iri naro rinatakaga kusemaga. niriripasua rikichwa rababarako. siuendege kure kwenyemiapari ya midini. siunajifanyagaga ni shehe. rroo,
NI KWELI SIASA ZA NYERERE ZILICHANGIA KUWAOGOPESHA HIVYO KUWAFANYA WAJIRUNDIKE KWENYE FLAT ZA KUPANGA BADALA YA KUJENGA..HII NI KUTOKANA NA ILE LAND CONTRACT YA NYERERE YA MIAKA 99
NI KWELI KUHUSU HIYO POLICY YA LAND CONTRACT YA MWALIMU LAKINI NA WAZAWA NAO HAWAKUENDELEZWA KWA KUJENGEWA MAZINGIRA BORA YA KILIMO CHA KISASA!HAPO NDIO ILIKUWA MBAYA..KUTEGEMEA KILIMO KAMA UTI WA MGONGO WA UCHUMI WAKATI UTEKELEZAJI WAKE UKIZIKWA NA VIONGOZI CORRUPT WAKISHIRIKIANA NA HAWA WENZETU!Namsifu sana Mhe Nyerere kwa ile land policy yake...unafikiri wageni enzi hizo wangeruhusiwa ku-own land kama vile Kenya thubutu leo kama kungekuwa na mbongo angeishi au kujenga maeneo ya Masaki,Msasani yaani posh area.
mchawi wa Tanzania ni rushwa.......wahindi, waarabu na wazungu mtawaonea bure tu.
ikidhibitiwa rushwa hapo mambo yoooote yatakuwa shwari!!.
Mada baabu kubwa sana tena nadhani dawa itaanzia hapa hapa kwa msukumo ule ule wa JF..Hapendwi mtu!..
Katika swala hili tuna matatizo mawili, la kwanza ni kuwepo na hawa kunguni (wageni) wasosikia maji ya moto na wajanja sana kuwakamata pindi panapotokea mwanga. Yawezekana kabisa kuwa ni uchafu wetu sisi wenyewe, lakini tatizo kweli ni uchafu wetu na je uchafu huo ni upi?... hivyo ni wapi haswa usafi unatakiwa...
Kwanza hii tabia ya kusema nchi yetu ni ya Utulivu na Amani, hili neno linatakiwa kupatiwa tafsiri yake maanake hivi sasa linatumika kutubeza. Kama nilivyosema toka mwanzo kuwa Amani na Utulivu inawezekana imetokana na Ujinga wetu tukianza toka enzi za wakoloni (utumwa). Sasa basi isije kuwa huo uvivu wa kifikiri (ujinga) ndio haswa shina la hawa mafisadi (kunguni) kuendelea kuzaana hali kati yetu huwafanya kitoweo cha maskini hivyo tunachokiona ni matunda ya kile tunachopanda. Kwa maana hiyo basi tatizo ni sisi wenyewe toka ngazi za juu hadi chini ambako maskini hushabikia hawa mafisadi kwa sababu tu hupata zaka zao kila Ijumaa. Wapo wanaojipanga ktk majumba ya wahindi kila siku kusubiri chochote na hawa watu huwezi kuwaambia kitu maadam kunguni hawa ni kitoweo kwao.
Hivyo basi ni muhimu sana kuondoa fikra za utumwa na kuamini kwamba Amani na Utulivu una mazuri pekee bali Amani na Utulivu inaweza kuwa ndio sababu kubwa ya uzembe wa mtu mweusi na kuna kila haja ya kutafsiri neno hili pale haki inapotumika. Tukiondoa uvivu wa kufikiria na kukaa kabisa kuendelea kuwa watumwa nadhani hii itakuwa hatua moja kubwa sana. How?.. hilo ni swali zito sanaaaa na naweza weka swali moja hapa sote tukabaki domo wazi?.. Je, kuna mtu anafahamu ujazo wa Almasi tuliyokuwa nayo Mwadui?... Haya madini yameanza chimbwa kabla ya Uhuru na hadi leo zaidi ya miaka 50 mali inaondoka nchini kila siku.. Je, kuna mtu kisha fikiria kuwa hapa tunaibiwa sana?...Noo!....utasikia wazungu wawekeshaji tunawahitaji, jamani toka kabla ya Uhuru mbona Shinyanga ndio kwanza inazidi kuwa maskini zaidi ya miaka ya Nyerere?...Amani na Utulivu!
