Riwaya: Mwanamke Kama Mama Yangu

Riwaya: Mwanamke Kama Mama Yangu

RIWAYA: MWANAMKE KAMA MAMA YANGU

MTUNZI: KELVIN KAGAMBO

SEHEMU YA TISA (9)

ILIPOISHIA…

Hebu vuta picha ungelikuwa ni wewe. Unarejea nyumbani humkuti Mke wako na mbaya zaidi unakuta amemtelekeza mtoto namna ile. Hiyo haitoshi anakupelekea unapata hasara kwa kuvunja kitasa cha mlango kama hivi nilivyofanya mimi, ushishie hapo tu, kumbuka kuna nguvu kazi ambayo uliitumia wakati wa kuvunja mlango wa stoo na kadhalika. Ni maudhi hakika.
Nilipanga kumuadhibu tena adhabu ambayo ingerandana na kosa lake ni kipigo tu na sidhani kama kuna nyingine.

SHUKA NAYO…

Basi baada ya kuhakikisha mwanangu amekuwa safi nikaka nae pale tukitazama televisheni huku nikifanya mawasiliano na fundi wa kuja kunirekebishia mlango wangu.
"Leo siwezi kuja Bosi wangu labda kesho" akanambia fundi.
Basi sikuwa na jinsi, nilijipanga kulala mlango wazi kwa uzembe wa Ashura.

***********************
Tangu saa tisa mchana niliporejea nyumbani hadi saa 12 za jioni Mke wangu hakuwa amerudi.
Mnamo saa moja na robo hivi ndipo aliponusisha pua yake nyumbani. Alirejea akanikuta sebuleni na Mwanangu na bila shaka alitaraji kunikuta kwani gari niliegesha nje hivyo ilimtambulisha kuwa nimerudi.
"Heee! Umeru..di?" akaniuliza kwa uoga tena swali ambalo jibu lake lilikuwa wazi kuwa nimerudi na ndiyo maana nipo nyumbani. Sikumjibu, nilimtazama tu huku nikitamani Mungu anigeuze kuwa Simba mkali ili nimrukie na kumjeruhi vibaya Mwanamke huyu mpuuzi.
"Ulikuwa wapi?"
"Aaah, nilikuwa hapo kwa Mama Alphonce" akanijibu kwa kujiamini akidhani labda nilirejea nyumbani muda huo.
"Wapi?" nikamuuliza kana kwamba sikusikia jibu lake la awali.
"Jamani si hapo" akanijibu mara hii akiwa na shaka na jibu lake.
Nikamuweka mtoto pembeni, nikasimama na kumsogelea wakati huo akirudi nyuma kwa woga.
"Unaenda wapi?" nikamuuliza huku nikimfuata
"Wewe si unataka kunipiga" akanijibu huku kama anataka kulia.
"Nikupige kwani umekosea nini"
"Mimi sijui nikuulize we..." akataka kusema lakini kabla hajamalizia sentensi akagundua kwamba alifika mwisho wa kurudi nyuma kwa kugusa sofa. Hapo nikapata fursa ya kumtia mikononi. Nikamshika kwa nguvu mkono wake wa kulia.
"Ulikwenda wapi?" nikamuuliza, hapo hata sura yangu ikiwa imebadilika kabisa kuwa ya kikatili. Sikutaka masihala tena na laiti kama atajichanganya kidogo tu basi atajuta kunifahamu.
"Nili...kuwa kwa Mama...Alp...." akataka kunidanganya tena lakini safari hii sikutaka kumpa nafasi ya kufanya hivyo. Kabla hata hajamaliza sentensi yake hiyo nilimuwasha kibao kimoja cha nguvu kwenye shavu lake la kushoto na kumpeleka mpaka chini.
Sikuamini kama ni mimi niliyefanya vile kwani hata siku moja sijawahi kumuadhibu mwanamke kwa mtindo huo, alijiliza pale chini na kunifanya nimuonee huruma.
"Automatically" nikajikuta nimenywea, huruma ilinivaa ghafla na ikawepo kila sababu ya kumbembeleza Mke wangu ikiwezekana kumuomba msamaha kabisa.

Nikachutama kwa unyonge ili kumkaribia pale alipokaa akilia huku kichwa amekilaza kwa chini na kufunika uso kwa mikono.
Nikapeleka mkono wangu kwenye bega lake ili nimbelembeze na kumuomba msamaha kwa kile nilichofanya lakini ghafla Mke wangu alikurupuka na kunisukumia mbali, nikadondoka.
Akasima, akanitazama kwa jicho la kishankupe lililojaa shari, hasira na kisirani juu yangu.
Akanipandisha, akanishusha tena kwa dharau kana kwamba sikuwa Mume wake, hiyo haitoshi akanitemea na mate kiasi kisha akatimka kuelekea chumbani.
Kilikuwa ni kitendo cha utovu wa nidhamu hasa kwa mtu ambaye nimemlipia pesa zangu nyingi na kumuoa na si hayo tu ni mimi ambaye humpanda linapokuja suala la sita kwa sita na si yeye sasa inakuaje anidharau kiasi hiki (Si lugha nzuri niliyoitumia lakini imenibidi, dharau za Mke wangu zimevuka mipaka na viwango).

Sikumfanya kitu kwa kweli kwani niliamini kwamba laiti ningeamua kucharuka basi lazima tungegawana majengo ya Serikali; Ningepelekwa Gerezani na yeye Muhimbili tena ICU kama si Mochwari.
Nimeumbwa na hasira mbaya kweli kweli na nilijigundua kipindi nasoma sekondari.
Niliwahi kumtandika jamaa mmoja aliyenikorofisha hadi alipoteza fahamu na kujisaidia haja kubwa. Nilidhani amepoteza maisha, nikakimbia na hata nyumbani sikuonekana kwa siku kadhaa lakini nashukuru Mungu alinisaidia, Jamaa huyo hakuwa amekufa na wala sikuadhibiwa vikali.
Nikajifuta mate aliyonitemea na kunyanyuka, nikarudi kwenye sofa nililomuweka mwanangu nikaketi pembeni yake. Akawa ananitazama huku akikenua hadi nikahisi labda alielewa lile tukio lilitukia.

Lakini haiwezi kuwa kweli, ni mtoto mdogo tu ambaye bado hajawa na uwezo wa kujua baya na jema. Labda alicheka kwasababu mtu ampendaye alikuwa pembeni yake.
Nilimbembeleza akalala na nikautumia muda huo kuandaa chakula cha jioni.
Ilinibidi nibebe jukumu hilo kwani Mke wangu alijifungia ndani tangu nimcharaze kibao. Nilipanga kupika wali kwa samaki. Basi nikachambua mchele na kuandaa samaki kisha nikapika.
Nilipoivisha nilitenga mezani na kuanza kula huku nikiacha chakula kingine kwenye 'hot pot' ili Mke wangu ale atakapoamka.
Aliamka na kuja sebuleni kabla hata sijamaliza kula, akasogea hadi yalipokuwa mabakuli yenye wali na samaki. Akafunua lile lenye wali, akatazama kisha akafunika halafu akafunua na hili lenye samaki.

Nikamuona kakunja mdomo kana kwamba kile kilichokuwa ndani ya 'hot pot' kilimchefua.
"Karibu kula" nikamwambia na nilifanya hivyo ili kujua kama bado alikuwa na hasira ama zilikwisha.
"Unakula, unajaza mavi ili ukienda chooni upate cha kukinya" akanijibu hivyo tena kwa madoido yenye kuashiria dharau ya nyota tano.
"Unasemaje!?" nikamuuliza nikiwa siamini kama kuna siku moja Ashura angethubutu kunijibu jeuri namna ile.
"Ujasikia ama unataka faida? Kula mwenyewe hiyo mitapishi" akanambia.
Sikutaka kuwa Hitla, nikatumia maneno laini yenye busara tele ili kuhakikisha 'temper' yangu haipandi kwani kujibizana kungepelekea nipandwe na hasira na pengine ningemfanza kitu mbaya.
"Ashura Mke wangu hufahamu kuwa unakufuru kwa kuita chakula matapishi" nikamwambia.
"Chakula kitakuwa hicho, ngoma ya wanaokula ipigwe nawe utatoka" akanijibu kwa kejeli zaidi.
"Sawa, sikukulazimisha kula, waweza kurudi ndani kuendelea kulala"
"Hovyo, kulala kwangu kunakuhusu nini, mtazame sura yake ilivyompauka kama shuka la gesti" akanitusi.
Hakika alikokuwa akielekea kulikuwa ni kubaya na sidhani kama ningeweza kuvumilia.
"Ashura hebu naomba kaa mbali na mie nisije nikakupi...." nikataka kusema lakini alidakia kabla hata sijamalizia sentensi yangu.
"Unipige? Kama mwanaume kweli uliyekamilika kuanzia juu hadi chini thubutu kunyanyua Mkono wako na kunipiga" akanitisha. Nikashindwa kuvumilia, nikajikuta nimenyanyuka kwa hasira na kumfuata lakini kabla hata sijamfikia akanyanyua bakuli yenye mchuzi wa samaki na kunimwagia.

Alifanya hivyo ili kujihami kwani alifahamu fika kwamba kipigo cha paka mwizi ndicho kilichokuwa kikifuata.
Lakini angelijua hata asingefanya upuuzi huo kwani ndiyo alikuwa amenipaka pilipili ya macho. Hasira zikanivaa tena ni mara mbili ya kawaida na niliapa kumfanya kitu mbaya sana.
Nikatupa jicho na kutazama jinsi mchuzi ulivyochafua fulana yangu nyeupe niliyovalia, ilikuwa ni jezi ya Manchester United na nililetewa zawadi na Binamu yangu aishiye jijini Manchester, Uingereza.

