Roho ni nini? inaenda wapi baada ya kufa?

Roho ni nini? inaenda wapi baada ya kufa?

Mbona hata sasa hatuna uhuru wa kuchagua kurudi nyuma katika muda? Ningetaka kurudi 1982 nikae na wapendwa fulani waliofariki, lakini siwezi.

Utasemaje tumepewa uhuru wa kuchagua wakati hatuwezi kurudi nyuma katika muda?

Ukisema kunyimwa uhuru wa kuchagua ni kuwa ma robot, mbona sasa hatuwezi kurudi nyuma katika muda, kwa hiyo kwa kushindwa kurudi nyuma katika muda tunakuwa ma robot?

Mungu kwa nini hakuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani kama isivyowezekana kurudi nyuma katika muda?
.
Mimi naamini kuna Mungu, wewe unaamini hakuna mungu.
Nihakikishie wewe kwanza kwamba mungu hayupo ili iwe chachu ya mimi kukuhakikishia kinyume chake.

Kwanza mimi nasema Mungu ninaeamini yupo ndie hupanga yale yote yanayoendelea katika maumbile na kwamba sisi hatuna hiyari ya kuyafanya vinginevyo mf wa makuzi, kuzeeka na hatimae kufa.

Sasa wewe kama huamini yupo ambaye ndiye hupanga hayo tungetamni kuona kutokuwepo kwake kufanye hayo yaliyoamriwa kuwa kinyume chake. Laa kama hutaweza basi uliisha kusalimishwa kwake hata kama hukutaka kujisalimisha maana hili halipo katika hiari yako. Yeye ndie mmiliki wako.
 
4 amefanyika bora kupita malaika, kwa kadiri jina alilolirithi lilivyo tukufu kuliko lao.Mwana ni Mkuu kuliko Malaika

5 Kwa maana alimwambia malaika yupi wakati wo wote,Ndiwe mwanangu,Mimi leo nimekuzaa?Na tenaMimi nitakuwa kwake baba,Na yeye atakuwa kwangu mwana?

6 Hata tena, amletapo mzaliwa wa kwanza ulimwenguni, asema,Na wamsujudu malaika wote wa Mungu.

7 Na kwa habari za malaika asema,Afanyaye malaika wake kuwa pepo,Na watumishi wake kuwa miali ya moto.

8 Lakini kwa habari za Mwana asema,Kiti chako cha enzi, Mungu, ni cha milele na milele;Na fimbo ya ufalme wako ni fimbo ya adili.

9 Umependa haki, umechukia maasi;Kwa hiyo Mungu, Mungu wako, amekutia mafuta,Mafuta ya shangwe kupita wenzio.

10 Na tena,Wewe, Bwana, hapo mwanzo uliitia misingi ya nchi,Na mbingu ni kazi za mikono yako;

11 Hizo zitaharibika, bali wewe unadumu;Nazo zote zitachakaa kama nguo,

12 Na kama mavazi utazizinga, nazo zitabadilika;Lakini wewe u yeye yule,Na miaka yako haitakoma.

13 Je! Yuko malaika aliyemwambia wakati wo wote,Uketi mkono wangu wa kuumeHata nitakapoweka adui zako chini ya nyayo zako?

14 Je! Hao wote si roho watumikao, wakitumwa kuwahudumu wale watakaourithi wokovu?

Waebrania1:5-14. Ukielewa utamwelewa Yesu.

Yesu alipokimbilia kwenye Mlima wa Zaituni na huku akisakwa na Mayahudi alijitenga na wanafunzi wake. Huko faraghani aliomba hivi:

Ee Baba, ikiwa ni mapenzi yako, uniondolee kikombe hiki; walakini si mapenzi yangu, bali yako yatendeke. Malaika kutoka mbinguni akamtokea akamtia nguvu.

Luka 22.42-43

Hapa tunaona mambo matatu muhimu:

1. Yesu anamwomba Mungu. Yesu anamwabudu Mungu. Wawili hao ni mbali mbali, na vyeo vyao ni mbali mbali. Yesu ni mtumwa mnyonge mwenye kuomba na kuabudu. Na Mungu ni Mwenyezi Mungu mwenye uwezo wote na mwenye kustahiki kuabudiwa pekee, hata na Yesu, mwenye kutakiwa msaada pekee, hata na Yesu.

2. Mapenzi ya Mungu ni mbali na yale ya Yesu. Yesu hataki kuuliwa, ananyenyekea na kuomba kwa Bwana wake: "uniondolee kikombe hiki" cha mauti. Yesu hana azma hata chembe ya kufa msalabani, kifo cha mhalifu, kifo cha laana kama maadui zake Mayahudi walivyoazimia kumpatilisha nacho. Lakini anakiri kuwa ni mapenzi ya Mungu sio yake yeye yatendeke. Yeye hana hila wala nguvu za kuzuia kudra ya Mwenyezi Mungu.

3. Yesu, Mwana wa Adamu, anakata tamaa. Imani inampunguka. Kavunjika moyo. Ikabidi "Malaika kutoka mbinguni akamtokea akamtia nguvu."

Jee, yaelekea kuwa Yesu ndiye Mungu? Yaelekea kuwa yeye na Mungu kuwa ni sawa? Kama upo wasiwasi wo wote wa kujibu hayo, mwenyewe Yesu anajibu kama anavyo hadithiwa na Yohana kuwa kasema:

Baba ni mkuu kuliko mimi.

Yohana 14.28

Na mwishoni naye yupo mslabani:

Na kama saa tisa, Yesu akapaza sauti yake kwa nguvu akisema, Eloi, Eloi, lama sabakthani? yaani, Mungu wangu, Mungu wangu, Mbona umeniacha?

