Riwaya ya kipelelezi: Wakala wa Siri

Riwaya ya kipelelezi: Wakala wa Siri

View attachment 1972096

WAKALA WA SIRI EP 04
Mtunzi; Robert Heriel
0693322300

ILIPOISHIA

Fernanda akakimbia lakini macho na akili yake vikashikwa na machale kuwa mbele yake kunatatizo, akapunguza mwendo, akatembea kwa tahadhari, kitambo kidogo macho yake yakashtuka kuona kizuizi kilichozuia njia, Fernanda akasogelea kile kizuizi, akashusha pumzi nzito na matumaini ya kuwatoroka wale watu wabaya yakayeyuka. Njia ilikuwa imezibwa na kizuizi mfano wa Pangaboya kubwa lenye kutu, Fernanda akaenda kulishika lile pangaboya kubwa lenye kutu; akalizungusha kwa nguvu zake zote lakini hakuwa na nguvu hata kidogo ya kuweza kulizungusha, akajaribu tena kwa nguvu zake zote lakini ilikuwa kazi bure, halikuzunguka, Fernanda akaona ajaribu kupitisha kichwa kwenye nafasi ndogo iliyokuwepo kwenye lile pangaboya ili apite upenda wa pili, kichwa chake kikafanikiwa kupita akapokelewa na harufu mbaya ya uvundo iliyokuwa upande wa pili na giza nene kushinda alipokuwa anatoka. Lakini ingekuwa bora harufu hiyo kuliko kukamatwa na wale watu wabaya wenye roho za kikatili. Fernanda akajaribu kupitisha mabega yake lakini hilo likashindika, akajaribu zaidi na zaidi lakini hakuweza, akarudisha kichwa chake akawa anapumua kwa kasi, akageuka nyuma akaona kwa mbali mwanga wa kurunzi ukisogea kwa kasi kuja kule aliko,

ENDELEA..

“ Sasa hapa nitafanya nini? Mbona nimekamatika kirahisi hivi, sitakubali kukamatwa mzima mzima kama kuku wa sikukuu” Fernanda akawaza huku akiuangalia ule mwanga wa kurunzi unaokuja upande wake. Akili yake ilikuwa kama ngeredere anayerukia tawi hili na hili kumkimbia mkulima aliyeiba mahindi yake. Fernanda akageuka tena upande wenye kizuizi mfano wa pangaboya kubwa ya chuma iliyoshika kutu, mara hii mwanga ulikuwa umeongezeka kutokana na miale ya kurunzi ya wale watu wabaya, Fernanda akalikagua lile pangaboya kwa juu akaona kitu mfano wa Mkasi kilichozuia lile pangaboya lisizunguke, kwa upesi huku akijua hana muda mwema uliobaki, akarukia ule mkasi na kuuvuta kwa chini, lile pangaboya likaanza kuzunguka, “Vizuri” akasema kimoyomoyo. Akageuka nyuma wakati huu wale watu wabaya walikuwa washamuona na kuanza kumrushia risasi ambazo zilikuwa zilimpunyua na kulipiga lile pangaboya. Fernanda hakuwa na muda wa kupoteza, akasubiria upande wa pangaboya wenye nafasi kubwa ya yeye kupenya, hata hivyo kumbe lile pangaboya lilikuwa likizunguka polepole lakini kadiri linavyoendelea kuzunguka ndivyo linavyoongezeka kasi yake. Fernanda kwa kuona hivyo akarukia ile nafasi na kuzamia upande wa pili, kisha akalishika lile pangaboya na kulizungusha kwa kasi kuliongezea kasi yake ili wale wavaa suti za mauti wasimfikie. Kitendo cha kufanya kulizungusha lile pangaboya kulifanya kasi yake iongezeke maradufu asiwepo mtu awezaye kupita katikati yake. Fernanda akashusha pumzi kwa nguvu baada ya kukamilisha kazi hiyo nzito.

