Pre GE2025 Roma aeleza hisia zake Vyama vya Upinzani kuwatenga wasanii katika shughuli zao

Pre GE2025 Roma aeleza hisia zake Vyama vya Upinzani kuwatenga wasanii katika shughuli zao

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

JOHNGERVAS

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2016
Posts
1,011
Reaction score
1,681
Mimi nikiona mtu analaumu wasanii kwenda kwenye events za CC EM kufanya show huwa namshangaa sana!!Wasanii ni wafanya biashara, wame invest kwenye hiyo biashara ya muziki na wanahitaji return….

Kama ambavyo wewe umewekeza kwenye biashara yako, huwezi kubali upate hasara!!Show moja ya CC EM msanii analipwa 5M hadi 15M, na huyo ni msanii wa kawaida kabisa!!Wale A list, show moja wanakunja 25Mmpaka 50M na kuendelea!!

Unawezaje kukataa biashara kama hiyo, tena kwa kwenda kuimba dakika 2 tu hadi 10!! Unalipiwa accommodation plus transport tena na per DM unapewa!!Hata ungekuwa wewe ungekataa?Tuwe tu wakweli….Wangapi mngekataa?

Huu ni ukweli mchungu ambao wengi humu hawapendi kuusikia!! Na nimekuwa nikiusema sana for years….. Wapinzani hawatoi mchele ndomana wasanii hawaji huku!! Huku ni KUNJA NGUMI….Tusonge mbele MAKAMANDA…Since 2010 hizo ndio kauli zao!!Unadhani upinzani hawana pesa?

Sio kweli wanazo sana….si wanalipwa Ruzuku Billions per year!!Basi tu wasanii sio priority kwao!Na kama sio priority sasa kwanini wanawalaumu wakienda upande ule?Ujue sisi mnatuona tuna support upinzani ni kwasababu tu tuna PASSION na hii kitu, We are born to do this!!

Mimi & Kala Jeremiah tuliwahi kufanya show za upinzani tunapewa tu hela ya mafuta laki 1 tunaambiwa Safari njema KAMANDA, no Accomodation!!So inabidi upige iende irudi hiyo….Trip shamba Trip garage….Famasiala nini!!Tuko njiani tunawapigia simu wenzetu walioko upande ule sasa CC EMwanatuonyesha wanalipwa 5M show moja!!

Kampeni zinaisha upande ule wenzetu wote wana gari mpya, kiwanja na wengine wamejenga!!Sisi tunamaliza kampeni ***** tuko teee….tumechoka vipi!!Hatuna hata pesa ya luku home!!Na ukiwapigia simu hao wapinzani kuwaomba hata pesa za kushoot video mpya uendelee kuwepo kwenye ramani HAWAOKOTI KONGA!!

Haya mambo ndomana yalimshinda Kala Jeremiah akabwaga….na ndomana watu wakimsemaga huwa naruka nao kimlalomlalo Coz I know what we went through with my boy!!Wengine tumebakia basi tu tuna SOLID HEART….

tushaumizwa tushateswa na kutiwa vilema ila tupo tu mpaka watuueHakuna maslahi yoyote tunayopata, ila kule wenzetu wanafanya maisha Na siku tukifa maskini ndio nyie nyie mtatucheka na kutukebehi!!

Tukidata kwa depression tukawa mateja ndio nyie nyie mtatudhihaki!!Acheni madogo waimbie TAWALA wapige hela walee familia zao!!

Upinzani hela wanazo sema wameamua tu na hawajali!!Basi kama hamjali msiwaseme wasanii wale!!Endeleeni kimya kimya na sisi tulioamua kuchagua kufa maskini!! #RomaMkatoliki2025
 
Roma asichojua ni kuwa wasanii hawawezi kujihusisha na wapinzani kwani watashughulikiwa,hivi amesahau nini kilimkuta na kwa nini.
Kwa sasa ni hakuna au ni wasanii wachache wanaoweza kukubali kujihusisha na wapinzani maana atashughulikiwa hata kama wakimtangazia mpunga.
Ila pia wasanii wote hao yani kama tasnia nzima ya entertainment kuanzia wanamuziki, wachekeshaji, watangazaji wamehamia dodoma. Sijui wanalipwa na CCM, na kama wanalipwa na CCM wote hiyo fedha aliyotaja basi bila shaka kuna namna hakuna pesa ya serikali na pesa ya chama.
 
Ndio wametengwa kwa sababu ni waoga kuonekana wako upinzani. CCM imewabeba wote na wanaiimbia huko, vyama vya upinzani vikaona isiwe nongwa ngoja vipambane vyenyewe bila wasanii. wasanii wenyewe ni waoga
 
Pesa wanatafuna wenyewe na vimada wao, wasanii wanaambiwa kunja ngumi kamanda..!! 😹

Hata mimi nisingekubali huo upuuzi, wawaimbie tu veggies, kila mmoja atazame maslahi yake..!!
 
Ni kipindi cha kuelekea kampeni za uchaguzi mkuu. Roma anaona ni fursa ya kupiga hela, kama vipi aende tu CCM akaimbe kukandia upinzani. Upinzani utasonga mbele hata bila wasanii wa kuwatumbuiza
 
Roma asichojua ni kuwa wasanii hawawezi kujihusisha na wapinzani kwani watashughulikiwa, hivi amesahau nini kilimkuta na kwanini.
Nae ameanza kuwa mnafiki, wakati anajua kila kitu na kilichomkimbiza bongo ni hicho hicho
 
Pesa wanatafuna wenyewe na vimada wao, wasanii wanaambiwa kunja ngumi kamanda..!! 😹

Hata mimi nisingekubali huo upuuzi, wawaimbie tu veggies, kila mmoja atazame maslahi yake..!!
aidee
 
Back
Top Bottom