Mathayo 27.46
Yafaa hapa tujiulize: Yesu akimlilia Mungu gani hapo msalabani ikiwa naye mwenyewe ni Mungu? Au nini alikusudia aliposema: "Mungu wangu naye ni Mungu wenu"?Maneno hayo kama yanaonyesha cho chote basi yanaonyesha unyenyekevu wa Yesu mbele ya Mungu wake. La kustaajabisha ni kule kukata tamaa kwake na kuvunjika moyo.

Huwaje mtu wa imani, licha ya nabii na mwana pekee wa Mungu, akate tamaa na rehema ya Mwenyezi Mungu. Ama kuwa Mungu akate tamaa na Mungu, na kumyayatikia: "Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha", ni jambo ambalo halimkiniki kuwa.
Kwa uthibitisho ulio wazi Biblia inatwambia kuwa Yesu si Mungu, wala Mungu si Yesu.
 
samahani! Wewe mkristo wa dhehebu gani ambao wanafundisha kuwa Yesu ni binadamu?
Ha ha ha ...wewe hufuati maandiko ya kitabu u achokiamini, unafuata dhehebu!!!??? kanisa!!! ulishawahi kushika biblia ukasoma mwenyewe?

JE! MUNGU NA YESU NI MMOJA?

6- JE! MUNGU NA YESU NI MMOJA?

Makanisa ya Kikristo yanafunza ya kuwa Yesu Kristo si kama kuwa ni Mwana wa Mungu tu, bali hakika ni Mungu khasa.

Baba, Mwana na Roho Mtakatifu ni mmoja. Watatu katika mmoja, na mmoja katika watatu. Wote ni wa milele, wote ni sawa. Yesu ni Mungu, na Mungu ni Yesu. Hiyo ni imani ya Kikristo, ambayo inaaminiwa na karibu Wakristo wote.

Hebu tuifunue Biblia tutazame inasema nini katika jambo hili? Mt Paulo katika barua yake ya kwanza kuwapelekea Wakorintho aliandika. Naam, na sisi tumeonekana kuwa mashahidi wa uongo wa Mungu; kwa maana tulimshuhudia Mungu ya kuwa alimfufua Kristo, ambaye hakumfufua, ikiwa wafu hawafufuliwi.

1 Wakorintho 15.15

Juu ya kuwa Paulo anaambiwa ya kuwa akiamini kuwa Masihi (yaani Kristo) na Mwenyezi Mungu ni kitu kimoja hapa anasema: "Tulimshuhudia Mungu ya kuwa alimfufua Kristo." Ikiwa Mungu kamfufua Kristo, hawawezi kuwa wote wawili hao ni mtu mmoja. Mmoja alikuwa ni mtenda, mfufuaji, na wa pili alikuwa ni mtendwa, mfufuliwa. Kama Kristo ni Mungu mwenye uwezo wa kufufua basi maelekeo ni kusema: "Kristo kajifufua", sio kafufuliwa. Mwenye kufufuliwa ni mfu asiyejiweza kitu.

Katika kitabu cha Matendo ya Mitume inasimuliwa kuwa Mt Stefano alisema aliyoyaona yaliyo mbinguni.

Alisema:

Tazama! naona mbingu zimefunguka, na Mwana wa Adamu amesimama mkono wa kuume wa Mungu.

Matendo 7.56

Mwana wa Adamu ndiye Yesu, na kwa jina hilo ndio mwenyewe akipenda kujiita, sio Mwana wa Mungu. Hapo basi huko mbinguni Stefano anasema anamwona Yesu kakaa mkono wa kulia wa Mungu. Mwenye kukaa mkono wa kulia wa fulani hawezi kuwa ndiye yule yule fulani. Hayo ni maelezo ya mbinguni. Ni wazi basi kwa ushahidi wa Biblia kuwa Yesu hakuwa Mungu mbinguni kama alivyokuwa si Mungu duniani.

Yesu alipokimbilia kwenye Mlima wa Zaituni na huku akisakwa na Mayahudi alijitenga na wanafunzi wake. Huko faraghani aliomba hivi:

Ee Baba, ikiwa ni mapenzi yako, uniondolee kikombe hiki; walakini si mapenzi yangu, bali yako yatendeke. Malaika kutoka mbinguni akamtokea akamtia nguvu.

Luka 22.42-43

Hapa tunaona mambo matatu muhimu:

1. Yesu anamwomba Mungu. Yesu anamwabudu Mungu. Wawili hao ni mbali mbali, na vyeo vyao ni mbali mbali. Yesu ni mtumwa mnyonge mwenye kuomba na kuabudu. Na Mungu ni Mwenyezi Mungu mwenye uwezo wote na mwenye kustahiki kuabudiwa pekee, hata na Yesu, mwenye kutakiwa msaada pekee, hata na Yesu.

2. Mapenzi ya Mungu ni mbali na yale ya Yesu. Yesu hataki kuuliwa, ananyenyekea na kuomba kwa Bwana wake: "uniondolee kikombe hiki" cha mauti. Yesu hana azma hata chembe ya kufa msalabani, kifo cha mhalifu, kifo cha laana kama maadui zake Mayahudi walivyoazimia kumpatilisha nacho. Lakini anakiri kuwa ni mapenzi ya Mungu sio yake yeye yatendeke. Yeye hana hila wala nguvu za kuzuia kudra ya Mwenyezi Mungu.

3. Yesu, Mwana wa Adamu, anakata tamaa. Imani inampunguka. Kavunjika moyo. Ikabidi "Malaika kutoka mbinguni akamtokea akamtia nguvu."

Jee, yaelekea kuwa Yesu ndiye Mungu? Yaelekea kuwa yeye na Mungu kuwa ni sawa? Kama upo wasiwasi wo wote wa kujibu hayo, mwenyewe Yesu anajibu kama anavyo hadithiwa na Yohana kuwa kasema:

Baba ni mkuu kuliko mimi.

