Roma Mkatoliki amwibua Mwakyembe, adai hana elimu ya kumshauri yeye mwenye digrii 4. Kama anapenda siasa aanzishe chama cha siasa

Roma Mkatoliki amwibua Mwakyembe, adai hana elimu ya kumshauri yeye mwenye digrii 4. Kama anapenda siasa aanzishe chama cha siasa

Kwani kufundisha vyuo vikuu ndo kuwa na akili? aliyesema kaokotwa jalalani hakuwa professor wa chuo kikuu kabla ya kuokotwa? Huyu ahurumiwe tu.
Mtu anaweza kuwa na digrii hata 10 lakini akawa wa hovyo kuliko hata wa darasa la saba. Kwani si kuna mtu ana Phd lakini ukimsikiliza utazani anaongea kibajaji? Hizi sumu zimewathiri sana hawa ma Phd wetu hawako vizuri kabisa maana tulikuwa tunajiuliza kunani kumbe mlipigwa sumu na siri mmeitoa wenyewe.
 
Tulimumu, zamani wasomi walikuwa wanogopeka na kuheshimika saana, leo msomi hana toauti na ambaye hakusoma kwani hata ongea yao inajidhihirisha, wanaweza hata kusoma magazeti ya Udaku, zamani walikuwa wanabeba Daily News, Sunday News, The Citizen na mengineyo ndio yalikuwa magazeti yao
 
Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni kile kinachobakia baada ya kuondoa yote uliyofundishwa darasani.

Kwa mujibu wa Einstein kuna watu wakiondoa yale waliyofundishwa darasani, vichwa vyao vinabaki vitupu. Kitu pekee walichojaza kichwani ni walichofundishwa darasani. Hawa ndio hujisifia vyeti, au idadi ya "digrii" walizonazo. Hawana akili, japo wana elimu.

Einstein alisema hakuna uhusiano kati ya elimu na akili. Kuna watu wana elimu lakini hawana akili, na wengine wana akili lakini hawana elimu. Ni bora uwe na akili ukose elimu, kuliko uwe na elimu ukose akili.

Icons wa Sayansi kama Isaac Newton, Galileo Galilei na Archimedes of Syracuse hawakuwa na elimu yoyote ya cheti, diploma wala degree, lakini walikua na AKILI. Ugunduzi wao mpaka leo unaiongoza dunia.

Akili siku zote ni "superior" kuliko elimu kwa sababu akili ndio ilibuni elimu. Yani watu wenye akili walikaa wakaweka utaratibu wa mtu kukaa darasani na kujifunza kwa kipindi fulani, kisha apimwe kwa mitihani na atunukiwe cheti. Ubunifu huo ulifanywa na wenye akili. Kama huamini jiulize mtu wa kwanza kutunukiwa degree duniani alifundishwa na nani?

So mtu mwenye akili lakini akakosa elimu, ni msaada kwa jamii kuliko mtu mwenye elimu lakini akakosa akili. Mark Zukerberg hakumaliza shule lakini kwa kutumia akili amebuni mifumo rahisi ya mawasiliano kupitia mtandao.

Yeye ndiye mmiliki wa Facebook, Whatsapp na Instagram. Wale maprofesa waliomuona "kilaza" darasani leo wanatumia ubunifu wake kuendesha maisha yao. Kama sio FB basi wanatumia Instagram au Whatsapp. Maprofesa wenye elimu kubwa wamezidiwa ujanja na "kilaza" mwenye Akili.

Usijidharau kwa uchache wa madarasa ulionayo, unaweza kuwa na akili nyingi kuliko mwenye degree 4.

Kumbuka Einstein alisema akili ni kile kinachobakia baada ya kuondoa yote uliyofundishwa darasani. Jiulize ukiondoa yale uliyofundishwa darasani unabaki na nini? Yani ukiondoa hiyo diploma, degree au PhD unayojivunia, kichwa chako kinabaki na nini?

Kama kuna kitu kinabakia basi hicho kinachobakia kinaitwa "AKILI". Na kama hamna kinachobakia basi hilo bichwa halina tofauti na mtungi wa gesi.
#SinaAkili
#NinaDegree4

Malisa GJ
Naomba hii atumiwe moja kwa moja Dr Mwakyembe na Dr wa Korosho pale juu.
 
"Kama msanii unang'ang'ana kuimba siasa na kukosoa serikali basi amua kuachana na muziki uanzishe chama cha siasa. Lakini kama unataka kupata maslahi kwenye muziki, basi nyimbo hizo hazilipi. Haiingii akilini nina shahada nne halafu msanii ambaye hajaenda hata shule anatunga nyimbo za kunikosoa. Wewe na darasa la nne lako sijui la 7 utanionya mimi mwenye degree nne na nimefundisha vyuo vikuu mbalimbali?"

