ROHO ni nini?

ROHO ni nini?

Cc Donatila
Cc Demiss
Naona mnagoogle definition za roho na quotes za bible..mnatupanga hapa kwamba mpo deep spiritually...
Hahaah weee nimecheka sana
 
ROHO NI NINI

Hii ni miongoni mwa elimu ngumu sana katika kutolea maelezo. Lakini nitajotahidi kadiri nijuavyo lakini ajuaye zaidi ni Mungu.

Roho ya mtu huumbika (nurtured) sambamba na kuumbika kwa mwili wa mtu anapokuwa tumboni mwa mama yake yaani kama inavyojulikana mtu hadi awe kiumbe kamili huanza kutoka kwa baba kama tone la shahawa (sperms) ambapo katika shahawa moja ndipo hutokea mtu mmoja (naomba tusahau juu ya mapacha ili tuelewe kwa urahisi), hivyo roho huwemo ndani ya shahawa katika hali ya udhaifu (delicate and elusive) na wakati shahawa inapoingia kwenye ovary ya mwanamke ili irutubishwe kuwa kiumbe kamili hapo hapo pia roho iliyomo ndani ya shahawa nayo inarutubika sambamba na shahawa yenyewe pindi shahawa inapokuwa kiumbe kamili nayo roho inakuwa kamili na uhai unakuwa umekamilika, hivyo roho inaanzia kuwemo ndani ya shahawa na hukuzwa ndani ya tumbo la mama sambamba na kukuzwa kwa mwili mzima wa mtoto ndani ya tumbo la mama.

Basi ili tuweze kuifahamu roho inatupasa tutoe mifano ya vitu tunavyoishi navyo, Roho siyo sehemu ya mwili kama vile jicho au mkono au sikio nk, yalivyokuwa ni sehemu ya mwili lakini roho inayo mahusiano ya kiathari (cause and effect) na mwili mfano kama mtu atukanwe vibaya hapo moja kwa moja atapata maumivu katika roho na anaweza kutoka machozi kwa uchungu na utaona hayo machozi ni dalili kuwa mwili umepata athari halikadhalika kama mtu apewe mateso makali ya mwili athari itaenda kwenye roho kiasi kwamba mwili unakuwa si mahali pazuri kwa roho kukaa na hivyo roho huondoka na hatua hiyo tunaiita kifo, pia mtu anapofanya Ibada kwa vitendo (kimwili) anaipa athari za kiibada hiyo roho yake.

Kifupi ni kwamba roho imejificha ndani ya mwili kama vile moto ulivyojificha ndani ya njiti ya kiberiti, njiti ni njiti na moto ni moto wala havifanani lakini vinahusiana.
mkuu nazani wewe ni muelewa wa mambo nmepata kitu kutoka kwenye maelezo yako
1.ila kuna kitu kinaitwa emotion yani hizi ni feelings mtu anazopata kutokana na situation yeyote jinsi ubongo utakavo interprt kulingana na ushushu wa sensory organs eithr furaha,maumivu n.k kwa mfano ukipigwa unaumia...maumivu ni consiousns ya ubongo ili kuprotect tissue zisipate majeraha katika sehem uliojeruiwaa ila kwa maelezo unamaanisha maumivu yako rohoni je roho ni ubongo??...kiziwi akitukanwa hawezi kupata maumivu kwa sababu ubongo haujapewa taarifa ina maanisha kiziwi hana roho? au unaeza ukanieleza unaelewa nn unavyosikia neno emotion na inatofautiana vipi na roho ..?
 
Roho ipo ndani ya moyoo[emoji23][emoji23][emoji23]
kwa sehemu gani apoo
Screenshot_2018-08-07-11-40-34-1.jpg
 
Tuanzie hapo kwenye neno "viumbe" kwa maana nyingine mada yako inatakiwa kujadiliwa kiimani kwani unapozungumzia "viumbe" maana yake kuna "muumba" aliyeviumba ambaye kwa neno la jumla wanamwita Mungu. Kabla hatujaenda mbele, chagua mada yako ijadiliwe kwa imani ipi maana kuna imani nyingi kila moja ikiwa na mtazamo tofauti kuhusu "roho".
unaweza elezea katika muktadha wowote uwezao kulingana na majarida mbali mbali nauwezo wako wa kufikiria na ukajiridhisha bila chembe ya wasi kuwa hii ndiyo rohoo...
 