Yohana 14.28

Na mwishoni naye yupo mslabani:

Na kama saa tisa, Yesu akapaza sauti yake kwa nguvu akisema, Eloi, Eloi, lama sabakthani? yaani, Mungu wangu, Mungu wangu, Mbona umeniacha?

Mathayo 27.46

Yafaa hapa tujiulize: Yesu akimlilia Mungu gani hapo msalabani ikiwa naye mwenyewe ni Mungu? Au nini alikusudia aliposema: "Mungu wangu naye ni Mungu wenu"?Maneno hayo kama yanaonyesha cho chote basi yanaonyesha unyenyekevu wa Yesu mbele ya Mungu wake. La kustaajabisha ni kule kukata tamaa kwake na kuvunjika moyo.

Huwaje mtu wa imani, licha ya nabii na mwana pekee wa Mungu, akate tamaa na rehema ya Mwenyezi Mungu. Ama kuwa Mungu akate tamaa na Mungu, na kumyayatikia: "Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha", ni jambo ambalo halimkiniki kuwa.
Kwa uthibitisho ulio wazi Biblia inatwambia kuwa Yesu si Mungu, wala Mungu si Yesu.
 
.
Mimi naamini kuna Mungu, wewe unaamini hakuna mungu.

Imani haina shurutiwala nguvu,unaruhusiwa kuamini chochote,kuna "Universal Declarationof Human Rights"inatetea haki yako ya kuamini, mradi usivunje sheria tu. Katiba ya Tanzania inatoa Uhuru wa kuamini, sina nia ya kujadili imani.

Nina nia ya kujadili ukweli.

Vitu viwili tofauti.

Nihakikishie wewe kwanza kwamba mungu hayupo ili iwe chachu ya mimi kukuhakikishia kinyume chake.

Kisichopo hakiwezi kuthibitishwa kwa uhakika, kwa sababu hakipo.

Kama umeibiwa, mwizi kavunja dirisha lako kaingia ndani mwako, kashika kitasa kwa ndani, kafungua mlango, kaiba, wakija wataalamwa polisi wataweza kuona alama za vidole za mwizi.

Lakini, kama hakuna mwizi aliyeingia utathibitishaje kwamba hakuna mwizi aliyeingia?

Utasema hizi hapa alamaza vidole za mwizi ambaye hajaingia ndani humu?

Ukichunguza utaona,nje ya logical analysis, kuthibitisha kisichopo kwamba hakipo hakuwezekani.

Kwa sababu hakipo ili kithibitishwe kwamba hakipo.

Uthibitisho wa logicalanalysis nimeutoa hapojuu,proof by contradiction. Soma.

Kwanza mimi nasema Mungu ninaeamini yupo ndie hupanga yale yote yanayoendelea katika maumbile na kwamba sisi hatuna hiyari ya kuyafanya vinginevyo mf wa makuzi, kuzeeka na hatimae kufa.

Kufa hakuthibitishi Mungu yupo, kufa kunathibitisha Mungu hayupo.

Kwa nini?

Mnasema Mungu anauwezo wote, ujuzi wote na upendo wote.

Mwenye ujuzi wote,uwezo wote na upendo wote, anatakiwa kuwa na nature ya kutotaka kuwatenganisha viumbe wake wanaopendana.

Kifo kinatenganisha vumbe wanaopendana.

Hivyo, kifo ni ushahidi kwamba Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote hayupo.

Angekuwepo asingeruhusu kifo kiwezekane katikaulimwengu wake.
Sasa wewe kama huamini yupo ambaye ndiye hupanga hayo tungetamni kuona kutokuwepo kwake kufanye hayo yaliyoamriwa kuwa kinyume chake.

Suala si kuamini, suala ni kuthibitisha.

Unaweza kuthibitisha Mungu yupo?

Laa kama hutaweza basi uliisha kusalimishwa kwake hata kama hukutaka kujisalimisha maana hili halipo katika hiari yako. Yeye ndie mmiliki wako.

Kabla ya kufika kote huko, unaweza kuthibitisha Mungu yupo?
 
Mkuu Alwatan habari yako, mkuu huwezi jifunza jambo kwa watu wasio na ujuzi na jambo hilo zaidi itakuwa ni mabishano yasiyo na tija,michango itolewayo humu kuhusiana na swali lako haikidhi kiu yako ya jibu.
Nilikushauri na pia narudia tena kama unataka elimu kuhusu majambo haya haswa kwa upande wa uislam basi wako wanachuoni wenye elimu juu ya haya mambo, kinyume cha hapo ni mabishano yasiyo na tija na ukomo pia
Huyo hataki kuelewa swali lake limejibiwa vizur na clip niliyompa ...hajaisikiliza na kuielewa anarudia swali lilelile thread nzima!!!
 
Na jua linaweza kupiga supernovae leo lisichomoze kesho.

Kushindwa kuthibitisha kitu kama kipo au hakipo hakuoneshi lolote kuhusu kuwapo au kutokuwapo hicho kitu.

Unaweza kushindwa kuthibitisha kitu kipo, kwa kitu ambacho hakipo.

Unaweza kushindwa kuthibitisha kitu kipo, kwa kitu ambacho kipo.

Kwa hiyo kushindwa kuthibitisha kitu hakuna maana yoyote.

Ukitaka kujua kitu kipo, njai pekee ya kujua kwa hakika, ni kuthibitisha kwamba kipo.

Ndiyo maana nakuuliza, unaweza kuthibitisha Mungu yupo?

Kamaunaweza, thibitisha.

