Roho yangu inaanza kukaa mbali na huyu ndugu yangu, je nina makosa mimi kutopokea simu zake?

Watu Wa namna hiyo wapo. Yaani wanakuwa over concerned kuhusu maisha yako, wanatamani yaani ufanikiwe ili mioyo yao ifurahi.. Kiufupi anakupenda na anashindwa kujizuia kukufuatilia
Kabisa yaani
 
Nimeandika nikafuta. Aseee ngoja ninyamaze tu.
 
we boya kweli me natamani mtu aniulize nn nafany ww unasema aunt anakusumbuaa daah
 
Jirekebishe wewe binafsi,achana na imani za wananzengo shangazi yako ana upendo wa kweli juu yako,
Akikuuliza mjibu ili nafsi yake pia ifurahi na usimfiche maana pia aweza kuwa anakuombea juu ya kazi za mikono yako na malengo yako kwa ujumla
 
Shangazi yako hana shida mwenye shida ni wewe mwenye msongo wa mawazo
 
Jirekebishe wewe binafsi,achana na imani za wananzengo shangazi yako ana upendo wa kweli juu yako,
Akikuuliza mjibu ili nafsi yake pia ifurahi na usimfiche maana pia aweza kuwa anakuombea juu ya kazi za mikono yako na malengo yako kwa ujumla
The best comment
 
Huyo shangazi yako kama bado mmbichi,nakushauri mgonge..maana ndicho anachokihitaji kwa sasa.
But hizo ni observation zangu
 
Sijaelewa kabisa

Aliyeelewa MSAADA tafadhari
Ufahamu wangu mdogo kuhusu sisi waswahili, ndg yetu mtoa mada tayari yupo kwenye habari za ushirikina.......anahisi anonewa kijicho na huyo shangazi yake. Kwamba 'si bure kumfuatilia huko, lazima kuna namna (anataka kumroga asiendelee)'!
 
Mi sioni kama umekosea,maana kuna watu wengi wa aina yako hawapendi kuulizwaulizwa maswali hata yawe ya ubora kias gani.Sasa,jitahidi umwambie katikati ya story tena huku mkicheka kwamba hupendi udadisi wake
 
Ni ndugu yangu mtu mzima, namwita shangazi, sijawahi gombana nae, na binafsi namwona ni mtu mwema kwangu, na nimefahamiana naye toka utoto wangu hadi utu uzima huu, kipindi cha likizo nlikuwa nashinda kwake miezi mingi kabla ya kwenda home, ila kipindi cha hivi karibuni amekua na tabia ambazo zimefanya roho yangu ianze kumkataa.

Kila mwezi atanipigia simu, hili la kunipigia simu sina shida nalo, Maana hata mm huwa nampigiaga simu.

TATIZO LINAPOANZIA:
Kila nikiongea naye kwenye simu, ananiuliza maswali ambayo mara nyingi mm binafsi sipo huru (comfortable) Kuyajibu daaah..

1)Kila akinipigia simu lazima aniulize nipo wapi, nikikwepesha kumjibu atanisisitiza mpaka nimwambie niko wapi..
2)Nikimwambia napigaa mishe za kilimo, simu zitakazofuata ataniuliza mara nne nne kilimo kiliendaje.
3)Muda mwingine ananiuliza kama biashara nilizofungua bado zipo
4)Kila akinipigia ananiuliza kazi nlizo-apply zimeendaje

Kutokana na hayo maswali hapo juu, yani nimeanza kujitenga naye kimya kimya mpaka yeye Kuna siku aliniuliza mbona najitenga nae, ila nahic hajajua kwanini namkwepa, ila in general shangazi yangu tangu nimfahamu amekuwa ni mtu mkarimu Sana kwangu.

Huyu shangazi yangu Huwa anasema baadhi ya ndugu Zake wengine hawapokeagi simu zake, nahisi ni kwasababu ya hii tabia yake ya kuuliza maswali.

Labda mm ndio nina tatizo, Wenye uzoefu naombeni mnipe mawazo yenu kwenye hili, ili kama nina makosa nijirekebishe

Mkuu ukiona roho inakataa pahala Uzingatie yawezekana huyo aunt sio poa ila take your time kabla hujareact
 
Sisemi shangazi yako ana changamoto ila nina babu yangu kiukoo ,nimefahamiana naye ukubwani ni mtu anajihusisha na uganga wa kienyeji maswali yake ni kama hayo unayopata toka kwa shangazi

Binafsi sipendi kuulizwa ulizwa maswali kuhusu maisha,mshahara,niko wapi narudi lini, niliamua kupiga block tu maana ilikuwa haipiti siku 2 lazima niulizwe

Yote kwa yote akili za kuambiwa changanyia na za kwako
 
Tabia hizo inaonyesha anapenda kuharibu maendeleo ya watu, atakuwa anajaribukukufatilia kwa njia za giza na akishindwa anakuuliza ili afanye yake. Usishangae kwanini wengine wanamkimbia, itakuwa wamegundua kitu juu yake.

Endelea kukaa nae mbali, muhimu usimueleze issue zako zozote. Watu kama hao wanapenda kusikia mtu ana matatizo tu. Usiongee yako hata kwa watu wa karibu nae asiyasikie, ndio maana wengi tunafanya yetu na kunyamaza baada yanaonekana tu kama wakiyaona. Usimruhusu akaja kwako leo hata mbeleni.

Sali pia

Hahaha Umejuaje ana tabia ya kupenda kusikia Mtu ana matatizo, hlf umenikumbusha, mm huyu aunt yangu ni mwaka wa 9 huu sijawahi kumuombaga hela, sanasana ikitokea event za kifamilia saa ingine mm nachangia pesa nyingi kiasi..

1)Sasa kwenye maongezi, Nsipoenda kwake ataniambia mbona huji, huna nauli, biashara hazikuingizii hela?

2)Siku ingine ataniambia maisha magumu, huenda ipo siku nitaenda Kwake mimi na mke wangu nimwambie tuna siku tatu hatujala (Sijaoa)

3) Siku fulani aunt akaniambia kuna kipindi ulikua unagawa pesa, tukasema huyu hajui kama Hizo pesa zitakuja kuisha..

Mmmh ingawa alivoniambia ni uhalisia wa maisha lkn nikasema huyu mtu mbona imagination zake kwangu ziko negative Keenly witnessj Niwaheri
 
Hata mkipendwa mnasema anakufuatilia.

Sometimes ulivyo ni maombi yake,
 
Kumbe ukweli unaujua kabisa...mwanga huyo
 
Back
Top Bottom