RIWAYA: Wivu-Beka Mfaume

Casuist

JF-Expert Member
Joined
Jul 23, 2014
Posts
1,189
Reaction score
2,970
Habari wanajukwaa, kuna softcopy kadhaa nnazo za hadithi tofauti nkaona si vibaya ku-share ikizingatia watunzi wake wameziweka public hivyo kutohesabika kama wizi wa kazi za watu au kuharibu mapato.. Kila siku nitaweka sehemu moja, watakuwepo ambao wameshazisoma lakini pia kutakua na wengi ambao hawajahi kuzisoma,



 


mtunzi: Beka mfaume.

Sehemu ya pili


 
Mtunzi: Beka mfaume.

Sehemu ya tatu
 
MTUNZI:BEKA MFAUME

SEHEMU YA NNE

 
mtunzi: Beka mfaume

sehemu ya tano

 
MTUNZI: BEKA MFAUME

SEHEMU YA SITA





***DINA ameanza kazi rasmi, John SAILASkwa roho upande anakubaliana na hali huku akiamini kuwa DINA amewekwapale kama chambo.
LAITI kama John angekuwa na pesa huendaangemzuia DINA asifanye kazi lakini JOHN ni maskini.
***JE?Richard atafanikiwa kumrejesha DINA katika himaya yake????
 
[FONT=Helvetica, Arial, lucida grande, tahoma, verdana, arial, sans-serif][/FONT]MTUNZI:BEKA MFAUME

SEHEMU YA NANE
[FONT=Helvetica, Arial, lucida grande, tahoma, verdana, arial, sans-serif]
[/FONT]
[FONT=Helvetica, Arial, lucida grande, tahoma, verdana, arial, sans-serif]
"Nimekupa uisome ili ujuehaitawezekana kufunga ndoa, hadi miezi mitatu ipite! Hukuyaonamasharti niliyoandikiwa? Si umeona siruhusiwi kuchukua ruhusa zaidiya siku moja? Ndoa inahitaji uwe huru, ikibidi uwe na ruhusa yazaidi ya wiki moja, wengine huchukua hadi likizo. Kwa hiyo tareheuliyoitaja haitowezekana. Itabidi tusubiri hadi baada ya miezi mitatundio tufunge ndoa!"

Kauli hiyo ikamnyong'onyesha John,ikamchanganya kwa muda huku akiuona mpango wake ukielekeakushindwa.

Hakukubali!

"Tunaweza tukaoana bilasherehe!" John alisema kama aliyekurupuka huku akionekana kukosaumakini.

"Usinichekeshe John! Tuoane bila ya sherehe kisanini?" Dina aliuliza katika hali inayomshushua John.

Johnakaanza kuueleza uwongo wake, Dina akausikiliza mwanzo hadimwisho.

"Muda wa wewe kwenda kusoma na muda niliopewa kazinihautatofautiana sana," Dina alisema kwa utulivu baada yakumsikiliza John.
"Mimi nitakuwa tayari kukusubiri hadi urudi!Kwani kuna haraka gani mpaka tufunge ndoa kwenye mazingira kama hayoyasiyo na sherehe? Nitasubiri hadi utakaporudi ili tuweze kufanyakitu cha uhakika. Hata hivyo, unadhani upande wetu utalikubali wazolako? Eti tuoane kwanza halafu sherehe baadaye? Najua nao watakujibukama hivi ninavyojibu. Mimi nakuomba usisumbuke kuwapa ushauri huoupande wa kwetu. Nakushauri kitu kimoja," Dina akanyamaza nakumwangalia John aliyekuwa amesimama kama aliyeumbuliwa hukuakionekana kukosa hoja.
"Fanya hiyo mahari iletwe kamaulivyopanga. Itakuwa vizuri ukiilipa kabla hujaondoka nchini iliuonekane kweli una dhamira ya kunioa!"

Pigano la kwanzadhidi ya Richard, John akakiri amekwishalipoteza!

***

RICHARDakiwa amekiegesha kidevu juu ya vidole alivyovifumbata pamoja hukumikono yake ikiwa imeegemea juu ya meza ya ofisini kwake, alikuwaametulia katika hali hiyo kwa muda mrefu na kuonekana kutekwa mawazona kitu alichokuwa akikifikiri. Ilikuwa kama fumbo mfumbie mjinga!Alikuwa akikifikiria kitendo cha kuajiriwa Dina hapo ofisinikilivyokuwa kimemshitua, kilimshitua kutokana na kitendo hichokufanyika siku chache baada ya kutoka kuzungumza na baba yake kuhusumsichana huyo huyo ambaye alikiri anampenda na yupo tayarikumuoa.