mkuu nazani wewe ni muelewa wa mambo nmepata kitu kutoka kwenye maelezo yako
1.ila kuna kitu kinaitwa emotion yani hizi ni feelings mtu anazopata kutokana na situation yeyote jinsi ubongo utakavo interprt kulingana na ushushu wa sensory organs eithr furaha,maumivu n.k kwa mfano ukipigwa unaumia...maumivu ni consiousns ya ubongo ili kuprotect tissue zisipate majeraha katika sehem uliojeruiwaa ila kwa maelezo unamaanisha maumivu yako rohoni je roho ni ubongo??...kiziwi akitukanwa hawezi kupata maumivu kwa sababu ubongo haujapewa taarifa ina maanisha kiziwi hana roho? au unaeza ukanieleza unaelewa nn unavyosikia neno emotion na inatofautiana vipi na roho ..?
Naomba nifafanue tena kwani
nadhani utakuwa hujanielewa vyema, mimi nilijaribu kuonyesha kuwa kuna mahusiano kati ya Mwili na Roho na nikatoa mfano labda inapotokea mtu katukanwa hupatwa na maumivu/uchungu (bad feelings) katika roho na moyo (mind) ni kama "receptor" wa hayo matusi na anaweza kutokwa na machozi hiyo inakuwa ni athari kutoka rohoni kwenda mwilini pia inapotokea mtu kapata furaha hapo anakuwa na good "feelings" rohoni na moyo au (mind) in this case serves as a receptor, na mtu huyo unaweza ukimuona akitabasamu au kucheka kwa furaha maana yake ni kwamba ujumbe wa fursha uliopokelewa na moyo (minds) umepelekwa kwenye roho na baadaye kupokelewa na mwili ndiyo matokeo yake mtu akatabasam na kucheka, nikatoa mfano wa mwili kuathiri roho kwamba kwa wale watu wanaofanya ibada kwa matendo ndiyo wanaouzoefu mkubwa sana ni namna gani mwili unavyoathiri roho hasa ukiwa unafanya maombi katika sijda (prostration stance).

Sipingi mtazamo wa taaluma ya biology ulioutoa ila tu mada yote ilikuwa inahusu mahusiano kati ya mwili na roho na ugumu hapa ni kwamba roho siyo "tangible organ" kama ini, mapafu,jicho nk, itakayoweza kujadiliwa kibailojia.
 
ROHO NI NINI

Hii ni miongoni mwa elimu ngumu sana katika kutolea maelezo. Lakini nitajotahidi kadiri nijuavyo lakini ajuaye zaidi ni Mungu.

Roho ya mtu huumbika (nurtured) sambamba na kuumbika kwa mwili wa mtu anapokuwa tumboni mwa mama yake yaani kama inavyojulikana mtu hadi awe kiumbe kamili huanza kutoka kwa baba kama tone la shahawa (sperms) ambapo katika shahawa moja ndipo hutokea mtu mmoja (naomba tusahau juu ya mapacha ili tuelewe kwa urahisi), hivyo roho huwemo ndani ya shahawa katika hali ya udhaifu (delicate and elusive) na wakati shahawa inapoingia kwenye ovary ya mwanamke ili irutubishwe kuwa kiumbe kamili hapo hapo pia roho iliyomo ndani ya shahawa nayo inarutubika sambamba na shahawa yenyewe pindi shahawa inapokuwa kiumbe kamili nayo roho inakuwa kamili na uhai unakuwa umekamilika, hivyo roho inaanzia kuwemo ndani ya shahawa na hukuzwa ndani ya tumbo la mama sambamba na kukuzwa kwa mwili mzima wa mtoto ndani ya tumbo la mama.

Basi ili tuweze kuifahamu roho inatupasa tutoe mifano ya vitu tunavyoishi navyo, Roho siyo sehemu ya mwili kama vile jicho au mkono au sikio nk, yalivyokuwa ni sehemu ya mwili lakini roho inayo mahusiano ya kiathari (cause and effect) na mwili mfano kama mtu atukanwe vibaya hapo moja kwa moja atapata maumivu katika roho na anaweza kutoka machozi kwa uchungu na utaona hayo machozi ni dalili kuwa mwili umepata athari halikadhalika kama mtu apewe mateso makali ya mwili athari itaenda kwenye roho kiasi kwamba mwili unakuwa si mahali pazuri kwa roho kukaa na hivyo roho huondoka na hatua hiyo tunaiita kifo, pia mtu anapofanya Ibada kwa vitendo (kimwili) anaipa athari za kiibada hiyo roho yake.

Kifupi ni kwamba roho imejificha ndani ya mwili kama vile moto ulivyojificha ndani ya njiti ya kiberiti, njiti ni njiti na moto ni moto wala havifanani lakini vinahusiana.
umeandika kitu kikubwa sana kaka,ila watu wamekipuuzia.
 