“ Nimeweza kuwaponyoka, lakini sasa huku ninakoenda ni wapi, nitatokea wapi. Giza la humu ndani linanitia hofu, harufu ya mahali hapa ni mbaya kama nini, sijui huku wanatupaga nini?” Fernanda akawaza huku akitembea polepole akiliacha lile panga boya likizunguka kwa kasi na kutengeneza upepo wenye harufu mbaya ya uvundo wa lile handaki. Fernanda akasonga mpaka alipofika sehemu ambayo akakanyaga kitu mfano wa matope, “ Sijui ni chemba ya maji take?” Fernanda akawaza. Akasonga akizidi kukanyaga majimaji na matope ya maji taka huku harufu mbaya ikishambulia pua yake, giza nene lililomfanya asione hata hatua moja lilizidi kumfunika, wala hapakuwa na tofauti yoyote kama angetembea kwa kufumba macho au akiwa ameyafumbua. Lilikuwa ni giza kuu,

“ Sikuwahi kufikiri kama kuna giza kama hili tangu nimezaliwa” Fernanda akawaza huku akizidi kusonga. Harufu ilizidi kuongezeka lakini hakuwa na chaguo, ilikuwa ni kheri harufu mbaya na giza kama lile kuliko kukamatwa na wale watu aliowaona kama mashetani wa makaburini. Akiwa anatembea mawazo yake yakaanza kuchora taswira katika ubongo wake;

“ Naitwa Stanslaus Mahige, naingia popote, hakuna mlango ambao utafungwa nisiufungue. Hata hivyo sijaja hapa kueleza habari hizo. Kilichonileta ni jambo moja tuu. Tafadhali nambie, Sajenti Warioba Yupo wapi?”

“ Tokea lini Sajenti Warioba anaishi hapa? Au kuna mtu kakuambia Sajenti yupo hapa? Mmeenda kwake hamjamkuta?”
Fernanda alisema.

“ Sikiliza wewe Mwanamke, sijaja hapa kujibishana na wewe, nambie Sajenti yupo wapi?”

“ Sijui Sajenti yupo wapi? Mwenyewe namtafuta, nani kakutuma umtafute Sajenti, na unamtafuta kwa nini?”

“ Hakuna asiyejua kuwa Sajenti ni adui wa nchi, yeye ndiye aliyeiba chipu ya Darubini ya maabara, yeye ndiye kaiba Cadava, yeye ndiye kaiba sampo za uchunguzi, tena akamtorosha Mateka wa ushahidi, sasa kaamua kutoroka. Huyajui mambo haya au upo pamoja naye kwenye uovu wake? Embu niambie Sajenti yupo wapi hiyo ndio salama yako, usiponiambia utajiingiza kwenye matatizo makubwa”
Fernanda ubongo wake ulikumbuka tukio lake la Stanslaus Mahige, kijana huyu ndiye alikuwa wakwanza kumvamia nyumbani kwake akimuamuru amwambia mahali alipo Sajenti Warioba.

“ Itakuwa Stanslaus Mahige alitumwa na hawa watu, lakini watu hawa ni kina nani? Inaonekana ni watu hatari sana, wakatili wenye roho za kishetani, lakini ikawaje Meja Venance Kagoda akawa na ushirika nao, mambo haya yananichanganya sana, lakini naamini majibu yote yatakuwa katika simu niliyonayo niliyoichukua chumbani kwa Meja Venance” Fernanda akawaza wakati akiwa anatembea katika matope yanayonuka giza likiwa limemfunika asiweze kuona anakanyaga nini.

Kitambo kidogo akavuka eneo lenye matope akawa anakanyaga mchanga wa changarawe, “ angalau hapa” akajisemea mwenyewe huku mkononi akiwa bado anabastola yake ambayo aliamini haikuwa na risasi zaidi ya mbili, hata hivyo bado aliiona itamsaidia kwa namna moja ama nyingine. Harufu na eneo lile ikawa imebadilika kutoka katika kuwa harufu mbaya kama ya maji taka na sasa akawa anasikia harufu mbaya ya kemikali kama ya madawa hivi. Akasonga lakini kadiri alivyokuwa akisonga akaanza kuhisi kuzunguzungu, bila shaka ni ile harufu mbaya ya kemikali ndio ilikuwa inamuathiri,

