Road trip update: Dar - Mtwara - Dar | Hali ya Barabara inatisha | Ila nimetumia mafuta ya Tsh 150,000/= tu!

Road trip update: Dar - Mtwara - Dar | Hali ya Barabara inatisha | Ila nimetumia mafuta ya Tsh 150,000/= tu!

Mad Max

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2010
Posts
35,566
Reaction score
104,386
Basi wakuu nikaenda Mtwara kutokea Dar na kurudi Dar. Trip ilikua ni kupunguza stress za huu mji, na haikua direct, nilienda kwa vituo vitatu jumla, na nilitumia Fit Hybrid.
76739ac2c5a5cdac8c8dfd1667959157.jpeg

Safari ilianzia Mlimani City Puma pale, nikaweka wese la 100k nikachomoka. Kwasababu ya mvua, AC almost ilikua off na nilikua very slow, kwasababu ya barabara, mvua inapunguza visibility na fuel efficiency inakua nzuri sana.
12fb203e24a2a7ab513aaeb376aa1da5.jpeg

Kwahiyo kituo cha kwanza ni Dar hadi Kilwa Kivinje, hapo sikulala ila nilizurura like 2 hours baada ya kupark gari. Kilwa Kivinje ni kamji flani hivi ka-wavuvi kana vibe lake lakini kamepoa sana.
674ad239e28a8826c5ed924198c159c2.jpeg

Then nikaondoka nikaenda Kilwa Masoko hapa nikalala. Hadi hapa nikawa nimetumia zaidi ya kilometa 320. Huu ni mji mkubwa zaidi, na ndio makao makuu ya Wilaya. Nao ni mji mdogo, ila una vibe zaidi ya Kivinje, ofisi kubwa zipo hapa pia.

Hali ya barabara tokea Dar hadi Kilwa ni mbaya. Kwa rate ya 10, ningeipa 6.5 hivi. Ni ngumu sana kuendesha gari zaidi ya 60 km/h kwa muda wa zaidi ya dakika 10 kabla haujakutana na korongo.
IMG_8163.jpeg

Kesho yake ikawa safari ya kwenda Lindi. Kilwa hadi Lindi ni zaidi ya kilometa 140 hivi. Njiani hamna kitu chochote cha maajabu, so ni kuendesha tu. Hii ndio barabara mbovu kuliko zote ulizowahi kukutana nazo. Kuipa 4/10 ni kuipendelea sana. Serious yale sio mashimo ni makorongo barabarani.
IMG_8187.jpeg

Baada ya kufika Lindi nikaspend a day na kulala. Ni kamji flani kazuri kwa kukaa siku 2 hadi week ila aada ya hapo kanaanza kuboa. Kana mitaa iliyopangika kama Tanga, barabara yoyote inatoa, ila wana challenge kubwa sana maeneo ya kulala. Unagusa Lodge ya kawaida sana ambayo Dar haizidi elfu 25 huku unaambiwa elfu 50.
IMG_8251.jpeg

Kesho yake safari ya Mtwara ikaanza, barabara nayo mbaya tu like 5/10. Jumla ni kama kilometa 110 hivi, kwahiyo ndani ya masaa mawili nikawa nimefika. Nahindwa kuprove ila kiwanda cha Dangote kwa namna moja kinachangia sana kuharibika kwa hii barabara. Nasema ivo kwasababu ukishavuka hiki kiwanda, barabara sio mbaya sana. Just my theory!
IMG_8227.jpeg

Mji poa, sema una vurugu kama Dar flani so hapakunivutia ata kulala na kukaa sana nikaondoka. Ninavyoondoka nikaweka mafuta kituo cha Puma ya Elfu 50 tu. Kile kituo hafu wezi, wanasema hawana risiti ila kuna ujanja wanafanya. Maza Faka!
IMG_8303.jpeg

Nilichopenda kuhusu Mtwara ni kamji flani kanaitwa Mikindani, ni kama 10 km kabla haujafika Mtwara mjini. Ni mji wa Kihistoria kama Bagamoyo, hapa wakati wa kurudi nilisimama na kuzurura kama 1 hour. Pa zuri sana, unaweza kaa pale ata siku 2 panamuonekano flani wa kipekee. Pia wana view nzuri sana ya bahari.
IMG_8314.jpeg

Baada ya hapo ni trip ya kurudi Dar. Nikasema nitest uwezo wangu wa kuendesha non-stop. So baada ya kufika Lindi nikala hafu nikaanza kuondoka mazima, ishakua saa 2 usiku hapo.

