Riwaya: Mwanamke Uliyekula Pesa Zangu Nakutafuta

Riwaya: Mwanamke Uliyekula Pesa Zangu Nakutafuta

Sehemu ya 23

Niliikimbiza gari kwa mwendo wa kilomita 120 kwa saa, jamaa nao walizidi kutufuata. Katika kona moja, almanusura gari letu lianguke kwani mbele palikuwa na lori lililokuwa linakimbia upande usio wake, bahati, nikalikwepa kwa mafanikio. Wale jamaa waliokuwa wanatukimbiza, walipojaribu kulikwepa, dereva akazidiwa na mwendokasi, gari likaserereka mpaka katika mtalo. Niliyaona hayo kupitia kioo. Ukawa mwisho wa kimbizakimbiza.

Niliendesha gari mpaka katika hoteli moja huko Kolkata, nikaliacha sehemu ya wazi tena iliyo salama ili mwenye nalo aweze kulipata. Sikusahau kufuta alama za mikono na ushahidi mwingine.

** ** **​

“Hello,” niliongea katika simu nikiwa nimejilaza, niliyezungumza naye, tulionana uso kwa uso, Asi nilimweka mbali kidogo ili asiharibu mambo.

“Yes baby…” alijibu Deepa.

“Nakuaga, siku yoyote kuanzia sasa narudi nyumbani, nimehitajika haraka, baada ya wiki mbili nitarudi kukusalimia,” nilisema ukweli mwanzoni kisha nikadanganya huko mwisho.

“Ooooh, jamani!” msichana mwenye mshangao alilalamika. “Naumia sana kukukosa Mako, ukiondoka urudi kwa muda uliosema tafadhali.”

Tulizungumza mengi mpaka nilipokata simu. Pia, tulikubaliana kuendelea kupiga soga katika mitandao ya kijamii.

Asi aliyekaa kwenye kochi mbele yangu, aliuliza kivivu, “Ulikuwa unaongea na nani?”

“Rafiki aliyesaidia kukupata,” nilijibu kibabe kisha nikabadili mada ya mazungumzo. “Nenda kaoge, kaa tayari, jamaa wanaweza kutuvamia muda wowote. Hakuna amani mpaka tuwe tumerudi nyumbani.

Wakati Asi anaoga, nilipanga mipango ya safari kuelekea New Delhi. Sikuwa na hamu hata kidogo ya kusafiri kwa basi tena. Mazira niliyokutana nayo yalinikatisha tamaa. Hapo ndipo nilipopata wazo la kusafiri kwa ndege. Lakini haingekuwa salama kutembea katika mitaa ya Kolkota kuitafuta tiketi, kwa vyovyote lazima watu wake Akshay wangekuwa wametega katika maeneo ya stendi, stesheni, bandarini na katika viwanja vya ndege.

Nilijaribu kununua tiketi ya ndege kwa njia ya mtandao ikashindikana, ukweli ukabaki kuwa, kama ninataka tiketi, nitaipata uwanja wa ndege. Hofu yangu kubwa ni kwamba, nilikuwa tofauti sana na Wahindi hivyo kugundulika ilikuwa ni rahisi mno hata kama ningefanya njia za kujibadili kidogo. Mfano, katika muda wote niliokuwa hapo Kolkata, nilifanikiwa kuona watu weusi wanne tu na Asi akiwemo. Hivyo niliamua kuangalia ratiba ya safari na niende uwanja wa ndege saa nne kabla ya safari, natambua gharama ya nauli ingekuwa kubwa, lakini hakukuwa na njia salama zaidi ya hiyo. Baada ya kutazama ratiba, nikagundua palikuwa na ndege ya kuondoka siku hiyohiyo saa kumi na moja jioni, nami nikapanga saa nane mchana, niende uwanja wa ndege, nichukue tiketi kisha niisubiri hiyo ndege.