Na ukishindwa, unajuaje kwamba yupo, umeshindwa kuthibitisha tu kwamba yupo, na si kwamba hayupo na umeshindwa kuthibitisha yupo kwa sababu hayupo?
Hatuwezi kuthibitisha kuwa jua litachomoza kesho au halitachomoza,hivyo hatuna jinsi ila ni kuisubiri tu kesho.

Na suala la uwepo wa mungu nalo pia mwisho wa siku tutaweza kujua kiuhakika kuwa ni kweli yupo au hayupo.
 
Kwa hiyo unakubali kwamba kwa sasa huna uhakika?
 
Nyie mawazo yenu ni nchi kufikirika ...Kuwa mkristo pekee haitosha kujua Yesu Ni Mungu au la
 
Sawa, sinatatizo na imani, nina tatizo na imani potofu.

Hata ukipanga mkutano wa kesho, unapanga kwa imani.Unaamini kesho itakuwepo, jua litachomoza,hutafariki usiku wa leo. Hiyo yote ni imani. Bila imani hatuwezi hata kupanga mambo ya kesho.

Sina tatizo na imani, nina tatizo na imani potofu.

Kama imani, Chidi Benz ana imani kwamba ametoa nyimbo na wasanii wakubwa kina Rihanna na 2Pac.

Hiyo ni imani pia.

Na anaweza kukwambia u prove kwamba hajatoa hizo nyimbo, ukashindwa ku prove.

Lakini kumbe imani hiyo ni potofu, Chidi Benz hajatoa nyimbo hizo.

Sasa, utajuaje kwamba imani yako wewe ni sahihi, Mungu yupo, na si imani potofu kama ya Chidi Benz, kwamba unaamini Mungu yupo wakati hayupo?
Kwanza la suala Chid Benz sio la imani na hata mwishoni alisema ni ulikuwa utani.

Hata hivyo tulipofika ni pazuri,kwanza moja ya jambo linalonifanya niamini mungu ni huu ulimwengu(hili linaelezwa sana) hivyo ukiliangalia hilo suala ni wazi imani yangu ya kuwepo mungu naona ni sahihi kabisa.
 
Ulimwengu unakufanyaje uamini Mungu?

Mbona unasema mambo unayaacha yanaelea elea hewani tu bila ufafanuzi kama mtu ambaye ana matatizo ya kujieleza vizuri?
 
Yesu alipozaliwa na mwanamke lengo lilikuwa kuuvaa mwili wa duniani kwa sababu yeye ni roho..Na ili uweze kukaa na kumudu mazingira ya dunia lazima uwe na mwili wa mnyama,,binadamu,,ndege,,mdudu au bacteria nk.The same baharini lazima pia uwe na mwili wa samaki au viumbe wa baharini...Kwa kuwa Yesu ni Roho na anaeishi katika mbingu ambayo ndiko makao na makazi ya roho,,,hapa duniani ilim,,bidi kuvaa mwili ili awe na ufananio na viumbe wa realm hii ya dunia,,,chek (Waebrania 10:5)) Ukisoma vizuri utaona anauongelea mwili akiwa nje ya mwili

"""Kwa hio ajapo ulimwenguni asema,Dhabihu na toleo hukutaka,,lakini mwili uliniwekea tayari."""" Kwa kufikiria deeply utaelewa kwamba Yesu angelikuwa ndani ya mwili asingeongea maneno hayo.Alikuwa kwenye realm ya uhalisia wake nje ya mwili.
Asante
 
Damu itamwagika hapa [emoji124] [emoji124] [emoji124] [emoji124] [emoji124] [emoji124]
 
Unajichanganya.

Kwa nini Mungu hakuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani kuwepo kama alivyoumba ulimwengu ambao time travel haiwezekani?

Hujajibu swali hili.

Ukisema habari za uhuru aliopewa mtu,hilo si jibu.

Baba hampi mtoto wake mchanga asiye na akili pevu maziwa na sumu, ili tu mtoto awe na uhuru wa kuchagua kunywa maziwa aishi au sumu afe.

Huyo baba akifanya hivyo, kisha mtoto akachagua sumu na kufa, atashitakiwa na kufungwa.

Sasa kwa nini Mungu ambaye alikuwa na uwezo wa kutupa viumbe vyake maziwa tu, asitupe sumu kabisa, kwa nini katupa maziwa na sumu?

Kwa nini tumuhukumu huyu baba mwenye uwezo wenye mwisho, upendo wenye mwisho na ujuzi wenye mwisho hukumu mbaya, wakati mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote tunamsifu kwa kufanya kitu kile kile?

Naona tumefika kwenye point ambayo tunaanza kuelewana na ninaomba niende na wewe hatua kwa hatua kwanza swali ulilolileta la kwanza nishalijibu lakini naona bado hatujaelewana basi narudia tena Mungu aliuumba ulimwengu mkamilifu usio na taabu, kifo wala njaa na Alipanga mwanadamu autawale huu ulimwengu hayo mabaya unayoyasema yaani Mungu Aliuumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana ili swali linajibiwa kwa muktadha huu kwamba Mungu alitaka mwanadamu amtii na amheshimu na amuabudu na haya yote yangewezekana kama mwanadamu angelichagua kwa moyo wake mwenyewe kumtii kumheshimu na kumuabudu na tofauti na hapo yaani Mungu angemuumba mwanadamu ambaye anayohulka ya kumtii Mungu ya asili ambayo ni tofauti na moyo wa mwanadamu unavyochagua basi tungemuabudu Mungu kwa shuruti yaani sio kwa mapenzi yetu wenyewe bali kwa sababu ametufanya tumuabudu.

