SIN 66
Muandishi…………………………………………….EDDAZARIA G.MSULWA(G.Authour)
Age ……………………………………………………18+
Simu………………………………………………… 0657072588(whatsapp) au 0768516188
ILIPOISHIA
“Ninakupenda sana Jery. Wewe ndio ulikuwa mwanaume wangu wa kwanza kuingia kwenye maisha yangu na uliweza kunivumilia kwa kila jambo. Kwanini niache kukupenda?”
Julieth alizungumza huku nafsi yake ikimsuta kwani ukweli ni kwamba moyo wake upo kwa Evans.
“Nina imani kwamba bikra yangu ume itunza na leo sinto kufanya kitu hadi pale tutakapo funga ndoa yetu na kuivunja bikra ambayo niliivumilia na kuitunza kwa kipindi chote tulicho kuwa pamoja.”
Jery alizungumza kwa furaha sana na kumfanya Julieth kujikaza tu katika kutabasamu ila ukweli ni kwamba hadi hapo alipo hana bikra na ni siku mbili tu zilizo pita Evans aliivunja bikra yake.
ENDELEA
“Kuna zawadi moja nime kununulia mke wangu, ila nitakupatia mara tu baada ya kufunga ndoa yetu”
“Zawadi gani?”
“NItakuambua siku tukifunga ndoa”
Gafla Julieth simu yake ikaanza kuita, akaitazama na kukuta ni namba ya baba yake. Akashusha pumzi na kuipoke.
“Yes Dady”
Julieth alizungumza kwa kuigiza kwani hata kumuita hivyo baba yake kwa madoido ni kumpumbaza Jery asiweze kuelewa chochote kinacho endelea.
“Upo wapi?”
“Mmmmm nipo some where dady”
“Sema up wapi kwa maana nina hitaji ufike hapa nyumbani haraka iwezekanavyo”
“Kuna nini baba?”
“Kuna tatizo, hivyo njoo sasa hivi”
Nabii Sanga alizungumza kwa msisitizo. Na kumfanya Julieth kuanza kutawaliwa na wasiwasi.
“Mpenzi wangu kuna nini?”
“Ba…baba anasema kwamba nyumbani kuna tatizo”
“Tatizo gani?”
“Sielewi mume wangu. Nahitaji kwenda sasa hivi”
“Basi acha nikupeleke”
“No acha niende tu”
“Hapana, wewe ni mke wangu na isitoshe nyumbani kwamba kuna matatizo. Siwezi kukuacha uende peke yake tena uendeshe gari ikiwa mimi nipo na nina walinzi kibao. Hivyo nyanyuka tuondoke”
Jery alizungumza kwa msisitizo huku akinyanyuka. Akaibeba pochi ya Julieth, akamshika mkono na wakaanza kutoka ndani hapo. Wakaongozana na walinzi wake hadi eneo la mapokezi.
“Funguo za gari lako zipo wapi?”
“Ndani ya hiyo pochi”
Jery akafungua pochi yake na kumkabidhi funguo hiyo mmoja wa walinzi wake. Wakaingia kwenye gari walizo kuja nazo hapo hotelini, huku mlinzi mmoja akiendesha gari la Jery na wakaondoka eneo hilo la hotelini.
***
“Sasa mwanangu ana kuja. Atakuletea huyu panya wako”
Nabii Sanga alizungumza kwa msisitizo mara baada ya kukata simu.
“Sio panya ni mume wangu”
“Una mume gani sasa pale?”
Nabii Sanga alizungumza kwa dharau huku akimtazama Magreth aliye lowana mashavu yake kwa machozi. Baada ya dakika ishirini, wakasikia mingurumo ya magari ikisimama nje hapo. Mrs Sanga akachungulia dirishani, akastuka sana mara baada ya kumuona Jery na Julieth wakishuka kwenye gari moja huku wakiwa wameongozana na walinzi wanao mlinda.
“Mungu wangu!!”
“Kuna nini?”