Wakati huo, Asi alitoka bafuni kuoga, ilikuwa asubuhi saa tatu. Alitoka akiwa kajifunga taulo mali ya hoteli ile. Jinsi alivyoloa maji, rangi yake tamu nyeusi, miguu minene kiasi cha kufanana na chupa ya bia na jinsi alivyokuwa amebinuka kidogo, mapigo yangu ya moyo yalibadilika ghafla, yakawa yanadunda kwelikweli. Nikamrukia kabla hajajifuta, tukadondoka kitandani, lakini akaibana miguu yake kwa nguvu, nami nikatumia mabavu yangu nikaisambaza miguu ile laini, nikawa katikati juu yake, lakini sasa akanishika mkono uliokuwa umeshika kiungo changu cha uzazi tayari kukielekeza kunako kiungo chake yeye. Nilimwacha aushike mkono ule, nami kwa sababu ya uzoefu wa mambo haya, ramani naifahamu hata bila ya kushikwa mkono kwa hivyo nikawa nafanya juhudi za kuzamisha bila kushika kwa mkono, lakini kila nilipogusa alijitikisa, akanisukuma na zoezi likawa gumu. Jasho likanitoka hata sasa nikagundua njia pekee ya kufanikisha adhma yangu ni kutumia nguvu zaidi, kukunja sura na kutunisha misuli. Halafu nafsi ikanisuta, nikawaza, nimekuja kuokoa au kubaka? Kwa nguvu alizotumia, Asi hakuwa tayari, nikamuacha, nikiwa nimenuna lakini nina tabasamu ili ajisikie yuko nyumbani. Kwa taarifa tu hata usiku tuliolala na kuamka asubuhi hiyo, nilijaribu tukio hilo, Asi akatumia nguvu kujihami, nami nikamwacha alale unono.

“Nisamehe Bwana Mako,” aliomba msichana akijifunga taulo lake vizuri ambalo awali nililibwaga kitandani.

“Huna kosa Asi, wewe ndiyo unapaswa kunisamehe, kusema kweli ninachotaka kufanya hakiko sawa! Lakini nimeuona msimamo wako, nakuahidi sasa uko salama.”

Msichana Asi alitulia, aliyaamini maneno yangu, hofu yake ikapungua, akalibwaga taulo, akawa kama alivyozaliwa, kisha akatembea kwa mbwembwe kama twiga kwenda kuchukua nguo yake ya ndani aliyoiweka juu ya meza, aliifikia na kuivaa, kisha akamalizia kwa kuvaa suruali na mavazi mengine.

Inaendelea...

Kuwa wa Kwanza Kupokea mwendelezo wa Riwaya hii Kwa kujiunga katika Group la bure WhatsApp, Gusa Hapa Kujiunga

Tupate Wadhamini:

Soma: Jinsi ya Kuomba Chuo Mwaka 2022
twasubili muendelezo
 
Sehemu ya Nane

Sasa ilikatika miezi miwili na wiki moja tangu kumpoteza Asi. Nimefanya juhudi hii na ile kumtafuta lakini sijampata. Likizo yangu pia, ilikuwa imebakiwa na wiki tatu tu. Katika hali ya kukata tamaa, niliamua kwenda kusalimia wagonjwa katika hospitali ya Mwananyamala.

Majira ya saa kumi jioni, mwanamume aliyevalia suti ya kijivu na viatu vyeusi alionekana akipita katika geti la hospitali na kwenda moja kwa moja mpaka katika wodi ya watoto. Hakupata shida kupita getini kwa sababu ya ile suti lakini pia, ule ulikuwa muda wa kuona wagonjwa. Mwanamume huyo, alikuwa mimi Mako. Mtu mwenye jina moja kama mbwa!

Niliingia mpaka ndani ya wodi iliyohudumu watoto wadogo, vitandani walilala watoto na pembeni walikaa wazazi wao. Nilianza kwa kumsalimia mama mmoja aliyekuwa vitanda vya mwanzo karibu na mlango.

“Mama mwanao amepatiwa matibabu,” niliuliza baada ya salamu.

“Hajapatiwa baba, wamesema mpaka helaa!” alijibu Mama wa mtoto, machozi yakimlenga.

