Roho inaniuma nimetimiza miaka 35 sina mtoto wala maisha

Bata batani

JF-Expert Member
Joined
Nov 11, 2011
Posts
3,217
Reaction score
3,694
Roho inaniuma jamani leo nimetimiza miaka 35 kamili sina mtoto wala sina maisha licha ya kutumia miaka 10 katika kupambana na maisha.

Uzee sasa umepiga hodi taratibu hapa nilipo nahisi naanza kuchanganyikiwa kwa umri huu mpaka leo hii naishi maisha ya kubangaiza nipate hela ya kula miaka 35 yote hii.
 
Badili mazingira, mbinu za utafutaji na uongeze bidii.
 
Usiogope, wako watu wanamaisha na watoto lakini ni wagonjwa sana, wako watu wana maisha ila hata mtoto wa dawa hawana.
 
Mkuu pole sana....tupo pamoja just jana tuuu nimewaza hivi ningekuwa na mtoto tangu chuo....Mkuu tujilipue au uansemaje.
 
Mimi nina miaka 31 sasa hivi, niko kama wewe ila niko MAKINI.

Ni bora uwe na familia lakini usiwe na hela. Utapambana hata kuilisha kwa GENGE. Elimu watoto watapata hata ELIMU BURE.

Jambo la msingi tu usizae watoto wengi.

Punguza matarajio, oa mwanamke wa kawaida uanze maisha.

Tatizo letu vijana tuna matarajio na ndoto kubwa sana, mwisho wa siku umri unatutupa mkono wakati PESA HATUNA na FAMILIA hatuna.

Tunabaki kuzurula kwenye familia za watu kupiga stori za MAJUNGU.
 

Pambana kwanza hapa mbona unalia lia eakati mjomba kakusaidia sana?

Kodi umelipiwa kabisa miezi 6, oa sasa hata hao wanaouza mihogo uendelee na life
 
Huna maisha kivipi? Pambana uyashinde maisha wewe! Usikubali hata siku moja maisha yakushinde.

Angalia ulipo jukwaa ni wapi! Ili ufanikiwe, ni lazima ubadili mwendendo wako mbaya wa maisha! Hakuna namna. Miaka 35 huna mtoto? Maana yake huna madhara, au!!!
 
Nyie si huwa mnasema huwezi kujitolea ukalipwa laki kwa mwezi. Pambana utafika tu.
 
Tatizo unakata tamaa kwa kujilinganisha na wengine. Unasahau kila mtu ana njia yake. Relax man it's just a life. Pambana mzee tafuta marafiki waliofanikiwa. Wata hamsha hali ya kupambana. Life is one time offer use it well.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…