Kuajiriwa kwa Dina katika mazingira aliyoyachukuliakuwa ni ya kumshitukizia ambayo yalifanyika kimya kimya kishaakakabidhiwa awe chini ya uongozi wake, Richard aliwaza jinsi babayake alivyokuwa hakufanya tena rejea ya mazungumzo yaliyomhusumsichana huyo tokea pale mara ya mwisho walivyolizungumzia suala lakena matokeo yake ni kumleta hapo akiwa amekwisha ajiriwa.

Richardalidhani kuajiriwa kwa Dina hapo ofisini kungekuwa ni sababu tosha yakumfanya baba yake alirejeshe tena suala la msichana huyo kwenyemjadala wao uliokuwa haujamalizika kuhusu kumuoa, lakini alishangaakumwona baba yake hakufanya hivyo! Ukimya huo wa baba yakeulimshangaza, lakini pia, alishangaa na kujiuliza kwa nini baba yakehakutaka kumshauri au kumdokeza kama alikuwa na mipango ya kumwajiriDina?

Awali katika siku za mwanzoni, ajira hiyo ya Dinailimsumbua kichwa kutokana na kumchukulia Dina kuwa ni adui yakebaada ya kumkataa na kisha kukubali kuposwa na John. Tukio hilo laDina kuajiriwa na kisha kuletwa kwenye idara yake kufanya kazi; tenabila ya barua ya ujulisho, lilimfanya apigwe na butwaa na kutomwelewababa yake kwa uamuzi huo. Akawa anajiuliza mara kwa mara, ni ninikilichomfanya baba yake amwajiri msichana huyo wakatialikwishamfahamisha kuwa, alikataa kuolewa naye?

Lakini wingula uteguzi wa kitendawili hicho kilichokuwa kimemuweka kwa sikukadhaa kwenye sintofahamu iliyokuwepo kati yake na baba yake kuhusuajira hiyo ya Dina, Richard alianza kukitegua kitendawili hicho baadaya baba yake kumwandikia barua ya kiofisi zikiwa zimepita takribanisiku tano tokea Dina kuajiriwa. Aliikumbuka barua hiyo iliyomjulishakuwa, Dina atakuwa chini ya uongozi wake na ikamjulisha kiwango chamshahara ambacho angelipwa.

Kiwango cha mshahara ndichokilichokuwa chachu ya kumzindua akili! Mara ya kwanza alipokuwaakikisoma kiwango hicho alijikuta akiamini kuna makosa ya kisarufiyaliyofanyika kwenye barua hiyo, lakini baada ya kuona kiwango hichokilikuwa kimeenda sambamba kwa kurudiwa kimaandishi, akawa amepigwana butwaa baada ya kuona hakukuwa na maantiki yoyote iliyostahilishaDina alipwe mshahara mkubwa kama huo wakati hana ujuzi wowote wakazi!

Richard alikumbuka jinsi alivyoingiwa na ushawishi wakwenda kumkabili baba yake mara baada ya kuletewa barua hiyo iliamwulize ni kwa nini alimwajiri Dina bila ya kushauriana na yeye haliakijua kuwa yeye na Dina hawaelewani? Isitoshe, pia alikusudiakumwuliza ni kwa nini ameamua kumlipa mshahara mkubwa kama huo wakatiwapo wafanyakazi walioajiriwa wakiwa na ujuzi wao ambao hawapatimshahara kama huo? Akakumbuka kabla ya kuuchukua uamuzi huo wakumkabili baba yake, alijiwa na wazo lililomfanya asite kuuchukuauamuzi huo baada ya kujiuliza kuwa, huenda kuna sababuiliyomlazimisha baba yake kumwajiri Dina na kuamua kumlipa mshaharawa aina hiyo. Wazo hilo ndilo lililompa nafasi ya kuufikiria uamuzihuo wa baba yake na kabla hajaenda mbali kifikra ndipo alipowezakukitegua kitendawili hicho alichotegwa na baba yake!