Usingizi ulinizidi njiani nikapark mahala nikalala aisee but nkafika Dar safe.

Summary:
  • Umbali niliotembea wote ni kilometa: 1,230
  • Mafuta niliotumia ni Tsh 150,000/=
  • Average fuel consumption inayosoma ni: 31 km/L
  • Average Speed ni ndogo sana: 30 km/h
  • Masaa gari lilikua ON ni: 42 hours
IMG_8324.jpeg

IMG_8327.jpeg
Uwa napenda trip za kuzunguka, yaani mfano unatoka Dar unaenda Mtwara then Songea kisha Njombe, Iiringa, Moro then Dar. Ila hii ya kwenda na kurudi, mara nyingi safari ya kurudi haiwi na excitement sana. Nitatafuta nyingine ya kuzunguka.

Pamoja!
 
Mad Max Una Akili nyingi Sana ndugu yangu, hakuna therapy nzuri duniani kama kusafiri hii ni zaidi ya tiba na afya ya Akili.
Ukitaka kuishi maisha ya furaha duniani Fanya safari kama hizi ....aisee kuna vibe Fulani hivi halielezeki kabisaa.

Mwaka Jana nilipita hiyo barabara kutoka DAR - MASASI Kwa bus Tu, njiani sijakutana na gari ndogo Hadi nafika nangurukuru kutokana na ubovu wa barabara, Hali ya hii njia ni zaidi ya shamba la mpunga sijui serikali imeenda wapi Hadi barabara inakuwa hivi
 
Kusema kweli ukiona kichwa haijatulia, tafuta ata uende Moro sio lazima kudrive. Inasaidia sana mkuu. Pamoja.

Aisee hii barabara ya kusini yaani aibu. Aisee kuna mashimo unakutana nayo hafu ghafla tu. Nina uhakika tatizo sio umri wa barabara ile aliekula contract kazingua.

Daraja la Mkapa limetengenezwa safi sana na madaraja mengine ya Mt Rufiji. Naamini hamna mvua ya kuzuia mawasiliano.

Tatizo kuu ni barabara yenyewe
 
Mzanzibar atasema swala la barabara sio mambo yake!! Safi sana kwa kuboresha afya ya akili kwa safari isio umiza.
Kazi ni kipimo cha utu
Wabunge wao wapige kelele aisee. Kuna siku tulikua humu tunaongelea safari ya kwenda Songea kupitia Mtwara aisee mara 100 upite Morogoro. Utasimbuliwa na jam ya maroli ila ukivuka Moro ushatoboa.
 
Kusema kweli ukiona kichwa haijatulia, tafuta ata uende Moro sio lazima kudrive. Inasaidia sana mkuu. Pamoja.

Aisee hii barabara ya kusini yaani aibu. Aisee kuna mashimo unakutana nayo hafu ghafla tu. Nina uhakika tatizo sio umri wa barabara ile aliekula contract kazingua.

Daraja la Mkapa limetengenezwa safi sana na madaraja mengine ya Mt Rufiji. Naamini hamna mvua ya kuzuia mawasiliano.

Tatizo kuu ni barabara yenyewe
December MUNGU akitupa uhai nitaenda MASASI pengine barabara itakuwa imetengenezwa angalau
 
Honda Fit ya mwaka gani hiyo. Kwa utundu wako mbona hujabadilisha lugha kwenda kiingereza?.

Mtwara ungejaribu kuzunguka chuno road hadi bandarini then uikamate zambia road hadi pale round ya mnarani ulipochukua picha.

Nilitegemea kutoka pale mnarani ungenyooka na Tanu road hadi kanisani kule kupitia Bima, pana-view moja mzuri sana ya lile kanisa ukitokea pale Puma.
 
Back
Top Bottom