Maheshiyaq
Member
- Apr 5, 2023
- 73
- 73
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mwendelezo mkuu tunasubiriTAALUMA ILIYO POTEA NDIYO KUMI KAKA
Mkuu kitambo SanaUMETAZAMA BILA SHAKA
sikujua kama kuna mashabiki. asanteni sanaHii story kaitelekeza kabisa yaaani hata hatujali mashabiki wake..[emoji3578][emoji3578]
Sent from my A004SH using JamiiForums mobile app
sijaitelekezaHii story kaitelekeza kabisa yaaani hata hatujali mashabiki wake..[emoji3578][emoji3578]
Sent from my A004SH using JamiiForums mobile app
Poa mkuu bado tunaimani na wewsikujua kama kuna mashabiki. asanteni sana
We waitsijaitelekeza
Mkuu kitambo SanaTAALUMA ILIYO POTEA NDIYO SEHEMU YA KUMI
Mkuu tuendeleeTo the end (mpaka mwisho) 15
Tariq Haji
0624065911
Baada ya saa tatu kupita.
Idadi ya wadahiliwa ikawa imefikia sitini na tatu, na mpaka wakati huwo si Baston wala Shanequeen aliesema lolote.
Ding dong!!
Sauti ya kengele ikasikika na mlango ukaanaa kujifunga, ni katika wakati huwo kivuli cha mtu kikapenya kwa kasi na kuburuzika ardhini.
"Wwooh! Nimewahi" alijisemea mtu huyo akiinuka na kujikumuta vumbi kisha akaelekea kwenye viti na kukaa. Baada ya sekunde chache mlango ukajifunga kabisa na hiyo ikawa ni ishara kuwa kwa siku hiyo hakuna mtu mwingine atakaeruhusiwa kujiunga.
"Karibuni sana" aliongea Baston akipiga kofi moja kali mno, lilisababisha mpaka baadhi kuziba masikio. Shanequeen alikuwa amesimama nyuma, wakati huwo alionekana kama mwanajeshi kakamavu.
"Jina langu ni Baston, nina uhakika mtakuwa mumelisikia kwa namna moja ama nyingine kabla ya kuja hapa. Mimi ndio kiongozi wa henga namba tano. Nyuma yangu ni naibu wangu Shanequeen, nae pia mtakuwa mnamfahamu" aliongea na sauti yake ilikuwa tulivu mno mpaka iliogopesha.
"Wote mko hapa si kwasababu ya uweledi wa vipaji vyenu au kwa ushawishi wenu. Kwangu mimi nyote mko sawa tu, haijalishi una daraja A katika uhusiano na itherium au daraja F. Kwa maneno mingine nyinyi wote ni wajinga wajinga tu msiokuwa na jambo lolote la kujitamba"
"Eti nini?" sauti za chini kwa chini zilisikika, wengi walionekana kukerwa na kauli hiyo kutoka kwa Baston.
"Kimya" alinguruma na ukumbi mzima ukazizima, hakuna hata sauti ya mdudu iliyosikika.
"Sheria ya kwanza na muhimu kwa jeshi ni ipi" aliongea Baston kwa sauti ya juu. Mmoja kati ya wadahiliwa akanyoosha mkono, Baston akatikisa kichwa na kumpa nafasi ya kujibu.
"Kutii amri bila shuruti" alijibu kwa kujiamini
"Vizuri sana, hilo ni jibu pendwa sana. Swali linalofuata ni kwamba ikitoka amri uingie kwenye shimo la moto, je?
Utaingia?"
Kimya kikatawala, hakuna aliekuwa na jibu la swali hilo. Wote waliangaliana wakitarajia labda angetokea mmoja wao akajibu.
