walipo kina Elvis na team yake yatazuka mapambano,hisia zangu zinazidi kunituma kwamba huo ni usiku mbaya sana kwa frank coz ameshanusa harufu ya mzimu Elvis he must die,hakuna aliyewahi kuonana na mzimu akabaki hai,huyo mume wa Elizabeth sina uhakika kama kweli amekufa inawezekana kifo kimekuwa faked,hii ngoma ni nzito na huu ni usiku wa damu,let's wait and see ,nitarudi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ngoma inogile,frank ameshakusanya team ya vijana wake na wanaenda kuchukua silaha kwanza,nahisi hizo silaha wanaenda kuzichukulia palepale walipo kina Elvis na team yake yatazuka mapambano,hisia zangu zinazidi kunituma kwamba huo ni usiku mbaya sana kwa frank coz ameshanusa harufu ya mzimu Elvis he must die,hakuna aliyewahi kuonana na mzimu akabaki hai,huyo mume wa Elizabeth sina uhakika kama kweli amekufa inawezekana kifo kimekuwa faked,hii ngoma ni nzito na huu ni usiku wa damu,let's wait and see ,nitarudi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tumosa popote ulipo, ninamtaimu Brigedia Frank nizichukue silaha na nije kukubana na kukuweka mateka ili upunguze hiii arosto
 
Back
Top Bottom