Kiratiba Yanga kapata bahati sana kucheza na Mamelodi Sundowns, Tarehe 27 mwezi huu timu ya taifa ya Afrika kusini yenye wachezaji 10 wa Mamelodi itakuwa na mchezo nchini Algeria siku mbili mbele au tatu Mamelodi watapaswa kuwa Dar es Salaam.
Kuna taarifa za ndani ya Mamelodi kujaribu kuomba endapo wangepangiwa timu yoyote ile kutoka Tanzania wachezaji wao wasicheze mchezo dhidi ya Algeria kutokana muda mchache wa kujiandaa pamoja na umbali wa safari kutoka Algeria to Tanzania. Wao walipendelea wacheze na ES Tunis ssb ya urahisi wa kutoka Algeria to Tunisia. Logistics za mchezo dhidi ya Yanga hazitakuwa rafiki kwao.