Roho inaniuma sana, mabati niliyoezekea nyumba yangu yamepauka sana

Ubabaishaji ni mwingi sana.ukienda na fundi kununua mabati ndio kabisa kuna ujinga mm nilinunua bati bomba ila zimepauka hadi naona aibu.fundi mmoja alipanda kurekebisha sehemu akaniuuliza hizi bati mbona umenunua used ? Nikamwambia nimechukua kabisa keko pale ndani bati bomba.kaniambia kuna uhuni umefanyika hizi bati zipo tofauti alafu aina moja...washenzi sana hawa watu.
 
Yaani nimefanikiwa kujenga nyumba tena kubwa ila sijahamia bado vitu vichache nihamie, lakini kinachoniuma kipindi napaua (kupiga bati)niliaminishwa kuwa bati za kampuni fulani (hapa siitaji jina) ni nzuri na nikaonyeshwa nyumba ya jirani yenye hizo bati kuwa hazipauki.

Nilikubali baada ya kukagua na nikajiridhisha kila kitu, nikaenda nunua hizo bati pale Tazara nikapaua nyumba vizuri tu, sasa ni miaka 4 tangu nipaue sijahamia lakini zile bati kwa kweli zinatia kinyaa zimepauka hadi sina hamu ya kuhamia tena huko.

Hapa kinachoniuma zaidi nyumba ya jirani zake rangi iko vile vile na ni yeye aliniagizia alikonunua hadi bei ni hiyo hiyo, na hata jirani na ofisini kuna bati kama hizo hizo zimezungushiwa kama fensi sehemu wanakojenga hazijapauka kila siku naona ni mpya na nashindwa elewa hapa kuna siri gani kwenye hiyo kampuni nyingine zipauke nyingine zisipauke!

Hapa nawaza je! Ninunue bati zingine au ninunue rangi ya bati nikapake upya kwa mkono?

Ushauri wenu naombeni.
Walikuchukulia Rejected ziiile.... Kule TBC ndan ndani..... Nilikua natafutaga kiboko bati, nikOneshwa sample og alafu nikalipia wakawa wanapakia famba....

Nina historia pale, nilileta utata pesa ikarudi, nikaenda kuchukua Tag tukabeba mazaga ya ofisi yao wakaja kuyagomboa tukagawana pesa, nikasepa na misumari...

Mapimbi saana
 
Mbona rahisi tu. Kama bati ni nzima na tatizo ni rangi tu nashauri kanunue rangi unayoipenda paka bati lako maisha yaendelee. Sioni tatizo la kung'oa hizo bati na kuweka nyingine
 
Kuna mtu kanishauri hivyo hivyo ila yeye kaniambia ya plascon eti nipake kwa ufagio (softbroom)kama hizi wanzofagia nazo ndani eti ndio rangi itakolea vizuri na akakazia nisutumie mashine eti nikitumia mashine zitajapauka tena baadae
Plascon au kampuni yoyote PVA inapakwa kwa mkono tu na fundi rangi mzuri.
 
Yaani nimefanikiwa kujenga nyumba tena kubwa ila sijahamia bado vitu vichache nihamie, lakini kinachoniuma kipindi napaua (kupiga bati)niliaminishwa kuwa bati za kampuni fulani (hapa siitaji jina) ni nzuri na nikaonyeshwa nyumba ya jirani yenye hizo bati kuwa hazipauki.

Nilikubali baada ya kukagua na nikajiridhisha kila kitu, nikaenda nunua hizo bati pale Tazara nikapaua nyumba vizuri tu, sasa ni miaka 4 tangu nipaue sijahamia lakini zile bati kwa kweli zinatia kinyaa zimepauka hadi sina hamu ya kuhamia tena huko.

Hapa kinachoniuma zaidi nyumba ya jirani zake rangi iko vile vile na ni yeye aliniagizia alikonunua hadi bei ni hiyo hiyo, na hata jirani na ofisini kuna bati kama hizo hizo zimezungushiwa kama fensi sehemu wanakojenga hazijapauka kila siku naona ni mpya na nashindwa elewa hapa kuna siri gani kwenye hiyo kampuni nyingine zipauke nyingine zisipauke!

Hapa nawaza je! Ninunue bati zingine au ninunue rangi ya bati nikapake upya kwa mkono?

Ushauri wenu naombeni.
Muwe mnachukua warranty Ili yakipauka kabla ya muda kampuni husika I rehabilitate na wakizingua nenda Mahakamani.
 
Relax bro hiyo ipo kwa wote
Niliezeka bati upande umepauka na upande mwingine zipo vile vile,nyumba ipo kama ina aina 2 za bati,ila nilinunua sehemu moja,duka moja bei moja...ila ukiangalia kwa jirani bati zipo poa tu
Ilimradi sinyeshewi haina shida
Kupauka lazima itapauka ila ishu ni mda wa kupauka..

Hapo utakuwa ulichanganyiwa hizo bati.
 
Ubabaishaji ni mwingi sana.ukienda na fundi kununua mabati ndio kabisa kuna ujinga mm nilinunua bati bomba ila zimepauka hadi naona aibu.fundi mmoja alipanda kurekebisha sehemu akaniuuliza hizi bati mbona umenunua used ? Nikamwambia nimechukua kabisa keko pale ndani bati bomba.kaniambia kuna uhuni umefanyika hizi bati zipo tofauti alafu aina moja...washenzi sana hawa watu.
Ukinunua hakikisha unapewa waranty na risiti
 
Back
Top Bottom