“ Harufu hii inaweza kuwa ni sumu, au pengine inaweza kuwa kemikali inayoathiri mfumo wa ufahamu. Nahisi kichwa kizito” Fernanada akawaza wakati anaongeza mwendo haraka haraka kuondoka eneo lile akitarajia mwendo mfupi ujao atakuwa ameepa harufu ile ambayo tayari imeanza kumdhuru. Akasonga kwa kitambo cha dakika mbili kwa mbali macho yake yakaona mwanga, moyo wake ukalipuka kwa tumaini, akazidisha mwendo lakini muda huu akaanza kuuona mwili wake unazidi kuwa mzito na macho yake yakiona mawenge,

“Fernanda don't die in this place, do your best! Move forward. There is hope, the Light is waiting for you. Come on Fernanda! Jikaze! Usikubali Fernanda” Mawazo ya Fernanda yalimsemesha akiwa anatembea akiyumba yumba kama mlevi kutokana na kizunguzungu, akishika ukuta huku akijikokota kuufuata mwanga aliouona mbele yake. Tayari alikuwa keshazidiwa, hali yake ilikuwa tete, asingejiongopea kuwa hana uwezo tena wakusonga mbele, ingawaje moyo wake ulikuwa radhi lakini mwili ulikuwa dhaifu. Fernanda akasimama akiwa kalegea kama mlenga, akakaa chini, akiwa pale chini, taswira nyingi kama filamu iliyorekodiwa zilipita katika kichwa chake. Akamuona Sajenti akiwa amepanda Farasi wa rangi ya udongo mwenye doa jeupe kichwani, Sajenti alikuwa kava kofia kubwa kama cowboy wa mexico, alikuwa amevaa shati jeupe ambalo hajalifunga vishikizo na pensi, akawa anakuja kwa kasi na farasi akiwa anatabasamu huku shati lake likipepea kwa upepo wa kasi ya Farasi, Fernanda nate akatabasamu. Sajenti akasema ; Don’t die in this place” kisha akaanza kumeguka na yule farasi kama vile kichuguu cha mchwa kinavyomeguka. Fernanda akashtuka, kumbe yalikuwa ni mawazo yaliyovurugwa na zile kemikali.

Fernanda akaanza kutambaa kama mtoto mdogo akiwa amebakiza hatua kadhaa aufikie mwanga hafifu uliokuwa mbele yake. Alipoukaribia ule mwanga akashangaa kukuta reli ya treni iliyokuwa ikitoka upande wake wa kushoto ikielekea kulia na hivyo kutengenaza makutano kama alama ya jumlisha. Eneo hili halikuwa na ile harufu ya kemikali, ingawaje bado Fernanda mwili ulikuwa mzito na kizunguzungu kilimzingua. Fernanda akaona apumzike pale, akakaa kwenye ile reli. Akiwa kapumzika usingizi ukimmendea huku mawazo mengi yakiweka foleni ndefu ubongoni mwake, mara akashtuliwa na sauti ya gari moshi iliyokuwa inatokea upande wa kushoto. Akageuka upande wa kushoto lakini hakuona kitu kutokana na giza lakini bado sauti ya gari moshi inayokuja alikuwa anaisikia. Fernanda muda huu akiwa amepata nguvu kidogo baada ya kupumzika akaona muda wa kuondoka mahali pale umewadia, Fernanda akawaza kuwa ataitumia Treni hiyo inayokuja kujikomboa kutoka mahali pale. Dakika moja iliyofuata Fernanda alikunja uso wake na kuyafinya macho yake baada ya mwanga mkali kutoka kwenye gari moshi uliokuwa ukimmulika usoni akiwa katikati ya reli. Gari moshi lilikuwa umbali wa mita hamsini lakini mwanga wake uliweza kuangaza umbali mrefu, Fernanda akaweka mkono wake usoni kuziba mwanga usimpige machoni huku akijitahidi kuangalia ile Treni kwa umakini. Looh! Macho yake hayakuweza kukubali, akiwa bado kasimama alishtuka kuona mdomo wa bunduki na mlengaji akiwa juu ya kichwa cha Treni vikiwa vinamtazama, upesi akajirusha pembeni huku akifukuzwa na milio ya risasi, Fernanda akaamka upesi na kuanza kukimbia akiiacha Reli, akanyooka moja kwa moja kule mwanga ulipokuwa unatokea, Treni ilipofika mahali alipokuwa amesimama akasikia watu wakishuka huku wengine wakimshambulia kwa risasi, Fernanda alikimbia kwa nguvu zake zote huku mwanga hafifu ukimsaidia. Nyuma yake wale watu hawakutaka kumpa nafasi ya kutoroka, walimuandama kama kivuli cha kifo. Ghafla bin vuu jambo baya likatokea, mbele ya Fernanda kama hatua kumi lilikuwepo shimo refu lakini juu yake kulikuwepo na tundu kubwa linaloingiza mwanga kutokea juu. Nyuma yake wale watu wabaya walikuwa hawapo mbali, walikuwa wakija kwa uhakika wa kumpata Fernanda; Akasimama, akageuka nyuma kuwatazama watu wale, kisha akageuka kulitazama lile shimo ambalo ndani yake mwanga ulikuwa ukiingia, chini kabisa ya lile shimo kwa mbali akaona kuna kamba mbili, wakati bado hata hajatambua rangi ya kamba zile, akahisi maumivu yakipenya katika bega lake la kulia, na punde akaanguka chini ya lile shimo refu lenye giza kwa chini licha ya kuwa kulikuwa na mwanga ukitokea juu yake.

