Riwaya: Kijijini kwa Bibi

Riwaya: Kijijini kwa Bibi

RIWAYA : KIJIJINI KWA BIBI.

MTUNZI : ALEX KILEO..

SEHEMU YA KUMI NA TISA.

mama kayoza akaendelea,

"baba
yako aliponiona aliniangalia kisha
akawa kama anataka kusema kitu, ila
nguvu hakuwa nazo, akaishia
kukunyooshea kidole, kisha akakata
roho, Alafu wewe ukapoteza fahamu,
nilijisikia uchungu sana, nilianza
kulia kwa kwikwi pale mlangoni, nililia sana kiasi kwamba nikapoteza fahamu, nilizinduka nikaendelea kulia ila
cha kushangaza bibi yako
akuonyesha wasiwasi kabisa na wala hakutoa chozi la uchungu kuonesha kuwa amempoteza mwanae, badala
yake aliniambia kuwa yule mzimu wa
ukoo ameingia mwilini kwako wewe Kayoza
kwa ruhusa yake, yaani ruhusa ya bibi yako.

akaniambia kuwa kuanzia
hapo hakutakuwa tena na shida, na
kama shida itatokea ni kwa ajili ya
kukulinda wewe (Kayoza), na sharti
kubwa ambalo mzimu alitaka
uzingatie ni kwamba, usifanye
mapenzi mpaka uoe na pia ukae mbali na harufu ya damu ya aina yoyote na uepuke kuwa mtu wa hasira hasira. Shangazi yako hajawahi kumwambia hivyo?" Mama Kayoza akamuuliza mwanae,

"Uwa ananisisitizia sana hayo mambo na kiukweli niliyamudu sana, hakuwahi kuniambia sababu ya mimi kutofanya hivyo" Kayoza alimjibu mama yake,

"Kwanini hajakwambia?" Mama kayoza akamuuliza mwanae,

"Mimi sijui" Kayoza akajibu,

"Labda alikuwa na sababu zake" Mamá Kayoza aliongea huku akiinuka kitini,

"Sasa mbona tena unaondoka?" Kayoza alimuuliza mamá yake,

"Naenda jikoni kuangalia maharage, yasije yakaungua bure" Mamá kayoza aliongea huku akifuata uelekeo wa jikoni.

******************

Sajenti Minja alirudi mpaka nyumbani kwake na kupanga nguo zake katika mabegi kwa ajili ya kujiandaa na safari, kwa maana alishajua kuwa kesho kukikucha ni lazima aitwe ofisini ili akakabidhi vitu muhimu vya kiaskari.

Alipomaliza kupanga vizuri nguo zake, aliingia bafuni kuoga na kisha alipotoka tu alipotoka tu bafuni, akaona njia nzuri ya kupumzisha kichwa ni kulala. Akaingia chumbani kwake na kulala.

_____________________
SIKU ILIYOFUATA..
_____________________

Kama alivyotegemea kuwa ni lazima siku hii aitwe ofisini na ndivyo ilivyokuwa.
Sajenti Minja baada ya kuamka na kupata kifungua kinywa, alipokea simu kuhitajika kufika ofisini kutoka kwa mkuu wa kituo chake cha polisi.

Alijitayarisha haraka haraka na kuondoka mpaka kituoni na moja kwa moja akaenda kwenye ofisi ya mkuu wake,

"Kaa hapo" Mkuu wake alimwambia huku akimuoneshea kiti kilichopo pembeni. Sajenti Minja akakaa.

"Barua yako nimeipata na kuipokea asubuhi hii, nimeipitia na kwa upande wangu sina tatizo" Mkuu wake alimwambia huku akiwa anaandika andika vitu katika karatasi,

"Asante sana mkuu kwa kunielewa" Sajenti Minja aliongea huku akimshukuru Mungu kwa kuitikia maombi yake,

"Sasa cha muhimu ni kunikabidhi bastola uliyopewa na ofisi na namba zako za kazi na kitambulisho pia" Mkuu wake aliongea na kisha Sajenti Minja akavitoa vitu vyote alivyotakiwa akabidhi,

"Hivi hapa mkuu" Sajenti Minja aliongea huku akiviweka vile vitu juu ya meza,

"Mpaka hapa mimi na wewe tumemalizana" Mkuu aliongea huku akimuangalia Sajenti Minja,

"Nashukuru mkuu, kwa hiyo naweza kuondoka?" Sajenti Minja aliuliza,

"Kumbuka kuwa hapa ulikuja kufanya kazi tu, ila muajiri wako ni jeshi la wananchi, kwa hiyo ni lazima uende uko ndio watakupa majibu yao kama wamekubaliana na wewe au lah" Mkuu alimpa maelezo Sajenti Minja,

"Hakuna shida, nitaenda pia uko" Sajenti Minja aliongea huku akitabasamu,

"Wapo nje wanakusubiri" Mkuu aliongea na kumfanya Sajenti Minja ashtuke,

"Wananisubiri?" Sajenti Minja akauliza,

"Ndio" Mkuu aliongea huku akinyanyua mkonga wa simu na kubonyeza namba fulani, akawa anasubiri upande wa pili upokee simu,

"Mimi nimeshamalizana nae, nawasubiri nyinyi mkuu" Mkuu wa polisi aliongea kwenye simu na kisha akairudisha simu mezani,

"Sasa Kwanini wamenifuata?" Sajenti Minja aliuliza baada ya mkuu wake kukata simu,

"Mimi sijui, labda Ndio utaratibu wenu wanajeshi" Mkuu alijibu kabla hawajasikia mtu akigonga hodi,

"Pita ndani" Mkuu alijibu kisha wakaingia ndani wanajeshi wawili waliovaa gwanda zilizoandikwa MP begani, wakampigia saluti mkuu wa polisi,

"Nyoosha mikono mbele" MP mmoja aliongea huku akiitoa pingu na kuishika mkononi,

"Mambo gani tena ya kufungana pingu" Sajenti Minja aliongea huku akipingana na wale MP, alishangaa anapigwa makofi mengi sana yasiyokuwa na idadi,

"Minja acha ukorofi, sikiliza unachoambiwa na kumbuka ndani ya jeshi hakuna maombi, kuna amri tu" Mkuu wa polisi alimwambia Sajenti Minja ambaye alionekana kukubaliana nae na akakubali kufungwa pingu na kisha wale MP wakatoka nae nje na kumuingiza ndani ya gari nyeusi iliyokuwa na namba ya jeshi.
Kisha ile gari iliondoka.

****************

Baada ya kutoka jikoni, mama Kayoza alirudi sebuleni na kwenda kwenye jokofu na kuchukua maziwa fresh na kujimiminia kwenye glass,

"Na sisi tunataka" Kayoza akamwambia mama yake,

"Mimi Ndio nimeongea sana, kwa hiyo ni muhimu kulainisha koo" Mama Kayoza aliongea huku akitabasamu,

"Sawa, endelea na story" Kayoza akamwambia mama yake,

Ngoja niendelee, Baada ya miaka
miwili tangu baba yako afariki,
nilitaka kuondoka ili niende sehemu
nyingine nikaanze kuishi maisha ya
kujitegemea, kipindi hicho ulikuwa
una umri wa miaka mitatu, Ilo wazo langu
lilipingwa na shangazi zako na baba
zako, mimi kuona hivyo nikawa naenda
sana kanisani kufanyiwa maombi,
kumbe yale maombezi yalikuwa
yanaleta madhara katika mzimu wao,
ila kwa kuwa mzimu ulishanipa
ahadi ya kutonidhuru ukawa
unavumilia tu, Siku moja wakati
nimelala na wewe usiku, nakumbuka
nilikuwa nasoma biblia, bila kutarajia nilikuona ukiinuka na
ukakaa kitandani, mimi nikajua labda
unataka kukojoa, nikakuvua nguo
kisha nikakushusha chini ukojoe
kwenye kopo, ila cha ajabu macho
yako yakawa meupe ya kung'aa na
meno yakakutoka yakawa marefu, mimi kuona hivyo nikahisi hatari nikataka kukimbia, ila ulinishika mkono na kunivuta na nikaangukia kitandani, hili nalo lilinishangaza, yaani mtoto wa miaka mitatu uwe na nguvu ya kunivuta na nikaanguka?

Baada ya mimi kuanguka, ukaniangalia kwa sekunde kadhaa
kisha ukasema kuwa umenivumilia
kwa muda mrefu sana, hapo ndio
nikagundua kuwa aliekua anaongea
ni mzimu na wala sio wewe, kwa sababu
ya muonekano wako, na maneno
ulivyokuwa unayatamka kwa ufasaha,
wakati katika hali yako ya kawaida
ulikuwa huwezi kutamka maneno
vizuri.

Nakumbuka uliniambia ikifika
kesho niondoke, maana nimeshindwa
kulipa fadhira, ulidai ulinipenda sana ila maombi ninayofanyiwa uko kanisani ninapoendaga uwa yanamfanya anakosa raha, kwa hiyo basi, hana sababu ya kuniadhibu kwa kuwa aliniahidi kuwa kamwe hawezi kuniadhibu, ila cha kufanya ni mimi kuondoka hiyo kesho asubuhi.

Kesho yake ilipofika,
nikamwambia bibi yako kilichotokea,
ikabidi awaite wanaukoo wote ambao walikuwa jirani na pale tunapoishi na kuwaelezea yote niliyoambiwa na mzimu.

wakakubaliana niondoke,
ila wewe nikuache, na kuhusu malezi
yako, atakaehusika nayo ni shangazi yako
mkubwa, ambae alikuwa anakaa
kigoma, nikakubali kwa roho safi, kwa
makubaliano ya kila baada ya miezi
miwili ningeenda kwa shangazi yako kukuangalia......

******ITAENDELEA******

the Legend☆
 
RIWAYA : KIJIJINI KWA BIBI.

MTUNZI : ALEX KILEO..

SEHEMU YA ISHIRINI.