Chachuya kukitegua kitendawili hicho ilimjia Richard baada ya kuuwaziamshahara ambao angepewa Dina na kuyawekea mashaka maamuzi hayo.Akahisi lazima kungekuwa na sababu nyuma ya maamuzi hayoyaliyolazimisha Dina aanze kazi na mshahara kama huo. Ndipoalipogundua kuwa kiwango hicho cha mshahara kilikuwa ni aina yachambo kilichovikwa kwenye ndoana alichotegeshewa Dina ilikumlainisha na aione familia ya mzee Ken ipo karibu naye. Ulikuwamtego! Richard aliwaza. Mtego ambao ulikusudiwa kwa Dina ili aulegezemsimamo wake wa kukataa kuolewa na familia hiyo! Richard alitabasamupeke yake baada ya kugundua kuwa, Dina amechezwa shere kwakutengenezewa wigo asioweza kuutoka; wigo utakaomfanya amkubali iliasiupoteze mshahara huo!

Richard akakiri kwa mtaji huo,isingekuwa ajabu kumwona Dina akiurudisha uhusiano uliokuwa umetowekakati yao!

Ghafla akamkumbuka John! Akakumbuka kuwa, Dina yupokaribu kuolewa na John! Badala ya wazo hilo kumwingiza kwenye unyongekama ilivyokuwa awali kila alipokuwa akikumbuka jambo hilo, safarihii Richard alijikuta akiliwazia jambo hilo kwa mtazamo tofauti.Kilichomfanya awe na mtazamo huo tofauti ni kule kuajiriwa kwa Dinahapo ofisini. Aliamini kuletwa kwa Dina na kuwekwa karibu yakekungemwezesha kuua Tembo kwa ubua. Richard alitengeneza tabasamu laushari baada ya kujiona safari hii ana nafasi kubwa ya kumpata Dinahata kama ataolewa na John! Aliamini bado angekuwa na nafasi yakumchukua na kutembea naye kwa siri akiwa ameolewa!

Wazo hilola kuja kutembea na Dina akiwa ameolewa na John lilimfariji mno nakujisikia burudiko kwenye moyo wake. Aliuona huo ndio ungekuwa wakatimwafaka wa kulipiza kisasi kwa John! Na kwake ingekuwa ni furahailioje kama angefanikiwa kukifanya kitendo hicho katika mazingirahayo Dina akiwa ameolewa! Kitendo hicho kingemfurahisha zaidi moyowake kwani angejiona angekuwa analipiza kisasi katika njiainayostahili, na ingekuwa ni nafasi yake ya kumdhihirishia John kuwaalifanya makosa kumpora Dina akiwa mikononi mwake! Alitaka liwefundisho kwa John ili mara nyingine asivamie maeneo yanayomilikiwa nawatu wenye pesa kama yeye!

Kisasi chake alitaka kisiishie kwakumchukulia John mke wake halafu iwe basi; lakini pia, alitaka Johnaje atambue kuwa yeye anatembea na mke wake! Na sio tu John ajue kuwamkewe anatembea na yeye, lakini pia, aliapa kuitumia nafasi hiyokuhakikisha anamdhibiti Dina kimapenzi hadi awe chizi kwa ajili yakena John alifahamu hilo! Alipenda amwone John akitesekea penzi kamaalivyoteseka yeye wakati alipokuwa akimbembeleza Dina warudiane.Alitaka kusiwepo maelewano kati ya John na Dina kwenye ndoa yao.Alipania kuisambaratisha ndoa hiyo, alitaka amshuhudie Johnakihangaika kwenda kuomba msaada kwa Padri ili kuiokoa ndoa yake bilaya mafanikio! Alitaka Kanisa lifikie mahali likubali kuvunjwa kwandoa hiyo, kisha yeye ndiye aje kumuoa Dina!

Lakini wakatiakiifikiria mikakati hiyo ya kumsulubisha John na kumrudisha Dinakwenye himaya yake ya mapenzi, Richard alikiri bado kulikuwa natatizo mbele yake ambalo alikiri kuwa ni kubwa na linalohitaji ainanyingine ya maamuzi! Tatizo hilo aliliangalia kama vile Mwanasayansianavyokiangalia kirusi cha hatari kinachotaka kujipenyeza kwenyemfumo mzima wa mawasiliano ya chombo muhimu.
AlikuwaMohsein!