WAtu kama nyie siku zote mpo. Hamfikirishi akili Bali mnavuta Kiti kusubiria wengine waje kuchangia. Hata kutoa definition ya roho kule Google kutuletea hapa UMESHINDWA. Ila kuvuta Kiti na kusoma michango ya wengine umeweza. Shubamitiiii!!
Wala hujakosea.

Kwasababu napenda kujifunza ndio maana nimevuta KITI niketi ili nipate kujifunza kutoka kwa wenye kufikirisha AKILI zao, nikisoma Michango yao inatosha sana kwa Mimi kujifunza.

Sihitaji kufikirisha AKILI kwa kitu/jambo ambalo WADAU wengine wameshafikirisha AKILI.

Wewe mwenye kufikirisha AKILI mbona umeshindwa kufikirisha AKILI yako na kuleta JIBU hapa, na badala yake umeamua kunishambulia MIMI.!

Inashangaza sana!
 
Ajielewi uyo muuza machungwa.
 
Kifupi Roho ni (SPIRIT) ambayo kila kiumbe aliye Hai anayo.
Roho (spirit) ni muungano wa NAFSI (SOUL) NA Akili (MIND).

Ndo kusema combination ya NAFSI (SOUL) na AKILI (MIND) ndo inaleta kitu kiitwacho SPIRIT (ROHO) ya mtu.

Roho (SPIRIT) huwa haionekani. Roho ni structure nzima (muundo) wa mtu. Roho ndo inafanya NAFSI (SOUL) na MIND (Akili) vifanye kazi. Ikiwemo mifumo yote ya mwili wa binadamu. Ndo mana roho (SPIRIT) ikishatolewa na Muumba linalobaki ni li MWILI tu.
Roho Aina umri. Haimanishi mtoto akiwa na miaka miwili basi roho yake pia ina ukubwa wa miaka miwili lahasha!.. Roho inayowekwa kwa mtoto mdogo anaezaliwa ndo hiyo hiyo ataishi nayo mpaka uzeeni. Ndo kusema mtoto mdogo wa miaka miwili Ana ROHO yenye kutambua mambo mengi makubwa Sema tu MUNGU mwenyewe kwa kupitia kanuni na Sheria Zake za Milele (Eternal Laws) huwa anakataza watoto wadogo na wachanga kutumia uwezo mkuu wa ROHO walizo nazo kipind cha udogo wao.
Ndo. Maana utakuta wakati mwingine mtoto mdogo Ana fanya vitu vikubwa vya kushangaza watu. Na tunamuita MTOTO WA AJABU au EXTRA ORDINARY ni kwa sababu tu MUNGU kamruhusu kidogo atumie uwezo mkubwa wa ROHO ulio ndani yake. So kifupi ROHO haina umri. Wala haikua na urefu au unene au umri wa kutoka utotoni mpaka ukubwani.
Eti mwenye miaka 96 roho yake ni kubwa sana kushinda mwenye miaka 12 hakuna kitu kama hiko. ROHO ni ile Ile uliyowekewa mwanzoni na MUNGU.

Viumbe vyote Hai vina ROHO ikiwemo majani, maji, ardhi, miti, wanyama, selihai za miili yetu ambazo zinatengeneza organ za maumbile yetu. Maji na kadhalika.

Roho ni highest intelligence ya kiumbe Hai, ndio inayo control Nafsi (soul) na mind (akili).

KWA wale wana fizikia wanaweza kuelewa mfano huu katika kutofautisha Roho (spirit), Nafsi (soul) na Akili (mind).

Atom si tunaijua? Ina kuwa formed na vitu vidogo ndani yake kama Proton, neutron.

Hivyo hivyo kwa roho (spirit) ni Ile the smallest particle.. Injini ya soul na mind.

MUNGU ndie incharge wa ROHO, MUNGU hakuziumba (create), ROHO Bali anajua namna yake yeye alivyozileta kwenye existence. Literatures nyingi wanasema MUNGU aliziamrisha ziwepo zikatokea.
Maana kitu chochote kinachokua "created" kuumbwa huwa kinakufa.
Roho haijaumbwa na ndo mana roho haifi hata mtu akifa yenyewe inaelekea kwenye ulimwengu wa roho kusubiria hatua zingine.

MUNGU wakati anaanza mpango wa kuandaa Dunia kwa ajili ya maisha ya binadamu. Alitumia roho (intelligences) kwenye kutoa majukumu na roho zingine (intelligences) walikubali KUSHIRIKI kwenye uumbaji wa MUNGU wawe kama majani, wengine walichagua kuwa miti, wengine kuwa maji na wengine kuchukua nafasi mbali mbali ili kuipendezesha Dunia.