"Katika henga namba sheria ya kwanza ya jeshi ni kuwa hai, haijalishi ni kwa namna gani. Kwa kuwa hai tu ndio kunampa sifa mwanajeshi. Waliokufa wanakumbukwa
katika siku maalum tu ila waliohai huangaliwa kwa macho
yaliyojaa faraja"
"Waliokufa hawalindi tena amani, sikatai kama walikuwa wakilinda amani. Lakini wakati walipoanguka thamani yao ikabaki kwenye vitabu na maneno tu. Leo hii hata nikiwauliza swali mnitajie kumi tu ambao mnawakumbuka
kwa kujitolea kwao basi mtashindwa. Na huwo ndio ukweli usiopingika"
"Wengi wamelaza maisha yao chini wakiamini ni jambo jema zaidi. Je wamefanya hivyo kwa ajili ya nani, nchi, familia au nani. Yote kwa yote, mwisho wa siku wamesahauliwa na kumezwa katika mzunguko wa wakati"
Maneno hayo kutoka kwa Baston yalikuwa kama kuwamwagia maji ya baridi, hata Shanequeen alihisi hasira ikimpanda lakini alifahamu fika kwamba maneno hayo yalikuwa ya kweli.
"Umewahi kujiuliza kwanini mwanajeshi wa daraja la chini kabisa imekuwa kazi kwake kupanda cheo. Wanaoweka roho zao rehani ni wengine na wanaopata medani za
kijeshi ni wingine waliokaa katika ofisi zao miguu juu. Iko wapi faraja ya yote haya, narudia tena iko wapi faida ya
yote haya. Na yote ni kwasababu ya kauli moja tu 'fuata
amri kama pofu, kiziwi au bubu' ni ujinga wa hali ya juu"
"Inatosha, huko ni kuwakosea heshima wazee wetu waliotangulia. Ni kuwafanya kujitolea kwao kusionekane na faida yeyote ile. Hayo ni matusi" mmoja kati wadahiliwa akasimama na kupaza sauti akipingana na kauli za Basto.
"Ndio nimesema sasa, kama huwezi kumezea mlango ule pale na kama unataka ndondi pia unakaribishwa. Ila ukitaka ndondi nakuahidi ukitaka ndondi nitakutwanga kweupe kweusi mpaka usahau jina lako. Mimi sitaki kulea watoto wasioweza kudhibiti hisia zao" alijibu, siku hii ya leo hata Shanequeen alijikuta akirudi nyuma.
Alieongea akaokota begi lake na kuelekea mlango, akafungua na kutoka. "Kama kuna mwingine anataka kuenda afanye hivyo" aliongea. Wengine watano wakainuka na kuondoka bila hata kuangalia nyuma.
"Tuendelee kama hakuna mwingine" aliongea na kutabasamu kisha akaendelea.
"Ushindi ni ushindi tu, haijalishi umepatikana kwa njia gani. Adui yako anaweza akakudhihaki kwa maneno makali na machafu, akakutia hasira na kukufanya upoteze uwezo wako wa kufikiri. Kanuni ya kwanza ya henga namba tano, mwanajeshi anatakiwa awe na akili iliyozungukwa na ukuta wa chuma ili asiruhusu dhihaka za wengine kumpanda kichwani"
"Kanuni ya pili ya henga namba tano, mwanajeshi anatakiwa awe na akili ya vita. Vita haichagui wakati, kuna wawakati itakukuta hujajiandaa na itabidi upambane"
"Na kanuni ya tatu ya henga namba tano, hakuna amri inayofuatwa kwa upofu. Sisi sio wanyama, inabidi tutumie
bongo zetu kabla ya kukurupuka, karibuni henga namba tano"
Hapo sasa wote wakagundua kwanini maneno yote yalisemwa mwanzo, haikuwa rahisi kwa wengi kujizuia. Wapo ambao machozi yaliwatoka lakini kwa namna moja ama nyingine waliamini kauli za Baston zilikuwa na mashiko.
"Okay, najua kila mmoja ana ndoto zake. Wengine wanataka kuwa marubani, wengine washauri wa vita na mambo mbali mbali. Yote hayo yatasubiri, kwa miezi sita nitakwenda kuwavunja vunja na kuwatengeneza kuwa na sura za kazi" akanyamaza na kuwaangalia.
"Niaminini ninaposema nitawavunja vunja kwasababu huwezi kutengeneza bila kuvunja. Hivyo kwa miezi sita henga namba tano haitashiriki katika jambo jingine lolote.