“Matibabu ni lazima, pesa italipwa baadae,” nilisema kwa sauti iliyosikika pote mle. Mama mmoja aliyekuwa kitanda cha tatu akadakia, “Mheshimiwa hata mwanangu hajapatiwa matibabu,” kabla sijakaa sawa, bibi mmoja akapaaza sauti, “Mkuu wa mkoa nisaidie mjukuu wangu hajapewa dawa siku ya tatu baba.”

Ama hakika bibi yule sijui aliwaza nini kuniita mkuu wa mkoa! Ni kweli siku tatu zilizopita, mkuu wa mkoa alibadilishwa ama wengine wanasema alitumbuliwa na wananchi hawakumfahamu vyema mkuu wao mpya ambaye hakuwa ameanza kuonekana katika Luninga.

Sasa kitendo cha yeye kuniita mimi mkuu wa mkoa, kiliamsha watu wote wodini mle, macho yao yakawa kwangu hata manesi na madaktari wakanyanyuka katika siti zao wakija mahali niliposimama.

“Nkuu wa Nkoa kaja kwa ku shtukiza… patachimbika humu ndani nakwambia, atatumbuliwa ntu baada ya ntu,” alisema bibi mwingine aliyekuwa anamuuguza mjukuu wake.

“Unapiga simu wapi?” nilimfokea nesi ambaye alionekana kupiga simu kuwaita wakubwa wake. “Usipige simu, usimuite yeyote, hapa nimekuja kwa kushtukiza na nitaingia kila wodi kwa kushtukiza.”

“Sawa mkuu,” walijibu watumishi wale wa afya. Wagonjwa wakatabasamu.

“Sasa sikiliza,” niliendelea. “Wagonjwa watibiwe, pesa italipwa baada ya matibabu, tuhakikishe tunaokoa uhai kwa gharama yoyote. Pesa zipo tu na haziwezi kamwe kufanana na thamani ya uhai wa mwanadamu.”

“Ndiyo mkuu,” walijibu.

“Natoka humu katika ziara yangu hii ya kushtukiza, msipige makelele wala msinifuate, pia msipigiane simu, nakwenda kwenye jengo lile wodi ya wazazi, nawatakia utekelezaji mwema.”

Nilitoka katika wodi ile na kuanza kuelekea wodi ya wazazi. Nilikuwa na hofu kwamba, watu wangeongezeka zaidi, lazima ningegundulika kuwa mimi siyo mkuu wa mkoa. Hii ingekuwa kesi kubwa tena ya aibu. Vilevile sikuwa nimepanga kuwa nitambulike hivyo, ni watu niliowakuta wodini ndiyo walinipachika cheo hicho.

Nilitembea haraka nikazipandisha ngazi za jengo la wodi ya wazazi. Nilikuwa napiga jicho nyuma kwa kuibia, kumbe maelekezo yangu hayakufuatwa, kuna manesi walishapiga simu na nyuma kiasi cha hatua mia mbili, niliona watu wengi wakija nilipo, niliweza kuwatambua watu hao, mmoja wao alikuwa Daktari mkuu wa hospitali hiyo. Alikuwa anakuja nilipo akiongozana na madaktari wengine watano na askari watatu.

Sasa niliiona hatari iliyokuwa inaninyemelea. Daktari mkuu na wenzake wote wasingeshindwa kutambua kuwa mimi sikuwa mkuu wa mkoa hata kama mkuu mpya wa mkoa hakuwa ameanza kuonekana katika Luninga. Wazee hawa wanawafahamu viongozi wote kwani ni jamaa zao.

Nilitembea haraka nikalifikia jengo la wazazi na sasa nilikuwa ndani ya jengo hilo lililo juu kimo cha ghorofa moja. Niliwaacha mbali watu wale lakini nao walikuwa wakija kwa kasi zaidi. Niliingia wodini kama ninayesalimia watu. Jengo hili lina upande wa kushoto na kulia, mimi nilielekea kulia, nikatembea mpaka mwisho na bahati njema, mapokezi hapakuwa na daktari wala nesi na wodi nzima ilikuwa na mgojwa mmoja tu aliyekuwa anaongezwa damu na alilala usingizi.