“Jery ana kuja na walinzi wake”
“Nini?”
Nabii Sanga kwa haraka akakimbilia naye dirishani na kuwaona Jery na Julieth wakija ndani hapo. Wakakaa kwenye masofa huku wakijikausha kana kwamba hakuna kitu chochote kinacho endelea. Julieth na Jery wakaingia ndani hapo, Magreth na Julieth wakashangaa sana kukutana hapa kwa maana Magreth kumbukumbu zake za mwisho alikutana na Julieth kwenye mgahawa wake akihitaji kupewa msaadawa kujua ni namna gani anaweza kufungua mgahawa kama wa kwake.
“Hi mom. Hi Dady”
Julieth alizungumza huku akimkumbatiana na mama yake, kisha akambusu baba yake shavuni.
“Jery karibu sana”
“Asanteni sana wazee wangu. Tumestuka sana yulipo sikia kwamba kuna tatizo hapa nyumbani?”
“Yaa ni kweli ni tatizo dogo tu lakifamilia.”
“Ahaa basi wazazi wangu nombeni mimi niondoke ili niwape nafasi ya kuzungumza”
“Mbona mwanangu una wahi hivyo?”
Mrs Sanga alizungumza huku akinyanyuka.
“Mama yangu ni vyema nikawapa nafasi ya kuyajadili mambo ya kifamilia na isitoshe nimekuja pasipo mualiko rasmi hivyo nitakuja siku nyingine rasmi hapa nyumbani”
Ucheshi wa Jery ukazidi kuwavutia nabii Sanga na mke wake. Jery akaondoka nyumbani hapo na walinzi wake.
“Huyu malaya amefwata nini hapa nyumbani kwetu?”
Julieth alizungumza kwa jazba kubwa huku akimtazama Magreth aliye jikuta akicheka kicheko cha kejeli.
“Yaani malaya ni mama yako aliye tembea na Tomas, baba yako aliye tembea na mimi na wewe uliye tembea na mume wangu Evans hivyo naamini umesha jua nani ni malaya kati yenu na mimi”
“Magreth funga bakuli lako kumbuka kwamba hapa upo nyumbani kwangu”
“Haijalishi, ila twendeni kwenye point. Wewe nina imani huyu uliye kuja naye hapa ni mpenzi wako. Sasa ujije ukajikuta nina kuharibia kwake kwa maana sinto kuwa na huruma katika hilo”
Julieth akajawa na mshangao mkubwa sana mara baada ya kusikia Evans ni mume wake Magreth.
“Umekosea, Evans wangu sio mume wako”
“Muulize baba yako kwa maana yeye ndio aliye jaribu kumfukuza Evans wangu kwangu kwa kutumia bastola kutokana tu na wivu wake”
Julieth taratibu akaanza kupata picha taratibu. Evans alimuadisia kwamba mwanaume wa mwanamke ambaye akuwa ni mpenzi wake, alimfukuza nyumbani kwa mke wake kwa kutumia bastola. Machozi ya hasira na kinyongo cha kujiona ni mjinga yakaanza kumtiririka Julieth machoni mwake. Kitu kinacho mtia uchungu zaidi ni jinsi alivyo mkabidhi usichana wake mwanaume ambaye aliamini kwamba ni wa maisha yake yote.
‘Baba na Evans wameshea mwanamke mmoja ohoo Mungu wangu’
Julieth akanyanyuka na kukimbilia chumbani kwake na kuwafanya watu wote kujawa na mshangao. Mrs Sanga naye akanyanyuka na kukimbilia chumbani kwa Julieth, akamkuta akiwa amekaa kitandani huku akilia kwa uchungu.
“Mwanangu vipi?”
“Yaani baba na Evans wametembea na yule malaya pale eheee?”
Mrs Sanga akashusha pumzi kwa maana swali hilo lina uponda ponda sana moyo wake.
“Mama yaani nimetoa bikra yangua mbayo nilipanga kumpa Jery ila leo hii nime mpa yule mjinga. Ahaa……inaniuma mama”
Julieth alizidi kulia na kumfanya mrs Sanga kumkumbatia mwanaye huyo wa kike.