Katika kipindi hicho mtakuwa mnafanya mambo manne tu. Kula, kulala, kusali kila mtu kwa dini anayoamini na mazoezi"
"Wanaume nifuateni mimi, na wanawake mtafuata VSL (Vice squad leader) Shanequeen. Kesho saa kumi na moja alfajiri tutaanza mazoezi" alimaliza kuongea na kuwapa ishara wanaume wamfuate. Wakaelekea katika mabweni husika yalioandaliwa kwa ajili ya wanaume.
"Kuna vitanda vya kutosha humo, kila mtu achague kitanda anachotaka" aliongea na kuondoka. Alipotoweka tu kila mtu akashusha pumzi, wengine wakakaa kitako jasho likiwatoka.
"Nani aliesema huyu Baston sukuma toroli, hili jamaa ni zimwi"
"Mungu wangu wee, kwanini nimekuja huku"
"Ningejua ningebakia tu nyumbani nikaendelea kulima mpunga"
Kila mmoja alisema lilikouja kichwani mwake, mtikisiko walioupata haukuwa wa kawaida hata kidogo. Walijua jeshini ni sehemu ya mpela mpela lakini si kwa kiwango hichi.
Baston alipotoka huko akaelekea zake jikoni kwa ajili ya kuandaa chakula. Chakula cha watu zaidi ya hamsini haikuwa kazi ndogo, ilihitaji misuli ya maana kucheza na upawa na nyungu.
Wakati huwo huwo Shanequeen alikuwa akitoka mabweni ya waschana alipomuona Baston akielekea jikoni nae akafuata nyuma.
"Leo umetumia kauli kali sana, kwanini?" aliuliza alipoingia jikoni.
"Kuna wakati ni kheri kuwachapa ukweli usoni mwao kuliko kuwapetipeti, kwa njia hiyo watajua thamani yao na kwa familia kabla ya kuamini kwa upofu na kutupa roho" Ka!!! Mkono wa sufuria kubwa ukapinda.
Mkuu unajua....umenikumbusha nami enzi hizo nimeingia jkt daah afu kambi yenyewe BULOMBORA hahaha ilikuwa ni mauajiTo the end (mpaka mwisho) 16
"Mi natoka kidogo" aliongea Baston na kuondoka akimuacha Shanequeen asijue la kufanya. Alipofika nje akamuandikia Malik ujumbe wa kumtafutia watu ambao watahusika na usafi pamoja ma'akuli. Akaandika na vigezo kisha akautuma ujumbe huwo, akaingia kwenye yake na kuondoka.
Alirudi jioni sana, akiwa amefuatana na gari jingine kubwa la chakula, akatoa amri watu wote wakusanyike kisha wakapata chakula kwa pamoja. Baada ya pirika za chakula kila mmoja akaelekea kufanya jambo lake wakikubaliana wakutane saa kumi na moja alfajiri.
"Twende nikurudishe nyumbani" aliongea Baston kumwambia Shanequeen.
"Hapana leo nitalala hapa hapa,nina kila kitu ninachohitaji kesho" alijibu.
"Anha, sawa. Mimi pia nitakuwepo hapa hapa" aliongea. Baada ya hapo Baston akaelekea chumbani kwake. Ilikuwa ni desturi ya jeshi kuwa kila kiongozi alokuwa na chumba chake. Hakuchanganyika na wengine katika hilo. Akabadili nguo na kuvaa nguo za mazoezi kisha akaelekea gym.
Aliwakuta baadhi ya watu wakiendelea na mazoezi, aliwapa ishara waendelee na yeye akaelekea kwenye mashine ya kukimbiliana na kuanza kupasha. Pasha yake ilikuwa tofauti kidogo na wengine alikimbia kwa kasi kubwa kiasi kwa saa nzima bila kupumzika. Baada saa hilo kukatika ndio akaanza kutoka jasho.
Usiku huwo mazoezi yake yalikuwa ya kawaida sana, hakutaka kuwatisha watu wengine. Baada saa tatu ndio akawa amekamilisha mazoezi ya usiku huwo, na yeye ndie aliekuwa mtu wa mwisho kutoka gym. Akaelekea chumbani kwake na kuoga kisha akapanda kitandani kwa ajili ya kupitisha usiku.
Saa kumi na nusu Alfajiri.