Hapo ndipo Mungu akaamua kumpa mwanadamu free will ambayo ilimpa mwanadamu uwezo wa kuamua sasa ilibidi hii free will ipimwe kuwa je mwanadamu kweli atachagua kumtii Mungu kwa hiari yake mwenyewe na kumbuka hii hiari tayari alikuwa ameshapewa na Mungu ndipo basi mti wa mema na mabaya unapoingia ambapo uliwekwa ili kutathimini kama mwanadamu atatii maagizo ya Mungu kwa kuwa hiari au free will tayari anayo. Hapa tunaona baada ya Mungu kumpa onyo mwanadamu kuwa usile lile tunda na akampa na sababu kuwa ukila hilo tunda basi Hakika utakufa ndipo mtihani sasa wa kutathimini kama mwanadamu atamtii Mungu au atatii maagizo aliopewa na Mungu ukaanza na tunaona kuwa mwisho wa siku mwanadamu akakaidi maagizo ya Mungu na ndipo sasa dhambi inaingia ulimwenguni na kifo kinaingia ulimwenguni na hapo ndipo sasa mabaya yanaingia ulimwenguni.

Na swala la mabaya kuwezekana ni conditional kwa sababu mwanadamu angelichagua kumtii Mungu na kutii maagizo yake basi mabaya yasingekuwepo na huu ndio uliokuwa mpango wa Mungu kuwa mwanadamu amtii bila shuruti bila kulazimisha bali kwa maamuzi yake mwenyewe na tunaona kumbe baada ya ukaidi wa mwanadamu dhidi ya sheria ya Mungu ndipo mabaya yakawezekana ndio maana haya yote yalikuwa yameshikiliwa na free will kama tungelichagua kumtii Mungu basi hadi sasa tungelikuwa na ulimwengu ambao mabaya yasingelikuwepo lakini kisa ukaidi wetu ndio maana ulimwenguni mabaya yanawezekana na sio mpango wa Mungu mkuu.

Na pia inabidi ujue kuwa Adamu hakuwa mtoto bali aliuumbwa bali aliuumbwa mtu mzima kamili mwenye uelewa ndio maana alikuwa ana uhuru wa kuchagua na wa kuamua kwa hiari yake mwenyewe na mtoto hana hicho kitu hana hiari au uwezo wa kuchagua ndio maana Adamu na Hawa wote walikuwa wanaujua mti ule wa mema na mabaya uko wapi na ukoje unafanana vipi ili watakapokula wasije wakaleta kisingizio kuwa tuliufananisha.

Kwa hiyo mfano wako hauna mhimili na kama ungetaka uwe na mhimili ungeuweka hivi kama Baba yako na nna litumia hili jina kwa heshima zote angelikuwa anataka kupima kama unamheshimu na unamtii angechukua glasi mbili za maziwa moja ikiwa ina maziwa tu na nyingine ikiwa ina maziwa na sumu ndani yake na akakuonyesha wewe (na nnasema wewe nikiwa namaanisha kuwa una uwezo wa kujua kuwa haya ni maziwa na pili una uwezo wa kuchagua kunywa au kutokunywa yaani hiari au free will) na kukuambia kuwa maziwa kwenye glasi hii ya kwanza (tuiite glasi A) unaweza kunywa lakini maziwa kwenye glasi hii ya pili yaani glasi B usinywe maana siku utakapokunywa haya maziwa Hakika utakufa.

Je wewe ukienda kunywa maziwa kutoka kwenye glasi B huoni kuwa utakuwa hujamtii na cha pili kuwa utakufa maana ina sumu ndani yake na isitoshe ulikuwa na uhuru wa kuchagua yaani hiari au free will ya kunywa au kutokunywa na juu ya hilo kulikuwa na glasi A ya maziwa ambayo uliruhusiwa kunywa wewe huoni kama utakuwa umedharau maagizo ya Baba yako na umekaidi alichokuambia na pia inaonyesha humtii wala humheshimu.

Sijui tunaelewana mkuu.
 
Naona tumefika kwenye point ambayo tunaanza kuelewana na ninaomba niende na wewe hatua kwa hatua kwanza swali ulilolileta la kwanza nishalijibu

Swali ulilolijibu ni lipi?

lakini naona bado hatujaelewana basi narudia tena Mungu aliuumba ulimwengu mkamilifu usio na taabu, kifo wala njaa na Alipanga mwanadamu autawale huu ulimwengu hayo mabaya unayoyasema yaani Mungu Aliuumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana ili swali linajibiwa kwa muktadha huu kwamba Mungu alitaka mwanadamu amtii na amheshimu na amuabudu

Kwanini ni muhimusana kwa Mungu huyu kuwa na mwanadamu anayemtii na kumuabudu?

Manasema Mungu mkubwa sana kwa uwezo, ujuzi etc, kwa nini ni muhimu sana mwanadamu amuabudu Mungu huyu?

Huyu Mungu hana mambo muhimu zaidi ya kufanya kuliko kutakakuabudiwa na mwanadamu kama rais dikteta anayependa kupigiwa makofi na wananchi masikini?

na haya yote yangewezekana kama mwanadamu angelichagua kwa moyo wake mwenyewe kumtii kumheshimu na kumuabudu na tofauti na hapo yaani Mungu angemuumba mwanadamu ambaye anayohulka ya kumtii Mungu ya asili ambayo ni tofauti na moyo wa mwanadamu unavyochagua basi tungemuabudu Mungu kwa shuruti yaani sio kwa mapenzi yetu wenyewe bali kwa sababu ametufanya tumuabudu.

Mungu angeumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani, mwanadamu ana uwezo wa kuchagua mazuri tu, angepungukiwa na nini?

Mungu anapenda kuabudiwa kiasi kwamba ameona ni sawa ulimwengu uweze kuwa na mabaya yote haya ili yeye aabudiwe tu?

Huyo ni Mungu mwenye upendo kweli?