_______________
ILIPOISHIA...
_______________

Kesho yake ilipofika,
nikamwambia bibi yako kilichotokea,
ikabidi awaite wanaukoo wote ambao
walikuwa jirani na pale tunapoishi
na kuwaelezea yote niliyoambiwa na
mzimu.

wakakubaliana niondoke,
ila wewe nikuache, na kuhusu malezi
yako, atakaehusika nayo ni shangazi
yako
mkubwa, ambae alikuwa anakaa
kigoma, nikakubali kwa roho safi, kwa
makubaliano ya kila baada ya miezi
miwili ningeenda kwa shangazi yako
kukuangalia......

_____________
ENDELEA...
_____________
....uko kwa shangazi yako walikuwa
wanafuata masharti ya mzimu kama
kawaida.

kila mwisho mwezi
walikuchinjia mbuzi na kondoo,
damu walikupa ukainywa na sijawahi kusikia tena huo mzimu ukisumbua.

Sasa hayo matatizo yanayokukuta uko chuo labda ni kutokana na masharti kutotekelezwa
kwa sababu ya umbali uliopo" Mama
kayoza akawa amemaliza masimulizi
yake rasmi,

"mh, mbona ni shughuli
nzito?, sasa mama utanisaidiaje?"
kayoza alimuuliza mama yake,

"mwanangu sina msaada kwako"
mama kayoza akajibu.

"mama hamna
mganga yeyote wa jadi
unaemfahamu, ili anisaidie" kayoza
aliendelea kumtupia maswali mama
yake.

"kusema kweli upande wa
ushirikina huko mi sipaamini, ila..."
mama kayoza akawa kama anafikiria
kitu,

"Ila nini?" Kayoza akamuuliza mama yake,

"ila kuna mchungaji pale kanisani kwetu,
nitajaribu kumuomba msaada" Mama
kayoza akamalizia namna hiyo.

"hata hivyo ni sawa pia, sasa utaenda
kumwambia saa ngapi?" Kayoza kamuuliza mama yake.

"nitaenda
kumwambia jioni baada ya kula
chakula" mama Kayoza
akajibu.

"mambo si hayo bwana"
Kayoza akaongea huku akiwa na matumaini kibao ya kufanikiwa katika
zoezi hilo.

Baada ya kumaliza kula
chakula cha jioni, mama Kayoza
alijitanda vitenge vyake na kuelekea
katika makazi ya mchungaji.

Alipofika alikaribishwa na mtoto wa kike wa
mchungaji, ambaye alimpa taharifa Mama kayoza kuwa mchungaji
anaoga, ikambidi Mama Kayoza amsubiri mchungaji hadi
alipomaliza kuoga.

Mchungaji alipomaliza kuoga, akapelekewa
ujumbe kuwa kuna mgeni wake anamsubiri varandani.

Mchungaji akaenda mpaka
Varandani na kumkuta Mama Kayoza akimsubiri,

"karibu mpendwa"
Mchungaji akamkaribisha mama
Kayoza huku akimpa mkono,

"asante mchungaji" mama
kayoza akajibu.

Baada ya salamu na
kujuliana hali zao, mama kayoza
akamuelezea mchungaji mwanzo
mpaka mwisho wa matatizo aliyonayo
Kayoza.
Wakakubaliana hiyo kazi
angeifanya kesho yake
usiku.

***************

Sajenti Minja alipakiwa katika gari kwa makofi kama mharifu aliyekuwa anabishana na Askari.

Gari iliondolewa kwa mwendo wa kawaida lakini kipindi chote wakati gari ikitembea hakuna MP aliyemgusa Sajenti Minja.

Baada ya mwendo wa dakika kumi, Sajenti Minja alishatambua uelekeo wa anapopelekwa na alishaanza kupata wasiwasi mkubwa kuliko ule wa hawali.

"Jamani kwani nimefanya kipi kibaya?" Sajenti Minja aliuliza huku akiwatizama wale MP kwa zamu,

"Hauruhusiwi kuuliza wala kuongea kitu chochote" MP mmoja alijibu na Sajenti Minja akakaa kimya kwa kuwa alijua jeshini amri ndio kiongozi.

Gari iliyombeba Sajenti Minja iliingia katika geti moja kubwa ambalo lilifunguliwa na wanajeshi.
Gari ikapita ndani ya geti na ikatembea tena mwendo wa dakika tano mpaka ilipoenda kusimama mbele ya jengo moja lililokuwa limekaa peke yake.

Sajenti Minja akashuka na kuangaza lile eneo ambalo lilipambwa na wanajeshi wakiwa katika majukumu mbalimbali pale kambini.

Sajenti akaongozwa mpaka ndani ya lile jengo na kuingizwa katika ofisi moja nadhifu ambapo ndani ya hiyo ofisi walimkuta bwana mmoja mwenye umri wa miaka 40 - 45 akiwa amekaa katika kiti.

Sajenti Minja na wenzake wote wakampigia saluti kwa ukakamavu yule bwana.

"Asanteni vijana wangu, mnaweza kwenda nje na mniache na huyu bwana" Yule bwana aliongea kisha wale MP wakaelekea nje na kumuacha Sajenti Minja ndani tena akiwa amesimama,

"Polisi wamekubali uache kazi?" Yule bwana alimuuliza Sajenti Minja,

"Ndio mkuu" Sajenti Minja alijibu kikakamavu,

"Ni nani aliyetaka wewe uende ukafanye kazi polisi?" Yule bwana alimuuliza,

"Ni mimi mkuu" Sajenti Minja alijibu huku akiwa bado kasimama,

"Ulisema kwanini ulitaka kifanya kazi ya polisi?" Yule bwana alimuuliza,

"Ni kwa sababu nilitoka mafunzoni nje ya nchi, kwa hiyo niliitaji kupata sifa zaidi upande wa upelelezi wa ndani ili nipate nafasi ya kwenda kuongeza mafunzo ya nje ya nchi tena" Sajenti Minja alijibu,

"Je kazi ya upelelezi ulipewa uko polisi?" Yule bwana alimuuliza,

"Ndio nilipewa" Sajenti Minja alijibu,

"Nadhani umeikamilisha?" Yule bwana aliuliza,

"Hapana" Sajenti Minja alijbu,

"Kwanini?" Yule bwana aliuliza,

"Nimepata tatizo la afya, nikaona ni bora nipumzike" Sajenti alijibu,

"Lete cheti cha daktari kinachothibitisha wewe no mgonjwa" Yule bwana alimwambia Sajenti Minja,

"Nimekiacha nyumbani" Sajenti Minja alijibu ila alitoa jibu la uongo kwa maana hakuna cheti wala kitu chochote kinachoweza kuthibitisha yeye ni mgonjwa,

"Ni tatizo gani la kiafya ulilonalo?" Yule bwana aliuliza,

"Pumzi inanibana sana kiasi kwamba nashindwa kupumua" Sajenti Minja alijibu,

"Ooh pole, basi nenda kapumzike, tutaendelea baadae na maswali" Yule bwana aliongea,

"Sawa mkuu" Sajenti Minja alijibu na kuanza kuondoka,

"Unaenda wapi?" Yule bwana alimuuliza kwa mshangao,

"Umeniambia nikapumzike mkuu, naenda nyumbani" Sajenti Minja alijibu huku akisimama,

"Utapumzikia hapa hapa kambini ili nitapohitaji kuongea na wewe, nikuite" Yule bwana aliongea kisha akapiga simu katika namba anayoijua yeye na kumtaka yule anaongea nae aende ofisini, kisha akakata simu.

Baada ya sekunde kadhaa aliingia mwanajeshi na kusimama kikakamavu,

"Mpeleke huyu akapumzike" Yule bwana alimwambia mwanajeshi aliyeingia,

"Upande gani" Yule mwanajeshi aliyeingia akauliza,

"Kwa wenye Matatizo ya kupumua au kwa wagonjwa wa mapafu na kifua" Yule bwana alijibu na kisha akamshuhudia yule mwanajeshi akimuongoza Sajenti Minja kwenda nje ya ofisi.

Yule bwana akatoa tabasamu huku akitingisha kichwa kwa masikitiko.

************

Huyu mchungaji ambaye Kayoza atamtembelea anaitwa Batoromeo
mathayo wingo, jina maarufu
lililozoeleka na wahumini wake ni
Mchungaji Wingo, tokea ahamie pale
kanisani ana muda wa mwaka mmoja
na nusu, na watu wanaodaiwa kuwa
wachawi, wameshadondoka kwenye
eneo la makazi yake zaidi ya mara
nne, hii ilimjengea imani sana kwa wahumini wake na pia alijikuta waumini wengine kutoka makanisa mengine wakifurika katika kanisa lake kila siku ambayo alifanya maombi kwa ajili ya wagonjwa na walemavu.

Ndani ya muda mfupi Mchungaji Wingo aliweza kupata jina na heshima kubwa mkoani shinyanga.

***************

Kesho yake ilipofika, mama Kayoza na Kayoza
pamoja na Omari wakaongozana
usiku ule mpaka kwa mchungaji
Wingo, Walipofika, mchungaji na
familia yake, wakawakaribisha ndani,
na baada ya maongezi ya muda mrefu, mchungaji aliwaambia kuwa,
mama kayoza na Omari warudi
nyumbani, ila Kayoza abakie, kwa
sababu anataka akeshe nae huku wakimfanyia maombi na familia
yake, mama kayoza na Omari wakajiondokea zao, wakamuacha
kayoza kwa mchungaji...

KAMA MCHUNGAJI ANGEJUA KITAKACHOMTOKEA, ASINGEKUBALI
KUBAKIA NA KAYOZA...

******ITAENDELEA******

the Legend☆
 
RIWAYA : KIJIJINI KWA BIBI.

MTUNZI : ALEX KILEO.

SEHEMU YA ISHIRINI NA MOJA.

________________
ILIPOISHIA...
________________

Kesho yake ilipofika, mama Kayoza na
Kayoza
pamoja na Omari wakaongozana
usiku ule mpaka kwa mchungaji
Wingo, Walipofika, mchungaji na
familia yake, wakawakaribisha ndani,
na baada ya maongezi ya muda
mrefu, mchungaji aliwaambia kuwa,
mama kayoza na Omari warudi
nyumbani, ila Kayoza abakie, kwa
sababu anataka akeshe nae huku
wakimfanyia maombi na familia
yake Mchungaji.