***************************

ITAENDELEA.

Kitabu hiki kinamahusiano makubwa na Kitabu cha " MLIO WA RISASI HARUSINI" ambacho tayari kipo sokoni.

Jipatie Hardcopy kwa bei ya Ofa Tsh 10,000/= Ikatayodumu mpaka tar 14/10/2021

OFA hii isikupite!

MLIO WA RISASI HARUSINI

Kitauzwa Kwa Tsh 10,000 badala ya Tsh 15,000.

Mwisho WA OFA ni tarehe 14/10/2021

TUMA PESA KWA NAMBA

0693322300
Airtelmoney
Robert Heriel
Mwandishi bado hujajirekebisha tu. Hili tukio la treni na watu wenye bunduki halikufaa kuwa hapa. Linaharibu mtiririko wa riwaya. Hapa huyu mtu atajiokoaje sasa kama matukio yamepandiliana namna hii. Hayampi nafasi.
Unaharibu riwaya kwa kuandika matukio impossible.
 
Chief usitake ije kama unavyotaka tulia fuata mtunzi alichokuandalia
Nchi hii bado sana. Unatutungia vitu mtu akisoma anaona kavisa siyo halisia. Akikosolewa mnakasirika? Kukosoa ni sehemu ya fasihi. Huwezi kututungia vitu vinavyokiuka misingi ya fasihi halafu tuchekelee tu. Tatizo wasomi wa siku hizi wametumia google kwenye kusoma. Upeo wa kufikiri ni mdogo.
Ndio maana mnatunga vitu visivyowezekana kwa akili ya kawaida.
 
Chief usitake ije kama unavyotaka tulia fuata mtunzi alichokuandalia
Unakosea sana.
Mtunzi ameleta riwaya humu siyo watu wasahihishe bali waburudike,waondoe stress na kujifunza.
Kama wiki mbili hivi zimepita watu walidai mwendelezo,wewe unaleta upinzani.
Lete riwaya yako tuone kama ukweli wewe ni mahili kwenye mpangilio.
Ungekuwa na busara hata kidogo ungemshauri nje ya hapa.

Mleta riwaya mpuuze hiyo twende kazi

Sent from my TECNO CA7 using JamiiForums mobile app
 
Mwandishi bado hujajirekebisha tu. Hili tukio la treni na watu wenye bunduki halikufaa kuwa hapa. Linaharibu mtiririko wa riwaya. Hapa huyu mtu atajiokoaje sasa kama matukio yamepandiliana namna hii. Hayampi nafasi.
Unaharibu riwaya kwa kuandika matukio impossible.
Hebu leta ile yako uliyotunga ambalo lina mtiririko vizuri tuone .
 
Nchi hii bado sana. Unatutungia vitu mtu akisoma anaona kavisa siyo halisia. Akikosolewa mnakasirika? Kukosoa ni sehemu ya fasihi. Huwezi kututungia vitu vinavyokiuka misingi ya fasihi halafu tuchekelee tu. Tatizo wasomi wa siku hizi wametumia google kwenye kusoma. Upeo wa kufikiri ni mdogo.
Ndio maana mnatunga vitu visivyowezekana kwa akili ya kawaida.
Sidhani kama umelezimishwa kusoma
 
Mkuu naomba nisikujibu Kwa heshima ya wasomaji wengine.

