Kuna siku nilinunua Bati- baada yakufika site Fundi alipokuja alinipigia Simu kuwa zile bati sio za ALAF ni fake. Bahati nna Jamaa angu anafanya kazi ALAF nilipompigia akanielekeza namna ya kutambuwa ALAF original na Fake!
Niliporudi Dukani Mmoja ya alieniuzia (walikuwa wawili) akaanza maneno ya shombo. Mimi nikawaambia wanibadilishie zile Bati wanipe Original au wanipe pesa yangu! Vinginevyo Kesi nawausisha ALAF Ili wawasaidie kuwaonyesha Walipozipata hizo fake ALAF mwenzake aliposikia hivyo akanipa tena Bati 50 zingine.
Akalipia usafiri wa kupeleka original Bati site na kusomba zile fake kurudisha dukani. Ni Zaidi ya Mwaka Bati zote zipo na same color.Pole sana ila kama una risiti ya Hizo Bati washirikishe ALAF mwende Dukani mkakomae nao