Tendo bila kuchelewa nikajikuta nimemrukia Ashura, nikamuwasha kofi moja la kilo saba, akazunguka na kabla hajatulia nilimpiga kata funua moja iliyompaisha juu kimo cha ng'ombe wa kisasa na aliporudi chini ilikuwa ni kama kiroba cha matango kilichoangushwa na kuri aliyeishiwa nguvu.
Bado huikuwa imetosha, nikamnyanyua na kumsimamisha, tukawa tunalingana kwa kutazama uso kwa uso. Ghafla nikajikuta nimemtishwa ndoga moja kwenye paji la uso hadi akapasuka. Nikamwachia, akawa anakwenda chini bila kujizuia kama maiti.
"Tiii" akafika chini na hiyo ilikuwa imetosha.

***********************************
Mabenchi ya hospitali hayakuwa yakinitosha, tena naweza sema yalikuwa na miba kama sio moto.
Nikawa nakaa sekunde mbili mara nainuka tena huku dua zangu zikiwa ni kumuona Ashura anapona.

Ni baada ya kile kichapo kikali nilichomshushia. Alizimika ghafla na ilinibidi nimuwahishe hospitali kabla ya tatizo halijawa kubwa.

Nikiwa hapo mara waliingia ndugu zangu, Baba, Mama na Kaka zangu wawili ambao ni watoto wa Baba Mkubwa.
"Vipi? Nini kimetokea?" ndilo lilikuwa swali lao la kwanza kwangu kwasababu nilipowapa taarifa niliwaeleza kwamba Ashura amelazwa lakini sikuwaambia ni kwasababu ipi.

Sikuwajibu kwani bila shaka jibu langu lingeniponza, unadhani ukimueleza mtu kwamba Ashura amelazwa kwasababu nimempiga si ningeonekana punguwani. Wengi wangenichukulia mpuuzi kwa kumuadhibu Mke hadi kuwa mahututi.
"Jamal hebu tueleze nini kimetokea" Mama akambia lakini niliendeleza msimamo wangu wa kutojibu.
"Au umempiga mwenzako wewe?" Kaka yangu mmoja akauliza na kunifanya nisituke.
"Itakuwa, itakuwa umempiga mwenzio wewe" akaongezea Baba baada ya kuona jinsi nilivyosituka.
Sikuwa na cha kuongeza hapo, nikabaki nimenywea kama aliyemwagiwa maji baridi lakini kabla mjadala haujaendelea na kuwa mkubwa familia ya Mke wangu nayo ikaingia.
"Vipi jamani?" likawa swali la kwanza. Wakawa wanataka kufahamu hali ya mgonjwa.

Lakini kabla hata hawapatiwa jibu mlango wa chumba alichokuwa Mke wangu akihudumiwa ulifunguliwa na akatoka Dakatari. Tulimvamia ili atujuze hali anayoendelea nayo Mke wangu.
****************************

ILI KUFAHAMU HALI YA MKE WANGU ASHURA USIKOSE SEHEMU YA KUMI YA RIWAYA HII.

KUPATA RIWAYA HII NA NYINGINE NYINGI UNAWEZA KUMTAFUTA NDUGU MWANDISHI KWA NAMBA TAJWA HAPO JUU.
 
RIWAYA: MWANAMKE KAMA MAMA YANGU

MTUNZI: KELVIN KAGAMBO

SEHEMU YA KUMI (10)

ILIPOISHIA…

Sikuwa na cha kuongeza hapo, nikabaki nimenywea kama aliyemwagiwa maji baridi lakini kabla mjadala haujaendelea na kuwa mkubwa familia ya Mke wangu nayo ikaingia.
"Vipi jamani?" likawa swali la kwanza. Wakawa wanataka kufahamu hali ya mgonjwa.
Lakini kabla hata hawapatiwa jibu mlango wa chumba alichokuwa Mke wangu akihudumiwa ulifunguliwa na akatoka Dakatari. Tulimvamia ili atujuze hali anayoendelea nayo Mke wangu.

SHUKA NAYOOO….

"Anaendelea vyema, Mungu amesaidia" akatujibu hivyo na kuongeza. "Subirini hapo, tutazungumza vyema zaidi" akasema na kuondoka kuelekea ofisini kwake.
Tuliketi kwenye benchi huku Mimi nikiwekwa kitimoto na kulazimishwa kusema kilichosababisha Ashura kuwa hospitalini hapo.

Idadi yao ilinifanya nishindwe kuendeleza msimamo wangu wa kutowaeleza. Ilinibidi niwe wazi kuwaeleza japo ilikuwa kwa taabu na kujing'atang'ata.
Kilichofuata ni lawama, nilisemwa hadi nikajuta kuwaeleza. Kila mtu aliniona Mimi ni mpuuzi na mvivu wa kufanya maumuzi. Nililaumiwa tena mbaya zaidi ni kwamba walinilaumu bila kujua chanzo cha Mimi kufikia hatua hicho.

Ndugu zake Mke wangu ndiyo walikuwa wakali kama pilipili, hawakutaka kuelekea la Muadhini wala la Mnadi Swala.
Walizungumza kwa hasira wakilaani kitendo nilichofanya tena wengine walikwenda mbali wakitaka nimpe talaka Mke wangu.

"Ndiyo umuache, ni heri arudi nyumbani akiwa mzima kuliko akarejea akiwa maiti kilema" walisema baadhi.

Ndiyo hivyo tena, kordo ya hospitali ikageuka kuwa mahakama, kila mmoja alinihukumu kwa jinsi alivyopenda yeye lakini kesi hiyo ilikatisha mara baada ya Nesi kuja pale na kuniita Mimi.
"Njoo kwa Daktari" akanambia.
Nikanyanyuka na kumfuata huku nikishukuru kwa kunichomoa kwenye kilinge kile cha kushambuliwa kama mpira wa kona.
Tukaingia hadi chumba cha daktari na huko nikamkuta Daktari ameketi akitusubiri.
"Karibu" akanambia aliponiona.
"Asante" nikamwambia huku nikiketi kwenye kiti.
“Naam Daktari umeniita, nini kinaendelea?” Nikamuuliza.
“Mkeo anaendelea vyema tu lakini hapa nimekuita kwa faida yako na si Mke wako? Akanambia na kunifanya nibaki njia panda.
“Kivipi?”
“Nataka tuzungumze kuhusu wewe”
“Mimi!
“Ndiyo”
“Sawa nakusikiliza’’

Jamal wewe ni kijana mwenzangu na tena sote ni wanaume, nimeona ni bora tuzungumze mambo machache kabla hujaangamiia" akaweka koma hapo, kisha akakaa vizuri na kuendelea.
"Kwanini umempiga mke wako namna ile ndugu yangu?" akaniuliza swali ambalo kama liliniudhi. Liliniudhi kwasababu tatu, kwanza ni kutokana na zile lawama nilizokumbana nazo kutoka kwa ndugu zangu, pili ni jinsi dharau alizoniletea Mke wangu na kupelekea nimuadhibu kiasi kile na tatu ni jinsi Daktari alivyohoji mambo yasiyomuhusu.
"Kwani vipi?" nikamuuliza kwa ghadhabu.
"Usipaniki, haya ni mazungumzo ya amani kwa faida yako ndugu yangu"
"Sawa, wewe unahisi kwanini nimempiga?"
"Kuhisi si jambo zuri sana kuliko wewe mwenyewe kunieleza kitu chenye uhakika"
"Nimempiga kwasababu ya dharau"
"Vizuri, unajua ndugu yangu hawa wanawake wetu tunaooa ni vichwa ngumu sana. Dharau kwao ni kama wameiendea kozi, kwahiyo usipokuwa makini watakuletea matatizo. Kwa mfano leo kakudharau umempiga na kumjeruhi namna hii. Kesho atakudharau zaidi na utampiga na kumjeruhi vibaya hata kukaribia kufa na hatimaye utaishia pabaya.
Ushauri wangu ni kwamba, kama unahisi anakuwa tatizo kwako hebu tafuta utatuzi mapema" akanambia.
"Kwahiyo wewe ungetatua vipi?" nikamuuliza kwani sikuoni ushauri katika jile alichokiita ushauri.
"Wewe ni Muislam kwahiyo kama unaona atakusababishia matatizo unaacha nae tu, hiyo ndiyo njia nyepesi" akanambia.
Hakika sikutegemea msomi kama yule kunishauri upuuzi wa namna hiyo.
Ni upuuzi kwasababu hakuangalia vitu vingi tofauti kabla ya kunishauri vile.

Hakuangalia kwamba nina mtoto wa miezi sita niliyezaa na Mke wangu hivyo kuachana kwetu kungeathiri maisha ya mtoto huyo.
"Nimekuelewa daktari na nitanyia kazi ushauri wako" nikamwambia ili kuepusha usumbufu.
"Sawa, mwaweza kumchukua mgonjwa wenu. Hilda, waruhusu" akanambia na kumwambia Nesi aturuhusu.

**************************
"Haiwezekani umpige mwenzio namna hii hata kama amekukosea kosa kubwa kiasi gani" aling'aka Baba Mkwe na hapo tukiwa kwenye kikao mara baada ya kurejea kutoka hospitali.
Tayari tulikwishatafuna zaidi ya robo saa ambazo zote hizo zilitumika kunilaumu mimi.
"Jamani Ashura kanifanyia dharau kubwa sana mjue" nilijitetea mara kwa mara lakini haikufaa kitu.
Kumuacha mtoto na yeye kwenda kusikojulikana wala hakukutiliwa maanani, kudharau chakula ninachokitafuta kwa jasho kwa kukiita matapishi na hata kunimwagia mchuzi yote hayo hayakuwa makosa, kosa ilikuwa ni kumpiga kiasi kile.

Kilikuwa ni kikao kirefu kweli kweli lakini muafaka ulipatikana. Wazazi wangu na wa Mke wangu walinionya kutompiga tena Mke wangu na endapo nitafanya hivyo basi nijue wazi kwamba nitalazimika kumpa talaka Mke wangu.
Ilinibidi nikubali ingawa niliamini kwamba sikutendewa haki kwani hata dini iliniruhusu kumuadhibu Mke wangu endapo anakosea ingawa si kumuadhibu kwa kumpiga Kata-funua namna ile.