Sanaa ya uandishi wa FASIHI ni Pana mno,

Kuna Fiction Novels ambazo kazi yake ni Kueleza mambo yasiyowezekana, yasiyokuwepo, yakufikirika,

Wasanii wote wakubwa Duniani Kwa upande wa RIWAYA wameandika Fiction Novels mathalani Shaaban Robert, Kezilahabi, E. Semzaba, Ngugi, Ole seyinka, n.k.

Nakushauri uwe msomaji wa RIWAYA nyingi ili uzidi kuijua Fasihi Kwa undani,

RIWAYA niliyoandika ni RIWAYA ya kipelelezi ambayo Asilimia kubwa nimetumia uhalisia.

Je ungesoma RIWAYA yangu ya "SIKU YANGU YA KUFA ILIPITA" si ndio ungetoa povu mpaka basi

😄😄😄

Relax hii ni KAZI ya Sanaa
 
Mwandishi bado hujajirekebisha tu. Hili tukio la treni na watu wenye bunduki halikufaa kuwa hapa. Linaharibu mtiririko wa riwaya. Hapa huyu mtu atajiokoaje sasa kama matukio yamepandiliana namna hii. Hayampi nafasi.
Unaharibu riwaya kwa kuandika matukio impossible.

😄😄😄😄

Hayampi nafasi Nani Mkuu?

Relax Mkuu, fuatilia Simulizi
 
Sawa Mkuu. Mimi sijui.

Muhimu usome
Mdogo wangu sisi wengine si watunzi ila ni wasomaji wazuri wa riwaya ni kweli anachosema/anachoshauli huyo msomaji matukio yanafulilizana mno kiasi inafikia kupunguza radha

Hao wengine wanachotaka wewe utoe hii hadithi na wao waisome hawana habari ya ubora
Mimi kwa ushauri tu fuata ushauri unaopewa punguza kuunganisha matukio mengi kwa wakati mmoja ili kuleta uhalisia na radha
Mwisho nikupongeze wewe ni mtunzi mzuri jaribu kuzingatia ushauri utafika mbali katika tasnia hii
 
Nashukuru sana
 
Nchi hii bado sana. Unatutungia vitu mtu akisoma anaona kavisa siyo halisia. Akikosolewa mnakasirika? Kukosoa ni sehemu ya fasihi. Huwezi kututungia vitu vinavyokiuka misingi ya fasihi halafu tuchekelee tu. Tatizo wasomi wa siku hizi wametumia google kwenye kusoma. Upeo wa kufikiri ni mdogo.
Ndio maana mnatunga vitu visivyowezekana kwa akili ya kawaida.
Sasa si uhame nchi mkuu
 
Mkuu tupia muendelezo please.
Achana na wakosoaji!
 
Mkuu naomba nisikujibu Kwa heshima ya wasomaji wengine.

Sanaa ya uandishi wa FASIHI ni Pana mno,

Kuna Fiction Novels ambazo kazi yake ni Kueleza mambo yasiyowezekana, yasiyokuwepo, yakufikirika,

Wasanii wote wakubwa Duniani Kwa upande wa RIWAYA wameandika Fiction Novels mathalani Shaaban Robert, Kezilahabi, E. Semzaba, Ngugi, Ole seyinka, n.k.

Nakushauri uwe msomaji wa RIWAYA nyingi ili uzidi kuijua Fasihi Kwa undani,

RIWAYA niliyoandika ni RIWAYA ya kipelelezi ambayo Asilimia kubwa nimetumia uhalisia.

Je ungesoma RIWAYA yangu ya "SIKU YANGU YA KUFA ILIPITA" si ndio ungetoa povu mpaka basi

[emoji1][emoji1][emoji1]

Relax hii ni KAZI ya Sanaa
Nimeshasoma zaidi ya vitabu mia tatu. Hivyo havitoshi?
 
Na kama utunzi wako ndio wa aina hii na kila unapokosolewa unakuwa mkali au kuejdelea kug'ang'ania aina ya huo uandishi wako. Hutofika mbali.
 
Back
Top Bottom