Mama kayoza na Omari
wakajiondokea zao, wakamuacha
kayoza nyumbani kwa mchungaji...

KAMA MCHUNGAJI ANGEJUA
KITAKACHOMTOKEA, WALA ASINGEKUBALI
KUBAKIA NA KAYOZA...

_______________
ENDELEA...
_______________

Baada ya mama kayoza kuondoka, Mchungaji alielekea katika chumba kimojawapo ndani ya nyumba yake na kukaa kwa muda wa dakika chache kisha akarejea tena mahali alipomuacha Kayoza,

"we ni mkristo wa dhehebu gani?" Mchungaji wingo alimuuliza Kayoza baada ya kukaa.

"ni mromani, romani catholic" Kayoza
alijibu huku akijaribu kutabasamu.

"ok, je unaamini katika
ulokole?" Mchungaji Wingo akarusha swali
jingine.

"mi naamini katika dini
yeyote na dhehebu lolote ambalo linafuata matakwa na njia za
Mungu" Kayoza akajibu,

"Umeshawahi kukaa peke yako hata siku moja na kufanya maombi?" Mchungaji Wingo alimuuliza Kayoza huku akimuangalia kwa umakini,

"Hapana" Kayoza alijibu,

"Na kanisani uwa unaenda?" Mchungaji Wingo aliendelea kumuuliza Kayoza,

"Hapana" Kayoza akajibu,

"Sasa unaamini vipi katika dini zinafuata matakwa ya Mungu aliye hai ungali wewe hufuati njia za Mungu?" Mchungaji alimuuliza Kayoza,

"Kuna kipindi uwa Nataka sana kwenda kanisani, ila uwa najikuta napata uvivu mkubwa sana" Kayoza alitoa jibu lililomfanya Mchungaji Wingo atabasamu,

"Wewe unafikiri ni kitu kinapelekea upate uvivu siku ya kwenda kanisani?" Mchungaji Wingo aliuliza tena,

"Mwanzo nilikuwa sijui, ila kwa hizi habari alizonieleza mama, nafikiri ni mzimu ndio ulikuwa unaniletea hali hiyo" Kayoza alijibu na kufanya mchungaji atabasamu tena,

"Mbona mama yako alikuwa anaenda kanisani akiwa chini ya huo mzimu?" Mchungaji Wingo aliuliza,

"Hivi mchungaji unadhani nyumba ya jirani yako unaweza kuitawala kama unavyoitawala nyumba yako?" Kayoza alitoa swali lililomfanya Mchungaji Wingo ashtuke kidogo,

"Unamaanisha nini kusema hivyo?" Mchungaji Wingo aliuliza,

"Mzimu kanifanya mimi kuwa nyumba yake, sasa anaweza kunikontroo atakavyo yeye, kwa hiyo mamlaka anayoweka juu yangu ni lazima yawe yana nguvu kuliko anayoweka juu ya mama yangu" Kayoza alimjibu Mchungaji Wingo,

"Jibu lako zuri sana, ila lina kasoro, hakuna kiumbe kitakachoweza kukutawala hapa duniani kama utamuamini Mungu" Mchungaji Wingo aliongea huku anaangalia mazingira ya sebuleni kwake,

"Kwa maana hiyo mimi simuamini Mungu?" Kayoza aliuliza,

"Hiyo ni Imani iliyopo moyoni kwako, kwa hiyo hilo swali jiulize wewe" Mchungaji Wingo aliongea huku akitabasamu,

"Kwani Mchungaji imani ipo kwenye nyumba za ibada tu?" Kayoza aliuliza,

"Hilo swali nitakujibu siku nyingine. Nikuletee maji ya baridi au ya moto?" Mchungaji Wingo alimuuliza Kayoza huku akitabasamu,

"ila mchungaji mimi sijaomba maji na wala sina kiu" Kayoza alijibu huku akionekana kumshangaa Mchungaji Wingo,

"Sijamaanisha una kiu, na sio kila unachopewa, kuna vitu unapewa bila hata kuomba" Mchungaji Wingo aliongea huku akiondoka na kumuacha Kayoza akimuangalia huku akitabasamu kutokana na maneno ya Mchungaji Wingo.

*******************

Sajenti Minja alitolewa moja kwa moja kutoka katika ofisi za mkuu wake wa jeshi na kuanza kupelekwa katika nyumba moja nzuri ambayo ilionesha haikuwa inakaliwa na mtu au anaekaa pale atakuwa hayupo au ni watu ambao hawapendi kelele, uzuri mwingine ni kwamba ile kambi ni ngeni machoni kwa Sajenti Minja ila si ngeni masikioni mwake kwa maana alishapata habari za kambi hii kutoka kwa wenzake wachache aliokutana nao mafunzoni.

Waliendelea kuisogelea ile nyumba huku kila mmoja akiwa kimya na uzuri wa ile nyumba kwa nje, tayari Sajenti Minja kichwani kwake alishatengeneza fikra za kule ndani ya nyumba kutakuwaje. Aliwaza kutakuwa na kitanda kikubwa, jakuzi, upepo mzuri wa Air condition na kila aina ya chumba kizuri ambacho mwanajeshi kama yeye anastahili kupumzika.

"Mheshimiwa vua viatu" Mwanajeshi aliyeongozana na Sajenti Minja aliongea na kumfanya Sajenti Minja atoke kwenye dimbwi la mawazo,

"Alaah! Kumbe tumefika?" Sajenti Minja aliuliza huku akitabasamu lakini yule Mwanajeshi hakushughulika kumjibu na badala yake alibonyeza namba zilizopo kwenye mlango na mlango ukafunguka, hapo ndipo alipokuta wanajeshi wengine wawili wakiwa mlangoni wakiwasubiri,

"Huyu wa wapi?" Mwanajeshi mmoja kati ya wale wawili aliuliza,

"Mgonjwa wa kifua" Mwanajeshi aliyeongozana na Sajenti Minja alijibu na kufanya Sajenti Minja ajikohoreshe kidogo,

"Kumbe kweli unaumwa? Twende ukapate matibabu upumzike" Mwanajeshi yule mwenye herufi zilizoandikwa MP aliongea na kumfanya mwenzake atabasamu na wakati huo huo yule Mwanajeshi aliyemleta Sajenti Minja aliishia mlangoni na kurudi alipotoka.

Wale wanajeshi wakiwa na Sajenti Minja walivipita vyumba kadhaa na mwisho waliingia katika chumba kimoja kilichoandikwa "BREATH",

"Ebu ruka ruka kichura chura kidogo ili mwili upate joto" MP mmoja alimwambia Sajenti Minja,

"Ni moja ya matibabu au?" Sajenti Minja aliuliza kwa mshangao,

"Ruka bwana, dawa unazotakiwa kunywa zinahitaji joto kubwa la mwili" Yule MP aliongea huku akimuangalia Sajenti Minja.

Sajenti Minja akaanza kuruka kichura chura kwa kasi huku akicheka na kubadilisha mitindo mbalimbali ya kuruka kichura chura.

Baada ya dakika mbili jasho lilianza kumtoka, akaamua asimame,

"Nadhani hapa nipo poa, mwili umeshachemka huu" Sajenti Minja aliongea huku akitabasamu, lakini alikuwa amekosea sana, alishtukia akipigwa kofi zito sana la shingo,

"Endelea kuruka, nani kakupa ruhusu ya kusimama?" MP mmoja aliongea kwa ukali huku akiwa amemkunjia uso Sajenti Minja,

"Kwani ni adhabu hii?, sio lazima niruke" Sajenti Minja nae aliongea kwa ukali huku akiwa amepaniki,

"Tutajua kama ni adhabu au sio adhabu" MP mwingine aliongea na kumpiga ngumi Sajenti Minja iliyompata vizuri usoni. Sajenti Minja alivyoona hivyo akaona imeshakuwa hatari, akaanza kupambana na wale MP, alipambana nao vizuri na akawadhibiti, maana alitoa kichapo cha hatari mpaka wale MP wakawa wanaogopa kumsogelea.

Sajenti Minja akiwa bado anajiamini kwa kichapo alichotoa, alianza kuondoka kibabe, ila hata kabla hajapiga hatua mbili alitokea mwanajeshi mwingine akiwa na bastola,

"Ukileta fujo nakufumua miguu, lala chini na uweke mikono juu" Mwanajeshi aliongea huku akiwa hatanii,

"Kwani kuna tatizo gani, mbona siwaelewi?" Sajenti Minja aliuliza,

"Lala chini ndio uhoji" Mwanajeshi aliongea kwa sauti kubwa na kumfanya Sajenti Minja akubaliane nae, akalala chini na wale MP waliokula kichapo wakamwendea na kumfunga pingu kwa nyuma, kisha wakambeba juu juu mpaka katika chumba kingine na kumuweka juu ya kiti cha chuma na kumfunga na kamba, kisha wakaanza kumpiga kwa hasira walimchakaza haswa.

Baada ya kuridhika na kipigo walichokitoa, ndipo alipoingia yule bwana mkuu wa jeshi aloyekuwa anamuhoji mwanzo kule ofisini, MP wakampigia saluti na kumsogezea kiti kwa kukiweka mbele ya kiti alichokalia Sajenti Minja,

"Umelijua kosa lako?" Yule bwana alimuuliza Sajenti Minja huku akimuangalia kwa huruma, lakini Sajenti Minja hakuweza kujibu kitu,

"Ulichofanya wewe ni kudhalilisha jeshi. Huwezi kuacha kazi kwa kuogopa kitu kwa sura wala muonekano. Ni bora ungeomba muda wa kujipanga tungekuelewa. Alafu ulipoamua kuacha kazi ukaamua utumie na kigezo cha kuumwa, hilo ni kosa pia, unadanganya wakati uliahidi kusimamia ukweli" Yule bwana mkuu wa jeshi aliongea kwa sauti ya upole ila iliyosikika vyema masikioni kwa Sajenti Minja.