Baba anampa mtoto mdogo asiye na akili pevu uamuzi wa kunywa maziwa au sumu, ili kusudi apate fahari tu kwamba mtoto anamsikiliza baba, wakati angeweza kuondoa sumu, mtoto anywe maziwa tu wala asipata nafasi ya kunywa sumu.

Huyu Baba utamsifia useme ana upendo?

Hapo ndipo Mungu akaamua kumpa mwanadamu free will

Tushaona mwanadamu hana free will, hawezi hata kurudi nyuma katika muda aende kupiga story na mama yake aliyefariki 1982.

Kwa hiyo habari za fee will ni uongo. Pia,vitabu vya dini vinasema tunamjua Mungu kwa neema zake tu, si kwa jitihada zetu. Hapo hamna free will. Wanaomjua Mungu hawamjuikwa sababu wamejitahidi kumjua, bali kwa sababu yeye amewachagua wamjue,sasa kwa msingi huo, free will iko wapi?

ambayo ilimpa mwanadamu uwezo wa kuamua sasa ilibidi hii free will ipimwe kuwa je mwanadamu kweli atachagua kumtii Mungu kwa hiari yake mwenyewe na kumbuka hii hiari tayari alikuwa ameshapewa na Mungu ndipo basi mti wa mema na mabaya unapoingia ambapo uliwekwa ili kutathimini kama mwanadamu atatii maagizo ya Mungu kwa kuwa hiari au free will tayari anayo.

Vitabu vya Mungu vinasema tunaokokakwa neema (Biblia). Quran inasema kuna watu Mungu atafanya mioyo yaoiwe migumu wasimjue Allah, hawa hata wakijitahidi vipi hawatamjua Allah, kwa sababu Allah mwenyewe atakuwa kaifanya mioyo yaoiwemigumu kumjua.

Sasa hawa wana free will gani?

Hapa tunaona baada ya Mungu kumpa onyo mwanadamu kuwa usile lile tunda na akampa na sababu kuwa ukila hilo tunda basi Hakika utakufa ndipo mtihani sasa wa kutathimini kama mwanadamu atamtii Mungu au atatii maagizo aliopewa na Mungu ukaanza na tunaona kuwa mwisho wa siku mwanadamu akakaidi maagizo ya Mungu na ndipo sasa dhambi inaingia ulimwenguni na kifo kinaingia ulimwenguni na hapo ndipo sasa mabaya yanaingia ulimwenguni.

Kwa nini baba mwenye uwezo wakumpa mwanawe maziwa tu, anywe ashibe, anampa uamuzi wa kuchagua maziwa anywe ashibe au sumu anywe afe?

Baba akitoa uchaguzi huo kwa mtoto ambaye hana akilipevu, utasema baba huyo ana upendo kweli?

Na swala la mabaya kuwezekana ni conditional kwa sababu mwanadamu angelichagua kumtii Mungu na kutii maagizo yake basi mabaya yasingekuwepo na huu ndio uliokuwa mpango wa Mungu kuwa mwanadamu amtii bila shuruti bila kulazimisha bali kwa maamuzi yake mwenyewe na tunaona kumbe baada ya ukaidi wa mwanadamu dhidi ya sheria ya Mungu ndipo mabaya yakawezekana ndio maana haya yote yalikuwa yameshikiliwa na free will kama tungelichagua kumtii Mungu basi hadi sasa tungelikuwa na ulimwengu ambao mabaya yasingelikuwepo lakini kisa ukaidi wetu ndio maana ulimwenguni mabaya yanawezekana na sio mpango wa Mungu mkuu.

Kwa nini baba mwenye uwezo wakumpa mwanawe maziwa tu, anywe ashibe, anampa uamuzi wa kuchagua maziwa anywe ashibe au sumu anywe afe?

Baba akitoa uchaguzi huo kwa mtoto ambaye hana akilipevu, utasema baba huyo ana upendo kweli?

Na pia inabidi ujue kuwa Adamu hakuwa mtoto bali aliuumbwa bali aliuumbwa mtu mzima kamili mwenye uelewa ndio maana alikuwa ana uhuru wa kuchagua na wa kuamua kwa hiari yake mwenyewe na mtoto hana hicho kitu hana hiari au uwezo wa kuchagua ndio maana Adamu na Hawa wote walikuwa wanaujua mti ule wa mema na mabaya uko wapi na ukoje unafanana vipi ili watakapokula wasije wakaleta kisingizio kuwa tuliufananisha. Kwa hiyo mfano wako hauna mhimili na kama ungetaka uwe na mhimili ungeuweka hivi kama Baba yako na nna litumia hili jina kwa heshima zote angelikuwa anataka kupima kama unamheshimu na unamtii angechukua glasi mbili za maziwa moja ikiwa ina maziwa tu na nyingine ikiwa ina maziwa na sumu ndani yake na akakuonyesha wewe (na nnasema wewe nikiwa namaanisha kuwa una uwezo wa kujua kuwa haya ni maziwa na pili una uwezo wa kuchagua kunywa au kutokunywa yaani hiari au free will) na kukuambia kuwa maziwa kwenye glasi hii ya kwanza (tuiite glasi A) unaweza kunywa lakini maziwa kwenye glasi hii ya pili yaani glasi B usinywe maana siku utakapokunywa haya maziwa Hakika utakufa.
Je wewe ukienda kunywa maziwa kutoka kwenye glasi B huoni kuwa utakuwa hujamtii na cha pili kuwa utakufa maana ina sumu ndani yake na isitoshe ulikuwa na uhuru wa kuchagua yaani hiari au free will ya kunywa au kutokunywa na juu ya hilo kulikuwa na glasi A ya maziwa ambayo uliruhusiwa kunywa wewe huoni kama utakuwa umedharau maagizo ya Baba yako na umekaidi alichokuambia na pia inaonyesha humtii wala humheshimu.
Sijui tunaelewana mkuu.