********************************
Maisha hayakuwa yenye amani kwa wiki ya kwanza, yaani mimi na Mke hatukuwa na maongezi ya ziada ya Mke na Mume zaidi ya kuuliza 'Soksi zangu ziko wapi?' na mengine ya kufanana na hayo.
Hali ilizidi kubadilika ndani na sasa mke wangu akawa na tabia ya usiri sana katika mambo yanayomuhusu, hakutaka kunishirikisha hata kidogo.

Hata simu yake sasa nilikuwa siigusi, muda wote utamuona nayo ama la anapokuwa mbali nayo na ikaita basi hutimua mbio nusura kuchomoka mguu ili tu aiwahi simu hiyo kabla ya mimi kuisogelea.
Kama binadamu, mwanaume, mwenye moyo, roho na nafsi yenye kutamani ni wazi kwamba nina wivu pia. Na wivu nao uliombwa kutokea sehemu kama hizi.
Niliingiwa na hofu na akili ikasadiki ya kwamba Mke wangu ananisaliti.
Ndiyo ananisaliti na kama hiyo haikuwa kweli kwanini hataki niguse simu yake? Hiyo ina maana ya ya kwamba anaitumia simu hiyo kufanya mawasiliano yanayokinzana na misingi ya ndoa; Anachepuka.
Sikutaka kulifumbia macho hilo ilinibidi nimhoji ili kama ana sababu za msingi anieleze.
"Hii simu ni mali yangu kwahiyo ni mimi pekee mwenye mamlaka ya kuigusa na kumruhusu mtu kuigusa pia" akanambia.
"Lakini mimi ni Mume wako"
"Ndiyo Mume wangu, lakini hii ni simu yangu sio simu ya ndoa. Weka simu ya familia kama una hamu sana ya kuchangia simu na mimi" akanambia hivyo kwa jeuri.

Hakika ilikuwa jeuri na jinsi nilivyo na hasira za karibu ilibaki kidogo nimbutue lakini nilifanikiwa kujiongoza baada ya kukumbuka onyo kali nililolopewa. Lile la kwamba endapo nitampiga ningelazimika kumpa talaka hivyo mwanangu Khadija angepata shida. Kuishi maisha bila wazazi wote wawili ni adhabu kwa mtoto.

Hayo ndiyo yakawa maisha yangu ndani ya nyumba yetu, Ashura alibadilika na kuwa tofauti na nilivyomdhania. Nilipanga kupeleka taarifa hiyo kwa wazazi wake ili kama kuna uwezekano wamuelekeze mtoto wao jinsi ya kuishi na mume.
Kabla ya kufanya hivyo niliomba ushauri kwa rafiki yangu kipenzi Maige nikiamini atanipa ushauri mzuri wa uhakika na wenye manufaa.

"Unajua huko unapoelekea ni kutafuta kuachana na mke wako kisha kumpa shida mtoto wenu mdogo ambaye hata mwaka hajamaliza. Wewe unadhani wazazi wako wakijua visa na vituko anavyokufanyia mkeo wataacha kukushinikiza uachane nae. Watakwambia umuache na hapo ndipo mtoto wenu ataanza kutaabika kwa kuishi na mama wa kambo au kuishi na bibi" alinambia.
"Kwahiyo wewe unanishauri nifanye nini?"
"Wewe ndiye mwanaume, ndiye mwenye mamlaka ya kuiongoza familia. Sasa kwanini ushindwe kumuongoza mwanamke uliyemuoa kwa kumlipia mahali" akanambia.
"Sasa ndiyo nifanyaje?"
"Kaa naye, zungumza naye kwa utaratibu na unyenyekevu. Mueleze jinsi unajisikia vibaya pindi anapokufanyia mambo hayo na bila shaka atakuelewa. Kama bado atakuwa kichwa ngumu basi umtishe kwamba asipojirekebisha utamtandika talaka" akanishauri.
Hata Mimi niliona amenishauri kitu kizuri sana kwani nilikuwa nampenda Mke wangu na endapo tungelisogea kesi hiyo kwa wazazi basi ni wazi kwamba ingekua kubwa na kupekea wawili sisi kutalakiana.

**********************
Sikutaka kupoteza muda kuutumia ushauri wa rafiki yangu ninayemuamini katika ushauri. Nilirejea nyumbani siku hiyo nikiwa nimeichagua kwa kujadili matatizo yetu na Mke wangu.
Ili kumvutia nilimnunulia zawadi nzuri anayoipenda ili asilete mushkheri wakati tunazungumza.

Niliketi naye ndani na nikazungumza naye taratibu. Nilijitahidi kuongoza hasira zangu ili nisitibue mambo.
"Nimekutana na wanawake wa ngapi lakini nikakuoa wewe, ujue kwamba kuna sifa za upekee niliziona kwako.
Ukweli ni kwamba tabia njema, kulelewa katika dini na uzuri wako ndivyo vilivyonishawishi." nilianza kwa kumpamba namna hiyo hapo nikitafuta gia ya kumuingia.
"Lakini sio siri umebadilika sana Mke wangu, si wewe Ashura niliyekuoa mwaka mmoja uliopita. Unanijibu jeuri, unafanya mambo bila kufikiri vyema mke wangu, unamuacha mtoto ndani tena kwa kumfungia mlango na wewe unakwenda kusipojulikana, hujali wala huna hofu kwamba huenda mtoto akapatwa na tatizo.
Nini nimekukosea, nieleze ili nikuombe msamaha na yaishe" nikamwambia kwa hisia na uchungu.
Mara nikamuona anatokwa chozi, pengine maneno niliyomwambia yalimgusa.

Akaendeleza kilio chake na mimi nikaitumia nafasi hiyo kuendelea kumbandika maneno makali ya kumjaza uchungu zaidi.
"Kwanini unanitesa Ashura, nakupenda lakini wewe unanifanya kama mimi si mwanadamu, si mume wako wala si mume mwenye kutimiza majukumu yangu. Kama uliolewa na mimi kwa shinikizo nieleze ili nijue nakusaidiaje kukuweka huru kuliko kunitaabisha namna hii"
"Basi Jamal...." nilimsikia akipayuka namna hiyo huku akilia. Akanyanyuka na kukimbilia chumbani akiniacha niko pale namtazama nisiwe na uhakika wa kwanini kafanya vile.
Nikanyanyuka na kuelekea huko lakini nilikuta amejifungia mlango huku sauti ya kilio chake ikisikika. Nikajua maneno yangu yamemchoma na kumgusa kweli na ndiyo maana akawa vile.
Kweli tangu siku hiyo mambo yakarudi kwenye mstari, niliishi na mke wangu kwa takribani wiki tatu bila mikwaruzano ya aina yoyote ndani ya nyumba.
Hata simu yake sasa nilipewa nafasi ya kuigusa na kuibofya kadri nitakavyo.

*****************
Siku hiyo nilikuwa nyumbani, alitoka kwenda kusuka na kuniacha mimi na mtoto. Kwa bahati alisahau simu na wala hakurudi kuifuata. Nahisi alikumbuka akiwa amekwishafika mbali na ndiyo maana hakurejea.
Nusu saa tangu kuondoka simu ikaita, kwa mara ya kwanza iliita wakati nina kazi lakini ilipoita mara ya pili nilikuwa nimemaliza. Nikaifuata lakini kabla sijaichukua na kuipokea ilikatika. Hata hivyo niligundua kuna meseji ziliingia kabla ya simu hiyo kupigwa. Zilikuwako meseji zipatazo tatu na zote zilitoka kwenye namba ambayo haikuwa imehifadhiwa kwenye simu kwahiyo sikuweza kufahamu ni na nani huyo mtu.

Zilikuwa ni meseji fulani ambazo zilinifungua mara nilipozisoma.
Moja ilisomeka. "Ashura wenzio hali yangu mbaya laazizi hebu naomba urudishe moyo wako nyuma ili nikomboke katika dhahama na mateso haya nipatayo"

Nyingine ilsomeka “naomba pokea simu yangu mahabuba" na ya tatu ilisomeka"Nidharau lakini kuna siku utahitaji huduma yangu"
***************************
MESEJI ZA NANI NA NI HUDUMA GANI HIYO AMBAYO MKE WANGU ATIHITAJI TOKA KWAKE,

UKIITAJI RIWAYA HII KWA HALAKA ZA UNAWEZA WASILIANA NA MWANDISHI KWA NAMBA TAJWA HAPO JUU.
 
RIWAYA: MWANAMKE KAMA MAMA YANGU

MTUNZI: KELVIN KAGAMBO

SEHEMU YA KUMI NA MOJA (11)

#Tembelea http://riwayatakatifu.weebly.com kwa Riwaya zaidi.

ILIPOISHIA…
Zilikuwa ni meseji fulani ambazo zilinifungua mara nilipozisoma.
Moja ilisomeka. "Ashura wenzio hali yangu mbaya laazizi hebu naomba urudishe moyo wako nyuma ili nikomboke katika dhahama na mateso haya nipatayo"

Nyingine ilsomeka “naomba pokea simu yangu mahabuba" na ya tatu ilisomeka"Nidharau lakini kuna siku utahitaji huduma yangu"

ENDELEAAAA….
Ni nani huyo? Ndiyo lilikuwa swali langu la msingi mara baada ya kumaliza kusoma jumbe zote hizo lakini hapo tayari nilishapata picha ya kila kitu kilichojificha.
Kupitia meseji hizo niligundua kwamba kumbe wakati mke wangu ananifanyia vituko vile alikuwa na kijaamaa kilichokuwa kikimzuzua lakini sasa ameachana nacho na kurudi katika mstari nyoofu wa ndoa.

Lakini swali la msingi lililosalia ni kufahamu nani huyo jamaa mwenye kujigamba kwamba kuna siku Mke wangu atahitaji huduma yake.
Nikachukua simu ya Mke wangu na kumpigia, simu yake ikaita kidogo tu na kupokelewa.
"Haloo" nikazungumza na pengine hilo lilikuwa ni kosa kwani jamaa huyo alikata simu punde tu aliposikia sauti yangu. Bila shaka alichukua uamuzi huo baada ya kung'amua kwamba mwenye mali nimegundua hila zake.