Alimwona Mohsein kama mtu aliyekuwa akihatarishaharakati zake ziingie kwenye ugumu usio wa lazima. Na tatizo halikuwakwa Mohsein mwenyewe, bali lilikuwa ni Dina! Aligundua Dina alikuwaakimpenda Mohsein. Kulikuwa na dalili za wazi zilizokuwa zikionyeshwana Dina kuwa amekwisha kimahaba kwa Mohsein na akalikumbuka tukio lakuwafumania wakiwa wamevigusisha pamoja vichwa vyao kwa aina fulaniya mahaba wakati alipokuwa amewaingilia ghafla ofisini.

Tukiohilo lilikuwa likimtafuna Richard, wivu na chuki ya kumchukia Mohseinikawa imejijenga, na hakutaka kujidanganya; kwa sababu dalili zotezilikuwa ziko wazi zikionyesha kuwa, kama kuna mtu anayeweza kumpataDina kirahisi bila ya kujali kikwazo cha uchumba uliopo kwa John basiMohsein ndiye mwenye nafasi hiyo! Richard akajionya endapo hatochukuahatua za haraka, uwezekano wa Mohsein kumchukua Dina mbele ya machoyake usingezuilika!

Richard alikiri hilo ni tatizo na akalionani kubwa na la hatari! Asingekubali litokee huku akiliona! Afanyenini? alijiuliza. Amfanyie fitna Mohsein afukuzwe kazi? Aliiona hiyondio njia pekee itakayomuweka kwenye amani, lakini pia, aliogopakitendo hicho kingeweza kigandulika na Mohsein kuwa, amefukuzwa kazikwa ajili ya kuonewa wivu dhidi ya Dina! Hilo lingeweza kumchocheaMohsein kufanya juhudi za ziada kuhakikisha anatembea na Dina kamasehemu ya kulipiza kisasi! Richard alipolifikiria hilo, mchomo wawivu ukapenya moyoni mwake! Akajionya kuwa, maamuzi yoyote yakumfukuza kazi Mohsein yangeleta janga badala yasuluhisho.

Akajaribu kujituliza na kufikiri kwa kutumia uwezowa akili badala ya akili za nguvu. Akajiuliza, ni njia ipi yakuitumia ili Mohsein aachane na fikra za kumtaka Dina kimapenzi? Njiapekee aliyoiona kuwa inaweza ikamsaidia, ni kufanya kila njia iliMohsein ajue kuwa, yeye ndiye aliyemwajiri Dina na Dina yuko hapo kwaajili yake. Alikuwa na uhakika endapo Mohsein atalifahamu hilo, basiangeogopa kujihusisha kimapenzi na Dina kwani angeelewa, Dina ni maliza bosi wake!

Kwa kuwa alikuwa na safari ya kikazi ya kwendaMorogoro, Richard akapanga mara atakaporudi kutoka Morogoro ndipoangeyaonyesha makucha yake kuwa yeye ndiye bosi na mmoja wa wamilikiwa kampuni hiyo. Akaamini, mwelekeo wa uelewa huo ungemtishaMohsein!

Laiti angelijua kosa analolifanya, kamwe Richardasingeenda safari hiyo ya Morogoro!



* * * **

Ilikuwa siku ya pili tokea Richard alivyokuwaamekwenda Mkoa wa Morogoro kwa ajili ya kufanya ukaguzi wa ndani wamahesabu kwenye kituo chao cha mafuta ambacho ni kikubwa kulikovingine vyote mkoani humo. Mohsein akawa amekaimu nafasi yakekiofisi.

Ilikuwa ni kawaida kwa kila inapokuwa Richard hayupoofisini kikazi, Mohsein ndiye anayekaimu madaraka yake, labda itokeewote wasafiri safari moja ya kikazi. Siku ambayo Richard aliondokakwenda Morogoro aliacha maagizo kwa Mohsein kuwa, kukahesabiwe vifaaalivyokuwa ameviorodhesha kwenye nyaraka aliyomkabidhi Mohsein ilivikahesabiwe upya baada ya kutokea utata wa orodha kamili ya mahesabukuhusu vifaa hivyo vilivyokuwa vimehifadhiwa stoo na alitaka shughulihiyo ifanyike siku hiyo hiyo aliyokuwa akisafiri ili akirudi akutemajibu.