Taa za mabweni yote mawili zikawaka zikifuatiwa na king'ora, kililia kwa sauti kali sana. Kuruta wote wakashuka vitandani na kusimama mbele ya vitanda vyao. Bweni la wanaume mlango ukafunguliwa, akaingia Baston ambae tayari alishakuwa katika vazi rasmi la mazoezi.
Mguu sawa!!
Akanguruma Baston, kuruta wote wakafunga miguu na kutoa saluti ya jeshi. Baston akatikisa kichwa na kutabasamu kuonesha kuridhika.
"Mna nusuu saa ya maandalizi, kumi na moja kamili muwe uwanjani. Kuchelewa hakutovumiliwa" aliongea na kugeuka kisha akaondoka. Na upande wa waschana ulikuwa hivyo hivyo.
Kumi na moja kamili, Baston alikuwa amesimama mbele ya umati mkubwa wa watu waliovalia nguo za mazoezi. Pembeni alikuwa Shanequeen ambae nae alikuwa karika vazi lake la mazoezi. Isipokuwa lake lilikuwa tofauti kidogo na wengine wote.
"Leo mtaanza na kukimbia kilometa tano, hiyo ndio kiwango cha chini. Baada kilometa tatu kukamilika kila mmoja wenu atavaa hizi bangili, zipo kuanzia kilo moja mpaka nne ila bi vyema mkaanzia chini" aliongea na kufafanua.
"Kabla hamjaanza nitawafundisha nyimbo ya kuimba"
'Sisi ndubwi, watoto wa vyura'
'Tunazaliwa majini, tuna vichwa bila miguu'
'Tunalia lia bila mpango kwasababu hatuna uwezo wowote, tupo tupp tu sisi watoto wa vyura'
Baada ya kuwafundisha nyimbo hiyo wakaanza mazoezi, akabakia Baston na Shanequeen.
"Ngapi leo?" aliuliza Shanequeen
"Utakazokwenda wewe nitakwenda mara mbili kwa muda huwo huwo"
"Mimi leo naenda kilometa kumi kwa dakika arobainii"
"Mi ntakwenda ishirini"
"Uzito ninaovaa ni kilo nne kila mguu"
"Nitavaa nane kila mguu"
Wakafanya maandalizi, wote wawili wakaangalia saa zao na kuweka muda wanaotaka. Wakaanza kukimbia, na baada sekunde chache Baston akaongeza kasi na kumuacha Shanequeen. Yeye alitakiwa kukimbia kilometa mbili kwa moja ya Shanequeen. Uwanja waliokuwa wanautumia ulikuwa na urefu wa mita elfu moja (kilometa moja) .
Baada dakika arobaini na tano, Baston na Shanequeen wakawa washamaliza. Baston akawatupia macho wengine na kuwaona wanavyotaabika. Tabasamu jembamba likajichora usoni mwake na kumfanya Shanequeen amshangae.
"Kwanini umewapa umbali mrefu siku ya kwanza" aliukiza akipepesa macho yake makubwa ya mviringo.
"Utaona baada ya miezi kadhaa" alijibu kwa mkato na kuanza kunyoosha viungo.
Funga fungua miezi mitatu ikawa imekatika kama upepo wa mvua, kati ya watu sitini waliojiunga walikuwa wamebakia arobaini na tisa. Kumi na moja waliamua kujitoa kwa hiari zao.
Siku hii watu arobaini na tisa walikuwa wamesimama katika mistari ikiyonyooka. Miili yao ambayo mwanzo ilikuwa rojo rojo ilikiwa imeanza kukaza kasoro wachache.