Nilimpigia tena na tena lakini hakupokea na sasa nikaamua kubadili uamuzi na kumpigia kwa kutumia simu yangu.
Nikainakiri namba ile kutoka kwenye simu ya Mke wangu na kumpigia lakini sikuamini kile ninachokiona mara baada ya kupiga namba ile.
Unajua simu yangu ina tabia fulani, kama unaandika namba kama hivyo nilivyofanya na kuipiga hujiandika jina kama tayari namba hiyo iko kwenye "phonebook".
Namba hiyo pia ilikuwa kwenye phonebook ya simu yangu na nilipoipiga tu ilijiandika jina la Maige; hiyo ikiwa na maana ya kwamba namba ile ilikuwa ya Maige.

Unajua sikutaka kuamini kirahisi kama hivyo unavyoamini wewe, nilichukua simu ya Mke wangu na kutazama kama namba niliyoiandika ilikuwa ndiyo ile iliyotuma meseji.
Nilikuwa sawia, wala sikukosea kuinakiri namba ile.
Sasa nikaamua kupiga moja kwa moja ili nimueleze kuwa nimekwishafahamu kila kitu.
"The number you are calling is not reachable, please try againi later" (Namba ya simu unayoipigia haipatikani kwasasa, tafadhali jaribu tena baadae) nilijibiwa hivyo na sauti ya mtandao iliyorekodiwa maalum kwa kutoa taarifa pindi simu ya unayempigia inapokuwa haipo hewani.

Jibu la haraka lililokuja kichwani mwangu ilikuwa ni Maige kanizimia simu baada ya kugundua kuwa ni mimi ndiye niliyempigia. Bila shaka hata hofu ilimtawala huko alipokuwa.
Nikatuliza jazba na hasira zangu ili nisitende bila hekima, halafu nikamtoa Mke wangu katika sekeseke hilo nikiamini si yeye mwenye makosa kwani yawezekana alikwishaachana na Maige muda mrefu ndiyo maana Maige akatuma meseji za aina hiyo, zenye kumbembeleza waelendeze wizi wao.
Lakini kweli Maige anastahiki kunifanyia hivi? Mtu ambaye nilimuamini na kumchukulia kama ndugu yangu, rafiki yangu wa kufa na kuzikama lakini ni kinyume.

Kumbe ni ADUI NYUMA YANGU, anayejikinga jua kwa kivuli changu. Hakika Wahenga ni watu wenye hekima na hunena kwa busara sana, nimesadiki hilo waliposema 'Kikulacho kinguoni mwako' na ndiyo hiki ninakiishi mimi.
"Hata kama hapokei simu yangu, kesho nitakutana nae kazini na huko ndipo mambo yatanoga zaidi kwani nitazungumza nae ana kwa ana na hakika sitaacha jambo hili liende hivi hivi" niliahidi.

Ili kuweka uthibitisho niliamua kubadilisha kadi ya simu (Line/Sim Card) ya Mke wangu na kuiweka kwenye simu yangu halafu 'Line' yangu nikaiweka kwenye simu yake.
Nilifanya hivyo ili zile meseji siendelee kubaki kwenye simu kwani endapo Ashura angeziona angezifutilia mbali.
Alirejea baadae nyumbani na wala hakuwa na hofu wa haraka ya kutaka kujua chochote kuhusu simu yake na hiyo ilitosha kuwa dalili ya kwamba hivi sasa ni mwanamke msafi.
"Khadija amekusumbua?" hilo ndilo lilikuwa swali lake la kwanza kuniuliza. Alishughulika na mtoto kwanza kabla na nusu saa baadae ndiyo akaulizia kuhusu simu yake.
"Baba Khadija, mbona hii simu haina majina yangu" aliniuliza hapo akimaanisha 'contacts' alizozikuta kwenye simu hiyo hazikuwa zile alizozihifadhi yeye.
"Nimebadilisha line, yako ipo kwenye simu yangu" nilimueleza na wala sikuona kama alichukia suala hilo.
Akachukua simu yangu na kumpigia Mama yake.
Hakujua kilichotokea kwani hakufanikiwa kuziona meseji zile za kishetani zilizotumwa na Maige.

********************

Usingizi haukuja usiku kana kwamba nimefunga ndoa na Kukesha. Hata jua nililihisi limechelewa kutoka, yaani kwa kifupi usiku wa siku hiyo ulikuwa ni mrefu kweli kweli.
Majogoo yaliwika na kumpa ruhusa ya Mke wangu kuniamsha. Niliamka na kuelekea bafuni ambapo tayari mke wangu alikwishniandalia maji na mswaki.

Nilijisafi huku mawazo na hasira juu ya IBILISI Maige zikinitawala. Nilipomaliza kuoga nilipatiwa chai na Mke wangu na baada ya kunywa nilianza safari ya kuelekea kazini.
Njia nzima mawazo yalikuwa ni Maige na huwezi amini hiyo ilinisababishia nione safari ndefu ingawa siku hiyo hakukuwa hata na foleni kama ilivyokawaida ya Dar es Salaam.
Nilifika kazini na nilipoingia ofisini tu jicho langu liliangaza pahala ambapo Maige huwa anakaa. Sikumuona.
"Maige amefika?" nilimuuliza mfanyakazi mwenzetu niliyemkuta.
"Ndiyo amefika muda mrefu tu" nikajibiwa.
"Yuko wapi?"
"Sifahamu ila yupo" akanambia.
Basi nikatulia kwenye sehemu ya kazi na kuanza kazi ndogondogo huku nikiwa sina 'mood' ya kufanya kazi hata kidogo.
Punde akaingia Maige na alipofungua mlango tu macho yangu yalivaana naye. Nilitamani niwe chui mkali wa mbugani Serengeti, nimrukie, nimjeruhi kwa kumkwaruza kwa makucha hadi kufa.
Lakini hiyo isingewezekana, mimi ni binadamu tu, tena niishie kwenye jamii yenye kufuata sheria ina maana kuua kungesababisha nipandishwe kizimbani na kugongwa nyundo kadhaa jela.
"Kaka, kaka, nina majanga kweli kweli" akasema akiwa mbali kabla hapa hajafika nilipokuwa mimi na hiyo ilinifanya niwe makini kusikiliza hayo majanga anayoyazungumzia.
"Niulize majanga gani basi" akanambia.
"Majanga gani?" nikamuuliza.
"Jana nimepigwa ngeta aisee, bonge la kabali mbao mitaa ya Mwananyamala hadi nikaona mtoa roho huyu hapa" akanambia.
"Duuuh!" nikashituka kinafki. "Ikawaje sasa?"
"Wamenikomba kila nilichokuwa nacho braza, pochi yangu ilikuwa na laki moja na elfu kumi na simu pia" akanambia na kunifanya nipagawe kwani mpango wangu wa kumueleza ukweli juu ya kile nilichokiona kwenye simu ya Mke wangu ungekosa nguvu.
"Hadi simu!?" nikamuuliza.
"Hadi simu, yaani wamenirudisha nyuma sana na ni heri wangechukua pesa wakanachia simu yangu" akanambia.
Nikaishiwa 'pozi', unadhani ningeanzia wapi kumshutumu. Bila shaka ingekuwa ni rahisi sana kwake kukwepa shutuma zangu.
Angenambia tu kwamba pengine meseji hizo zilitumwa na mtu aliyemuibia simu.

Na unajua ni ngumu sana kumshuku mtu wako wa karibu kwenye kesi kama hizo. Kama si kweli basi atahisi humuamini na hiyo inaweza ikahatarisha hata urafiki wenu.
Nikatulia na kujaribu kukumbuka Maige ni mtu wa aina gani katika maisha yangu.
Nikakumbuka jinsi alivyowahi kunieleza kwamba kuna siri kati ya Mke wangu na Mama yake, kipindi kile ambacho Mke wangu alijifungua.

Hilo jumlisha na mengine mengi yalimtafsiri Maige kama mtu wa muhimu sana kwenye maisha yangu, rafiki wa karibu mwenye msaada hasa nyakati za shida na matatizo.
Lakini bado nilikuwa na shaka naye, si unakumbuka kuna siku simu yake iliingia meseji kutoka kwa mtu ikimueleza kwamba anawashwa na anahitaji kukunwa, na ndiyo siku hiyo ambayo nilirejea nyumbani na kukuta Mke wangu amekwenda kusipojulikana tena kwa kumuacha mtoto.

Mawazo hayo yakasababisha ukinzani katika mtazamo wangu juu ya Maige. Nikashindwa nimuweke upande gani. Hasi ama chanya, moto ama baridi au hata wa kusuka ama kunyoa.
Nilichanganyikiwa.

Nikatuliza akili na kuona itakuwa hekima zaidi kama nitafanya uchunguzi wa kimya kimya kabla ya kumuibukia na tuhuma za uhakika zenye ushahidi wa kujitosheleza.
Sikumuonesha hata zile meseji, nilitaka mpaka nitakapohakikisha kwamba ni yeye aliyetuma ama ni huyo aliyemuibia kwa kumpiga kabali mbao.
"Pole sana" ndiyo lilikuwa neno langu la kwanza kumwambia.
"Nishapoa, vipi umekunywa chai" akaniuliza swali la kawaida kutoka kwake.
"Hapana" nikamjibu.
"Kuna chapati hapa, unaweza kuzitumia" akanambia na kazi ikaendelea.
Nilifanya kazi lakini si kwa ari kama ili kawaida yangu, na kuhusu zile chapati sikuzigusa, niliogopa nikiamini angeweza kuniwekea hata sumu.

Sikuwa na mazungumzo naye na hata yeye aligundua kuna tofauti, akaniuliza lakini sikumueleza ukweli.
Mda wa 'lunch' tuliongozana nikiwa katika hali ile ile ingawa yeye alijitahidi kunipigisha stori.