Obviously huyo Adam hakuwa na akilipevu ndiyo maana akashawishika.

Kwa nini Mungu mwenye ujuzi wote, uwezo wote na upendo wote alimpa uchaguzi wa mema na mabaya Adam wakati alikuwa na uwezo wa kumpauchaguzi wa mema tu katika dunia ambayo mabaya hayawezekani?

Hujajibu swali hili.

Ukisema alitaka wanadamu wawe watii, utii unamuongezea nini Mungu? Kwa nini anapenda utii ambao unakuja na mabaya mengi sana?

Unaweza kumpa mwanao sumu apate chance ya kufa ili upate ufahari tu kwamba asipokunywa sumu ni mtii?

Mbona ukiwa baba kama huyo mwanadamu utaitwa katili? Mungu wenu katili?
 
Imani haina shurutiwala nguvu,unaruhusiwa kuamini chochote,kuna "Universal Declarationof Human Rights"inatetea haki yako ya kuamini, mradi usivunje sheria tu. Katiba ya Tanzania inatoa Uhuru wa kuamini, sina nia ya kujadili imani.

Nina nia ya kujadili ukweli.

Vitu viwili tofauti.

Kisichopo hakiwezi kuthibitishwa kwa uhakika, kwa sababu hakipo.

Kama umeibiwa, mwizi kavunja dirisha lako kaingia ndani mwako, kashika kitasa kwa ndani, kafungua mlango, kaiba, wakija wataalamwa polisi wataweza kuona alama za vidole za mwizi.

Lakini, kama hakuna mwizi aliyeingia utathibitishaje kwamba hakuna mwizi aliyeingia?

Utasema hizi hapa alamaza vidole za mwizi ambaye hajaingia ndani humu?

Ukichunguza utaona,nje ya logical analysis, kuthibitisha kisichopo kwamba hakipo hakuwezekani.

Kwa sababu hakipo ili kithibitishwe kwamba hakipo.

Uthibitisho wa logicalanalysis nimeutoa hapojuu,proof by contradiction. Soma.

Kufa hakuthibitishi Mungu yupo, kufa kunathibitisha Mungu hayupo.

Kwa nini?

Mnasema Mungu anauwezo wote, ujuzi wote na upendo wote.

Mwenye ujuzi wote,uwezo wote na upendo wote, anatakiwa kuwa na nature ya kutotaka kuwatenganisha viumbe wake wanaopendana.

Kifo kinatenganisha vumbe wanaopendana.

Hivyo, kifo ni ushahidi kwamba Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote hayupo.

Angekuwepo asingeruhusu kifo kiwezekane katikaulimwengu wake.

Suala si kuamini, suala ni kuthibitisha.

Unaweza kuthibitisha Mungu yupo?

Kabla ya kufika kote huko, unaweza kuthibitisha Mungu yupo?
.
Hakuna anaeshurutisha imani na ndio maana hata wewe umebaki huru katika imani yako ya kutokuwepo Mungu.

Basi kama unakiri kwamba huna shaka na swala la imani ila ku proof imani iliyo kweli ndipo nikakutaka wewe unipe proof ya imani yako ya kutokuwepo Mungu.

Kama huna uwezo wa ku proof kwa nini wewe umtake anaeamini uwepo wake ku proof?
 
Masahihisho kidogo. Sio nabii Nathan, bali ni nabii Samuel. Na maandiko hayasemi kuwa roho iliyoongea na Sauli ilukuwa ya shetani. Alikuwa ni Samweli mwenyewe. Fuata maandiko yanavyosema, sio mawazo ya watu wa theolojia. Kama shetani alimpandisha Bw. Yesu juu ya mnara wakati alipojaribiwa na shetani unaonaje isiwezekane mchawi wa Endori kupandisha kivuli cha nabii Samweli?.
Kwa mimi ninavyoelewa hapa ni kwamba yule mwanamke mpunga pepo alitumia pepo la utambuzi kumpasha mfalme Sauli habari ya mambo yatakayo tokea. Japo shetani anao uwezo wa kumpatia mtu maono.
 
.
Hakuna anaeshurutisha imani na ndio maana hata wewe umebaki huru katika imani yako ya kutokuwepo mungu.
Basi kama unakiri kwamba huna shaka na swala la imani ila ku proof imani iliyo kweli ndipo nikakutaka wewe unipe proof ya imani yako ya kutokuwepo mungu.
Kama huna uwezo wa ku proof kwa nini wewe umtake anaeamini uwepo wake ku proof?
Kwanza kabisa, kamanilivyoeleza hapo juu, kisichopo,hakina proof nje ya logical construct,kwa sababu hakipo.

Huwezi kufanyia proof kitu ambacho hakipo kwamba hakipo. Kwa sababu, ilikufanya proof (iliyo nje ya logical constructs tu) inabidi kiwepo.

Nakikiwepo, huwezi kukifanyia proof kwamba hakipo, kwa sababu kipo.

Ukitakaku prove kwamba mwizi kaingia kwako,unaweza kufanya forensic fingerprint ukapata fingerprints za huyo mwizi.

Unaweza kuangalia security camera ukamuona mwizi kaingia.

Kama hakuna mwizi aliyeingia, uta prove vipi kwamba hakuna mwizi aliyeingia? Utatoa fingerprints za mwizi useme "hizi hapa fingerprints za mwizi ambaye hajaingia kwangu,hivyo hakuingia. Nime prove. Fingerprint hizi hapa" ?

Au utatoa mkanda wa security camera uoneshe kwamba "hii hapa video inaonyesha mwizi kaingia kwangu,hivyo huu ni ushahidi mwizi hajaingia"?

