Roma: Boss Ruge amehangaika na sisi kuanzia asubuhi mpaka sasa tupo pamoja naye

Mission kama ile ya kuteka kituo cha radio na tv mbele ya cctv camera.Inaonekana ni akili ileile na watu ni walewale.Same shit different day.Joyce Wowowo na baba yake watakuwa wanajua.
 
Baada kupatikana kwa msanii Roma na Moni pamoja na producer wao Bin laden nini kimeendelea sasa....... [emoji51][emoji51][emoji51][emoji51]
 
Kesho kuna tukio gani jingine linaloingiliana na la ROMA kuongea ?
 
Nadhani hii nayoo ni movie kama zingine tuu...!!
 
Ikiwa Roma alikuwa ametekwa alijuaje Ruge alikuwa ana muhangaikia? walikuwa pamoja?
Huu ni ushahidi kuwa ROMA hakutekwa bali ni michezo ya watu hahaha
 
Kila mtu mpenda haki na demokrasia katika nchi yetu anapenda kusikia ni nini kiliwapata kina Roma pamoja wenzake...

- Ni nani aliyewateka?
- Walipelekwa wapi?
- Walifanywa nini?
- Aliyewateka alikuwa na lengo gani?

Sasa sisi kama watanzania tumekuwa tukisisitiza waseme ukweli bila woga hata kama maisha yao yatakuwa hatarini kiasi gani ila tunawataka waseme ukweli, Sasa hoja yangu ni hii, kwa unafiki wa tulio wengi ni nini tutakifanya kama watanzania endapo watatutajia aliyewateka?

Nini tutakifanya endapo kama utekaji huo utakuwa ulifanywa na kiongozi wa serikali/ raia wa kawaida?

Je, tutaendeleza unafiki wakusema tunaishauri serikali/rais achukue hatua wakati alishasema tusimpangie cha kufanya?

Nini tunaenda kufanya kama tukiujua ukweli na muhusika wa huu unyama!?

Tuweke itikadi zetu kando, tujadili kama watanzania. UNAFIKI NI DHAMBI MBELE ZA MUNGU.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…