*****************
Nilirejea nyumbani nikiwa na mbinu mpya ambayo ningeitumia kung'amua ukweli. Mbinu hiyo nilipata njiani nilipokuwa nikifikiria jinsi gani nitafanya ili kupata ukweli.
Niliwaza kumuuliza Mke wangu moja kwa moja bila kuzunguka wala kujiumauma na muitikio wake ndio ungenijuza kwamba ni kweli alikuwa na mahusiano na Maige au laa.
Nilifika nyumbani na kumkuta mke wangu anaanda chakula cha jioni.

Nilioga kwanza na kisha nikajumuika mezani na tukapata msosi wa pamoja na mtoto wetu Khadija, tulipomaliza ikawa ni muda wa kulala na ni muda huo ndio niliopanga kuutumia kuzungumza na Mke wangu.
"Kwanini uliamua kutembea na Maige?" nilimuuliza hivyo mara tu tulipozima taa na kupanda kitandani.
Akashituka na nikawa nasubiri jibu lake ili nijue ni kweli alifanya hivyo ama si kweli.
"Lakini Jamal Mume wangu, hayo si yalishapita" akanijibu na hilo likawa jibu tosha la kuthibitisha kwamba Ashura alitembea na Maige.
"Yamepita, mbona bado anakutumia meseji?" nikamwambia.
"Meseji gani?"
"Hivi unadhani kwanini nimebadilisha line yako na kuiweka kwenye simu yangu?" nikampa taarifa kwa mtindo wa swali.
"Nisamehe Mume wangu, lakini mimi tayari nimekwishaachana naye ila ni yeye ambayo bado anaendeleza usumbufu"
"Nilikuwa siyafahamu yote hayo lakini sasa ndio nimepata kujua laana ulizo nazo mwanamke wewe, unawezaje kutembea na rafiki yangu na nawezaje kukusamehe" nikamwambia.
Kweli sikuwa nikifahamu lakini kwasababu nimefahamu sidhani kama naweza kumsamehe.
Je, ungelikuwa ni wewe ungelisamehe?

Eti Mke wako atembee na rafiki yako wa karibu kabisa halafu umsamehe, unaweza?.
Binafsi siwezi kumsamehe wala kusahau labda tu kuvumilia kuendelea kuishi naye kwasababu tayari tuna mtoto, tena mdogo ambaye hajatimiza hata mwaka.
Nililala nikiwa nimevimba kwa hasira na uchungu, sikutegemea kwamba Maige na Mke wangu wangekuwa wabaya kwangu namna ile.

Sasa nilipanga kesho kumuamkia Maige na kumchana 'live', tena si kumchana tu bali kulifikisha mbali suala hilo, hata kwa mabosi kama itawezekana.

Nilidamka asubuhi na mapema na kuondoka kuelekea kazini bila hata kumuaga Mke wangu na hiyo ilikuwa ni kwasababu ya hasira. Sikutaka hata kumuona na ingewezekana ningemcharaza talaka tatu na nikabaki mwenyewe ila kilichokuwa kikinizuia kufanya hivyo ni mtoto wangu alikuwa mdogo sana.
Nilifika ofisini lakini 'mbaya' wangu bado hakuwa amewasili, hata hamu ya kufanya kazi sikuwa nayo, nilikaa kishari na laiti kama ningelikuwa na bastola ningelimuua Maige ili nikanyee debe Segerea, Keko au hata Ukonga.
"Jamal, unaitwa na Bosi ofisini kwake" mara nikasikia nikiambiwa hivyo, halikuwa jambo la kawaida na hiyo ikasababisha niogope kidogo.
"Kuna nini tena?" nikamuuliza aliyenipa taarifa huku nikadhani labda niliboronga kazi ya jana kutokana na kuifanya nikiwa na hasira na kisirani.
"Acha maswali ya mtani jembe wewe, nenda kamuulize anayekuita" akanijibu jamaa huyo huku akiendeleza na kazi zake.
Nikanyanyuka toka kwenye kiti changu, nikazunguka meza yangu ambayo ilikuwa na kompyuta pamoja na makaratasi kadhaa. Nikatembea kuelekea ofisi kwa Bosi na nilipobisha hodi akaniruhusu nipite.

**************************

KWANINI BOSI ANANIITA? USIKOSE SEHEMU YA KUMI NA MBILI KUPATA JIBU LA SWALI HILO.

KUPATA RIWAYA HII NA NYINGINE NYINGI UNAWEZA WASILIANA NA NDUGU MWANDISHI KWA NAMBA TAJWA HAPO JUU.
 
RIWAYA: MWANAMKE KAMA MAMA YANGU

MTUNZI: KELVIN KAGAMBO

SEHEMU YA KUMI NA MBILI (12)

ILIPOISHIA….

"Jamal, unaitwa na Bosi ofisini kwake" mara nikasikia nikiambiwa hivyo, halikuwa jambo la kawaida na hiyo ikasababisha niogope kidogo.
"Kuna nini tena?" nikamuuliza aliyenipa taarifa huku nikadhani labda niliboronga kazi ya jana kutokana na kuifanya nikiwa na hasira na kisirani.
"Acha maswali ya mtani jembe wewe, nenda kamuulize anayekuita" akanijibu jamaa huyo huku akiendeleza na kazi zake.
Nikanyanyuka toka kwenye kiti changu, nikazunguka meza yangu ambayo ilikuwa na kompyuta pamoja na makaratasi kadhaa. Nikatembea kuelekea ofisi kwa Bosi na nilipobisha hodi akaniruhusu nipite.

ENDELEA…..

"Keti hapo" akanambia huku akinieleza kwenye kiti maalum kwa ajili ya wageni, nikakaa.
"Naam Bosi"
"Eeeh, unajua Jamal wewe ndiye mtu wa karibu sana wa Maige humu ndani si ndiyo" akaniuliza, alikuwa sahihi lakini nilitamani kumwambia kwamba huo ukaribu wetu unaelekea mbioni kuisha.
"Ndiyo" nikajibu kinafiki.
"Sawa, aaamh, kuna taarifa hapa inamuhusu Maige, na kwasababu ni wewe ndiye mtu wake wa karibu nimeona ni vyema ingekufikia wewe kwanza kabla ya mtu yeyote yule" akanambia, nikapatwa kimuhemuhe cha kutaka kufahamu ni taarifa gani hiyo inayomuhusu Maige, nilitamani iwe ni ya kufukuzwa kazi ili akome na Jua kali la Bongo, si unajua njaa haina Baunsa.
"Ndiyo" nikajibu huku kimoyo changu kikidunda kama nipo kwenye 'Danger zone' ya BONGO STAR SEARCH.
"Nimepigiwa simu muda huu kwa namba ya Maige, mtu aliyenipigia anasema kwamba Maige amepeta ajali muda si mrefu na amefariki papo hapo kwani kichwa chake kimepasuka, ubongo nje" akasema Bosi na kufanya moyo wangu utake kuchomoka kwenye eneo lake la kawaida.
Ilikuwa ni ngumu kwangu kuamini kile nilichoambiwa, na si ngumu kuamini tu bali hata kuitafsiri taarifa hiyo ilikuwa ni shughuli nzito. Nilishindwa kuelewa kwamba ni taarifa nzuri kwangu ama mbaya.

Lakini kuna kitu nikakumbuka, Maige alinieleza kwamba ameibiwa simu sasa imekuaje itumike namba yake kutoa taarifa.
Nikaingiwa shaka. Nikahisi labda mtu huyo aliyemuibiia ndio anafanya upuuzi wa namna hiyo na labda ni kweli ni yeye aliyetuma meseji za mtindo ule kwa Mke wangu ingawa zilikuwa zimebeba ukweli ndani yake.
"Lakini Bosi unajua kuwa Maige ameibiwa simu yake na huyo aliyemuibia amekuwa na tabia ya kutumia watu meseji, hata mimi alimtumia meseji Mke wangu akimtongoza. Nilidhani ni Maige lakini nilipokuja kumuuliza ndiyo nikapata taarifa kwamba simu yake imeibiwa" nikamueleza Bosi kwa kirefu namna hiyo.
"Eti eeeh, basi ngoja tumpigie tuthibitishe" akanambia na kutoa simu yake kisha kupiga namba ya maige.
"Hapatikani" akanambia "Ngoja nirudie" akasema na kupiga tena lakini mambo yakawa yale yale, hiyo ikazidi kutuweka njia panda.
"Kwani alisema ajali imetokea wapi?" nikamuuliza.
"Ni Tabata Barakuda"
"Ngoja nichukue bodaboda niwahi, si umesema muda si mrefu"
"Ndiyo hata robo saa sidhani kama imefika" akanambia.
Sikuwa na cha kupoteza, nilichomoka ofisini muda huo huo na kuchukua bodaboda ili kuwahi eneo la tukio na kuthibitisha kama ni kweli adui yangu amekumbwa na majanga yale.

Bodaboda naye aliendesha kwa sifa kama yupo kwenye mashindano, si unajua chizi ukimkabidhi rungu, jua njia aliyosimama yeye haipitiki. Sasa dereva wa bodaboda nimempa ruhusa ya kwenda mwendo kasi,hebu vuta picha mwenyewe.

Barakuda hii hapa, tukawasili. Nikiwa kwa mbali nikaona kusanyiko kubwa la watu na hiyo ikawa ni ishara kamili kwamba eneo lile ndilo lilitokea ajali na pia foleli ambayo ilisababishwa na magari kushindwa kupita eneo lle lililojaa watu.
Niliteremka haraka mara baada ya kuwasili eneo hilo,nikawasukumasukuma watu ili kupata nafasi ya kuona kitu kilichozingirwa na watu wale.
Nilipata nafasi ya kuona walichokuwa wakikitazama lakini sikuona nilichokifuata.

Hakuwepo Maige kama nilivyotaraji lakini eneo lote lile lilikuwa limetapakaa damu kana kwamba kuna mtu aligongwa.
"Nani kagongwa?" nikamuuliza mtu wa pembeni yangu kana kwamba alikuwa akimfahamu Maige.
"Maswali gani hayo ya kiboya unauliza" akanambia mtu huyo na hakuishia hapo aliendelea "Sasa unaniuliza nani kagongwa mimi nitamjuaje?"