Pili, Kuna fumbo kubwa sana ktk tiba ya maradhi yetu ambayo tayari yameisha jenga hekalu ndani ya viini vya damu yetu. Nitakubaliana sana na Mwafrika wa kike kuwa ni muhimu kutumia hekima na busara ktk swala zito kama hili kwani hao maskini wanaotegemea kunguni ni asilimia 80 ama chini kidogo ya Wadanganyika wote... (under a dollar a day) Ni vigumu kuweza kuwafikia ama kuwafagia wote kwa msukumo mmoja. Ni vigumu sana kumwambia kila Mdanganyika kuwa Fisadi kwa rangi zake ni adui yako hali ndiye anayempa mlo mmoja kwa siku...
Kwa hali mimi nadhani ipo njia rahisi zaidi, Njia ambayo ni wazi kabisa kuwa hawa Mafisadi ni asilimia 2 kama sio 1 ya Watanzania. Hivyo basi ikiwa kunguni hawa ni kidogo nadhani ni rahisi zaidi ku - deal nao iwapo kila chumba (mkoa na wilaya zake) wataweka karantini na kuhakikisha mkakati wa Mafisadi unatekelezwa kiasi kwamba hakuna pa kukimbilia..Message itafika haraka kwa maskini ikiwa hakuna kunguni hawa..
Pamoja na maelezo hayo marefu nadhani dawa ni kuwasaka hao mafisadi na kuwaadhibu.. hao maskini wakikosa mkuu ama mheshimiwa wa kumwomba msaada wataanza kutia akili. Mfano huu ni sawa na kusema leo hii ikiwa serikali itawabana waagizaji wote wa mali feki nchini basi ni rahisi zaidi kuwaondoa Machinga barabarani lakini hatuwezi kufikiria kuwabana Machinga hali mali inazidi kuingia nchini. Tazama hata drugs, swala sio kwenda Afghanstan ama Colombia kukata mzizi ila ni kuwatambua mafisadi waagizaji wa madawa haya ya kulevya na kuwapa adhabu kubwa...wala sio kuwakamata watumiaji drugs kuwa ndio dawa rahisi maanake hawa akili zao tayari zimekubwa na Ujinga (Amani na Utulivu).
Ndio maana nchi za kiarabu na Israel ni zisizokuwa na ulevi huu wa madawa. Dawa ni kuwabana Waagizaji na kujenga chuki ya ulevi huo yaani Cocaine ni haramu...Tuwabane Mafisadi na Uhujumu uchumi uwe haramu na hauna kinga kwa rais wala mwananchi na adhabu yake kubwa kiasi kwamba hakuna mtu atakayefikiria kujaribu.
Kwa kuhitimisha maneno yangu nakubali kabisa kujenga chuki na hawa mafisadi wachache na itafutwe Expel ama Rungu kuwaondoa hawa kunguni, lakini tukitaka kuwatazama Wadanganyika ambao tayari ni waathirika kwa Ujinga wao (Amani na Utulivu basi tutachukua karne nyingine kufikia hata nusu ya population kupata kuelewa!
Viongozi wetu wangekuwa wazalendo we unafikiri hawa Waasia wangepenya wapi?
Usishangae wakamtuma huyu jamaa ajiitwaye MAB.... ndani ya JF akatuharabia mjadala wetu hapo awali
Nakubaliana na wewe lakini jinsi gani ya kudhibiti hii rushwa?tufanye kama China? mtoaji na mpokeaji wote kata kichwa...barbaric... i would not suggest it.
Kuna kitu kimoja sisi watu weusi i mean duniani kote tuna udhaifu mmoja ambao nashindwa ku figure out if it is genetic or something else.
Udhaifu wetu ni u-selfishness tunaangalia matumbo yetu tu,hatuna vision ya baadae list ni ndefu....
LAKINI BADALA YA KUWAWEKA HAO MAPIMBI MIFUKONI ILI WAKWEPE KODI HAIONYESHI MAPENZI KWA TAIFA!WOTE WANA MAKOSA..LAKINI WAO WALIKUWA NA NAFASI YA KUIJENGA NCHI HII BADALA YA KUI CORRUPT NA KUI BANKRUPT!huo u-barbaric waweza kuwa ndio unaotakiwa!!! mchana hapa nimeuliza ni mafisadi wangapi weusi wameshatingishwa kortini na kuhukumiwa???!! hakuna alojibu, watu wanarukaruka......oooh jiitu patel kakimbia!! alaah, serikali imeripoti interpol kuwa inamwitaji kujibu mashtaka??kimyaaaaa, domo zege!! ebo, tatizo ni sisi, miafrika mibwege. tazama yule pimbi mkapa....wallahi, yule bwana lazima diabetic, type 2 inamtandika, kwa mwendo wake huu hana miaka kumi hapa duniani!!! lakini bado yumo tu, tumbo utafikiri ana mimba ya watoto kumi......babu hutosheki???.