"Hongereni kwa kumaliza miezi mitatu ya mwanzo, najua wengiwenu mtakuwa mnanichukia kwa namna moja ama nyingine, ila niwaambie tu ukweli mimi sijali. Kuanzia leo nitawagawa katika makundi kadhaa, makundi hayo ndio yatakuwa vitengo vyenu husika. Nitawagawa kutokana na kile mlichokionesha katika miezi hii mitatu. Kundi la kwanza litakuwa ni la kombat, la pili litakuwa ni la taaluma ya vita, la tatu litkuwa la intelijensia na la nne litakuwa ni la watu wa afya"
"Kundi la kombat ndio litakuwa kundi ambalo linaingia vitani kupambana na ndio litkuwa kundi kubwa na ndio kundi kuu. Kundi. Kundi la taaluma ya vita litakuwa ubongo wa kikosi chetu, kazi yake itakuwa ni kusoma vita, kudadavua, kupanga na kufanya maamuzi. Kundi la intelijensia ndio litakuwa macho na masikio yetu. Kazi ya kundi hili itakuwa ni ukusanyaji wa taarifa na kuzidavua kama ni za kweli ama laa. Kundi litafanya kazi ndani ya nchi yetu na pia ndani ya nchi nyingine. Kundi la mwisho litakuwa ni la watu wa afya, hawa watahusika na ulindaji na kuhakikisha afya za watu wote katika kikosi chetu zinakuwa vyema wakati wote".
Akanyamaza kidogo na kuwaangalia, akawaacha kama dakika tano ili kuwapa nafasi ya kumumunya kile alichosema. Kisha akaendelea.
"Nitataja majina ya kila watu ambao watakuwa katika kundi fulani. Majina matatu ya mwanzo ndio watakuwa viongozi wa makundi hayo".
"Kundi la taaluma ya vita; Kelly Adams, Miryam Jesus na Batista Thomas na akawataja waliobakia kisha akawapa amri wasogee pembeni. Kundi la intelijensia; Mareck Hans, Nissen khan na Festina Justine kisha akawataja waliobakia na kuwaambia wajitenge. Kundi la watu wa afya; Marry Mars, Sasna Kunal na Fatemah Ayyub na wenzao kisha akawaambia wajitenge".
"Kundi la Kombat nitakuwa mimi Baston, Shanequeen na mmoja ambae atashinda katika mashindano maalum atapata nafasi ya kuwa kiongozi wa tatu"
Kundi la kombat lilikuwa na jumla ya watu kumi na tano, la taaluma ya vita lilikuwa na watu kumi, la intelijensia lilikuwa na watu kumi na nane na ndio lilikuwa kundi kubwa zaidi na la watu wa afya lilikuwa na watu sita tu.
"Kwa yule ambae atakuwa hajaridhika na mpangilio huu, anaruhusiwa kukata rufaa. Na kuanzia kesho kila kikundi kitafanya mazoezi yake kwa wale ambao wapo na mimi salini na semezeni na Mungu unaemuamini. Mungu awasaidie, hehehe" aliongea Bastona kucheka. Kwa sekunde chache alionekana kama izraeli mtoa roho hata Shanequeen alihisi baridi ikidarizi uti wake wa mgongo. Wengine wakameza mafunda makubwa ya mate na kuwaangali watu kumi na tano ambao walikuwa katika kundi la Baston na kutikisa vuchwa, walisikitika.
Shusha pindi mkuuTo the end (mpaka mwisho) 18
Malik akatikisa kichwa akimuangalia Baston, "huyu mshkaji hajui chochote kuhusu hisia za wanawake" alijisemea moyoni mwake. Baada ya maneno hayo kutoka kinywani mwa Baston, uso wote wa Shanequeen ukawa mwekundu. Akainuka na kuondoka bila kusema jambo, Baston akashangaa sana kwasababu hakuona kama amefanya jambo lolote baya.
"Kwani mwili unajengwa na matofali? Si na chakula" alijisemea mwenyewe na kunywa kinywaji kilichokuwa katika gilasi kisha akainuka na kumfata Shanequeen. Japo mwanzo hakutaka kufanya hivyo lakini alihisi moyoni kukosa utulivu.
Nje ya mgahawa huwo wa kitajiri alikuwa amefura kwa hasira, mara kadhaa alipiga miguu yake chini kwa nguvu. Wakati huwo watu zaidi ya kumi wakamzunguka.
"Edward tafadhali niache" alifoka
"Hahaha, nilishakwambia wewe ni wangu na leo lazima nikuchukue nikakufaidi" aliongea Edward akiramba midomi yake.
"Siku zote kuna watu ambao hawayathamini maisha yao, hata akipewa nafasi mia moja za kujirekebisha. Hatofanya mpaka aone anafika katika mlango wa kifo" sauti nzito ilitoka upande wa mlango wa kuingilia mgahawani.