Lakini baada ya Richard kuondoka, Mohsein akazembeakuianza kazi siku hiyo kama alivyokuwa ameagizwa, akasubiri hadi sikuya pili asubuhi ndipo alipoikabidhi kazi hiyo kwa kumpa Dinaakaifanye badala ya kuifanya yeye.

Ilikuwa ni kazi ya sikumoja, lakini Dina akaingia nayo siku ya pili akiwa badohajaimaliza!

Ikiwa ndani ya siku ya pili kazi hiyohaijamalizwa, na ikiwa ni siku ya tatu tokea Richard alivyoondokakwenda Morogoro, ilipofika saa tano asubuhi, Mohsein akaanza kuingiwana mashaka kuwa, huenda Richard angerudi siku hiyo na kuikuta kaziikiwa haijamalizika. Kwa kumhofia Richard asije akaja kumbwatukiaatakapoikuta kazi hiyo haijamalizika na wakati jukumu hilo alipewayeye, Mohsein aliamua kumfuatilia Dina ili ajue amefikia wapi naendapo ikibidi amsaidie.

Alimfuata Dina aliyekuwa peke yakekwenye hiyo stoo ambayo haikuwa kubwa ya kutosha na iliyozungukwa namakabati ya chuma yaliyokuwa wazi ambayo yalibeba vifaa mbalimbalivya kampuni, akamkuta yupo katikati ya kuhesabu.

"Badohujamaliza?" Mohsein alimwuliza Dina.

"Ungenikutanimekwishamaliza," Dina alijitetea.
"Lakini kulikuwa nabaadhi ya maboksi ilibidi niyapangue kwanza kisha ndio nikaendeleakuhesabu."
"Kwani bado sana?"

"Kama utanisaidia,tutamaliza mapema."
"Umebakiza upande upi?"

Dinaakamwonyesha Mohsein upande wa makabati yaliyokuwa na vifaa hivyo.Mohsein akaenda kuhesabu. Iliwachukua dakika arobaini na tano hadikuimaliza kazi hiyo.

"Chukua hesabu nilizozipata ili uingizekwenye mahesabu yako," Mohsein alisema huku akimpa Dina karatasialiyokuwa akiingizia nukuu za hesabu zake alizozipata.

Dinaaliichukua karatasi hiyo na kusogea kwenye mwanga zaidi ambakoalikwenda kuegemea kwenye kabati lililokuwa na uwazi na kuutumiauwazi huo kama meza ya kurekebishia hesabu zake huku akiwa amesimama.Mohsein akajiunga naye. Wakasaidiana kuzifanya pamoja hesabuhizo.

Wakati walipokuwa wakiendelea kuzifanya hesabu hizo,mabega yao yalikuwa yakigusana mara kwa mara na hali hiyo kuonekanani ya kawaida kwao hadi walipomaliza na kupata uhakika wa hesabuwalizozirekebisha.

"Nakushukuru kwa msaada wako," Dinaalisema, akiwa amegeuka kumwangalia Mohsein.

Mohseinakamwangalia Dina. "Usijali," alisema.

"Lazima nijalibwana…" Dina alisema na kutabasamu huku akiendelea kumwangaliaMohsein.
"Ningekuwa sijaimaliza hii kazi kama sio wewe kuja nakunisaidia!"

Mohsein naye akatengeneza tabasamu na kusema,"Poa."

Ghafla kukajenga ukimya kati yao ulioleta faraghahumo ndani huku kila mmoja akishindwa kujisogeza alipokuwa amesimama.Wakatekwa na ukimya, kisaikolojia wakajiona wapo kwenye faraghailiyojitokeza huku kila mmoja akikiri nafsini mwake kuwa ilikuwa najambo mbele yao linalohitaji kufanywa kati yao. Wakaangaliana, wakawamabubu kwenye vinywa vyao, lakini macho yao yakawa yanazungumza lughaya ukimya ambayo kila mmoja aliielewa maana yake. Mapigo ya mioyo yaoikaanza kwenda kasi. Mohsein akawa wa kwanza kuonyesha kusudio lakekwa kuuangalia mdomo wa Dina, akauinamisha uso wake na kuusogezausoni kwa Dina na mdomo wake kuulengasha mdomoni mwa Dina!

