Roho ni nini? inaenda wapi baada ya kufa?

Pia unapoongelea uungu katika wakristo wa kweli Utatu Mtakatifu ni jambo la kuzingatia na linalofanya uungu wa Yesu kutokuwa wa kutilia shaka wala wa kuquestion.

Hii ni moja ya jambo la msingi sana katika Ukristo. Mwisho kama mwana wa binadamu ni binadamu kamili na mwana wa Mungu ni Mungu kamili.
 
Mkuu nahisi kuwa una shupaza shingo tu wakati ukweli uko wazi mbele yako jiulize kwanini Baba na Mama wakipata mtoto wanataka huyu mtoto husika awatii na kuwaheshimu na isitoshe mtoto anapoleta ukaidi kuna msemo tumezoea kuusikia kuwa nimekuzaa mimi na mimi ndo niliyekulea na pia kuwa tumbo miezi tisa nimekubeba hii inaonyesha ni jinsi gani ambavyo wazazi wanastahili kupewa heshima kwa sababu bila wao watoto wasingekuwepo yaani wao ndio waliowaleta ulimwenguni hivyo heshima yao lazima iwepo.

Sasa kama mzazi anapewa heshima hivi na anapewa hii heshima kwa sababu ndiye aliyemleta huyu mtoto ulimwenguni na pili ndiye aliyemtunza huyo mtoto yaani kamlea sasa je vipi Mungu aliyetuumba je hapaswi kuheshimiwa na je hapaswi kupewa utii kwa sababu Yeye ndiye aliyetuumba bila Yeye sisi tusingekuwepo na ni kwa uwezo wake mimi na wewe tupo hai hadi sasa je huyu Mungu hapaswi kuabudiwa na kupewa sifa na kutukuzwa kwa hiyo Yeye ndiye aliyetuumba na tunapaswa kumuabudu kwa sababu bila Yeye tusingelikuwepo
 
16 Na bila shaka siri ya utauwa ni kuu.Mungu alidhihirishwa katika mwili,Akajulika kuwa na haki katika roho,Akaonekana na malaika,Akahubiriwa katika mataifa,Akaaminiwa katika ulimwengu,Akachukuliwa juu katika utukufu.

1Timotheo3:16

Uungu wa Yesu unaweza ukauelewa taratibu kama ukitafakari na kutafiti...Hivi wamjua mfalme Melkizedecki ambae Ibrahim alimtolea fungu la kumi baada ya kutoka vitani

MWANZO14:18-19 umejaribu kumfuatilia kwa undani??
 
Uwepo wa Mungu hauondolewi na contradiction za viumbe wake.
Namna watu wanavyomtafsiri Mungu ni katika kiwango cha ufahamu wao ulipofikia.
Ni sawa na mtu aliyeliona sikio la tembo na asiuone mwili wote, kama akili yake haitamtuma kwamba kuna makuzi ya kielimu kuhusu kile anachokifahamu na kwamba upeo wake sii absolute basi atang'ag'ana kwa nguvu zote kwamba tembo ni lile sikio.

Kwamba mungu ana upendo wote? Maana ya upendo ni nini na umeipata wapi. Upendo wa Mungu ni kwenda chini ndio kwenda juu. Na utii ndio ithibaki. Wewe una namna yako ya kutafsiri upendo. Baba anaweza akawa anamchapa mtoto wake viboko kwa masahihisho na hili linasukumwa na upendo na mwingine akawa hamchapi pia kwa sababu ya upendo.
Contradiction itainuka pale mmoja kwa mwingine atakapotaka kuwa ile hatua yake ndio upendo na sii ile ya mwingine.

Mungu ameumba kila kitu kiwe kama kilivyo na anaufahamu mwisho wake tokea mwanzo. Ni sawa na mcheza sinema hachezi isipokua kwanza amelichora wazo la kile anachotaka kiwe na kwamba kuna hatua ipi itacchuka nafasi gani hadi hitimisho.

Mcheza sinema anaujua mwisho wa sinema yake tokea mwanzo wa kuanza kwake. Vivyo hivyo Mungu.
 
Baba na mama wanataka mtoto awatii kwa sababu hawana uwezo wakuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani.

Wanamwambia mtotowao "mwanetu, tusikilize, tutii. Usiibe, usiue.Utaishia pabaya. Tutii."