Nikajikuta sina usemi kwani ni kweli nilikosea jinsi ya kuuliza, nikajisogeza mbali na jamaa huyo na kumsogelea mtu mwingine huku nikiwa nimejipanga kwa maswali yenye viwango.
"Dada aliyegongwa hapa ni mwanaume mwanamke?" nikamuuliza.
"Mwanaume"
"Wamemuwahisha hospitali, sio?"
"Hospitali au Mochwari, mtu hadi kajisaidia we unazungumzia masuala ya madaktari. Ngoma kwa mtunza maiti hiyo" akasema Mwanamke huyo ambaye pengine alikuwa na hamu ya kuulizwa.
"Ilikuwaje?"
"Si hayo masimu yao ya kisasa yanawazuzua. Alikuwa anavuka barabara huku anachezea mawasapu na matwita kumbe kuna kosta imetunguka huko, ilimzoaje" akasimulia tena kwa mshawasha kana kwamba alikuwa ananisimulia filamu ya kuchekesha ambayo yupo Majuto ua Mboto ndani yake.
Aisee, nilisisimka na shauku ya kutaka kujua kama mtu huyo ni Maige ama siye ndiyo ikazidi sasa.
"Itakuwa mwili wameuwahisha Amana eeeh?"
"Sina uhakika ila nadhani itakuwa hivyo" Akanambia, sikuwa na cha kupoteza, nikachukua bodaboda safari ya kuelekea Amana ikaanza.
Dakika kadhaa tu nilifika Amana na kuulizia Mochwari zilipo, nilipatiwa maelekezo na kupita mwenyewe hadi huko.
"Kuna mwili umeletwa kutoka kwenye ajali ya gari Tabata" nikautolea maelekezo
"Wewe ni nani yako?" akaniuliza Mtunza maiti.
"Ndugu yake, nimepigiwa simu kwa namba yake na mtu ambaye alikuwa eneo la tukio" nikamwambia.
"Mimi sina shida na hayo maelezo yako, wewe nieleze marehemu ni ndugu yako kivipi" likanambia jamaa hilo kwa kisirani.
"Ni ndugu yangu mtoto wa Baba yangu Mkubwa na pia nimfanyakazi mwenzangu" nikamwambia.
"Wewe jamaa sijui mtu wa wapi wewe, huelewi. Haya hapa haturuhusu ndugu mmoja kuja kugundundu mwili peke yake" akanambia.

Unajua hawa jamaa watunza maiti Mochwari ni watu ambao wasumbufu mno na ukiona wameanza kuleta kona kona za namna hiyo basi jua anataka rushwa.
Nawafahamu, nikamvuta pembeni na kumtongoza kwamba nitampa pesa.
Akakubali tena kiulaini tu kwani hicho ndicho alichokuwa akikitaka.
Akaniingiza hadi ndani ma kunisogeza hadi kwenye limeza lipana kama kitanda ambalo juu yake ulikuepo mwili ulioufunikwa kwa shuka.
"Sogea hapa basi acha uoga kama wa kike" akanambia kwani nilikuwa nyuma nyuma. Nikasogea na kusimama pembeni ya meza hiyo huku moyo wangu ukienda mbio kwa uwoga.
Akafunua.

Haki ya Mungu nilijikuta nafumba macho, sikutegemea kumuona Maige akiwa maiti tena kwa namna ile. Nilishindwa kuvumilia, nikajikuta namwaga chozi na hata kama Maige angenifanyia kosa kubwa namna gani lazima hali ile ingenikuta kwasababu Mimi ni Binadamu.
"Unalia nini sasa, wewe si umetaka kumuona ndugu yako" akanambia Jamaa huyo ambaye yeye wala hakuonekana kuogopa hata chembe.
"Ndiye huyu ama si yeye, mtazame kwa makini" akanambia, sikuwa na jinsi, nikajitahidi kuutaza mwili ule wa Maige.
Alikuwa amepondeka upande wa kushoto wa kichwa chake na kutengeneza tundu ambao lilifanya nyama nyama za ndani ya kichwa na hata ubongo pia kuonekana. Huwezi kutazama mara mbili kama una roho nyepesi lakini nilijitutumua kuutazama ili nijue kama alikuwa ni yeye kweli.

Hata hivyo ilikuwa ni ngumu kumtambua kutokana na sura yake kubadilishwa na umbo jipya la kichwa ambalo pengine ni tairi ya gari ilimkanyaga; lakini nilimtambua kwani alikuwa na alama mbili ambazo zilimtambulisha kuwa ni yeye.
Kwanza Maige ana kidoti cheusi chini ya mdomo; yaani ni kama kama kinyama fulani hivi.
Pia ni lile fulana jeupe alilovaa ambalo lilikuwa na nembo ya kampuni yetu kifuani.
Bila shaka ni yeye na wala sikuwa nimekosea.
"Wewe mbona unaleta ufala sasa, ndiye huyu ama siye" likanikaripia lile jamaa litunza maiti baada ya kuona nachelewa kumpa majibu.
"Ni yeye" nikajibu huku kwikwi za majonzi na uchungu zikiniandama.
"Haya, kawaambie na wenzako mje kuchukua mzoga wenu" akanambia jamaa huyo kana kwamba yule aliyekufa pale hakuwa binadamu. Akafunika mwili na kunitoa.

Nikaondoka hospitalini hapo nikiwa tofauti na nilivyokuja.
Nilikuja na shauku hata ya kutamani kukuta Maige amekufa lakini naondoka na simanzi na majonzi ya kutamani Maige azinduke na kuishi tena japo kwa siku ya leo tu.
Nilikosa hata nguvu za kurejea kazini, nilinyoosha hadi nyumbani huku Bosi nikimpa taarifa kwa kupitia simu.

*************************

BADO KUNA MATUKIO MENGI SANA KUELEKEA KUJUA HATIMA YA MAISHA YA JAMAL…. HUNA SABABU YA KUKOSA MUENDELEZO WA RIWAYA HII MATATA.

PIA TEMBELEA: riwayatakatifu.weebly.com kwa riwaya nyingine.

WAWEZA WASILIANA NA MWANDISHI KWA NAMBA TAJWA HAPO JUU KUPATA RIWAYA HII NA NYINGINE NYINGI.
 
RIWAYA: MWANAMKE KAMA MAMA YANGU

MTUNZI: KELVIN KAGAMBO

SEHEMU YA KUMI NA TATU (13)

ILIPOISHIA….

"Haya, kawaambie na wenzako mje kuchukua mzoga wenu" akanambia jamaa huyo kana kwamba yule aliyekufa pale hakuwa binadamu. Akafunika mwili na kunitoa.
Nikaondoka hospitalini hapo nikiwa tofauti na nilivyokuja.
Nilikuja na shauku hata ya kutamani kukuta Maige amekufa lakini naondoka na simanzi na majonzi ya kutamani Maige azinduke na kuishi tena japo kwa siku ya leo tu.
Nilikosa hata nguvu za kurejea kazini, nilinyoosha hadi nyumbani huku Bosi nikimpa taarifa kwa kupitia simu.

ENDELEA…..

Tulimrudisha kwenye makao ya milele ambayo yameelezwa kwenye vitabu vyote vya dini kwamba kila nafsi itaonja umauti.
Habari za Maige zikawa zimekomea hapo na akawa amekufa akiwa adui yangu kwa ule ushenzi alionifanyia.
Ndiyo ujue kwamba duniani hakuna wa kumuamini na ili kuthibitisha hilo fanya utafiti.

Riwaya ya ADUI NYUMA YANGU iliyooandikwa na KELVIN KAGAMBO ilithubutu kueleza jinsi binadamu tusivyotafsirika kwa jicho la kawaida.
Raymond Gaya aligeukwa na Mwanamke aliyemuoa na kuzaa naye watoto. Unaweza ukamuona mtu yu karibu nawe zaidi ya ngozi ya mwili wako na ukadhani labda huyo ndiye rafiki.
Lakini utakuja kushangaa kwamba ni huyo anayekutokomeza na kukuangamiza mazima, akabadili kitambulisho ulichompa, kile cha urafiki na akawa Adui yako nambari Moja.
Maige asingekuwa mtu wa kutembea na Mke wangu na pia Mke wangu amepoteza sifa ya kuitwa Binadamu kwa kuthubutu kutembea na rafiki yangu.
Sina jinsi yameshatokea, acha tatizo hili liwe siri ya ndani, imezwe na nyumba yetu na asijue hata jirani.

*******************

"The Best Student of the year is....is....is....is Khadija Jamal Shomari" ilisikika sauti ya Mwalimu wa Taaluma wa shule aliyokuwa akisoma mwanangu Khadija.
Hiyo ilikuwa ni miaka sita sasa tangu kuzaliwa kwake na siku hiyo tulikuwa kwenye mahafali ya wanafunzi wanaohitmu wa chekechea wa shule anayosoma ili mwakani wajiunge na elimu ya msingi.

Naye alikuwa ni mmoja wao, na alipasua vibaya hadi kuwa Mwanafunzi bora kitaaluma. Nilifarijika sana kuwa na mtoto wa aina hiyo, lakini pengine si mimi tu bali hata Mama yake ambaye naye alikuwa hapo.
Nikamuona anachomoka toka eneo waliloketi wahitimu na kuelekea eneo ambalo Mwalimu wa taaluma alisimama, akamfikia; wakaongozana pamoja kuelekea kwenye Meza ya mgeni rasmi ili kupokea cheti chake.
Alikabidhiwa na kupiga picha kadhaa za tukio hilo kabla ya kupewa kipaza sauti ili kusema chochote.
Yaani mambo yalikuzwa kweli kweli, mahafali ya vidudu tu yaliwekewa vidokezo kweli kweli.
Nikawa najiuliza sasa ni pumba gani ambazo mwanangu Khadija atazizungumza. Eti mtoto wa miaka sita, umpe kipaza sauti atoe azungumze kwenye sehemu ya watu wengi kama vile, ataongea nini?.