Nilifungua dirisha kubwa la vioo kisha nikatoka kwa kushuka taratibu, nilipoona kimo cha chini ni kidogo, nilijitupa kikomandoo, kisha kwa kuinama, nikakimbia mpaka ulipo ukuta, nikauparamia kama mjusi na kuukwea mpaka kilele chake, halafu ‘puuu’, nilikuwa nje ya hospitali. Huko nyuma sikujali kama kuna mtu aliniona au hakuniona.

Inaendelea...

Tupate Wadhamini:

Kwa Mahitaji ya kuandikiwa CV, Barua ya Maombi ya Kazi na Masomo kwa Wanafunzi wanaorudia mitihani, Gusa Hapa Tuwasiliane Whatsapp.
Mwamba anajua sana
 
Sehemu ya 14

Zilipita siku tatu baada ya kuachana na Akshay, mtu ambaye alisaidia sana kunipa mwanga juu ya mtu niliyekuwa namtafuta. Nilikaa katika ukumbi wa vinywaji hapa Mayank Hotel, nikiwa miongoni mwa watu wengi waliokuwa eneo hili, nilitafakari kwa kina kauli ya Akshay kusema, ‘Babuu kapata matatizo, tuna mtu mwingine sasa.’ Pia, Babuu aliwahi kuniambia ‘ajenti’ anayemtumia ni Akshay, hivyo kwa vyovyote lazima Akshay anafahamu alipo Asi.

Wakati nikiwa katika lindi la mawazo, nilishtushwa na mhudumu aliyekuwa akinishika bega, nilimgeukia, akanikabidhi karatasi aliyodai ilikuwa bili yangu.

“We dada, mimi sijatumia vitu vyote hivi… kinywaji changu ni hiki tu!” nililalamika.

“Ooooh… Samahani kaka, kuna dada kakaa pale katikati kasema wewe ndiyo utamlipia,” alijibu mhudumu akiunyoosha mkono wake katikati ya watu. Nami nikashtushwa na huyo dada na nikashangaa nawezaje kuwa na dada India! Macho yalitambaa mpaka alipounyoosha mkono, nikamuona dada aliyemsema lakini sikuweza kumtambua kwa sababu alivaa kofia pana iliyoziba sura yake.

Tulitazamana kwa dakika moja mimi na yule mhudumu, yeye akisubiri nilipe bili ya dada nisiyemfahamu, na mimi nikitafakari nilipe au nisilipe.

“Samahani,” nilivunja ukimya. “Unaweza kumwambia huyo msichana aje hapa… mmmh… aje hapa kisha nakulipa pesa yako.” Mhudumu alikubali, alitembea kwenda kumuita binti, mimi sikubaki kijinga, niliiandaa bastola yangu aina ya Luger. Siku hiyo, Berreta niliiacha ndani. Nimekuwa katika mitego ya kijinga kama hiyo, hivyo isingekuwa rahisi kunasa.

Mhudumu alirudi akiwa kashika kikaratasi, akanipatia, nikasoma, kisha nikacheka sana baada ya kuona kilichoandikwa. Kikaratasi kilisomeka hivi:

“Mako, lipa bili yangu kwa kutumia pesa ulizopewa na baba yangu, bili ni ndogo, hata robo ya pesa haitatumika.”

Nilichomoa noti tatu, nikamkabidhi mhudumu, “Na yangu nimelipa kabisa,” nilimsisitiza, kisha akaondoka na kuniacha nimekaa kwa kuegemea kiti na mikono nimeiachia ninayecheka sana.