kusema group flani la watu ndio baya kutokana na rangi zao si sahihi!! sheria dhidi ya rushwa zipo, suala ni kuzi-enforce. mfano lowassa, anahitaji a day kwa pilato.....vinginevyo, hili ni chezo la kuingiza na wakulaumiwa si patel.
Nakubaliana na wewe.Ni kweli kabisa kuwa kunguni ni kunguni, rangi zake zinaweza tu kumtofautisha na kunguni mwingine na pengine mmoja kuwa na uwezo zaidi kuishi zaidi ktk hali fulani.
Nakubaliana na YournameisMine anaposema kuwa ni bora zaidi ku deal na kunguni aliyeko kitandani mwako.. yaani wazawa. Lowassa ni mfano bora sana wa hawa kunguni! just imagine a Prime minister kweli anakuwa msitari wa mbele ktk kuiteketeza nchi?...Mbona wakati wa Nyerere hatukusikia Patel wala Karamjee?... ilikuwaje tofauti na leo kiasi kwamba kunguni wasosikia dawa wamerudi?...Tutaendelea ku expel wageni wangapi wakati wengi wanazaana ndani ya pindo za godolo letu. Tazama watoto wa Lowassa, watoto wa Yona, watoto wa kufikia wa Mkapa, afadhali hata huto Steve pamoja na kumtetea sana baba yake lakini kidogo mzito kushiriki ktk Ufisadi kama huu. Kwa kuwachukia Wageni kweli tunaweza wapa watu kama Lowassa nafasi ile ile na hawa ni wabaya kuliko hata mgeni, kumbukeni maneno ya Mwalimu...wanakula bila kupoza wala kusaza.
Ila moja tu nalotaka kuongezea hapa, neno rushwa nadhani ni jepesi zaidi kwani mara nyingi Rushwa huhusiana na mtu kuchukua ama kujipatia fedha au huduma kinyume cha sheria. Je, yule anayemsaidia Patel kuweza kuiba mamillioni ya fedha kwa zawadi ya kumsomesha mwanae Ulaya tutamweka wapi?..wengine wanaona raha tu kuonekana ni wazuri wa kutoa misaada ya wizi hali wao wakisafisha mikono yao.
Bila shaka neno UHUJUMU UCHUMI ndilo linatakiwa kutumika zaidi. Wote wahujumu wa uchumi wetu kwa rangi zao wawe Watanzania ama wageni inatakakiwa wafagiwe.. tena kwa kujisahihisha ktk kauli yangu ya mwanzo nimeambiwa kuwa kunguni hafi kwa Expel wala rungu isipokuwa baridi kali sana.. hivyo basi wote Mafisadi tuwaweke ktk freezing point... nayo ni kutaifisha kila walichokuwa nacho na kukata kabisa nyaya zao ktk kupata ajira sehemu yoyote ile wadhifa unaompa nafasi ya kuwa Management!.. warudi kijijini ama huko walikotoka wakiwa matupu...
BAAAHHH !!!
Huyu dada hana akili chochote....
Wahindi ndio waliyo leta economy ya TZ juu....
If Indians werent in Tanzania, probably our economy could have collapsed centuries back ....
Look in the History of Uganda...
Iddi Ameen aliwa fukuza wahindi hapo uganda....bada yake, you will see how the economy took the down turn....
If you remember, just few years back...At the time of Mkapa, huyu president wa Uganda alii visit hapo DAR !
Alisema kwa Mkapa jokingly kwenye speech " Kamaa Tanzania hawataki ma wahindi hapo, pelekini hapoo Uganda...they are most welcome there."
Right now, uganda economy is coming up...Coz most of the indians have come again, the government have given them special facilities of business.....One of the major companies which employs thousands of local ugandan workers is owned by INDIAN...
People get employment, they get good salaries...if the government and the local people like us try to understand them and support the wahindis....
They are Gift given to us by God to lift our economy up my dear brothers !
ππππ
tusianze ubaguzi
kama ufisadi tuongee ufisadi kwa jumla usitake tupigwe mawe nnjiani