Roho inaniuma sana, mabati niliyoezekea nyumba yangu yamepauka sana

Sio kila kitu chenye bei kubwa ni kizuri au kila kitu chenye bei ndogo ni hafifu.
Kuna watu wametumia Alaf Original kutoka kiwandani bati zimepauka.
Mnatuchanganya sasa,tununue bati gani sasa
 
Miaka mitatu kuelekea minne na Bado linawaka. Nilipata wakala wa kueleweka. Ila haya mambo ni kubahatisha tu. Kuna ujanja ujanja mwingi sana.

Hapo mkuu paka rangi tu. Usiingie gharama za kupaua upya.
 
Mtaani kwetu wote waliopaua na bati ya alaf na dragon hakuna iliyopauka, binafsi nimepaua na dragon.

Jambo la msingi nenda kiwandani bati ikatwe unaiona upewe na warranty, usichukue za bando.

Pia mtoa mada alichokosea ni kuchukua rangi ya blue, ikipauka inaonekana sana.
 
Nunua Bati nyeupe za alafu simba dumu zile og kabisa
Paua nyumba yako baada ya miaka mitani paka rangi

Note;
simba dumu og inamaandishi meusi yameandikwa alafu na namba namba ....pia zinakua na nembo ya simba ya kupigwa na Moto.

Feki zinakuwa hazina maandishi meusi ya alafu pia nembo ya simba inakua ya ndala kama Mpira flani hivi.
 
mwanzoni makampuni ya kuuza mabati walikuwa makini kupiga rangi, mabati yalikuwa hayapauki. Siku hizi bora ukanunua mabati yasiyo na rangi za viwandani ukapiga rangi wewe mwenyewe.
 
mwanzoni makampuni ya kuuza mabati walikuwa makini kupiga rangi, mabati yalikuwa hayapauki. Siku hizi bora ukanunua mabati yasiyo na rangi za viwandani ukapiga rangi wewe mwenyewe.
Alaf, hua wananunua 'coils' zikiwa colored kabisa toka SA, wao ni kuweka iyo mikunjo na hayo mawimbi ( roll forming )

sishangai izo kampuni zinapaka wenyewe hapahapa, bati baada ya miezi 6 hupauka
 
Alaf, hua wananunua 'coils' zikiwa colored kabisa toka SA, wao ni kuweka iyo mikunjo na hayo mawimbi ( roll forming )

sishangai izo kampuni zinapaka wenyewe hapahapa, bati baada ya miezi 6 hupauka
sidhani kama wananunua ikiwa zimeshapakwa. ingekuwa hivyo, wakisha press bati kuform migogo bati zingechubuka. MImi nilinunua Alaf mwaka 2006 mpaka leo ziko safi. 2015 nikampeleka jamaa yangu akanunua, ni aibu hata kusema ni za alafu. zimepauka vibaya
 
Alaf, hua wananunua 'coils' zikiwa colored kabisa toka SA, wao ni kuweka iyo mikunjo na hayo mawimbi ( roll forming )

sishangai izo kampuni zinapaka wenyewe hapahapa, bati baada ya miezi 6 hupauka
Nao hununua china ila ubora wake ndo tatizo
 
Inaniuma sana tena kama nikiangalia hizo bati walizofanya kama uzio sehemu ujenzi unafanyika ni kama zangu walah zinang'a utadhani kila siku wanapaka rangi wakati zinafanana na zangu rangi hiyo hiyo yaani daaa!!!
Hii kitu hujagundua? Slope ya paa huchangia na kupauka haraka kwa bati, kwa hiyo usitegemee bati iliyosimama ya fensi kupauka haraka.

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
Ila kuna fundi rangi kaniambia kupaka inatumika fagio laini ndio inakole na akakazia kuwa nikitumia mashine eti zitajapauka tena.au ananipanga hivyo maana mashine hana ili alambe kazi
Ni sahihi kabisa, Tena tumia ule ufagio wa kudekia wenye muundo wa kama tambi za kuweka kwenye vibatari
 
Coils zote huwa zinakuja zikiwa zina rangi kabisa ila kinachotofautisha ni Ile thickness ya coating. Kuna baadhi ya makampuni Yao hata ukichubua kwa mkono tu rangi inatoka.
 
AlAF hazipauki mkuu
 
Wao Tanzania humiliki zile mashine za kuweka migongo kwa design mbalimbali lakini yale macoil wanaagiza china au South Africa kilichofanyika zamani macoil yalitengenezwa kwa ufanisi kuanzia nje lakini siku hizi hata wao wanalipua tu na vile tunapiga tu mabati bila kujua hali ya hewa ya eneo husika na ushauri wa kitaalamu hatupati ndio hivo mfano wa coils hizo ni [emoji1541][emoji1541]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…