Roho Mbaya na Wivu wa Majirani: Kisa cha mtoto aliyetambaa hadi ndani ya gari Arusha kitufundishe umuhimu wa CCTV

Roho Mbaya na Wivu wa Majirani: Kisa cha mtoto aliyetambaa hadi ndani ya gari Arusha kitufundishe umuhimu wa CCTV

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
376,316
Reaction score
871,876
,Kuna usemi usemao "Ndugu wa karibu ni jirani." Lakini kwa nyakati hizi tunazoishi, msemo huu unaanza kupoteza maana kwa kasi sana.

Leo hii majirani wamekuwa chanzo kikubwa cha maumivu, fitina, na roho mbaya za waziwazi, mara nyingi zikisababishwa na wivu wa maendeleo au chuki binafsi zisizo na miguu wala mikono.

Tukio la hivi karibuni lililotokea mkoani Arusha limestusha nchi nzima na limenifanya nitafakari sana kuhusu usalama wetu na familia zetu mitaani.

Ni kisa cha mtoto mlemavu aliyekuwa akitafutwa kwa udi na uvumba, na hatimaye akakutwa ndani ya gari la jirani.
Cha kushangaza na kusikitisha zaidi, huyo mtoto alitambaa na kuingia mwenyewe kwenye gari. Yaani bila uwepo wa kamera za usalama (CCTV), ukweli wa hili jambo lisingejulikana kabisa!. Mama wa watu angesingiziwa bure na kushitakiwa kwa kitu ambacho hajakifanya.

Kamera zimeokoa maisha ya watu wawili hapa: mtoto mkemavu na mama aliyekuwa anaenda kusingiziwa.

Binafsi nimejikuta nikitafakari maisha tunayoishi mitaani kwetu. Ukiishi kwa upole na unyenyekevu, majirani wakorofi wanakuona mnyonge na kuanza kukanyaga haki zako. Ukiamua kuwa mkali na kuweka mipaka, unaonekana una mdomo, una maringo, na unaharibu sifa yako kwenye jamii.

Naomba tujadili wakuu:Je, umeshawahi kukutana na jirani mwenye kiwango hiki cha roho mbaya au utata? Ulimnyoosha vipi akashika adabu yake?

Kuhusu teknolojia: Je, unadhani imefika wakati sasa hivi kufunga kamera za CCTV nyumbani isiwe tena anasa, bali iwe ni hitaji la lazima la usalama kwa kila familia (hata kama ni za bei nafuu)?

Mbinu gani ni bora zaidi mtaani? Ni kumkaushia kabisa jirani mkorofi na kumpotezea (silent treatment), au ni kupambana naye kisheria ili kuondoa uoga?


View: https://www.facebook.com/share/v/1CtdTiFuLM/
 
Masikini ndio tunashida za kufuatiliana n.k.
Mkikaa majirani wenye kujimudu kifedha kelele waga zinapungua. Kila mtu yupo bize na mishe zake, wanakutana inapobidi tuu.
Ujirani wa kuombana moto na chumvi ni shida.
 
Huyo mama ashukuru hizo camera
Kuna matukio mengi sana ya hivi yamekosa ushahidi wa camera
Wahusika wameishia kulia na Mungu.

Nani atakuamini?
Na binadamu walivyo sharp kuhukumu na kutunga fitina
Mwanzoni mwa hiki kisa nilimuona huyo mama ana matatizo sana. Ila baada ya ushahidi wa CCTV nimeishia kumhurumia.. Je ni wangapi wanapakaziwa na kuhukumiwa bila makosa?
 
kuna jirani hapa kijana wake (23 yrs) alimrubuni mtoto wa jirani yake (11yrs) akamwibie hela ndani, jirani alipogundua akamfuata kindugu wakamalizana akarudishiwa hela yake 40k, bado hyo kijana akaendelea kumrubuni mtoto na vitisho juu, mtoto akasema kwa wazazi wake, wazaz wakaenda kwa mtendaj wa mtaa kushtak, cha ajabu wale wazaz wakamtorosha mtoto, baada ya malumbano ofisini wakafunga njia(kujenga ukuta) inayopita kwenye eneo lao et kwa nini jiran kaenda kuwastaki hawataki apite kwenye eneo lao wakat njia ni ya jamii nzima, tumepambana nao mke wa jamaa ameonga mpaka kumery kwa mtenda il ukuta usivunjwe, baada ya kuona danadana kwa mtendaj kwa sasa shaur lipo baraza la ardhi na tutapambana nao mpaka ukuta uvunjwe.. mmmmke zao.g
 
Mwanzoni mwa hiki kisa nilimuona huyo mama ana matatizo sana. Ila baada ya ushahidi wa CCTV nimeishia kumhurumia.. Je ni wangapi wanapakaziwa na kuhukumiwa bila makosa?
Wapo wengi tu.
Imagine mahali kunapikwwa vyakula,halafu apite mtu mwenye Nia mbaya aweke sumu bila kuonekana
Msala unamuanagukia aliekuwa anapika kwamba kaua.kwa taharuki nani atamuelewa.
Na kama hakuna camera?
 
NI i
kuna jirani hapa kijana wake (23 yrs) alimrubuni mtoto wa jirani yake (11yrs) akamwibie hela ndani, jirani alipogundua akamfuata kindugu wakamalizana akarudishiwa hela yake 40k, bado hyo kijana akaendelea kumrubuni mtoto na vitisho juu, mtoto akasema kwa wazazi wake, wazaz wakaenda kwa mtendaj wa mtaa kushtak, cha ajabu wale wazaz wakamtorosha mtoto, baada ya malumbano ofisini wakafunga njia(kujenga ukuta) inayopita kwenye eneo lao et kwa nini jiran kaenda kuwastaki hawataki apite kwenye eneo lao wakat njia ni ya jamii nzima, tumepambana nao mke wa jamaa ameonga mpaka kumery kwa mtenda il ukuta usivunjwe, baada ya kuona danadana kwa mtendaj kwa sasa shaur lipo baraza la ardhi na tutapambana nao mpaka ukuta uvunjwe.. mmmmke zao.g
Ni ile video nimeona watu wanatumia ngazi kufika upande wa pili maana umejengwa ukuta njiani
 
Kwa mjini hasa uswahilini ni bora kuweka mipaka tu na majirani,unatakiwa uwe kauzu,mkorofi na mpenda ugomvi ili majirani wasikuzoee,wakikuzoea utakuwa wameingia ndani wamechukua unga na chupi za mkeo wamejaribisha. Pia ukiwa na kausafiri usiwe mwema sana kumpandisha kila jirani.
 
Back
Top Bottom