Hivyo, ambacho hakipo hakina sehemukubwa ya kuwa proved kwamba hakipo.

Kilichopo ndicho kina proof.

Zaidi, kisichopokinaweza kuwa proved hakipo kwakutumia logical construct. Proof by contradiction.Ukiweza ku contradict kitu unanonesha hakipo, hakiwezikuwepo, kwa sababu dhana ya kuwepo kwake inajipinga yenyewe.

Ninaposemakwamba Mungu hayupo kwa sababu dhana ya kuwepo kwake inajipinga yenyewe,hiyo ni proof by contradiction kwamba Mungu hayupo.

Ni vipi dhana ya kuwepo Mungu ina contradiction?

1.Mnasema Mungu ni mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote.
2.Mungu mweye ujuzi wote, upendo wote na uwezo wote kuumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana wakati alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani ni contradiction.
3.Ulimwengu huu mabaya yanawezekana.
4. Ulimwengu huu ina m contradict Mungu huyo.
5. Mungu huyo hayupo.Kwa sababu ana contradiction.

Nime prove Mungu huyo hayupo kwa "proof by contradiction".

Ondoa contradiction hiyo u prove Mungu yupo.
 
Yesu alipokimbilia kwenye Mlima wa Zaituni na huku akisakwa na Mayahudi alijitenga na wanafunzi wake. Huko faraghani aliomba hivi:

Ee Baba, ikiwa ni mapenzi yako, uniondolee kikombe hiki; walakini si mapenzi yangu, bali yako yatendeke. Malaika kutoka mbinguni akamtokea akamtia nguvu.

Luka 22.42-43

Hapa tunaona mambo matatu muhimu:

1. Yesu anamwomba Mungu. Yesu anamwabudu Mungu. Wawili hao ni mbali mbali, na vyeo vyao ni mbali mbali. Yesu ni mtumwa mnyonge mwenye kuomba na kuabudu. Na Mungu ni Mwenyezi Mungu mwenye uwezo wote na mwenye kustahiki kuabudiwa pekee, hata na Yesu, mwenye kutakiwa msaada pekee, hata na Yesu.

2. Mapenzi ya Mungu ni mbali na yale ya Yesu. Yesu hataki kuuliwa, ananyenyekea na kuomba kwa Bwana wake: "uniondolee kikombe hiki" cha mauti. Yesu hana azma hata chembe ya kufa msalabani, kifo cha mhalifu, kifo cha laana kama maadui zake Mayahudi walivyoazimia kumpatilisha nacho. Lakini anakiri kuwa ni mapenzi ya Mungu sio yake yeye yatendeke. Yeye hana hila wala nguvu za kuzuia kudra ya Mwenyezi Mungu.

3. Yesu, Mwana wa Adamu, anakata tamaa. Imani inampunguka. Kavunjika moyo. Ikabidi "Malaika kutoka mbinguni akamtokea akamtia nguvu."

Jee, yaelekea kuwa Yesu ndiye Mungu? Yaelekea kuwa yeye na Mungu kuwa ni sawa? Kama upo wasiwasi wo wote wa kujibu hayo, mwenyewe Yesu anajibu kama anavyo hadithiwa na Yohana kuwa kasema:

Baba ni mkuu kuliko mimi.

Yohana 14.28

Na mwishoni naye yupo mslabani:

Na kama saa tisa, Yesu akapaza sauti yake kwa nguvu akisema, Eloi, Eloi, lama sabakthani? yaani, Mungu wangu, Mungu wangu, Mbona umeniacha?

Mathayo 27.46
Yafaa hapa tujiulize: Yesu akimlilia Mungu gani hapo msalabani ikiwa naye mwenyewe ni Mungu? Au nini alikusudia aliposema: "Mungu wangu naye ni Mungu wenu"?Maneno hayo kama yanaonyesha cho chote basi yanaonyesha unyenyekevu wa Yesu mbele ya Mungu wake. La kustaajabisha ni kule kukata tamaa kwake na kuvunjika moyo.

Huwaje mtu wa imani, licha ya nabii na mwana pekee wa Mungu, akate tamaa na rehema ya Mwenyezi Mungu. Ama kuwa Mungu akate tamaa na Mungu, na kumyayatikia: "Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha", ni jambo ambalo halimkiniki kuwa.
Kwa uthibitisho ulio wazi Biblia inatwambia kuwa Yesu si Mungu, wala Mungu si Yesu.

Nimependa ulipoona utata ukajiuliza Alikuwa anamaanisha nini? Kuna vitu ukivijua utaelewa mengi sana, kwa nini Yesu alikufa msalabani? Mwili wake una maana gani? Damu yake ina maana gani? Kuishi kama binadamu kuna maanisha nini? Na ni nini maana ya Agano(covenant🙂 au mikataba?

Kukujibu swali lako kuna kipengele kimoja kinalijibu kwa uzuri.

Wafilipi 2:5-11 nitaupaste hapa jukwaani kama utapenda.
 
5 Iweni na nia iyo hiyo ndani yenu ambayo ilikuwamo pia ndani ya Kristo Yesu;

6 ambaye yeye mwanzo alikuwa yuna namna ya Mungu, naye hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa ni kitu cha kushikamana nacho;

7 bali alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa ana mfano wa wanadamu;

8 tena, alipoonekana ana umbo kama mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba.

9 Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina;

10 ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi;

11 na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI BWANA, kwa utukufu wa Mungu Baba.

Wafilipi 2:5-11

Yesu Alikuwa na lengo alilokuwa akilitimiza na pia Alikuwa akifundisha maisha ya aina tofauti katika kukabiliana na changamoto za dunia
 
Back
Top Bottom