Mtukutu Mkuu
JF-Expert Member
- Jul 10, 2022
- 1,117
- 1,403
Endelea bob kama VP Mimi nitumie yote walau vipande kadhaa nikulipe Kwa Moto mmojaSehemu ya 24
“Asi, hakikisha umejiandaa vyema, saa nane tunaenda uwanja wa ndege na tutapaa kuelekea New Delhi, kisha baada ya hapo, tunarudi zetu nyumbani,” nilisema nikitabasamu, msichana akakubali kwa kichwa.
Saa nane na dakika kumi na tano tulikuwa ndani ya gari la kukodi. Mimi na Asi tulikaa viti vya nyuma, mimi nilikaa nyuma ya dereva na Asi alikaa pembeni. Japo silaha zangu nilishashusha chini, lakini msichana alionekana alipenda sana mapambano na mimi, alikuwa katingwa kwelikweli, akivichezea vidole vyangu. Kuna wakati alinikata kucha kwa meno, japo si jambo zuri sana kukata kucha kwa meno, lakini hata wewe ungemkataza?
Lakini ghafla gari aina ya ‘Van’ lilitupita kwa kasi kisha likasimama mbele. Dereva wetu akazikanyaga breki ghalfa asiyejua nini cha kufanya. Nilitazama nyuma, nako nikaona gari aina ya ‘Station Wagon’ nikatambua walikuwa wamoja na wameziba njia.
Niliwashauri wote ndani ya gari walaze vichwa chini, niliwatahadharisha kuwa, wale walikuwa watu wabaya na isingechukua muda kutudhuru. Nilimsogeza dereva pembeni, nikakaa panapo usukani, vita ikaanza.
Nilipotazama mbele, niliona watu wanne wameshuka, kila mmoja akiwa na bastola mkononi, nyuma ya gari hakuna aliyeshuka. Nikalitia gari moto, nikakimbiza kama ninayetaka kuwagonga, wote wakapisha na kuruka upande wa pili wa gari kisha wakazimimina risasi ambazo zilisambaratisha kioo chote cha gari lile aina ya ‘Hatchback’. Kwa sababu waliziba njia yote, niliingia nje ya barabara, tukanesanesa mpaka tuliporejea tena barabarani.
Kwa msaada wa ramani za google ambazo nilizitazama siku moja kabla ya safari, nilitambua uelekeo wa safari yangu. Hivyo niliendesha kwa kasi ili niweze kuwatoka washenzi wale. Lakini nao waliamua kwelikweli kutukamata.
“Dereva,” niliita, mzee wa Kihindi alilala akitetemeka mwili mzima, mikono kaipachika kichwani hata usipoangalia kwa makini, unaweza dhani ni panzi kapanda gari.
“Ndiyo…” aliitika, akatamani kuongea, lakini maneno hakuna.
“Sikiliza, hawa ni watu wabaya, wanataka kuiba gari lako,” nilidanganya. “Sikiliza tena, sasa tukifanikiwa kuendesha mpaka karibu na uwanja wa ndege, watarudi nyuma wenyewe kwa sababu pale pana kambi ya jeshi na majambazi hayapatani na watu wa majeshi, tukishindwa watapora gari lako. Shika usukani uendeshe, mimi nipambane nao kwa bastola.”
Tulibadilishana kwa ustadi, gari likayumba kiasi na kupunguza mwendo. Halafu nikakaa kiti cha nyuma nilipokuwa nimekaa mwanzo, nilimuona Asi akiwa kainamisha kichwa chini nikatambua ni mwanafunzi mzuri anayefuata maelekezo.
Kwa sababu ya kule kupunguza mwendo kwa gari letu, ‘Van’ ilitupata, ikawa pembeni, nikatazamana uso kwa uso na jamaa aliyeshika bastola, akaachia tabasamu, na mimi nikatabasamu, halafu akalenga shabaha ampige dereva, lakini alichelewa, nilimpiga risasi ya mkono, bastola ikadondoka chini, halafu dereva wangu akaongeza kasi zaidi, tukawa mbele wao nyuma na mgonjwa wao!
Kumpiga risasi mtu mmoja tu ndani ya ‘Van’ kuliwanyong’onyeza wote waliokuwamo bila kujali kuwa bado walikuwa na silaha na gari lilitembea vyema. Niliwaona wakiweka gari pembeni, nikakumbuka kuwa, watu wanapopigana bila kuwa na hamasa ya kueleweka, huwa hawapigani kwa uwezo wao wote. Sisi tulipigana kwa ufanisi katika vita vya Kagera kwa sababu tulipigania ardhi yetu iliyotaka kuporwa na Nduli asiye na aibu Idd Amin Dada. Askari wa Uganda walishindwa vita kwa sababu hawakuwa na hamasa ya kueleweka. Walipigana kwa sababu gani?
Ilibaki ‘Station Wagon’ ikitufuata kwa kasi. Kwa ufanisi mkubwa, nilifumba jicho moja, halafu nikalenga shabaha katika taili la upande wa kulia mbele, nchini India wanaendesha upande wa kushoto kama tunavyoendesha sisi Watanzania. Basi nikaruhusu risasi itoke, ikapasua taili la gari yao kwa sauti kubwa, halafu gari likayumba huku, likayumba kule kisha likaacha njia na kwenda kugonga mti. Sina hakika kama walipona. Yote yanawezekana!
Inaendelea...
Kuwa wa Kwanza Kupokea mwendelezo wa Riwaya hii Kwa kujiunga katika Group la bure WhatsApp, Gusa Hapa Kujiunga
Tupate Wadhamini:
Soma: Jinsi ya Kuomba Chuo Mwaka 2022
Huu ndo ulevi wangu nikikosa sigara basi navuta simulizi riwaya story na filamu