Kisha yule bwana akasimama huku akimuangalia Sajenti Minja,

"Mpelekeni sehemu tulivu apoze maumivu" Yule bwana aliongea na kuanza kuondoka huku akiwa haonekani kama ni mtu mwenye kupenda kucheka.

Yule bwana alitembea mpaka alipofika mlango wa kutokea nje ya lile jengo, ndipo aliposikia sauti kubwa ya Sajenti Minja ikipiga kelele kutokana na maumivu aliyokuwa anayapata muda huo,

"Siku zote mwanajeshi mpumbavu utulivu anaostahili ni huo unaoambatana na maumivu" Yule bwana mkubwa aliongea huku akitabasamu na wakati huo huo alikuwa anatoka nje ya lile jengo lililokuwa tulivu kwa nje, ila kwa ndani si sehemu salama kwa wanajeshi wenye makosa.

***************

Baada ya muda kidogo Mchungaji Wingo alirudi huku akiwa na jagi lililojaa maji,

"Muda wa maombi unakaribia, umejiandaaje?" Mchungaji Wingo alimwambia Kayoza,

"Kawaida tu, ila naimani tutafanikiwa" Kayoza alijibu,

"Ni bora umetanguliza Imani mbele, ni jambo jema" Mchungaji aliongea kwa imani,

"Nimekuletea maji hayo unywe, ingawa hujaniagiza ila itabidi unywe" Mchungaji Wingo alimwambia Kayoza,

"Haina shida, nitakunywa tu" Kayoza alijibu huku akiyamimina yale maji katika glass.

Muda wote ambao mchungaji alikuwa anaongea na Kayoza, watoto wake walikuwa wanatayarisha chumba cha kufanyia maombi.

Baada ya maandalizi,
mchungaji Wingo alimkaribisha Kayoza
katika chumba cha maombi, kisha
watoto na mke wa mchungaji Wingo
wakaingia katika chumba cha maombi,
huku kila mmoja akiwa amebeba biblia yake mkononi, hapo ilikuwa yapata saa tano za usiku
usiku.

Baada ya wote kujumuika ndani ya kile chumba, maombi yakaanza rasmi,
Mchungaji Wingo na familia yake
walikemea kwa juhudi zote, mpaka saa
saba usiku, Kayoza alikuwa kama
mwanzo, hakuwa na mabadiliko yoyote, Ila Mchungaji hakukata
tamaa, pia alikuwa anahisi
akishindwa kumtibu Kayoza, heshima
yake inaweza kushuka katika kanisa, kwa hiyo alizidisha maombi .

Ilipofika saa nane za usiku mabadiliko yakaanza kwa Kayoza, alihisi kizunguzungu, hakuna aliyeyaona hayo kabadiliko isipokuwa yeye mwenyewe.

Wakati maombi yanaendelea Mchungaji
akahisi, kuna nguvu nyingine iko kwa
nje, inashindana nae, kwa maana yeye alikuwa na uwezo wa kuona mpaka visivyoonekana. Ile nguvu iliyokuwa inatoka nje ilikuwa haimdhuru ila hakuwa akiitaka iendelee kumuingilia katika maombi yake. Akaamua atoke nje mara moja na akaiacha familia yake inamuombea Kayoza. Ile
kutoka nje, akakutana na watu zaidi ya kumi, wote wako uchi, wamejipaka
majivu usoni.

Mchungaji Wingo
hakupata tabu kuwatambua kuwa
wale ni wachawi. Katika kipindi cha
maisha yake ya uchungaji ameshakutana na hayo mambo mara nyingi tu.

Akaona dawa yao ni ndogo tu, akaanza kukemea, Baada ya kupambana nao kwa
muda wa saa moja, wale wachawi
wakawa wanaelekea kushindwa.

Ila ghafla mambo yakabadilika, Mchungaji Wingo akaanguka chini kisha akapoteza
fahamu. Sasa wale wachawi
wakasogea pale alipolala mchungaji huku wakiruka ruka kwa furaha na kuongea lugha isiyoeleweka. Walimsogelea kwa ajili ya kummaliza kabisa Mchungaji Wingo, ila kila
walipojaribu kurusha makombora
yao, hayakumdhuru
mchungaji.Wakajua sababu ya hayo
mambo ni kutokana na nguvu ya maombi ya familia ya mchungaji
waliyokuwa wanaendelea nayo chumbani.

Wachawi wote wakavamia
katika kile chumba kwa ajili ya kupambana na maombi ya familia ya Mchungaji, ni kitendo cha
dakika kumi tu, familia yote ya
mchungaji ilikuwa imepoteza fahamu ni kutokana na kwamba hawakuwa na imani ya kutosha.

Wachawi wakawabeba kisha wakawalaza nje ya geti pamoja na
mchungaji mwenyewe, kitu kilichowashangaza wachawi ni kuwa
kulikuwa na kijana ambae ni kayoza, toka wale wachawi waanze kuloga,
yeye hakudhurika, ndipo wachawi
wakafanya kosa la mwaka,
wakamweka kayoza katikati yao,
kisha, wakaanza kumloga, bila kutegemea, kayoza akabadilika na
kubeba taswira ya kutisha, wale wachawi mawazo yao yakaona zoezi
lao limefanikiwa, mmoja kati ya wale
wachawi, akamsogelea kayoza ili
ammalize kabisa, ni kitendo bila
kuchelewa, kayoza ndani ya sekunde
kumi alishanyonya damu wachawi
watatu, ndani ya dakika moja
alishamaliza wachawi wote, nao
akawatoa nje, kisha akawalaza
pamoja na familia ya mchungaji,
kisha akarudi katika chumba cha maombi na akapoteza fahamu.

Asubuhi kulipokucha, watu wengi sana walijaa nje ya nyumba ya
Mchungaji Wingo, na wote walikuja kuangalia watu ambao walilala nje ya nyumba ya Mchungaji huku wakiwa na alama za meno shingoni.

Kati ya watu waliolala getini alikuwepo pia Mchungaji mwenyewe na familia yake...

******ITAENDELEA******

the Legend☆
 
RIWAYA : KIJIJINI KWA BIBI.

MTUNZI : ALEX KILEO.

SEHEMU YA ISHIRINI NA MBILI.

_________________
ILIOPOISHIA...
_________________

Asubuhi kulipokucha, watu wengi sana walijaa nje
ya nyumba ya
Mchungaji Wingo, na wote walikuja kuangalia
watu ambao walilala nje ya nyumba ya
Mchungaji huku wakiwa na alama za meno shingoni na pia walikuwa uchi wa mnyama.

Kati ya watu waliolala getini alikuwepo pia
Mchungaji mwenyewe na familia yake ila wao walikuwa na mavazi yao.............

_____________
ENDELEA
_____________

...waumini wa mchungaji Wingo nao walikuwa
wengi sana, polisi walifika mapema sana katika
sehemu ya tukio, katika uchunguzi wao wa haraka haraka katika eneo lile,
waligundua watu kumi waliokuwa uchi wa
mnyama, wote walikufa na watu wengine sita
walikuwa wamepoteza fahamu.

Askari wakajadiliana wenyewe kwa wenyewe na mwisho wakaamua kuwabeba wale watu waliokufa huku wakiwa tayari wamepiga simu hospitali kwa ajili ya kuhitaji gari la wagonjwa, Ila baada ya muda kidogo, au tuseme kabla gari la wagonjwa halijafika mchungaji alizinduka na kujikuta yupo nje ya nyumba yake huku baadhi ya watu wakimuangalia na pia wakionekana wana maswali mengi vichwani mwao na mwenye majibu ni yeye mwenyewe Mchungaji Wingo

"Vipi, unajisikiaje?" Polisi mmoja alimuuliza Mchungaji Wingo baada ya kuzinduka,

"Namshukuru Mungu, maana ni mkubwa kuliko kila kitu hapa duniani" Mchungaji Wingo aliongea huku akiwatizama watoto wake na mkewe ambao nao walianza kuamka mmoja mmoja,

"Hapa ni kwako?" Polisi akamtupia swali jingine,

"Ndio, ni kwangu" Mchungaji Wingo alijibu,

" unaweza kutueleza ni nini kimetokea?" Polisi aliendelea kuhoji,

"Hapa tunajaza watu tu, ni bora tukafanyie mahojiano kituoni" Polisi mwingine alimshauri yule polisi aliyekuwa anamuhoji Mchungaji Wingo,

"Sasa si inabidi tuwabebe wote ambao ni wazima" Polisi aliyekuwa anahoji alimuuliza mwenzie,

"Hiyo ni familia yangu, mngewaacha tu, twendeni mkanihoji mimi mwenyewe, nadhani natosha" Mchungaji Wingo aliongea huku akilazimisha tabasamu,

"Hapana, ni lazima tuchukue Maelezo ya watu wrote" Polisi aliongea huku akimhimiza Mchungaji Wingo aelekee mahali gari la polisi lilipoegeshwa. Polisi wakambeba yeye na familia yake kwa ajili
ya mahojiano zaidi.