Mungu ambaye alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao kuiba na kuua hakuwezekani hata kufikirika maana hakupo, kwa nini aone haja ya kutaka utii ambao unakuja na kuwepo kwa mabaya mengi?

Angeumba dunia ambayo haina mabaya, ambayo haihitaji utii kwani haina uasi, angepungukiwa nini?
 
Unawezaje kuthibitisha kwamba Mungu yupo na si hadithi tu?

Sijaona ulipothibitisha Mungu yupo.

Unaanza kwa ksuema tu yupo. Thibitisha kwanza kabla ya kusema yupo.
 
Unawezaje kuthibitisha kwamba Mungu yupo na si hadithi tu?

Sijaona ulipothibitisha Mungu yupo.

Unaanza kwa ksuema tu yupo. Thibitisha kwanza kabla ya kusema yupo.
.
Kisayansi ni kwamba hakuna kitu cha kushikika kinachotokana na utupu.
Maumbile yanashika asili yake kwa mtizamo wako ni nini?
 
Ulimwengu unakufanyaje uamini Mungu?

Mbona unasema mambo unayaacha yanaelea elea hewani tu bila ufafanuzi kama mtu ambaye ana matatizo ya kujieleza vizuri?
Huu ulimwengu unanifanya nifikiri kuwepo kwa aliyeuumba na hapo ndipo imani ya uwepo wa mungu inapokuja.
 
.
Kisayansi ni kwamba hakuna kitu cha kushikika kinachotokana na utupu.
Maumbile yanashika asili yake kwa mtizamo wako ni nini?
Kama hakuna kitu cha kushikika kinachotokana na utupu, hilo linathibitishaje kwamba Mungu yupo?

Nauliza, unaweza kuthibitisha hii hela imewekwa mezani na Baba?

Unanijibu, kisayansi hakuna hela inayoweza kujiweka mezani yenyewe.

Jibu lako si la swali langu.
 
Huu ulimwengu unanifanya nifikiri kuwepo kwa aliyeuumba na hapo ndipo imani ya uwepo wa mungu inapokuja.
Kwa nini huu ulimwengu unakufanya ufikiri kuwepo kwa aliyeuumba?

Kwa nini ukufanye ufikiri "aliyeuumba" na si "kilichouumba" ?

Na kwa nini aliyeuumba ni lazima awe Mungu tu, na si kingine chochote?
 
Kwa nini huu ulimwengu unakufanya ufikiri kuwepo kwa aliyeuumba?

Kwa nini ukufanye ufikiri "aliyeuumba" na si "kilichouumba" ?

Na kwa nini aliyeuumba ni lazima awe Mungu tu, na si kingine chochote?
Hivyo ndivyo navyoamini na ndiyo imani yangu,hivyo kama unaona ni imani potofu unaweza kuonesha au kueleza upotofu wa hivyo navyoamini.
 
Hivyo ndivyo navyoamini na ndiyo imani yangu,hivyo kama unaona ni imani potofu unaweza kuonesha au kueleza upotofu wa hivyo navyoamini.
Hujajibu maswali.

Upotofu waimani yako ni kwamba unaamini bila sababu, nakuuliza, sababu zinazokufanya uamini hivyoni zipi, unajibu hivyo ndivyo unavyoamini.

Huna tofauti na anayesema yeye ndiye mzazi wa baba yake.

Ukimuuliza sababu gani inakufanya uamini hivyo, labda ana mantiki.

Anajibu hivyo ndivyo anavyoamini.

Mungu wako hayupo kwa sababu hana logical consistency.

Ana contradiction.
 
.
Wewe umekalia ubishi na sikulaumu kwa hilo maana ndiyo sehemu yako ya kufanya maisha yasonge.

Unaambiwa hakuna cha kushikika kutoka katika utupu unakuja na mfano usioendana kabisa.
Pesa kuwekwa au kutokuwekwa mezani kana uhusiano gani na material yaliyoitengeneza pesa? Nakuuliza tena, maombile ni ya kushikika mfano wa jua, sayari, wanyama nk. Asili yake ni nini?
 
Kama hujaelewa mfano, uliza.

Umesema hakuna kisichoshikika kilichotoka katika utupu.

Hilo halithibitishi kuwepokwa Mungu.

