Roho inaniuma sana, mabati niliyoezekea nyumba yangu yamepauka sana

Hata Rangi Nyeupe ni Rangi piaaa
 
Kuna Jamaa yangu alinunua bati kampuni iliyotajwa kwenye comment ya mwanzo Kabisa ila zimegawanyika mara mbili

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Kwani utalala huko kwenye mabati? Kama nyumba inavuja unasababu ya kusumbua ubongo hongera kwa kujenga .
 
Pesa zinakuwasha wewe, yani rangi imepauka unataka kubadili bati kabisa.
 
Nunua rangi paka Upya.

Life time ya rangi za mabati ni kati ya miaka 5 hadi 10 tu. Baada ya hapo wote zinapauka na kufubaa bila kujali ni kiwanda gani.

Sasa tayari una miaka minne. Uingie gharama ya kununua bati zingine?
Hapana. Pole kwa usumbufu huo ndio maisha ni bahati mbaya.

Pia aina ya rangi ina strength tofauti tofauti hata kama ni kiwanda hicho hicho kimoja.
 

Mfano mzuri ni kama ana miliki gari, ile tunayoita wheel balance ni kwa sababu ujazo wa tairi hauko sawa kutoka kiwandani tena ni kiwanda kimoja lakini ujazo haufanani, ndiyo maana tunongeza vile vichuma( balancing palletes/ rods) ili kufidia sehemu yenye ujazo dhaifu kwenye tairi.
Kwa hiyo ni kweli unaweza kukuta watu wa Quality Assurance and Control walizembea wakati wa uzalishaji kwenye batch aliyonunua mdau.
Namshauri akanunue ndoo 2 au 3 za Roof Paint, apate mchanganyo anaoutaka kisha apige bati. Zitarudi kuwa poa, lakini lazima ziwe Roof Paint!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…