Kifupi ni kusema kwamba vitu vyote vilivyo Duniani vinavyopendezesha Dunia ni roho (intelligences) ambazo zimechagua hiyo kazi mwanzoni kabisa kule kwenye uumbaji wa MUNGU.

Intelligences wengine tulichagua kuwa binadamu, ndo mana tukaja kuzaliwa na kuwa na Roho (SPIRIT).

Kumbuka neno Intelligence hapa limetumika Sawa na neno Spirit yote yanamanisha ni ROHO.
Lakini intelligence ni kubwa na ina uwezo zaidi.

Ndo mana Kuna mambo mengi sana yamejitokeza kwenye vitabu vyetu vitakatifu ambayo wengine hawajui kwa undani kwa nn yametokea, wao wanajua ni muujiza tu hapana. Ngoja nikufahamishe!!

YESU KRISTO ndo mkuu wa Roho zote, amepewa mamlaka hayo na MUNGU, Na kama tulivyoongea Mwanzoni kwamba hizi Roho (spirit) zote zinatoka MBINGUNI na zimechagua nafaid zao kwenye uumbaji wa Dunia kama intelligences.

Hivyo intelligences zote, AU kwa lugha rahisi roho zote zilizo kwenye Viumbe hai kama majani, maji, ardhi na nyingi ambazo nimezitaja ZINAMTAMBUA pasipo na shaka UKUU wa YESU KRISTO,.

YESU KRISTO ndo top. Yeye ndo Mkuu wa intelligences zote, roho zote yeye ndo anaongoza.

Hivyo wanamtambua kwa UKUU huo. Angalia kidogo kwenye BIBLIA takatifu YESU akiziamrisha hizi Roho ambazo zilichagua kuwa vitu hapa Duniani na ZIKAMTII.. mfano aliuambia upepo ukome wakati bahari ilipochafuka. Na upepo ukamtii ukatulia kimya Ile sio muujiza kwake yeye anajua kabisa wale walikua roho waliochagua kuwa upepo (intelligences) na akawaamuru watulie.
Pia Kuna sehemu kwenye BIBLIA aliwahi kusema "kama msiponisifu basi NTAYAINUA" mawe haya yanisifu. Alijua dhahiri kuhusu intelligences walio kwenye mawe na uwezo wao wa kuongea na sifa za kiumbe hai, sisi binadamu tunaamini mawe hayana uhai lakini mawe yana uhai na yanaweza kuongea sababu Kuna intelligences ambao walichagua kuwa mawe. Ndo mana YESU akasema NTAYAINUA" kwa lugha rahisi NITAYAAMURU haya mawe.

Pia Kuna mfano mwingine kwenye kitabu hiko Hiko cha BIBLIA AMBAPO YESU alikua Ana njaa akaona mti, akadhani Kuna matunda ili ale lakini hakukuwepo na matunda na kilichofata YESU akaulaani Ule mti.. Na BIBLIA INASEMA ukanyauka hapo hapo ni concept huyo hiyo ya UTII wa intelligence (roho) za Viumbe wengine ambao walichagua kuwa vitu hapa Duniani.

Waislam Kuna mafundisho huwa wanasema Kuna siku mkono wako utaongea na kusema mabaya yote, Kuna siku ulimi au Macho utatoa ushuhuda wa dhambi zako ni kweli kabisa. Hii ni kutokana na concept hii hii ya intelligences ambao wametumika kuumba huo mkono, AU jicho lako au Aina organi nyingine mwilini mwako.

Hata kwenyewe BIBLIA tunaona Ile story ya sauli na farasi AMBAPO punda aliongea na kuwasiliana na sauli, pale sauli alipokua anamfosi punda atembee ili akaue watu wa MUNGU punda alisema 'huoni Malaika mbele hapo njiani ". Ni Ile Ile muendelezo wa concept ya INTELLIGENCES ambao wamechagua kuwa PUNDA na wanyama wengine wakipewa ruhusa ya kuongea wa naongea.

MWISHO, Intelligences ndio yenye uwezo mkubwa sana, ndio inayokua ndani ya roho (spirit). Ndo mana wakati mwingine ni ngumu kutofautisha Kati ya intelligences na roho (spirit) sababu ziko ndani ya mwingine.

Na Roho (Spirit) ni muungano wa NAFSI (soul) na Akili (mind).

Nadhani nimeeleweka.
 
ROHO NI NINI

Hii ni miongoni mwa elimu ngumu sana katika kutolea maelezo. Lakini nitajotahidi kadiri nijuavyo lakini ajuaye zaidi ni Mungu.