"Baston, Baston, Baston inaonekana vile vipigo vya mwanzo hakutosha" aliongea Edward akimuangalia Baston kwa macho yaliyojaa kebehi. Ni kweli mara kadhaa Edward kila alipokutana na Baston kipindi cha nyuma aliamuru vibaraka wake wampige.
"Edward, hii ni mara ya mwisho. Ondoka" aliongea Baston safari hii ni kama alikuwa mtu mwingine kabisa.
"Hahaha, unanitishia. Una uwezo wa kunifanya niondoke hapa"
"Tatizo sio uwezo wa kukufanya uondoke, ila kwa namna yeyote ile hapa utaondoka na gari ya wagonjwa" aliongea Baston.
"Mpigeni huyo mbwa, msimuue mvunjeni tu miguu na mikono" aliongea akimvuta Shanequeen, japo Edward alikuwa mpuuzi mpuuzi lakini kiuhalisia alikuwa na nguvu kuliko binti huyo. Vibaraka kadhaa baada ya kupokea amri hiyo wakamzunguka Baston.
"Mimi sina shida na nyinyi, msinunue ugomvi"
"Hahaha mlemavu anatutishia maisha"
"Nimesikia huyu jamaa anapigisha watu mazoezi kama punda, eti anataka kuwafanya wawe na nguvu kuliko wale wenye uwezo wa juu wa kunyonya itherium"
"Hahaha hizo ni ndoto abunuasi na juha", Baston akabaki anawatizama tu huku tabasamu jembamba likijichora usoni mwake. Hawakujua dakika chache mbele ni kingewakuta, hawakujua kwanini Baston hakupigana hata alipoonewa kipindi cha nyuma na siyo kwamba hakuwa na uwezo wa kufanya hivyo. Bali aliamua kuishi maisha ya hivyi ili kuepusha macho ya wenye wivu kumshukia.
Tokea alivyokuwa mdogo baada ya kugundua kuwa mwili wake haukuwa na uwezo wa kuhifadhi utherium aliamua kubadilisha njia ya maisha yake na kuanza kufanya mazoezi ya kuujenga mwili huwo.
Dakika chache baadae Edward akiwa anamvuta Shanequeen akatahamaki ameshikwa bega. Akageuka kwa hasira ili kuangalia ni nani aliethubutu kumshika. Macho yake yakatua usoni kwa Baston, uso huwo ulikuwa na michirizi kadhaa ya damu lakini haikuwa ya kwake. Macho yakatua nyuma walipokuwa vibaraka wake, akakutana na hali ambayo hakuitegemea kabisa.
Vibaraka wake wote walikuwa wamelala chini bila fahamu. Macho yake yakarudi usoni kwa Baston. Alikuwa amepigwa na mshangao mzito, akili yake ilikuwa ikizunguka kwa kasi jinsi ya kutoka kwenye msala huo.
Pah!!
Kumi nzito ikatua kichwani na kumbamiza ardhini, papo hapo akapoteza fahamu. Hakujuwa hata nini kimetokea, ulimwengu wake ulikuwa kiza.
Snif!! Snif!!
Shanequeen akajitupa mikononi mwa Baston huku akilia, Baston alijitahidi kumnyamazisha lakini wapi. Ni kama vile bwawa lilipasuka ukuta, machozi yaliendelea kutiririka mashavuni mwa mschana huyo bila kizuizi.
"Baston kumetokea nini" Malik alifika na kuongea.
"Kuna nyumbu wachache walitaka kunishika kidevu" alijibu Baston.
"Ni wale waliolala kule bila fahamu"
"Ndio, Malik acha nimrudishe Shanequeen nyumbani kwao. Amepitia mengi leo" aliongea Baston. Malik akatikisa kichwa na kuelekea alipo Mayna. Baston nae akaelekea ilipo gari yake na kumsaidia Shanequeen kisha akaingia upande wa dereva na kuondoka eneo hilo.
"Sitaki kwenda nyumbani nikiwa katika hali hii" aliongea Shanequeen baada ya kunyamaza. Baston hakujibu kitu, alijua fika binti huyo alikuwa katika wakati mgumu sana. Akaelekea moja kwa moja nyumbani kwake.