Mohseinakasita kuupeleka moja kwa moja mdomo wake kinywani kwa Dina,akasikilizia marejesho ya Dina yatakuwaje. Dina akawa ameganda kamaaliyepigwa na shoti ya umeme, naye akajikuta akiuangalia mdomo waMohsein kwa macho yaliyoonyesha haiba ya kukubali kitendokinachofuatia, kisha akafumba macho. Mohsein akaupeleka mdomo wakekinywani kwa Dina na papi zao za midomo kugusana. Mohsein akaupitishaulimi wake..!

Dina akaupokea!

Kila mmoja alilihisi jotola ulimi wa mwenzake wakati ndimi zao zikinyonyana. Dina akauhisimkono wa Mohsein ukianza kumpapasa kwenye paja lake ukiwaumeipandisha juu nguo yake, akawahi kuuzuia alipouhisi ukitakakuingia ndani zaidi. Akaendelea kukaza msuli wake wa mkono kuuzuiamkono wa Mohsein uliokuwa ukitaka uende zaidi ya hapo.

Vita yakuzuiana mikono iliendelea huku ndimi zao zikiendeleakunyonyana!

*****

HAIKUWA wiki njema kwa John tokeaalivyojibiwa na Dina kuwa hakukuwa na uwezekano wa wao kuoana mapemakama alivyokuwa amekusudia. Sababu iliyokuwa imetolewa na Dina, Johnaliiafiki kuwa ni ya msingi, lakini alilaani kipengele kilichotumikakwenye barua ile kilichomnyima Dina kupata ruhusa ya kupumzika kikazihadi miezi mitatu ikatike! Kipengele hicho alikiona kama vilekilikusudiwa kuingia kwenye dhamira yake ya kumuoa Dinaisifanikiwe.

Hofu dhidi ya Richard iliendelea kujikita kilaalipoifikiria miezi hiyo mitatu ipite bure bila ya kufunga ndoa naDina, lakini wakati huo huo miezi hiyo ikitumika akimwona Dina akiwakaribu na Richard! Kihoro hicho ndicho kilichokuwa kikimtesa kwawivu! Hakuamini kama Dina angekuwa na ubavu wa kuendelea kuhimilivishawishi vitakavyofanywa na Richard kwa wakati wote huo, hali hiyoilimfanya awe na wingi wa hisia kuwa, Dina atamsaliti!

Hofuilikuwa ikimtawala na kumuweka kwenye hali ngumu kila alivyokumbukakuwashuhudia wanawake wengi wakiwaacha wanaume waliokuwa wakiwapendana kuwafuata wanaume wenye pesa! John alizidi kuumia moyoni jinsiwanawake hao walivyokuwa hawajali maumivu yaliyowakuta wanaumewaliokuwa nao baada ya kuwaacha, na wakati mwingine walidiriki hatakuwatolea maneno ya kebehi wakati wanaume hao walipokuwawakiwabembeleza warudiane.

Fedha! John alinyong'onyea baadaya kuikiri nguvu ya chombo hicho. Awali kabla ya Dina kuajiriwa nakampuni ya mzee Ken, John aliwahi kujisifia kuwa ni mwenye bahati yakumpata msichana aliyeumbika kama Dina aliyekuwa tayari kumkataamwanamume mwenye pesa kwa ajili yake na kukichukulia kitendo cha Dinakumkataa Richard kama kigezo chake cha kupendwa. Alikuwa akijiona nishujaa na kuhisi burudiko moyoni mwake kila alipokuwa akionana naRichard na kumcheka moyoni. Na wakati Richard alipokuwa akijaribukumbembeleza Dina ili warudiane, John alifikia hali ya kumshangaa nakumwona kama aliyepungukiwa na akili!
Hakutaka kuamini Dinaangeweza kumsaliti kupitia kwa mtu aliyekwisha kumkataa tokea awali.Lakini kwa upande wa pili hisia zilikuwa zikiendelea kumuonya marakwa mara kuwa, ukaribu wa kikazi kati ya Dina na Richardungewalazimisha watu hao wawili wajenge maelewano kati yao ambayoRichard angeyatumia kurejesha tena uhusiano wa mapenzi uliotoweka!John aliuhisi moyo wake ukienda mbio na dalili za kupandwa nashinikizo la damu zilikuwa zikimwashiria kutokana na wivu ulioitawalaakili yake. Akakiri moyoni kuwa, kitendo cha kurudiana kwa Dina naRichard kama kitafanyika kingemwumiza mno!