Dr.Harisson Mwakyembe (PhD), Waziri wa Habari, Sanaa na Michezo.!
Hapo ndiyo utajua tofauti ya mtu aliyeelimika na aliyehudhuria darasani
 
imefanya kushare tu wazee

Image may contain: 1 person, smiling, suit

Na Anderson Ndambo

HERI KIJANA MWENYE HEKIMA KULIKO MZEE MPUMBAVU.
Waziri wa habari na michezo ametamka maneno ambayo ni kichefuchefu kuweza kutamkwa na mtu wa elimu na umri wake mbele za jamii.
Amesema, Mtu mwenye elimu ya darasa la saba hawezi kuwa nasifa ya kumkosoa mtu mwenye elimu ya digrii 4. Kwamba Roma mkatoliki aliewasilisha ukosoaji wake dhidi ya serikali kupitia kipaji chake anakosa sifa ya kuikosoa serikali kwasababu elimu yake ni darasa la saba na wakati serikalini ni watu wenye digrii nyingi, upumbavu mtupu.
Kwa tafsiri ya jumla kutoka kwenye maoni ya msomi huyu mwenye PHD ya sheria ni kwamba.
1. Wanzania wote wenye elimu chini ya darasa la saba, hawana sifa za kuhoji au kukosoa jambo lolote lile tu kama mkosolewaji ana Elimu kubwa. Kwahiyo kukifanyika mauwaji kama ya Kibiti, Kigoma, Lindi na kwingineko, watanzania hawapaswi kuhoji au kukosoa kama hawana elimu zaidi ya darasa la saba.
2. Kukifanyika ufisadi na wizi wa mali za umma, kama kupotea fedha za umma za Trilioni 2.5, watanzania wote wenye elimu chini ya darasa la saba, wanakosa sifa ya kuikosoa serikali na kuhoji kwasababu watekelezaji wa wizi huo ni wenye elimu kubwa kama ya waziri.
3. Msingi wa kuikosoa serikali na watendaji wake ni elimu, kwamba wasio na elimu zaidi ya darasa la saba, hawana sifa na haki ya kuikosoa serikali ya Tanzania na watendaji wake kwenye makosa yoyote yale.
4. Waziri ameamua kuwaondolea watanzania wote wenye elimu chini ya darasa la saba haki ya kikatiba ya kutoa maoni, kuikosoa serikali.
5. Kwa uelewa wa msomi huyu mwenye PHD ni kwamba, ufahamu wa kupanda kwa gharama za maisha, umuhimu wa bima za afya, umuhimu wa kilimo kwa wakulima na wafanyabiashara unapatikana tu kwa watu ambao elimu zao ni juu ya darasa la saba. Kwamba watu wenye elimu chini ya darasa la saba, hawana haki na uwezo wa kujua ugumu wa maisha, kupanda kwa gharama za mahitaji muhimu. Haya ndio mawazo ya mtu mwenye phd.
Kwa kuhitimisha, ni sawa na kusema, kwenue uchaguzi mkuu ujao, Mwakyembe na wasomi wenzie wanaoamini kayika hilo na wasiotaka kukosolewa na watu walio na elimu ya darasa la saba, baasi wajiandae kuwatafuta wasomi wenzao watakao wapigia kura.
Nikisema ni heri ROMA MKAYOLIKI kijana mwenye hekima kuliko mzee pumbavu mwenye digrii 4 nitakuwa nimekosea. Hakika Viongozi hawana maarifa, hawataki kukosolewa.
 
"Kama msanii unang'ang'ana kuimba siasa na kukosoa serikali basi amua kuachana na muziki uanzishe chama cha siasa. Lakini kama unataka kupata maslahi kwenye muziki, basi nyimbo hizo hazilipi. Haiingii akilini nina shahada nne halafu msanii ambaye hajaenda hata shule anatunga nyimbo za kunikosoa. Wewe na darasa la nne lako sijui la 7 utanionya mimi mwenye degree nne na nimefundisha vyuo vikuu mbalimbali?"

Dr.Harisson Mwakyembe (PhD), Waziri wa Habari, Sanaa na Michezo.!
Wale walokuwa wanamsifia sana Mwakyembe miaka flani ya nyuma waje wamsifie na hili.

Amejaribu kuonesha uafrika wake sasa[emoji3][emoji3][emoji3]
 
Roma arudi shule jamani

Mtu anaefundisha au aliwahi kufundisha chuo sio wa kumfananisha na alieishia darasa la saba jamani huo ni ukweli usiopingika

Mwakyembe alipasua GPA kubwa Bachelor akabakizwa kuwa mwanataaluma UDSM huwezi fananisha na Msanii yeyote hapa nchini
Wasomi kibongobongo unafiki tu angekuwa hivyo angelikata chapisho lake la serikari tatu za muungano?
 