“Wanaume ni watu wabaya. Mwanangu huu ni wakati wa kufanya jambo juu ya maisha yako. Achana na huyo Evans, mtazame Jery ndio mwanaume sahihi kwenye maisha yako”
Mrs Sanga alizungumza kwa sauti ya upole hukua akimtazama Julieth usoni mwake. Julieth akajipangusha machozi yake kwa pamoja na kumkazia macho mama yake.
“Mama nina hitaji kumua Evans”
“Kwa nini?”
“Hawezi kunitoa bikra yangu na nikamucha hai ikiwa ni msaliti kwenye maisha yangu”
Mrs Sanga macho yakamtoka kisha baada ya muda akatabasamu kwani roho yake ya ukatili sasa ana anza kuiona ndani ya mwanaye huyo.
“Kamueleze huyo kunguni wako aniambie ni wapi alipo mume wangu. Nikamchukue la sivyo sinto ondoka hapa”
“Hivi wewe binti una jiamini nini, ikiwa mimi ndio nilikutoa kule uswahilini na kukupeleka kwenye maisha mazuri. Hivi una jua nina weza kukupokonya kila kitu”
“Hahaa hakuna tabu una weza kunipokonya. Ila kabla ya kunipokonya ulimwengu mzima utajua madhambi yako”
Nabii Sanga akafumba macho kwa sekunde kadha akisha akamatazama Magreth.
“Kitu unacho jaribu kukifanya wewe ni sawa na paya kuanzisha vita na panya ikiwa anatambau fika kwamba hana uwezo wa kuoambana na paka”
Nabii Sanga mara baada ya kuzungumza hivyo akanyanyuka na kuondoka sebleni hapo na kuelekea chumbani kwa binti yake.
“Hei Julieth yupo wapi Evans?”
Nabii Sanga aliuliza huku akikaa pembeni ya binti yake.
“Baba”
“Naam”
“Ninawaomba munisamehe kwa yale niliyo yazungumza jana”
“Tume kusamehe kwa maana tuna jua ulikuwa hujui kinacho endelea”
“Ni kweli, ila baba nina hitaji kufanya jambo moja”
“Jambo gani?”
“Nataka kumuua Evans. Hawezi kunitoa usichana wangu na nikamuacha hai. Atakuja kuniharibia kwa Jery”
Nabii Sanga akamtazmaa mke wake huku akishindwa kutoa jibu sahihi.
“Kwa sasa yupo wapi?”
“Hotelini”
“Hoteli gani na yupo chumba namba ngapi?”
Julieth akakaa kimya kidogo kisha akamtazama baba yake.
“Yupo hoteli ya X Royal chumba namba elfu moja na tatu?”
“Sawa”
Nabii Sanga akanyanyuka na kutoka chumbani hapo. Akarudi sebleni na kumkuta Magreth akiwa amesimama.
“Yupo hoteli ya X Roya chumba namba elfu moja na tatu. Kaishi maisha ya amani na huyu kijana wako, sinto hitaji uingilie tena kwenye maisha yangu umenielewa”
Magreth akanyanyua begi lake, akamtazama nabii Sanga kwa sekunde kadhaa kisha akamsogelea.
“Endapo kuna jambo lolote litamtokea Evans au mimi, basi nita hakikisha watu wa kwanza kushuhulika nao ni wewe na familia yako. Umeona uwezo wangu kidogo tu, ila nina uwezo hata wa kupigana ana wanaume kumi wenye uwezo mkubwa na nikawapiga hiyo kuwa makini na mimi”
Magreth akampiga nabii Sanga busu la shavuni kisha akaondoka nyumbani hapo. Breki ya kwanza akasimama katika hoteli hiyo, akashuka na moja kwa moja akaingia kwenye lifti na kupandisha gadi gorofa ya nne. Akatembea kwenye kordo hiyo na akaona chumba namba elfu moja na tato. Akasimama malangoni hapo kwa sekunde kadhaa na kuanza kuminya kitufe cha kengele.