Lakini ghafla ukumbi wote ulikaa kimya, mziki ukawa hausikiki, watu wakageuza shingo zao kumtazama msichana mrembo aliyetembea kwa madaha kuja nilipokaa. Alijikokota kama twiga, viatu vyake vikalia, ko, ko, ko! Kama kawaida yake, alivaa shati nyeupe na suruali ya jinzi yenye rangi ya bluu. Alipotembea na hasa alipokuwa hatua chache Kufika nilipo, nikauona uwazi katikati ya miguu yake, mapigo ya moyo yakaenda kasi kama ninayekimbia marathoni. Kufumba na kufumbua, malaika yule alikuwa mbele yangu, akanipiga busu la shavu, wala sidanganyi, mashahidi ni wale wahindi wenzake waliokuwa ukumbini pale. Basi nikawa mlenda nisiye na nguvu, katika hali hiyo, mtoto wa miezi mitatu, angeweza kunisukuma kwa nusu ya nguvu zake nikadondoka!

Alivua kofia akaitupa, akanitazama akitabasamu kisha akairamba midomo yake ya kike.

“Kwa nini uliondoka bila kuaga?” Deepa aliuliza akijiweka vizuri katika kiti. Nikataka nimweleze kilichotokea, lakini nikaona haikuwa busara, kwanza yale yalikuwa mambo ya kiume kati yangu na Akshay.

“Simu iliita, nikamuomba baba aage kwa niaba yangu,” nilidanganya.

“Hujambo sasa?”

“Sijambo, vipi wewe!”

“Sijambo pia…” nilijibu, nikamtazama usoni nikitabasamu, tabasamu ambalo lilificha ile hofu niliyokuwa nayo, Akshay alinionya nisizoeane na binti yake, nami niliogopa sana kuona binti kanifuata katika makazi yangu, kwanza sikuja kugombana na Wahindi, nilikuja kumtafuta Asi.

Baada ya kuzungumza kidogo, Deepa alichukua bilauri yangu, akaanza kunywa kinywaji kilichokuwamo, nami nikaanza kunywa kwenye chupa maarufu kupiga tarumbeta. Kama kawaida yake, mafunda mawili yalimchangamsha, lakini naamini hakulewa, akanyanyuka katika kiti, akaanza kucheza.

Zilipigwa ngoma za Kihindi zikachanganywa na zile za kizungu. Binti alicheza zote. Katika hali ya kushangaza sana, ikapigwa Amapiano, wala haikuwa ya msanii wa Afrika ya Kusini ambako ndiko chimbuko la mziki huu, ilipigwa Amapiano ya kijana Marioo kutoka Tanzania.

“Bia tamu, asikwambie mtu tutu, bia tamu…” Ulisikika wimbo, nami kwa furaha nikanyanyuka kuyacheza mapiano haya. Kwanza nilianza kwa miondoko ya kawaida, lakini mapiano yalipokolea, nikachukua kinywaji changu na kuanza kucheza nacho huku nikiwa kama ninayetaka kuuweka chini mgongo, Deepa akaiga, naye akaanza kucheza na bilauri juu ya mdomo. Wote tukaonekana tu wendawazimu wa kimataifa.

Tulicheza sana na Deepa alijifunza kwa haraka hata akaimudu miondoko. Tulicheza ‘Happy Feet Legwork’ ‘Amapiano Moon walk’ na tukacheza ‘Nkululu dance’. Nilitamani sana bwana ‘Dj’ aweke singeli, Deepa asaule pale chini nami nimdondokee bila kujali, lakini haikuwa hivyo. Singeli hayakuwekwa!

Tulicheza mpaka jasho likatutoka. Msichana akanisogelea na kuninong’oneza kitu sikioni, “Nimechoka, na watu wanatutazama sana, twende chumbani kwako Bwana Mako, kule nilipolala bila kudhurika!”

Inaendelea Kesho...

Kuwa wa Kwanza Kupokea mwendelezo wa Riwaya hii Kwa kujiunga katika Group la bure WhatsApp, Gusa Hapa Kujiunga

Tupate Wadhamini:

Kwa Mahitaji ya kuandikiwa CV, Barua ya Maombi ya Kazi na Masomo kwa Wanafunzi wanaorudia mitihani, Gusa Hapa Tuwasiliane Whatsapp.
Mzee Baba ulitaka usaule muhindi aloo
 
Back
Top Bottom