**********
"Kaa hapo, subiri nikakuandalie chai" aliongea Baston na kuelekea jikoni. Baada robo saa akarudi lakini akamkuta Shanequeen tayari kashalala. Akasimama kwa muda akitafakari, na baada kufanya maamuzi akambeba na kumpeleka katika moja kati vyumba vilivyokuwepo ghorofa ya kwanza. Akamlaza kitandani na kumfunika shuka, ila alipotaka kuondoka akamuangalia usoni.
"So beautiful" alijisemea moyoni mwake.
"Inakuwaje mtu anakuwa mrembo kiasi hichi", kwa dakika nzima alikuwa amepotea katika mawazo kedekede. Alipozinduka akatoka chumbani humo na kueleke ghorofa ya pili ambako ndipp kilipokuwa chumba chake. Akaingia bafuni kwa ajili ya usafi, alipotoka alivaa bukta nyepesi na kujibwaga kitandani. Haikupita muda mrefu usingizi ukamchukuwa.
Muda mchache baada ya Baston kuchukuliwa na usingizi, mvua nyepesi ikaanza kudondoka. Mlango wake wa chumbani ukafungulia. Akaingia mtu kisha ukafungwa, moja kwa moja mtu huyo akaelekea mpaka kwenye kabati kubwa na kufungua upande mmoja. Akatoa vitu kadhaa na kuelekea bafuni kuoga.
Harufu nzuri ya sabuni ndio iliosambaa chumbani humo muda mfupi baada ya mtu kuanza kuoga. Baada ya robo saa, akatoka chooni akiwa amevaa nguo nyepesi ya kulalia na kupanda kitandani. Mtu huyo hakuwa mwingine isipokuwa Shanequeen ambae alishtuka muda mchache uliyopita.
Jambo ambalo hakulifahamu Baston ni kwamba nyumba hiyo aliokuwa anakaa yeye mwanzo ilikuwa ni ya bibie huyo. Pua za Baston zikavuta harufu nzuri kama ya manukato, akageuka na mkono wake ukazunguka kiunoni mwa mschana huyo.
Shanequeen akashtuka kidogo na kugundua kuwa tayari siku hiyo alishafanya kosa. Mazoea yake ndio yalimfanya aelekee chumbani kwa Baston akidhani bado ni nyumba yake. Hata hivyo hakufanya jambo lolote, mapigo yake ya moyo yalianza kwenda kasi.
Harufu nzuri iliyotoka kwenye nyingi za mschana huyo ilimfanya Baston azidi kujisogeza karibu na miili yao ikawa tayari imegusana. Hali ya umotomoto ambao haukuwa wa kawaida ikamzindua Baston kutoka usingizini.
Macho yake yakatua katika nywele za Shanequeen, na bila mategemeo akaoandisha mkono wake juu. Viganjani mwake akahisi amekamata kitu kama puto.
Anh!!
Shanequeen akatoa sauti ambayo ilimfanya rijali huyo ashki za kiume kupanda. Nae mapigo yake ya moyo yakaanza kwenda kasi. Damu yake ambayo mwanzo ilikuwa ikizunguka kwa kasi ndogo ikaanza kuznguka kwa kasi kubwa.
"Bas... " Shanequeen aliita
"Shhh" alikatizwa, akatahamaki amevutwa na macho yake yakakutana na ya Baston. Lugha isiyotamkwa kwa mdomo bali na moyo ndio iliyofuata. Midomo yao ikakutana, na hisia zao zikajidhirisha moja kwa moja. Wakati hakuna aliejali la hiki wala kile, waliacha hisia zao kufufuata mkondo na asili kuchukuwa njia yake.
Aaanhh, Sss!!
Alilamika Shanequeen na kung'ata midomo yake baada ya kuhisi utepe uliofunga asali kuchanika na kusababisha maumivu ambayo yalichanganyika na raha.
Mkuu unajua....umenikumbusha nami enzi hizo nimeingia jkt daah afu kambi yenyewe BULOMBORA hahaha ilikuwa ni 😆😆😆😆😆😆