******************

Hii habari za hili tukio lililotokea nyumbani kwa mchungaji ilitangazwa na vyombo vya habari vya nchi nzima, habari zikawafikia wakubwa zake Sajenti Minja, Wakubwa zake, ikabidi washauriane,

" sasa tunafanyaje, au tumchague kijana mwingine aifuatilie hiyo kesi, kwa maana wapo wengi tu na si lazima awe Minja tu" Mkuu was polisi alimwambie mkuu wa jeshi,

"Hilo ni jambo zuri, hila kufanya hivyo ni kuitia aibu hii taasisi ya jeshi na serikali kwa ujumla. Huyu Minja hapo alipo hana hata miezi sita toka atoke mafunzoni Korea ya kaskazini, sasa huoni kumuachia asiendelee na hii kesi hayo mafunzo yake yatakuwa hayana manufaa yoyote kwa taifa?" Mkuu wa Jeshi alimuuliza Mkuu wa Polisi,

"Sasa kama kesi imemshinda tutafanyaje?" Mkuu wa Polisi aliuliza,

"Watuhumiwa unapowahoji na wakaonekana hawataki kusema ukweli uwa unawafanyaje" Mkuu was jeshi aliuliza huku akiiwasha sigara yake,

"Uwa nawashurutisha kwa kuwapa adhabu" Mkuu wa Polisi alijibu,

"Unawasulubu, si ndio?" Mkuu wa Jeshi aliuliza huku anamuangalia Mkuu wa Polisi,

"Ndio maana yake" Mkuu wa Polisi alijibu,

"Hill ndio jibu" Mkuu was jeshi aliongea huku akinyanyuka katika kiti,

"Kwa hiyo Minja nae utamsulubu?" Mkuu wa Polisi aliuliza,

"Sio nitamsulubu, tayari kishaanza kusulubiwa muda mrefu tu" Mkuu wa Jeshi alijibu huku akivaa miwani yake,

"Unamsulubia wapi?" Mkuu wa Polisi akauliza kwa mshangao,

"Nifuate" Mkuu wa jeshi aliongea huku akianza kupiga hatua kuelekea nje ya ofisi yake, wakatembea mpaka katika like jengo ambalo ndani ndipo yupo Sajenti Minja anasulubika. Walipofika walibonyeza kitufe cha kengele na baada ya muda kidogo mlango ulifunguliwa na akatoka mwanajeshi mmoja aliyewapigia saluti na kuwaachia mlango wazi ili wapite. Walipoingia ndani walinyoosha moja kwa moja mpaka sehemu alipokuwepo Sajenti Minja na kumkuta akiwa amewekwa ndani ya bwawa la kuogelea huku mikono yake ikiwa imefungwa kamba kwa nyuma na pia alifungwa jiwe kubwa ili asielee juu ya maji,

" mmemzamisha kwa muda Gani?" Mkuu wa jeshi aliwauliza vijana wake,

"Hii dakika ya ishirini" Mwanajeshi mmoja alijibu huku akiitazama saa yake mkononi,

"Dakika ishirini?, si atakuwa ameshakufa?" Mkuu wa Polisi aliuliza huku akishangaa,

"Hawezi kufa kirahisi hivyo, huyo anaweza kuzama hata siku nzima?" Mkuu wa Jeshi alijibu,

"Duh, aisee ni hatari sana" Mkuu Wa Polisi aliongea huku akisikitika,

"Mtoeni nje" Mkuu wa Polisi aliwaamuru vijana wake ambao walitekeleza agizo bila shurti yoyote. Wakamtoa Sajenti Minja nje ya maji na kumuweka pembeni. Sajenti Minja alikuwa amechoka na mwenye majeraha mengi sana usoni kutokana na mateso aliyokumbana nayo,

"Mfungueni hilo jiwe na mleteeni kiti" Mkuu wa Jeshi aliwaagiza vijana ambao walitii na kuleta kiti haraka,

"Kaa hapo mheshimiwa" Mkuu wa Jeshi alimwambia Sajenti Minja aliyekuwa anaugulia maumivu. Sajenti Minja akajinyanyua na kujiweka juu ya kiti,

"Mmempiga kama mharifu" Mkuu wa Polisi aliendelea kushangaa,

"Pole sana, sasa kilichotuleta hapa ni kitu kimoja" Mkuu wa Jeshi aliongea huku akimtupia gazeti lenye habari zilizotokea huko shinyanga kwa mchungaji. Sajenti Minja akaisoma ile habari kwa umakini mkubwa na kisha akamrudishia mkubwa wake gazeti lake,

"Umeielewa hiyo habari?" Mkuu wa Jeshi alimuuliza Sajenti Minja,

"Hapana Mkuu" Sajenti Minja alijibu,

"Hivo vifo waliokufa hao watu, havina tofauti na vifo vilivyokuwa vinafanywa na wale vijana unaowatafuta, kwa maana hiyo basi, sina budi kusema kuwa muuaji yupo shinyanga" Mkuu wa Jeshi aliongea huku akimuangalia Sajenti Minja ambaye naye alikuwa anamuangalia mkubwa wake,

"Sasa nambie unaendelea na hii kesi au bado umeshikilia msimamo wako?" Mkuu wa Jeshi aliuliza huku akiiangalia saa yake.

Sajenti Minja aakabaki kimya asijue la kujibu,

"Umesikia nilichouliza?" Mkuu wa Jeshi aliuliza huku akirudisha macho yake kwa Sajenti Minja,

"Ndio nimesikia mkuu" Sajenti Minja aliitikia kwa unyonge,

"Nipe jibu, maana kuna mambo mengine ya kufanya muda huu" Mkuu wa Jeshi aliongea kwa mamlaka,

"Naweza nikapata muda kidogo wa kufikiria?" Sajenti Minja aliuliza,

"Unahitaji muda wa dakika ngapi?" Mkuu wa Jeshi aliuliza,

"Nikipata angalau hata wa masaa kumi na mbili utanitosha" Sajenti Minja aliongea,

"Saa hivi ni saa kumi na mbili jioni, kwa maana hiyo mpaka kesho saa kumi alfajiri utakuwa una jibu, so ndio?" Mkuu wa Jeshi aliuliza,

"Ndio mkuu" Sajenti Minja alijibu,

"Mpelekeni akapumzike, mpeni kila atachohitaji" Mkuu wa Jeshi aliwaambia wale wanajeshi waliokuwa wamesimamia mateso ya Sajenti Minja,

"Sawa mkuu" Wanajeshi walijibu na kumuinua Sajenti Minja na kumpeleka wanapojua wao, Mkuu wa Jeshi akatoa tabasamu moja la karaha sana,

"Kesho akija na jibu tofauti na ninalolitaka mimi, Kambi itapata habari mbaya za mwenzao" Mkuu wa Jeshi aliongea huku akianza kuondoka,

"Utamuua au?" Mkuu wa Polisi aliuliza huku akimfuata,

"Hata wewe pia utajua kesho hiyo hiyo" Mkuu wa Jeshi alijibu na kumfanya mkuu wa Polisi anyamaze kimya.

***************************

Katika kituo cha polisi mahojiano kati ya
mchungaji na polisi yaliendelea vema, ila
mchungaji hakutaka kuwaambia kuwa mhusika
wa mauaji alikuwa nae, ila alichowaambia polisi
ni kwamba, hata yeye haelewi na hakumbuki kitu
chochote kilichotokea, zaidi ya kujikuta yuko nje
ya nyumba yake wamelala na familia yake na watu hasiowajua,

"Hiyo inawezekanaje?" Askari mmoja alimtupia swali Mchungaji huku akiwa ahamini maelezo yake,

"Hata mimi sijui imewezekanaje, ni kama maajabu Fulani hivi ya kiimani" Mchungaji Wingo alijibu huku akionekana dhahiri kushangaa,

"Kwa hiyo unadhani wale watu kumi ambao wamekufa kwa kunyonywa damu ni nani tutamuhusisha na vifo vile?" Askari akamtupia swali jingine,

"Sasa unaponiuliza mimi unataka nikujibuje, au unadhani nitasema unihusishe mimi na hivyo vifo?" Mchungaji Wingo aliuliza kwa sauti ya upole,

"Kisheria ni kwamba wewe na familia yako mpo hatiani kwa vifo hivyo" Askari aliongea huku akiandika andika katika kikaratasi kidogo juu ya meza,

"Sawa, ila hakuna mtu katika familia yangu ambaye ana uthubutu wa kuua hata mbu, sembuse mtu" Mchungaji Wingo aliongea kwa kujiamini,

"He nikikuweka ndani nitakuwa nimekosea ingawa unajitetea hivyo" Askari aliuliza,

"Siwezi kukupangia, fanya vile kazi yako inavyotaka" Mchungaji Wingo alijibu na kumfanya yule askari anyanyuke huku pingu zikiwa mkononi,

"Afande kati ya wale watu waliokutwa wamekufa kwa mchungaji, mmoja kumbe mzima" Askari mwingine aliongea wakati anaingia ndani ya chumba cha mahojiano,

"Kwa hiyo waliokufa ni tisa tu?" Askari aliyekuwa anamuhoji mchungaji aliuliza huku akianza kumfunga pingu mchungaji Wingo,

"Sasa huyo Mzee usimfunge pingu kwa maana yule mtu ambaye amezinduka amesema kuwa wamepata ajali na wala mtu yoyote asiusishwe na vifo vya wenzake" Askari aliyeingia aliongea na kumfanya mwenzake amkodolee macho,

"Una maana gani kusema hivyo?" Askari alimuuliza mwenzake,

"Kwa Maelezo ya yule mtu kule hhospitali, basis huyu mzee hana hatia" Askari mwenzake alijibu,

"Cha kuwashauri ni kwamba, kwa kuwa Huyo mmoja ameamka, ni vyema mngenipeleka na familia yangu mbele yake na aseme kama sisi tumewaua wenzake" Mchungaji Wingo aliongea kwa upole,

polisi walionekana kuridhika na maneno ya
mchungaji na familia yake, tena walimuamini
zaidi kwa sababu alikuwa mtumishi wa Mungu.
Baada ya mahojiano, polisi walimuachia
mchungaji arudi nyumbani kwake, ila wakamwambia wakimuhitaji watamfuata.

Mchungaji alipofika nyumbani kwake, moja kwa
moja akaenda kwenye chumba chake cha ibada,
akamkuta kayoza amekaa kimya anasoma biblia,
akamsalimia, kisha akamsimulia kilichotokea,
alafu akamrudisha kwa mama yake.

BAADA YA SIKU TATU..
__________________________

Jioni wakati wanaongea kuhusu mambo yaliyotokea siku tatu nyuma.