Roho ya mtu huumbika (nurtured) sambamba na kuumbika kwa mwili wa mtu anapokuwa tumboni mwa mama yake yaani kama inavyojulikana mtu hadi awe kiumbe kamili huanza kutoka kwa baba kama tone la shahawa (sperms) ambapo katika shahawa moja ndipo hutokea mtu mmoja (naomba tusahau juu ya mapacha ili tuelewe kwa urahisi), hivyo roho huwemo ndani ya shahawa katika hali ya udhaifu (delicate and elusive) na wakati shahawa inapoingia kwenye ovary ya mwanamke ili irutubishwe kuwa kiumbe kamili hapo hapo pia roho iliyomo ndani ya shahawa nayo inarutubika sambamba na shahawa yenyewe pindi shahawa inapokuwa kiumbe kamili nayo roho inakuwa kamili na uhai unakuwa umekamilika, hivyo roho inaanzia kuwemo ndani ya shahawa na hukuzwa ndani ya tumbo la mama sambamba na kukuzwa kwa mwili mzima wa mtoto ndani ya tumbo la mama.

Basi ili tuweze kuifahamu roho inatupasa tutoe mifano ya vitu tunavyoishi navyo, Roho siyo sehemu ya mwili kama vile jicho au mkono au sikio nk, yalivyokuwa ni sehemu ya mwili lakini roho inayo mahusiano ya kiathari (cause and effect) na mwili mfano kama mtu atukanwe vibaya hapo moja kwa moja atapata maumivu katika roho na anaweza kutoka machozi kwa uchungu na utaona hayo machozi ni dalili kuwa mwili umepata athari halikadhalika kama mtu apewe mateso makali ya mwili athari itaenda kwenye roho kiasi kwamba mwili unakuwa si mahali pazuri kwa roho kukaa na hivyo roho huondoka na hatua hiyo tunaiita kifo, pia mtu anapofanya Ibada kwa vitendo (kimwili) anaipa athari za kiibada hiyo roho yake.

Kifupi ni kwamba roho imejificha ndani ya mwili kama vile moto ulivyojificha ndani ya njiti ya kiberiti, njiti ni njiti na moto ni moto wala havifanani lakini vinahusiana.

Aisee kwahiyo kwenye kila sperm kuna roho?
 
Mungu hayupo thibitisha uwepo wake.
Bila shaka wewe utakuwa na tatizo la ufahamu lililokuwa kubwa sana na dawa yake ni elimu. Labda nikuulize hivi wewe una akili? Kama unazo thibitisha uwepo wa akili hizo.
 
Sisi waislamu tumepewa kitabu cha Qur'an. Kitabu ambacho mwenye hii dunia katuletea iwe ni muongozo wa maisha ya hapa duniani kwake. Kwa suala la roho nini? Si swali jipya makafiri wakati wa uhai wa kiumbe bora zaidi dunia mtume Muhammad swalallahu alaih wassallam waliuliza swali hili. Mtume Muhammad swalallahu alaih wassallam akaambiwa ajibu ifuatavyo;
وَيَسْأَلُونَكَ عَنِ الرُّوحِ ۖ قُلِ الرُّوحُ مِنْ أَمْرِ رَبِّي وَمَا أُوتِيتُمْ مِنَ الْعِلْمِ إِلَّا قَلِيلًا

(Ali Muhsin Al-Barwani)
Na wanakuuliza khabari za Roho. Sema: Roho ni katika mambo ya Mola wangu Mlezi. Nanyi hamkupewa katika ilimu ila kidogo tu.

-Sura Al-Isra', Ayah 85
 
Wahenga wetu wanafalsafa kama Socrates Plato na Aristotle walijaribu kujua roho ni nini lakini jibu halikupatikana . Jibu likikosekana basi imani huanzia pale , huenda jibu ni " kale kapumzi kanapoingia mara tu sperm inapoungana ba ovary " maisha yalianzia pale sasa kametoka wapi ni issue , sema tu ni Mungu ubishi uishe!
 
Roho ni umbile la pekee lisiloonekana ambalo linasadikiwa kuwemo pamoja na mwili katika binadamu na kuunda hisia... ni umbile linafananishwa na upepo au pumzi...

Cc: mahondaw
 
Hakuna kitu kinachoitwa roho. Ni illussion tu kinatchotufanya tuishi ni mifumo mingi ya mwili inayofanya kazi kwa kutegemeana sasa mfumo mmoja unapopata hitilafu kubwa na kushindwa kufanya kazi , huaribu mifumo mingine na syssterm nzima hufa. Ni sawa sawa na gari mfumo mmoja ukifa haliwezi kutembea
 
Back
Top Bottom