***
Evan mara baada ya kukaa dakika ishirini ndani ya chumba hicho, akatoka na kuingia kwenye mgahawa ulipo katika hoteli hiyo. Akaanza kunywa juisi huku akitazama mechi ya mpira pamoja na mashabiki wengine waliomo katika mgahawa huo.
‘Nina kwenda kuwa tajiri sasa’
Evans alizungumza huku akitengeneza picha za muono wa jumba walilo kubaliana yeye na Julieth kulinunua.
‘Sijui nimuambie aniadikishe jina langu?’
Evans alizidi kuwazia mafanikio hayo ambayoa amebakisha masaa kadhaa kabla ya siku hii ya keo kuisha.
“Habari yako kijana?”
Sauti ya mzee Mbogo ikamstua sana Evans aliye jikuta akimshangaa mzee huyo kwa maana hajawahi kumuona sehemu yoyote kwenye maisha yake.
“Salama. Shikamoo”
“Marahaba nina weza kukaa?”
“Ndio karibu”
Mzee Mbogo akaka katika kiti kichopo pembeni ya meza hiyo. Akaweka bahasha yenye rangi ya kaki, mezani hapo.
“Fungua ndani ya bahasha kuna zawadi yako”
“Samahani sana mzee. Una nifahamu mimi?”
Mzee Mbogo akatabasamu kidogo, akapiga fumba la maji aliyo fika nayo hapo mezani.
“Evans Richard Shika si ndio?”
“Nd….i…ioooo”
“Basi fungua ndani ya bahasha hiyo kuna zawadi yako”
Taratibu Evans akaichukua bahasha hiyo huku mikono ikimtetemeka mwili mzika. Akaifungua bahasha hiyo, picha ya kwanza kuitoa, ni picha yake na Julieth. Akastuka sana kwa maana picha hiyo ime pigwa wakiwa katika mgahawa ambao walikuwa wakipata chakula mchana wa siku ya leo. Akafungu picha ya pilis na kumshuhudia Julieth akiwa ameshika mikono na mwanaume mwengine ambaye hamtambui ni nani. Taratibu akatoa picha nyingine huku mapigo yake ya moyo yakizidi kumuenda kasi, akamshuhudia Julieth akiwa amekumbatiana na mwanaume huyo huku wakinyonyana lispi zao na nguo ambazo amevaa Julieth ndio nguo hizo hizo alizo ondoka nazo leo.
“Mzee ume zitoa wapi hizi picha?”
“Huyo binti anaitwa Julieth Sanga. Ni mtoto wa nabii mkubwa sana waha Tanzania, nabii Sanga nina imani kwamba una mfahamu. Pili huyo wa pembeni ni mwanaume wake anaitwa Jery Mtenzi, ni mtoto wa raisi Mtenzi aliyopo madarakani kwa sasa. Hivyo Evans kama ulikuwa na ndoto za kumuo huyo binti basi kaa naye mbali kwa maana kinacho fwata kwako ni kifo. Kwausalama wako ondoka kabisa ndani ya jiji la Dar es Salaam.”
Mzee Mbogo mara baada ya kuzumguza hivyo akaondoka huku vijana wake wanne wanao mlinda nao wakaanza kunyanyua kwenye meza walizo kuwa wamekaa na kuondoka naye na kumuacha Evans akiwa amenyong’onyea huku akihisi moyo wake ukichwanjwa chanjwa na viwembe kwani maumivu anayo yahisi hapo ni mara mbili ya maumivu aliyo sababishiwa na Magreth.
ITAENDELEA
Haya sasa, mambo yanazidi kunoga. Evans amefahamu ukweli juu ya mapenzi yaliyopo kati ya Julieth na Jery je ataondoka jijini Dar es Salaam? Endelea kufwatilia kisa hichi cha kusisimua, usikose se hemu ya 67