Sebuleni alikuwepo mama kayoza, Kayoza na Omari,

"Hili tatizo hata mimi linaanza kunitisha, ina maana hata mchungaji ameshindwa?" Kayoza aliuliza huku anamtazama mama yake,

"Hakuna kinachoshindikana kwa Mungu, sema tu hayo mambo yaliyotokea usiku yalimvuruga" Mama kayoza alimjibu mwanaye,

"Kwa hiyo lini tena naenda Kuombewa?" Kayoza aliuliza,

"Mchungaji amesema utakuwa unaombewa kila Siku kwa ajili ya kukujenga imani" Mama Kayoza alijibu,

"Kwani mimi sina imani?" Kayoza aliuliza,

"Yaani hauna kabisa, kwa ninavyofahamu mimi, hata ungekuwa na imani kidogo tu ungepona" Mama Kayoza alijibu,

"Alafu kitu Kingine, hii habari ya tukio lililotokea juzi kwa Mchungaji lilivyotangazwa nchi nzima, hivi huoni hatari iliyopo mbele yangu?" Kayoza aliuliza,

" mimi sioni tatizo, mbona hhakuna hata chombo cha habari kilichokuhusisha na hizo habari" Mama Kayoza alijibu,

"sawa, ila ukae ukijua kuwa Polisi wana akili sana kuliko sisi raia wa kawaida" Kayoza alimwambia mama yake,

"Wana akili kama sisi tu, mwenye akili kuliko sisi ni Mungu peke yake" Mama Kayoza aliongea kwa ukali kidogo,

"Sasa mimi sijamaanisha hivyo mama" Kayoza alijitetea,

"Mungu ni mkubwa kwa maana yoyote ile uliyoimaanisha" Mama kayoza alitilia mkazo maneno yake,
"Alafu nasikia kama mlango unagongwa vile"Omary aliongea baada ya ukimya wa muda,

"Hata mimi Nimesikia hivyo hivyo" Kayoza nae akamuunga mkono Omary

"Sasa si mkafungue, mbona mmelegea hivyo nyie?" Mama Kayoza aliongea kwa ukali.

Omary akasimama na kuelekea mlango ulipo, akaminya kitasa chini na kuvuta mlango, ile kufungua tu akakutana uso kwa uso na Sajenti Minja, Omary akarudishia mlango haraka na kukimbilia ndani............

******ITAENDELEA******

*Je Sajenti Minja atachukua hatua gani baada ya kumuona Omary?

the Legend☆
 
Wakuu nimeweka episodes nyingi kidogo sababu sitakua kabisa hewani kwa siku mbili hizi mpaka Ijumaa.
So kwa wale wanaoifuatilia riwaya hii tukutane Ijumaa, na episode nyingine ya Mkono wa Chuma itatoka pia siku hiyo.

the Legend☆
 
Wakuu nimeweka episodes nyingi kidogo sababu sitakua kabisa hewani kwa siku mbili hizi mpaka Ijumaa.
So kwa wale wanaoifuatilia riwaya hii tukutane Ijumaa, na episode nyingine ya Mkono wa Chuma itatoka pia siku hiyo.

the Legend☆
Ahsante kwa Taarifa The Legend naamini ukirudi utakuja na "memory card" mkononi😀😀
 
RIWAYA : KIJIJINI KWA BIBI.

MTUNZI : ALEX KILEO.

SEHEMU YA ISHIRINI NA TATU.

_____________
ILIPOISHIA...
_____________

"Alafu nasikia kama mlango unagongwa
vile"Omary aliongea baada ya ukimya wa muda,
"Hata mimi Nimesikia hivyo hivyo" Kayoza nae
akamuunga mkono Omary
"Sasa si mkafungue, mbona mmelegea hivyo
nyie?" Mama Kayoza aliongea kwa ukali.
Omary akasimama na kuelekea mlango ulipo,
akaminya kitasa chini na kuvuta mlango, ile
kufungua tu akakutana uso kwa uso na Sajenti
Minja, Omary akarudishia mlango haraka na
kukimbilia ndani............

______________
ENDELEA......
______________

Omary alivyofungua na kufunga mlango, kisha akarudisha
kichwa ndani, Sajenti Minja aliiona sura ya Omary na kupata mshtuko mkubwa sana, maana sura aliyoiona ndiyo ile ile inayotafutwa na serikali.

Sajenti minja bado alikuwa na uoga kutokana na lile tukio la kutaka kunyonywa damu,
kwa hiyo akabaki nje kaduwaa, huku anajiuliza
pale ndio kwa dada yake, au kakosea nyumba
kabla hajaamua chochote, akasikia mlango
unafunguliwa tena, kwa haraka sana Sajenti
Minja akatoa bastola yake, na kuilekezea mlangoni.

"vipi tena kaka, unataka kuniua mwenzio" ilikua sauti ya Mama Kayoza baada ya kufungua
mlango.

"nimemuona kijana ndani ambae anatafutwa nchi
nzima" Sajenti Minja akaongea kwa pupa huku bado akiwa anashangaa hali anayokutana nayo,

"ndio, karibu basi kwanza ndani, alafu ndio ujue
kwanini yupo hapa" mama kayoza aliongea kwa
busara,

"Haiwezekani kuingia humo, ngoja niwasiliane na Polisi makao makuu Shinyanga wake wanipe msaada" Sajenti Minja aliongea huku akiitoa simu yake mfukoni,

"We Joel acha ujinga, unatapopiga simu na kuwaita polisi utakuwa umeniweka hatiani mimi na sio huyo kijana uliyemuona" Mama Kayoza aliongea na kumfanya Sajenti Minja asitishe zoezi lake,

"Mbona sikuelewi Dada, unamaanisha nini kusema hivyo?" Sajenti Minja alimuuliza dada yake huku akimshangaa,

"Twende ndani utanielewa tu" Mama Kayoza alimwambia Sajenti Minja,

"Lakini dada ujue una hatari sana kuishi na Huyo kijana" Sajenti Minja aliongea kwa unyonge,

"Twende ndani bwana" Mama Kayoza aliongea huku akiingia ndani na Sajenti Minja akaingia ndani huku akiongozwa na
mama Kayoza, ila bastola yake, hakutaka kuificha tena, alivyoonekana, alikuwa amejiandaa
kwa lolote litakalotokea
Alipoingia sebuleni hakukuta mtu,

"kaenda wapi?" Sajenti Minja akauliza kwa mshangao na wasiwasi,

"baba vipi?!, mbona una haraka hivyo" mama
kayoza aliongea huku akiwa anaelekea sehemu kulipokuwa na vyumba ambavyo wakina Kayoza walikimbilia kujificha. Alipofika katika mlango wa chumba cha wakina Kayoza, aligonga na mlango ukafunguliwa,

"Haya twendeni mkamsalimie mjomba wenu" Mama Kayoza aliwaambia,

"Mama mbona unataka kutupeleka matatizoni?" Kayoza aliongea huku akiwa ana hofu kuu,

"Ebu twendeni uko, yule hana tatizo" Mama Kayoza aliongea na kuanza kutoka nje, nyuma yake alikuwepo Kayoza na Omary.

Walipotokea sebuleni Sajenti Minja akawaelekezea bastola na kuwafanya wakina Kayoza kutaka kukimbia ila mama yao aliwahi kuwashika,

"Mnakimbia nini nyie? Na wewe jiheshimu basi, kwangu ni mahali pa amani, hayo mabastola yako use unayatolea huko huko na sio hapa" Mama Kayoza aliongea kwa ukali huku anamuangalia Sajenti Minja,

"ehe!, dada unaishi vipi na wauaji?" Sajenti Minja akamuuliza mama kayoza huku bado bastola yake ikiwa mkononi,

"Ebu lifiche hilo libunduki lako ndio uhoji hayo maswali yako" Mama Kayoza alimwambia Sajenti Minja na Sajenti Minja akatii kwa kuirudisha bastola sehemu yake,

"Dada mbona unawatetea sana, ni nani zako Hawa?" Sajenti Minja aliuliza huku akiwaangalia kwa chuki wakina Kayoza,

"hao ni wajomba zako, huyo hapo ndio kayoza, na
huyo mwingine ni rafiki yake" Kama kayoza
alimwambia sajenti Minja huku akiwaonyeshea
kidole wakina Kayoza.

"Kayoza? Kayoza mwanao au?" Sajenti Minja aliuliza huku akiwa ahamini kilichozungumzwa na dada yake,

"Haswaa, Kayoza mwanangu ndio huyo" Mama Kayoza alijibu kwa furaha,

"alah!, kayoza ndio kawa mkubwa hivi?" sajenti
Minja alijishtukia kauliza bila matarajio.

"kawa mbaba haswa" mama kayoza akajibu.

Sajenti Minja akairudisha bastola yake kiunoni,
kisha akamgeukia kayoza,

"hujambo mjomba?" Sajenti Minja akamsalimia kayoza.

"sijambo shikamoo" kayoza nae akamsalimia
mjomba yake huku nae akiwa ahamini kinachotokea ingawa ni kweli aliambiwa Sajenti Minja ni ndugu yake,

"marhaba, za siku?" Sajenti Minja akaendelea kumjulia hali Kayoza tena kwa uchangamfu kama hawakuwa maadui muda mfupi uliopita,

"nzuri tu" kayoza akajibu.

"unanikumbuka mimi?" Sajenti Minja akamuuliza kayoza,

"sikukumbuki" kayoza alimjibu huku akitingisha kichwa kwa kukipeleka kushoto na kulia,

"kalikuwa kadogo sana" Sajenti Minja alisema huku akimgeukia dada yake.

"tena sana, kalikuwa na miaka sita, kipindi tulipoenda kumuona mimi na wewe kule kigoma" Mama kayoza akamjibu.

"ehe, kakuelezea sababu ya kufanya mauaji ya kutisha namna ile" Sajenti Minja akamuuliza dada
yake,

"yeye mwenyewe alikuwa hajui, hadi mimi nimemwambia ndio akajua" Mama Kayoza ndivyo
alivyomjibu sajenti Minja. Sajenti akaonekana kushtuka kutokana na lile jibu kutoka kwa dada yake,

"kwa hiyo wewe unajua
sababu?" Sajenti Minja akamuuliza Mama Kayoza.

mama kayoza akamuelezea mwanzo mpaka
mwisho wa tatizo analokumbana nalo Kayoza.