"Hi Ladies and Gentlemen" (Habari Mabibi na Mabwana) akaanza kwa mbwembwe na mikogo ya namna hiyo.
"I’m very happy, very glad to win this award, best student of the year. But I did not made it by myself, there is a big crew behind my succes and I have to thank all of them" (Nina furaha sana kushinda tuzo hii, Mwanafunzi Bora. Lakin katu nisingeweza kufanya hivi mwenyewe, Kuna kundi kubwa nyuma ya mafanikio haya na sina budi kuwashukuru) kikasema kimwanangu tena kwa kimombo na kunifanya nijivunie kuwa Baba yake lakini pia kulipa ada ile ambayo imewezesha yeye kuwa pale.
Akaendelea.
"Thanks to Dear God who always makes me healthful, to My dear Dady Mr Jamal Shomari, to My lovely Mommy Ashura, My teachers, My fellow students and lastly goes to My young Brother, Ally Jamal Shomari" akasema mwanangu na kuzidi kunikosha kweli kweli.

Ila alinikosha zaidi pale alipomalizia kwa kumshukuru na ndugu yake Ally ambaye ndio kwanza ana miaka mitatu tu. Bila shaka ni mbwembwe tu kwani sitaki kuamini kwamba allikuwa na msaada wowote katika ushindi wake.
Kila siku alikuwa akimchania daftari zake sasa inakuwaje naye awe ni miongoni mwa waliofanikisha mafinikio yake. Labda ni kwasababu alikuwa akimpenda tu kwani wanangu najitahidi kuwaelea katika mlolongo huo, wakupendana na kukumbukana kila pahala na muda wote.
Najua utashangaa kusikia mwanangu Khadija ana mdogo wake lakini hali ndiyo iko hivyo.

Ni miaka sita na miezi kumi na mmoja imekatika tangu mwanangu Khadija azaliwe. Kwasasa anasoma chekechea na pia mimi na Mke wangu tumefanikiwa kumpatia mdogo wake ambaye naye ana umri wa miaka mitatu na tumemwita Ally.
Ni watoto niwapendao hakika, wananipa raha na kunifanya nijihisi ni Baba, wananifanya niwe na nguvu ya kuweza kusimama mbele za watu na kusema "mimi ni Mwanaume tena wa shoka"
Hata hivyo si kwamba mhmi mdiye niwapendae tu, hapana bali hata wao wananipenda tena sana zaidi unavyofikiria.

Wananipenda mimi zaidi ya wampendavyo Mama yao.
Hiyo ni kweli na ni sahihi kwani siku zote kumpenda anayekupenda ni kitu bora zaidi; sasa kama ni hivyo wataanzaje kumpenda Mama yao ikiwa yeye hawapendi?
Ndiyo, hawapendi na ingawa upendo si kitu kionekanacho kwa macho lakini kuna viashiria vyake vinavyouwakilisha, usipoviona hivyo kwa mtu unayehisi anakupenda basi jua hakupendi.
Viashiria hivyo havikuwako kwa Mke wangu, hakuwa akiwajali watoto kwa lolote na kusababisha mimi Mume kubeba majukumu yake.

Kuwaogesha, kujua wamekwenda shule, wamelala pahala salama na mengine kama hayo ambayo kimsingi ni Mama yao ndiye aliyetakiwa kuyafanya, niliyafanya Mimi.
Hayakuwa makubaliano yetu lakini hali ilikuwa hivyo 'Automatically'. Sasa mtu hawashughulikii watoto kwa lolote unadhani ningewaacha, hawa ni wanangu, daumu yangu sina budi kuhakikisha wanaishi kibanadamu.

Hata ile siku ya mahafali yenyewe tu hakuwa akitaka kwenda kwa kisingizio cha kwamba anajihisi vibaya. Alienda baada ya kubembelezwa na kulambwalamwba kweli na watoto na pengine ni maneno ya Khadija ndiyo yaliyomfanya ajisikie vibaya na kukubali kwenda.
"Mama hutujali kwa lolote, hata siku moja hujawahi kushika daftari zangu ili kufuatilia maendeleo yangu ya shule. Au uliolewa na Baba kwa kulazimishwa kwahiyo unamchukia yeye na damu yake.
Mimi ni Mama mtarajiwa na najifunza jinsi ya kuwa Mke bora toka kwako, sasa kwahayo ufanyayo mimi najifunza nini unadhani?" alimwambia hivyo, haya maneno hayo yalimfanya ajisikie vibaya, akakubali kwenda ingawa kwa shingo upande.

Mahafali yalifika tamati mnamo saa kumi alasiri. Kila familia ikawa huru kuondoka kurejea majumbani kuendelea na shughuli zinginezo.
Mimi na familia yangu tukajikusanya kuelekea kwenye Vits yangu tukisaidiana kubeba maboksi ya zawadi alizipatiwa Khadija wangu.
Tukafika kwenye maegesho, karibu kabisa na gari. Nikafungua mlango wa nyuma (Boot) na kuweka maboksi ya zawadi huku wanangu na Mke wangu wakiiga kufanya hivyo pia.
Tulipomaliza zoezi hilo tuliingia garini tayari kwa safari lakini kabla hata sijawasha gari alikuja Mwalimu Makoronjo na kugonga kwenye kioo cha dirisha la upande wa dereva.
Nikafungua kioo huku sura nimeipamba kwa tabasamu la kumkaribisha Mwalimu Makoronjo; Mwalimu wa taaluma kwenye shule anayosoma mwanangu.
"Vipi Mwalimu?"
"Kwema, ningependa kupata wasaha wa kuzungumza na ninyi" akasema akimaanisha nafasi ya kuzungumza na Mimi na Mke wangu.
"Sawa hakuna tatizo ngoja tuteremke" nikamwambia.
"Hapana hapana, si lazima muda huu" hata tukiweka appointment haitakua vibaya kwani ni maongezi marefu" akasema mwalimu Makoronjo.
"Sawa, nipatie namba zako za simu basi" nikamwambia huku nikitoa simu yangu na kumkabidhi ili aandike namba zake.
Alipomaliza aliirejesha kwangu na kutuaga na safari yetu ikaanza. Katikati ya safari nilijaribu kupanga na Mke kwamba ni siku gani ingekuwa nzuri ya sisi kukutana na mwalimu na tuzungumze naye.
"Naona ni Jumapili" akanambia
"Sawa, basi nitampigia simu kesho nimwambie" nilimaliza na safari ikaendelea ambapo tulifika nyumbani na kufanya tafrija ndogo ya kifamilia kwa ajili ya kumpongeza mwanangu

***************************

MAISHA MAPYA BAADA YA ADUI MAIGE KUFARIKI, LAKINI BADO MKE WANGU AMEENDELEA KUWA TATIZO. NANI MWINGINE ANAMSUMBUA? USIKOSE SEHEMU YA KUMI NA NNE.
WAWEZA WASILIANA NA MWANDISHI KUPATA RIWAYA HII NA NYINGINE NYINGI.

TUKUTANE TENA KESHO KUTAMATISHA RIWAYA HII.
 
Hizi Riwaya kule Amazon Wana program mpya ambayo inakuwezesha kuandika kwa episode unapublish Kama series unalpwa kwa Dola kila atakaye like.Kuna watu wanatengeneza fedha hatari.Ni zama za wabunifu wa fasihi simulizi hizi.
 
RIWAYA: MWANAMKE KAMA MAMA YANGU

MTUNZI: KELVIN KAGAMBO

TEMBELEA KWA RIWAYA ZAIDI: http://riwayatakatifu.weebly.com/

SEHEMU YA KUMI NA NNE (14)

ILIPOISHIA….

Alipomaliza aliirejesha kwangu na kutuaga na safari yetu ikaanza. Katikati ya safari nilijaribu kupanga na Mke kwamba ni siku gani ingekuwa nzuri ya sisi kukutana na mwalimu na tuzungumze naye.

"Naona ni Jumapili" akanambia
"Sawa, basi nitampigia simu kesho nimwambie" nilimaliza na safari ikaendelea ambapo tulifika nyumbani na kufanya tafrija ndogo ya kifamilia kwa ajili ya kumpongeza mwanangu

SHUKA NAYOOOOO…..

Jumapili ya kukutana na Mwalimu Makoronjo ililfika, lakini kwa bahati mbaya siku hiyo nilihitajika kazini. Hata hivyo nilihitajika kwa muda mfupi tu kwahiyo ulikuwepo uwezekano wa kukutana na Mwalimu.
Nilifika kazini na kujaribu kukimbizana na muda ili kabla ya muda wa mihadi haujafika niwe nimekwisha kamilisha kazi. Lakini nilishindwa, Kazi zilinibana na kusabisha hata nikakosa nafasi ya kuchomoka na muda huo Mwalimu alianza kunitafuta katika simu.

"Haloo Mr. Jamal, niko karibu na nyumbani kwako, unielekeze" alinambia aliponipigia.
"Sawa, lakini mimi nimetoka mara moja ila ngoja nimpe Mke wangu namba yako, yeye atakusaidia kufika nyumbani. Mimi nitarudi hivi punde" nikamwambia.
Ikawa hivyo, nikampigia Mke wangu simu na kumueleza hali halisi kisha nikamtumia na namba ya Mwalimu ili afanye mawasiliano naye.

Robo saa baadae Ashura alinipigia simu na kunipa taarifa kwamba tayari Mwalimu ameshafika nyumbani na muda huo pia nilikuwa nimeshamaliza kazi na niko huru kuondoka.
Nikatoka mbio mbio kukimbia kwenye gari yangu ili niwahi nyumbani na kulinda heshima yangu kwa Mwalimu kwani ningeonekana mswahili kwa kushindwa kwenda na muda.
Mungu naye alinitazama kwa jicho la karibu sana kwani sikupata mushkheri wowote hadi nafika nyumbani.

Niliwasili na kukuta Mwalimu yupo sebuleni akizungumza na Khadija wakati Mke wangu akitayarisha chakula cha mchana.
Nilisalimiana na Mwalimu punde baada ya kufika nyumbani na pia nikajumuika naye hapo sebuleni na kupiga soga za hapa na pale wakati tukisubiri chakula.
Tuliongea mengi mengi sana na nilichogundua ni kwamba tulikuwa tukifafana kwa mambo tunayoyapenda na hiyo ilipelekea tusikose cha kuongea.