Akaingiwa na akiliya kutaka kumshawishi Dina aache kazi, lakini alijikuta akijijibumwenyewe kuwa hilo lisingewezekana! Aliamini hilo lisingewezekanakutokana na ukweli alioukiri mwenyewe kuwa, nyota yake ya mapenziilikuwa imefunikwa na nyota ya Dina! Dina alikuwa na sauti dhidiyake, alilolitaka ndilo litakalofanyika na aliamini Dina angelikataawazo lake hilo na asingekuwa na ubavu wa kumlazimisha!

Ndaniya nafsi yake alikuwa akiandamwa na hatia iliyokuwa ikimsuta kutokanana ukweli kuwa alikuwa akimpenda mno Dina. Hatia hiyo ikawainamuingiza kwenye hofu ya kuachwa na hata kudiriki kutawaliwa namawazo ya kijinga kuwa kusingekuwa na mbadala wa maisha mengine bilaya Dina! Akauhisi ule unyonge wa kutokuwa na ushawishi wa kumuwekaDina chini ya himaya ya amri yake ukimzomea.

Mawazo yakeyakarudi kule kule kwenye kuwahi kumuoa Dina mapema kabla ya Richardhajafanikiwa kurudisha uhusiano na Dina, aliamini hatua hiyo angalauingemuweka kwenye haki ya kummiliki Dina kuwa mkewe, haki ambayoangeitumia kukabiliana na Richard kama angediriki au hata kujihusishana Dina kimapenzi. Lakini ukweli huo ulikuwa mbali!

Alijuaasingeweza kumshawishi Dina aache kazi kwa sababu Dinaasingemsikiliza. Lakini pia asingeweza kumkabili Richard na kumuonyadhidi ya Dina kwa sababu Dina bado hajawa mkewe, na asingeweza kumvaaRichard kwa mkwara wowote kwa sababu mwenzake ana pesa inayowezakutumika kwenye vyombo vya sheria na vyombo hivyo kumgeukia yeye naakajikuta akiswekwa mahabusu au pengine hata gerezani!

Akiliyake ikajiwa na wazo la kimbilio la wanyonge; kwenda kwa waganga kwaajili ya ushirikina! Angalau kwa kiasi fulani wazo hilo lilianzakumfariji baada ya kuifikiria hatua hiyo. Hakuwa ni mtu aliyependakujihusisha na vitendo vya ushirikina, lakini aliamini ushirikinaupo. Alishawahi kuzisikia sifa za mara kwa mara walizokuwa wakisifiwawaganga waliopo kijijini kwao, sifa ambazo zilikuwa zikitolewa nawatu wa mkoa wao. Hatua ya kuwafuata waganga kama hao aliamini kamaataichukua ingemsaidia kupambana na Richard. Fikra za kujipamatumaini kuwa dawa ya mtu mwenye pesa ni kupambana naye kwa kutumianjia za kishirikina ikaanza kumtawala kichwani.

Kwa upande huoaliamini angemwendea fundi wa shughuli hizo na kumtaka afanye uchawiwake ili Dina anapomwona Richard aingiwe na hisia kama vile ameonakinyesi! Pili, angemtaka fundi huyo afanye utaalamu wake wa kuifanyanyota yake iitawale nyota ya Dina ili aweze kumdhibiti kimapenzi.Aliamini kitendo hicho kingemfanya awe na sauti mbele ya Dina na Dinaangegeuzwa kuwa kama Kondoo kwa kutii kila ambalo angelizungumza.Fikra hizo zikamrudisha John kwenye Ukamanda wa kujiona yupo tayarikurudi tena kwenye uwanja wa vita kupambana na Richard! Kwa mtazamohuo, John akaisifia akili yake kupata wazo la kishirikina!

Akaipangasiku maalumu ya kwenda kumwona mganga kijijini kwao!

* * * **
[/FONT]
 
MTUNZI:BEKA MFAUME

SEHEMU YA TISA


***RICHARD ameamua kuvunja ukimya katika vita hii anataka kusafiri na DINA kikazi…je? Kitatokea nini hukombeleni……MOHSEIN ana wasiwasi mkubwa sana juu ya jambohili…..WIVU umemtawala bila kutarajia…….
***VIPI harakati zaJohn na waganga wa jadi!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…