"Sasa utachugua mwenyewe umpeleke kwenye vyombo vya sheria au umlinde" Mama Kayoza alimaliza kwa maneno hayo na kumfanya Sajenti Minja ainamishe kichwa chini akitafakari,

"Kwa hivyo unataka kuniambia kwamba huyu Kayoza hawezi kuwa mtu bila sababu mpaka huyo mtu mwenyewe stake kumdhuru?" Sajenti Minja aliuliza baada ya muda kidogo wa kutafakari,

"Ndio hivyo na pia kama huyo mtu atataka avunje masharti ya mzimu" Mama Kayoza alijibu,

"Kumbe nilikuwa nataka kumdhuru mtu asie na hatia, tens ndugu yangu" Sajenti Minja aliongea kwa masikitiko,

"Na hayo majeraha usoni kwako ni ya nini?" Mama Kayoza alimuuliza Sajenti Minja,

"Hii ni adhabu ndugu yangu" Sajenti Minja alijibu,

"Adhabu?, adhabu gani kama umepata ajali?" Mama Kayoza aliuliza,

"Ndio adhabu zetu za kijeshi" Sajenti Minja alijibu,

"Na ulifanya kosa gani mpaka upewe hivyo adhabu?" Mama Kayoza aliuliza kisha Sajenti Minja akaeleza mwanzo mpaka mwisho.

"Kwa hivyo hii kesi ndio imekutesa hivyo" Mama Kayoza aliuliza,

"Yaani nnilikubali kuirudia kwa sababu nilitaka nipate mwanya wa kukimbia nje ya nchi kabisa" Sajenti Minja aliongea,

"Haya sasa, wewe kama mjomba kama baba, una maoni juu ya hili tatizo" Mama Kayoza alimuuliza Sajenti minja,

"Hapa hakuna njia zaidi ya mganga, kwa maana hili tatizo limekaa kihasili hasili sana" Sajenti Minja akashauri kuwa ni lazima Kayoza
apelekwe kwa wataalamu wa tiba za jadi,

"Haiwezekani, atapelekwa kuombewa atapona tu" Mama
Kayoza alipinga,

"Ujue mama kwenda kwa mganga sio kupinga nguvu ya Mungu, inawezekana huko ndipo Mungu atatusaidia" Kayoza alimshauri mama yake,

"Na pia tukienda kwa mganga sio mwisho wa kwenda kanisani, ikifika siku ya kwenda kanisani aende na ikifika siku ya kwenda kwenye tiba asili aende" Sajenti Minja aliongezea,

"Sawa, maana cha muhimu ni mtoto kupona" Mama Kayoza alikubaliana na kaka
yake na maongezi mengine yakaendelea huku Mama Kayoza akiandaa mezani chakula cha jioni.

Baada ya chakula cha pamoja, Sajenti Minja alimwambia kayoza kuwa kesho atakuja
kumchukua asubuhi, ampeleke kwa mzee mmoja
ambae ni mganga anaefahamika pale Shinyanga.

"Wewe si umekuja Leo tu, huyo mganga umemjulia wapi?" Mama Kayoza aliuliza kwa mshangao,

"Shinyanga nimekaa sana na naijua vizuri sana kuliko unavyodhani" Sajenti Minja alijibu huku akicheka na kumfanya Mama Kayoza aishie kuguna tu,

"Kwa hivyo umefikia wapi, au lodge?" Mama Kayoza alimuuliza Sajenti Minja,

"Kuna nyumba nimepewa na viongozi ambayo nitaishi kwa muda" Sajenti Minja alijibu,

"Mi nikajua utaishi hapa bwana na ndio maana Jana ulivyonipigia simu na kuniambia unakuja sikutaka kuwaambia hata wanangu kuwa unakuja" Mama Kayoza aliongea,

"Mimi naona niwaache, ila Kayoza jiandae kesho mapema nakuja kukuchukua ili nikupeleke kwa babu" Sajenti Minja aliongea huku akisimama,

"Mbona unaondoka mapema, hata hukai tuongee ongee" Mama Kayoza alimwambia Sajenti Minja,

"Ngoja niwahi kupumzika maana nnimechoka sana" Sajenti Minja aliongea na kisha akasindikizwa na Dada yake mpaka nje na kuondoka zake.

****************

Kesho yake, sajenti Minja aliwai kufika pale kwa
dada yake na kunywa chai kabisa, kisha Kayoza
na Omari wakajitayarisha, saa nne iliwakuta wapo
katika foleni ya kuingia kwa mganga,
foleni ilikuwa ndefu.

Baada ya kusubiri sana, muda wao ulifika na waliingia kuonana na
mganga saa sita kasoro, mganga akawaambia
kuwa tatizo lao ni kubwa, na wakitaka liishe, ni
lazima wapeleke maiti ambae katoka mochwari.
Ilikuwa ngumu, ila kwa ajili ya shida, wakasema wataipeleka usiku, mganga akasema itakuwa
vizuri sana hiyo maiti ikifika usiku, ili kazi ianze usiku huo huo.
Walipotoka kwa mganga wakaelekea moja kwa
moja hospitalini, walipofika, Sajenti Minja
akashuka ndani ya gari, kisha akaenda moja kwa
moja hadi mochwari, akaongea na mzee mmoja hivi ambae ndiye alikuwa mlinzi wa kile chumba cha kutunza maiti na alimueleza
kuhusu shida yake ni kutaka kupatiwa maiti moja, mara ya kwanza, babu
anaetunza maiti alikuwa mgumu kukubali, ila
alipoambiwa anapewa laki laki tatu, akakubali
haraka, na akampa mbinu ambayo sajenti Minja
atatumia kuchukulia maiti maiti usiku.

Wakampa babu pesa kiasi cha laki moja na wakakubaliana kuwa kiasi kilichobaki watammalizia usiku pindi watakapokabidhiwa maiti.

Kisha wakaenda zao nyumbani kusubiri muda ufike.

*****************

Usiku ulipofika, Sajenti Minja na wakina Kayoza
wakaenda nyuma ya chumba cha kuifadhia maiti,
ilikuwa saa tano usiku, hata watu waliokuwa
wanapita katika sehemu ya mochwari walikuwa
wanahesabika,
Yule babu mtunza maiti, akaingia ndani, akatoka
na maiti amembeba mabegani, kisha akafungua
geti la nyuma, akawakabidhi wakina Sajenti
Minja, kisha akapewa pesa yake iliyobakia na kuwaachia maiti yao.

Ile maiti waliiweka katika buti ya gari, kisha
wakaanza safari ya kwenda kwa mganga. Ulikuwa usiku tulivu na ukizingatia kulikuwa nje ya nje, basi kulikuwa na hali ya kutisha kidogo kutokana na mapori machache maeneo Yale.

Walipofika katika sehemu ambapo kulikuwa
kumetulia na kulikuwa na kapori kidogo, ni umbali
mdogo kutoka nyumbani kwav mganga aliyewaagiza maiti, walisimamishwa na gari
ya polisi wa doria waliokuwa wanaimarisha ulinzi kile kipindi cha usiku.

"mnaenda wapi?" askari mmoja akawauliza,

"nyumbani" Sajenti Minja akajibu huku wasiwasi mwingi ukiwa umemtawala,

"huku juzi tulipishana na watu nao tulipowauliza
wakasema hivyo hivyo, kesho yake tukasikia
majambazi yamepavamia na kuiba mali za watu, na nyie msije mkawa ni miongoni mwa hao waarifu" Askari yule akamwambia sajent Minja huku akiwa anawatilia mashaka,

"sisi hatuwezi kuwa majambazi, afande" Sajenti
Minja akajitetea,

"hatuwezi kuwaamini, hadi tuwakague" yule askari aliongea huku akimulika upande wa ndani wa gari kwa kutumia tochi,

"Sisi ni watu safi" Sajenti Minja aliongea huku ndani ya nafsi yake akiomba Askari wasikague buti ya gari,

"Na huku kuna mini?" Askari mwingine aliongea huku akifungua buti ya gari na kuwafanya wakina Sajenti Minja waishiwe nguvu....

******ITAENDELEA******

the Legend☆
 
RIWAYA : KIJIJINI KWA BIBI.
MTUNZI : ALEX KILEO.

SEHEMU YA ISHIRINI NA NNE.

______________
ILIPOISHIA...
______________

Walipofika katika sehemu ambapo kulikuwa
kumetulia na kulikuwa na kapori kidogo, ni umbali
mdogo kutoka nyumbani kwav mganga
aliyewaagiza maiti, walisimamishwa na gari
ya polisi wa doria waliokuwa wanaimarisha ulinzi
kile kipindi cha usiku.

"mnaenda wapi?" askari mmoja akawauliza,

"nyumbani" Sajenti Minja akajibu huku wasiwasi
mwingi ukiwa umemtawala,

"huku juzi tulipishana na watu nao tulipowauliza
wakasema hivyo hivyo, kesho yake tukasikia
majambazi yamepavamia na kuiba mali za watu,
na nyie msije mkawa ni miongoni mwa hao
waarifu" Askari yule akamwambia sajent Minja
huku akiwa anawatilia mashaka,

"sisi hatuwezi kuwa majambazi, afande" Sajenti
Minja akajitetea

"hatuwezi kuwaamini, hadi tuwakague" yule
askari aliongea huku akimulika upande wa ndani
wa gari kwa kutumia tochi,

"Sisi ni watu safi" Sajenti Minja aliongea huku
ndani ya nafsi yake akiomba Askari wasikague
buti ya gari,

"Na huku kuna mini?" Askari mwingine aliongea
huku akifungua buti ya gari na kuwafanya wakina
Sajenti Minja waishiwe nguvu....

____________
ENDELEA....
____________

...."ebu toa lock ya buti" Askari yule akamuamrisha Sajenti Minja baada ya kufungua buti bila mafanikio.

Sajenti Minja akaona akifanya uzembe kidogo,
anaweza kuvuliwa nguo bila kutegemea, kwa
maana kwa Sajenti kama yeye kukutwa na maiti
ndani ya gari ni aibu kubwa.