Kwa sababu, vinavyoshikika vilivyopo vinaweza kuwa havijatoka katika utupu, lakini pia havijatoka kwa Mungu.

Mfano wa hela iliyo mezaniunakujaje?

Kusema kwamba hakuna kinachoshikika ambacho hakijatoka kwenye utupu,ni sawa na kusema hakuna hela iliyo mezani iliyojiweka yenyewe mezani, lazima kutakuwa na namna iliyofanyika kuifanya hela iwe mezani.

Kufikiri kwamba ukisema hakuna kinachoshikika kinachotoka katika utupu ni uthibitisho wa kwamba kinachoshikika kimetoka kwa Mungu ni sawasawa na kusema ukiona hela imekaa mezani, lazima imewekwa na baba.

Inawezekana nyumba haina Baba, hela imewekwa mezani na mama.

Au nyumba haina baba, hela imewekwa mezani na mtoto.

Kwa nini unasemakwakuwa kuna hela mezani tu, basi hela imewekwa na baba?

Kwa nini unafikirikwa kuwa hakuna kinachoshikika kinachotoka katika utupu tu, na kinachoshikika kipo, basilazima kimetoka kwa Mungu?

Ndiyo maana nikakwambia, ukisema hakuna kinachoshikika kinachotoka katikautupu, hilo halithibitishi uwepo wa Mungu.
 
Naepusha kujadili mambo ambayo yameshajadiliwa sana,mimi nauelekeza mjadala tujadili vitu vipya ila naona ushazoea kurudia mambo yaleyale ili mwisho unaze kusema hakuna aliyeweza kuthibitisha kama kuna mungu.

Sababu zinazowafanya watu waamini zinajulikana hivyo sioni ulazima kuanza kulieleza kwa sana.

Na ndiyo maana nikakwambia kama unaona hii ni imani potofu basi onesha huo upotofu,maana imani ya mungu inajulikana.
 
Imani ya kuwepo kwa Mungu ni potofu kwa sababu inajipinga yenyewe. Ina contradictions.

Nimezitaja contradictions hapo juu,kamaunaweza kuziondoa, ziondoe.

The problem of evil is a big contradiction for an all knowing, all loving and allcapable Godhead.

This contradiction is not yet solved.

Because, such a God does not exist. he is fictitious.
 
Kwani Mungu alivyouumba ulimwenguni kulikuwa Kuna baya lolote si mpaka Adamu na Hawa walipokula tunda ndio mabaya yakajitokeza na kama wasingekula yaani wakatii mpango WA Mungu hayo mabaya si yasingekuwepo na unauliza kwanini aliweka vitu vingi at stake na hili linajibiwa kiurahisi Tu Kwa kuonyesha kuwa kumtii Mungu si jambo au swala Tu la maarifa ila kumtii kunampa mwanadamu uhai na kutokumtii Mungu muweza wa yote basi lazima kuwe na matokeo na matokeo yake Ni kifo.

Kwa hiyo swala la kumtii Mungu msingi wake upo kwenye uhai wa kiumbe husika kilichouumbwa yaani mwanadamu kwa kuwa kilichoumbwa hakiwezi kumuuliza Muumba mbona wafanya hivi na raha Ni kwamba mwanadamu alipewa uhuru na cha pili alipewa onyo kuwa akila atakufa kwa hiyo hili linaonyesha upendo wa ajabu na hata mabaya yalipoingia basi Yeye akaja kumkomboa mwanadamu kutoka katika dhambi hivi vyote vinaonyesha Upendo mkuu wa ajabu na Mungu sio dikteta mkuu bali Ni Upendo
 
Hiujaelewa swali langu si kwa nini ulimwengu una mabaya.

Hili si swali langu.

Swali langu ni, kwa nini Mungu kaumba ulimwengu ambao mabaya yanaweza kutokea wakati alikuwa ana uwezo wakuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezi kutokea.

Hjaelewa swali mpaka sasa.

Sishangai hujaweza kulijibu.

Mungu angeumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani, kutotii kusingewezekana kwa hivyo suala la utii lingekuwa moot.

Kwa nini hakuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani kabisa?
 
Hiyo akili yako ingewezaje kujua kuwa haya ni mazuri? Utajuaje mwanga bila Giza?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…