Nusu saa baadae chakula kilikuwa tayari, Mke wangu akaandaa mezani na kutukaribisha na kwa pamoja tukajumuika na kupata pilau ya Kuku safi iliyoandaliwa na Ashura. Alikuwa ni fundi wa kupika kwahiyo kula vitu vya namna hiyo toka kwangu haikuwa mara yangu ya kwanza ingawa kwa sasa nimevimiss.
Nime-miss mapochopocho hayo kwasababu siku hizi ameacha kupika na si kwamba ndiyo utaratibu tuliowekeana bali ameamua tu, kule kubadilika kwa tabia zake ndiyo kumezaa hayo, siku hizi mimi ndiyi nimekuwa kama mpishi.
Nashindwa hata nikamshitaki wapi kwani wazazi wangu yaani Baba yangu, Mzee Shomari na Mama yangu Bi Khadija wote ni marehemu kwa sasa; walifariki tangu mwanangu Khadija akiwa na umri wa miaka minne.

Kesi kama hizo labda ningezipeleka kwa Baba yangu Mkubwa lakini nako huko nilihofia, Baba yangu mkubwa ni mropokaji na angeweza hata kusababisha Mimi na Mke wangu tukaachana jambo ambalo sikuwa nikitaka kuona linatokea kwani naamini kuachana na Mke wangu kungepelekea wanangu kuteseka kweli kweli.

Niliwahi kupeleka kesi hizo kwa wazazi wake lakini kama hawakuwa wakizitilia maanani na pengine ni kwasababu Baba mkwe hakuwa na hali nzuri kiafya. Alikuwa akiandamwa na maradhi ya mara kwa mara na hivyo kupelekea nikakosa msaada wake.
Mama asingeweza kuchukua hatua yoyote zaidi ya kumuelekeza mwanaye jinsi ya kuishi vyema na mume wake lakini hiyo nayo haikuwa dawa ya ugonjwa wa tabia chafu anaoumwa Mke wangu.
Chakula kiliwekwa mezani nasi tukaanza kukifakamia. Tulikula kwa furaha kutokana na wingi wa walaji huku hatima ya mlo huo ikiwa ni mazungumzo ya sisi na Mwalimu Makoronjo.
Tuliketi nje, eneo ambalo nilipanda maua chini ya mti wenye kivuli na hiyo ilikuwa sehemu sahihi kwa aina ya mazungumzo aliyokuwa nayo.

Tulizungumza kwa muda mrefu, takribani dakika ishirini lakini mzizi au kiini cha mazungumzo yote hayo ni Mwalimu Makoronjo kutaka tumuendeleze Khadija kielimu kwani ni mtoto mwenye uwezo mkubwa sana.
Mwalimu alitushauri kwamba tumuhamishe shule anayosoma sasa na tumpeleke kwenye shule iliyo bora zaidi.
Hakuishia hapo, alikwenda mbali zaidi na kutueleza kwamba ingekuwa vyema zaidi kama angehama nje ya Tanzania na kwenda kusoma Kenya ambapo kwa mujibu wa maelezo yake ni kwamba kenya inatoa elimu ya kiwango cha zaidi ya Tanzania.
Unajua Mwalimu Makoronjo ni raia wa Kenya, amezaliwa huko Nairobi lakini alikulia Mombasa ambapo alimfuata Mama yake mara baada ya wazazi wake kutengana.
Kwahiyo akasomea huko na sasa anafanya kazi Tanzania hivyo ni rahisi kwa yeye kugundua kwamba ni nchi inatoa elimu bora kati ya hizi mbili.

Binafsi sikutaka kuona hilo likitokea, eti mwanangu nimuamishe nchi? Nisingeweza labda na mimi ningekwenda kuishi huko.
Kama ni elimu angeipata hapa Tanzania. Elimu ya kwetu ni bora na inamtosha sana cha msingi ni mimi Baba yake kumuunga mkono kwa kumpeleka shule za uhakika; za kulipia gharama kubwa.

Ukubali ukatae elimu ni ghali kwahiyo lazima iwe hivyo, kama Mzazi ama mlezi ujipinde kuhakikisha mwanao anatajarika kielimu.
"Wazo zuri mwalimu lakini ingependeza kama ungetupa muda mimi na Mke wangu tulijadili" nikamwambia lakini akili yangu tayari ikiwa imebeba jibu la hapana.
Nilitaka atupe muda ili nipate jinsi nzuri ya kumkatalia, papo kwa papo isingependeza.

Aliondoka na kutuacha na Mke wangu ambapo usiku tukiwa kitandani nilijaribu kuzungumza suala hilo na Mke wangu ili kujua naye ana mtazamo gani.
"Kwahiyo Mke wangu unashauri nini kuhusu hili la Khadija kwenda Kenya?" nilimuuliza hivyo tu, tena kwa ukarimu na utaratibu lakini jibu alilonipa lilinichosha na kunifanya hata nijute kumuuliza.
"Bwana vyovyote itakavyokuwa ni sawa tu kwanza mimi nataka kulala" akanambia maneno hayo huku akigeuka upande wa pili akinipa mgongo, akavuta shuka na kujifunika gubigubi kama ishara ya kwamba hataki stori na mimi.

Nikashindwa kumuelewa na hadi sasa simuelewi na sitamuelewa ni mwanamke wa aina gani, mwanamke asiyetaka kuzungumzia mambo muhimu ya familia yake. Mwanamke mwenye nguvu ya kumjibu mume wake vile atakavyo, hakika huyu si Ashura ninayemfahamu mimi,

Ashura niliyemuona na kuishi naye kwa upendo kipindi kile, nikampenda, akanipenda, tukapendana na kunifinya nijihisi huru kusema Ashura ni Mke wangu hata mbele ya kadamnasi.
Lakini huyu wa sasa siwezi, sina umwamba wa kusimama na kusema huyu ndiye Mke wangu kwani hana tabia za kupendeza za kuitwa Mke.
Lazima kuna kitu kitakuwa kimembadilisha.
Basi nikamuacha alale kama alivyotaka, nigaeukia upande mwingine tukawa tumepeana migongo na hadi pakakucha hivyo hivyo.

*******************

Siku ya tatu tangu Mwalimu Makoronjo alete lile pendekezo kwetu alinipigia simu. Alifanya hivyo ili kufahamu kwa tumefikia wapi ili naye aanze kufanya mipango.
Binafsi sikuridhia na nilichoona bora kumjibu ni kumwambia kwamba amuache Khadija amalizie elimu ya msingi hapa hapa Tanzania na nitampeleka huku pindi atakapofika sekondari.
Mwalimu hakuwa na jinsi na asingeweza kulazimisha ikiwa mimi ndiye mzazi wa mtoto.

*************************

Bas niliendelea kumtazama Mke wangu jinsi anavyolia kwa uchungu wa kupoteza watu muhimu kwenye maish; watoto na Mama.Lakini nadhani atalia sana pindi atakapogundua kuwa yeye ndiye msababishi kwani bila kuondokaq kwake mwanangu Ally asingepata tabu ya kwenda kumtafuta na hatimaye kupigwa na radi, pia kama Ally asingepigwa radi basi ni wazi kwamba mwanangu Khadija asingekufa kwa mshituko wa kuona maiti ya mdogo wake imeungua vile. Na pia Mama yake asingekufa kama asingesikia yale maneno ya muasherati mwenzake na Mke wangu (Mwanaume aliyekuwa naye huko)

Aliketi chini huku kilio kikipungua muda huu, pengine alichoka kwani alilia kwa muda mrefu sana huku wsisi sisi tukimtazama tu.
Mara Baba Mkwe akasimama, akatutazama sote tulioketi kwenye kochi na kusema "Kwaherini, nakwenda nyumbani" akaweka koma hapo, akavuta pumzi kwa sekunde mbili na kuongeza.

"Jamal huyu ni mke wako, una mamlaka ya kumfanya chochote upendacho. Kama utaamua kumuacha ni wewe; umpe talaka nami nitampokea kwasababu ni mwanangu wa kumzaa na hana Baba mwingine" akanambia hivyo kisha akaanza kutembea kuelekea mlangoni ambapo ndipo alipokuwa ameketi mwanaye. Akasimama pemsbeni yake akimtazama kwa huruma.

"Ashura... Nakutakia maisha mema kama mume wako ataamua kuendelea kuishi nawe, lakini nakukaribisha nyumbani kama ataamua kukuacha. Kwaheri" akamwambia sentesi fupi namna hiyo kisha akaondoka na kutuacha pale.
Na ndugu zangu nao wakasimama wote kwa pamoja.
"Kwaheri Jamal" wakaniaga na kuondoka na hatimaye ndani nikabaki mimi na Ashura tu.

Sikufahamu kwanini waliamua kufanya vile lakini yawezekana walinipa nafasi ya kufanya maamuzi. Bila shaka waliogopa hata kunishauri kwamba niendelee kuishi naye au nimeuache kwani kile kilichotokea kilikuwa ni kizito kwao hata kunipa ushauri.
Basi nikawa mwenyewe pale tena nikimtazama kwa hasira mke wangu kwani namhesabia kama ni mtu aliyeniharibia maisha yangu. Nilitamani nimuue pia ili aone uchungu ambao wameupata wanangu.

Yeye hakuthubutu hata kunyanyua uso wake kunitazama. Nikajikuta nimesimama huku nikiendelea kumtazama kana kwamba kuna jambo nataka kumueleza.

******************************

LEO SISEMI KITU ZAIDI YA KUKUSIKILIZA WEWE, NAOMBA UNISHAURI CHA KUMFANYA HUYU MWANAMKE, NIMUACHE AU NIENDELEE NAYE?

WAWEZA WASILIANA NA MWANDISHI KWA NAMBA TAJWA HAPO JUU KUPATA RIWAYA HII NA NYINGINE NYINGI KWA HALAKA ZAIDI.
 
Usimuache mkuu.
 
Back
Top Bottom