"unajua unaongea nani?" sajenti Minja akamuuliza yule askari wa doria kistaharabu,

"haijalishi, kukujua wewe nani nadhani hakutasitisha kukukagua. fungua buti bwana" yule askari akaongea kwa ukali.

"Ngoja nikuoneshe kitambulisho changu" Sajenti Minja akatoa kitambulisho chake, akamtupia yule
askari,

"alafu inaonekana una jeuri sana kijana?, unamtupia nani likitambulisho lako?" yule afande
akawa anaongea huku akiwa anamfuata Sajenti Minja akiwa na gadhabu, alipomfikia, yule askari
akamtandika sajenti Minja kibao cha nguvu.

"haya okota likitambulisho lako na unipe mikononi, sio unirushie, umeona mi limbwa
eeh!?", yule askari wa doria akahoji kwa ukali mpaka mate yakamtoka,

Sajenti Minja akaona asilete mabishano wakati wanachelewesha kazi kwa mganga, akakubali kuwa mjinga, akakiendea
kile kitambulisho, akakiokota kisha akampatia yule askari wa doria.

Yule askari akakipokea,
akashtuka baada ya kukiangalia kwa nje, maana kilikuwa cha kipolisi, alipokifungua kwa ndani, akakisoma ndani, kisha
akammulika Sajenti Minja na tochi usoni, ghafla
akampigia saluti, wale askari aliokuwa ameongozana
nao, kuona hivyo, nao wakampigia saluti Sajenti Minja.

"samahani sana mkuu, mi sikujua kabisa" yule
askari wa doria aliongea huku sura yake
ikionesha kama anataka kulia kutokana na hofu aliyokuwa nayo,

"usijali, ndio kazi inatakiwa kufanywa hivyo" Sajenti Minja ndivyo alivyomjibu, kisha
akamuuliza, "bado unataka nifungue buti?"

"ha...hapa...hapana mkuu" yule askari wa doria akajibu kwa sauti iliyojaa kitetemeshi.

"Kwa hivyo mnaweza kuturuhusu twende?" Sajenti Minja aliwauliza,

"Nenda tu mkuu, samahani sana kwa usumbufu" Askari alijibu huku akimrudishia Sajenti Minja kitambulisho chake.

Sajenti Minja akakipokea kitambulisho chake na wakaingia ndani ya gari, kisha wakaendelea na safari yao.

"wajomba pale bila kutumia akili tulikuwa tunaumbuka" Sajenti Minja alianzisha maongezi baada ya kuondoka eneo walilosimamishwa,

"Mimi ndio nilikuwa nimekata tamaa kabisa" Omari nae akachangia,

"Mimi akili niliyokuwa nayo ilikuwa ni kutoka nduki tu" Kayoza aliongea na kufanya wenzake wacheke,

"bila ya kitambulisho, sasa hivi sijui tungekuwa
wapi?" Sajenti Minja akasema huku akiwa anaipaki gari nje ya nyumba ya mganga.

Wakashuka, kisha wakaenda hadi mlangoni kwa
mganga, wakabisha hodi, wakafunguliwa na
msaidizi wa mganga,

"sisi tulijua hamuwezi kuja tena, maana giza limekuwa kubwa sana" Msaidizi wa Mganga
aliwaambia baada ya kuwagundua,

"tulipata matatizo kidogo njiani, ila yameisha" Sajenti Minja aliongea huku akiwa anaingia ndani na nyuma yake wakina Kayoza wakimfuata.

"Sasa itabidi ifanyike ingawa tumechelewa kidogo" Mganga aliongea baada ya kuwaona,

"Itakuwa vyema sana" Sajenti Minja aliongea,

"Sasa huyo kijana mwenye tatizo inabidi asogee hapa tumfanyie mambo kidogo" Mganga aliongea huku akitandika kitambaa cheusi chini. Kayoza akasogea na kuambiwa Amalie kile kitambaa cheusi na mganga akaanza kufanya matambiko.

Baada mganga kumaliza matambiko madogo pale
nyumbani, wale wasaidizi wa mganga, walikuwa
wanne, wawili wakambeba yule maiti na wawili
wengine wakabeba vifaa vya uganga, hapo
ilikuwa saa sita na dakika zake za kutosha,
mganga akawa anaongoza msafara.

"Hizi sehemu zinatisha ila mnabidi mzizoee" Mganga aliwaambia wakina Sajenti Minja wakati wakiwa njiani,

"Hizi sehemu za kutisha nimeshazizoea sana, labda vijana wangu hapa ndio wageni" Sajenti Minja alijibu,

"Kwa hivyo mambo haya ya kutembea kwa waganga ushayazoea sana?" Mganga alimuuliza Sajenti Minja,

"Hapana, kwa masuala ya kiganga mi ndio mara yangu ya kwanza" Sajenti Minja alijibu,

"Sasa hata mazingira ya kutisha umeyazoeaje?" Mganga aliuliza,

"Kutokana na kazi zetu mzee wangu" Sajenti Minja alijibu,

"Kwani nyie mnafanya kazi gani?" Mganga aliwauliza,

"Hao vijana wangu wanasoma chuo, mimi ni muangaikaji tu wa sehemu mbalimbali katika kutafuta ridhiki" Sajenti Minja alijibu,

"Sasa kama huyu kijana mwenye matatizo yupo Chuo huko chuo anaishi vipi na chuo mzimu" Mganga alihoji,

"Matatizo matatizo tu na ndio maana tumemleta hapa" Sajenti Minja alijibu na ukimya ukatawala tena njiani.

Walitembea mda wa saa nzima hadi sehemu za makaburini.

" inabidi tuchague kaburi moja ambalo limetengenezwa vizuri na liwe la mwanamke" Mganga alitoa maelekezo na wale wasaidizi wake wakatawanyika kila mmoja na upande wake wakitafuta hilo kaburi zuri alilozikwa mwanamke.

"Naona hili hapa linafaa" Msaidizi mmoja wa mganga alipaza sauti na watu wote wakaelekea eneo alilopo.

Walipofika katika kaburi moja lililosakafikiwa
vizuri, Mganga alilidhika nalo baada ya kuona kila anachokihitaji kipo.

Mganga akawaamuru wasimame, kisha
akachukua kikapu cha uganga akatoa vifaa vyake
akavipanga kulizunguka lile kaburi,

"Were kijana njoo ulale hapa juu ya hili kaburi" Mganga alimwambia kayoza,

"Mi naogopa mzee" Kayoza aliongea huku akiwa na wasiwasi,

"We mpumbavu mini, ebu lala hapo kabla sijakuchapa makofi, we unafikiri utaponaje kama ukikahidi maneno ya mganga" Sajenti Minja aliongea kwa ukali, Kayoza akakubali kulala hivyo hivyo huku aakitetemeka.

Baada ya Kayoza kulala juu ya kaburi, mganga akammwagia madawa yake Kayoza kichwani, haikuchukua
hata dakika moja, Kayoza akapoteza fahamu na kulala kama maiti,

"Haya mchukueni huyo maiti na mumlaze pembeni ya huyo kijana" Mganga akawaamuru wasaidizi wake
wamchukue yule maiti na kumlaza pamoja na
kayoza, wasaidizi wakatekeleza agizo.

"Kazi ndiyo inaanza, sharti kubwa na la kuzingatia ni kwamba kazi itakapoanza haitatakiwa ionekane damu ya kitu chochote kile" Mganga aliongea,

"Hata ya mbu?" Sajenti Minja aliuliza kutokana na eneo like kuwa na mbu wengi,

"ndio, kama mbu atakung'ata hata usimuue, maana ukimuua ile damu yake inaweza kuwa tatizo kwetu" Mganga aliongea kwa msisitizo,

"Na ikionekana ni kipi kitachotokea?" Sajenti Minja aliuliza,

"Huu mzimu tunaoutoa hapa, nguvu zake zipo kwenye damu ya kila kiumbe, kwa hiyo damu itakapoonekana, mzimu atapata nguvu na kati yetu hapa hakuna atakayepona" Mganga alitoa Maelezo,

"Hilo litawezekana" Sajenti Minja alijibu,

"Na pia kama mtu ana kidonda ajitahidi akizibe kisionekane" Mganga alitilia mkazo,

"Basi kazi ifanyike tu, naona Maelezo yako yamejitosheleza" Sajenti Minja aliongea,

"Kwa hiyo hapa kazi inayofanyika ni kuutoa huu mzimu kutoka kwa kijana wenu na kuuingiza katika maiti alafu kazi itayofuata ni kuizika hivyo maiti pamoja na mzimu" Mganga alimaliza.

Mganga akaanza kazi yake, alimwaga madawa
eneo lote, kisha akaanza kuongea lugha
anayoijua yeye, alifanya kwa nusu saa, kisha
likatokea dubwana la ajabu kwenye mwili wa
Kayoza, kila mtu alipata uoga isipokuwa mganga tu.

Sasa like dubwana likawa kama linavutwa kutoka kutoka kwenye mwili wa Kayoza, ila likawa
halitaki,
hiyo hali ilienda kama saa nzima, mganga
akaanza kuona mafanikio, lile dubwana lilishatoa
mwili mzima ikawa bado miguu, na mwisho hadi miguu ilitoka na likaanza kudumbukia katika ile maiti.

Mara ghafla panya akatokea
kichakani, alikuwa kama anakimbizwa na kitu,
akawa anaelekea kwenye miguu ya Omary, katika
jitihada za kumkwepa, Omary akajikuta anamkanyaga yule Panya,
damu ikaenea katika viatu vya Omari, mganga
aliliona lile tukio,
akajikuta anasema kwa sauti iliyokata tamaa

"tumekwisha...".

Na wakati huo huo mzimu ukachomoka kutoka katika mwili wa maiti na huku ukifoka kwa hasira kiasi kwamba ndege na wadudu waliolala maeneo Yale ya makaburini waliamka na kukimbia hovyo..............

******ITAENDELEA*******

*Je mganga atafanikiwa kuutuliza mzimu uliokuwa na hasira ya kudhuriwa au mzimu ndio utawamaliza wote waliotaka kumdhuru?

the Legend☆
 
Back
Top Bottom