Roho inaniuma sana, mabati niliyoezekea nyumba yangu yamepauka sana

Roho inaniuma sana, mabati niliyoezekea nyumba yangu yamepauka sana

Relax bro hiyo ipo kwa wote
Niliezeka bati upande umepauka na upande mwingine zipo vile vile,nyumba ipo kama ina aina 2 za bati,ila nilinunua sehemu moja,duka moja bei moja...ila ukiangalia kwa jirani bati zipo poa tu
Ilimradi sinyeshewi haina shida

Mi mwenyewe nikiangalia kwa jirani zake nikama kaezekajana ndio nachoka kabisa
 
Mkuu kuna Rangi inaitwa PVA roof, hii ni kwa ajiri ya kupaka kwenye bati au chuma, huwa mfano wa inter(inta) chukua ya kiwanda cha plascon, paka vizuri sana harafu njoo unipe mrejesho

Sawa mkuu nitafanya hivyo itabidi tuu hata mafundi zaidi ya 5wamenishauri kampuni hiyo hiyo.
Sory hivi kuna ubaya nikabadilisha rangi ingine?yaani bati ni blue nipake brown
 
Kweli ndio maana hapo juu nimemuuliza ni G30 au G28?
Huyo walimpa G28 badala ya hizo

Kwani geji ikiwa kubwa ndio og? Maana navyojua geji kubwa ndio zinakuwa laini zaidi
 
Ubabaishaji ni mwingi sana.ukienda na fundi kununua mabati ndio kabisa kuna ujinga mm nilinunua bati bomba ila zimepauka hadi naona aibu.fundi mmoja alipanda kurekebisha sehemu akaniuuliza hizi bati mbona umenunua used ? Nikamwambia nimechukua kabisa keko pale ndani bati bomba.kaniambia kuna uhuni umefanyika hizi bati zipo tofauti alafu aina moja...washenzi sana hawa watu.

Mi mwenyewe natamani kuuza nyumba sitaki kuziona hata maana paa limenigharimu sana na nyumba ni kubwa baraza 3 hizo canch tuu pamoja na ufundi ni milion 9 bado bati
 
Walikuchukulia Rejected ziiile.... Kule TBC ndan ndani..... Nilikua natafutaga kiboko bati, nikOneshwa sample og alafu nikalipia wakawa wanapakia famba....

Nina historia pale, nilileta utata pesa ikarudi, nikaenda kuchukua Tag tukabeba mazaga ya ofisi yao wakaja kuyagomboa tukagawana pesa, nikasepa na misumari...

Mapimbi saana

Daa naumia mno kwa kweli pole sana mkuu
 
Bati Za Rangi Ni Upigaji Mpya
Bora Kununua Za Kawaida Upake Rangi

Kabisa naamini hilo jamaa yangu yeye kapaulia hizi hizi za kawaida kumbe nazo kuna za kung'aa zaidi ambazo eti hazipatu kutu lakini kweli bhana tangu apige naona ziko vile vile
 
Back
Top Bottom