"Kama msanii unang'ang'ana kuimba siasa na kukosoa serikali basi amua kuachana na muziki uanzishe chama cha siasa. Lakini kama unataka kupata maslahi kwenye muziki, basi nyimbo hizo hazilipi. Haiingii akilini nina shahada nne halafu msanii ambaye hajaenda hata shule anatunga nyimbo za kunikosoa. Wewe na darasa la nne lako sijui la 7 utanionya mimi mwenye degree nne na nimefundisha vyuo vikuu mbalimbali?"

Dr.Harisson Mwakyembe (PhD), Waziri wa Habari, Sanaa na Michezo.!

Ulipokuja kutuomba kura za UBUNGE, ulitupigia magoti hata sisi tusiojua kusoma na kuandika. Isitoshe ulikubali kwa dhati kutusikiliza na kutekeleza mapendekezo yetu tuliyokushauri kwani sisi ndio wafalme wa maisha yetu na tunaojua ni vipi vijiji vyetu vitaondokana na matatizo hayo.

Leo unaturuka na kusema hatuwezi kukushauri kwa vile una degree 4 na umefundisha chuo kikuu, nasi hata darasa la saba hatujafika. Jamani, CCM ndivyo walivyo.

Tunakusubiri mwakani tu, 2020 tuone utatuambiaje? Vinginevyo tutakutosa na CCM yako twende kwa wanyonge wenzetu wapinzani. Usitukane wakunga na uzazi ungalipo.
 
Mi nafkiri angemshauri kwanza Harmonise na wimbo wake wa Magufuli hapo ningeekewa kuwa Roma na eye anapaswa aweje
 
maajabu msomi wa shahada nne hajui kazi za fasihi katika jamii
Aiseeee, these guys hawazi encourage kabisa kwenda kutafuta degree nyingine, ni kama kwenda kuongeza ujinga kwenye ujinga nilionao.
Degree zenyewe hizi za jalalani- Ni uchizi ulio ndani ya ukichaa. She""zi zao.
 
Kwa akili za degree nne za Mwakyembe tunahitaji kuwa na vyama vipya vya siasa...
Chama cha ROMA
Chama cha TRUBOI
Chama cha KALA
Chama cha NANDY
Chama cha HAMONAIZI
Chama cha DAIMONDI
Chama cha BEKAFLEVA
Chama cha MASHAUZI
Chama cha MSECHU
Chama cha.... (wengine sijasikia tungo zao)
_____
Hao wengi hawajamgusa, kaguswa na ROMA tu kwasababu hasifu na kuabudu namna watakavyo waabudiwa.
 
Hata wapumbavu huzeeka
imefanya kushare tu wazee

Image may contain: 1 person, smiling, suit

Na Anderson Ndambo

HERI KIJANA MWENYE HEKIMA KULIKO MZEE MPUMBAVU.
Waziri wa habari na michezo ametamka maneno ambayo ni kichefuchefu kuweza kutamkwa na mtu wa elimu na umri wake mbele za jamii.
Amesema, Mtu mwenye elimu ya darasa la saba hawezi kuwa nasifa ya kumkosoa mtu mwenye elimu ya digrii 4. Kwamba Roma mkatoliki aliewasilisha ukosoaji wake dhidi ya serikali kupitia kipaji chake anakosa sifa ya kuikosoa serikali kwasababu elimu yake ni darasa la saba na wakati serikalini ni watu wenye digrii nyingi, upumbavu mtupu.
Kwa tafsiri ya jumla kutoka kwenye maoni ya msomi huyu mwenye PHD ya sheria ni kwamba.
1. Wanzania wote wenye elimu chini ya darasa la saba, hawana sifa za kuhoji au kukosoa jambo lolote lile tu kama mkosolewaji ana Elimu kubwa. Kwahiyo kukifanyika mauwaji kama ya Kibiti, Kigoma, Lindi na kwingineko, watanzania hawapaswi kuhoji au kukosoa kama hawana elimu zaidi ya darasa la saba.
2. Kukifanyika ufisadi na wizi wa mali za umma, kama kupotea fedha za umma za Trilioni 2.5, watanzania wote wenye elimu chini ya darasa la saba, wanakosa sifa ya kuikosoa serikali na kuhoji kwasababu watekelezaji wa wizi huo ni wenye elimu kubwa kama ya waziri.
3. Msingi wa kuikosoa serikali na watendaji wake ni elimu, kwamba wasio na elimu zaidi ya darasa la saba, hawana sifa na haki ya kuikosoa serikali ya Tanzania na watendaji wake kwenye makosa yoyote yale.
4. Waziri ameamua kuwaondolea watanzania wote wenye elimu chini ya darasa la saba haki ya kikatiba ya kutoa maoni, kuikosoa serikali.
5. Kwa uelewa wa msomi huyu mwenye PHD ni kwamba, ufahamu wa kupanda kwa gharama za maisha, umuhimu wa bima za afya, umuhimu wa kilimo kwa wakulima na wafanyabiashara unapatikana tu kwa watu ambao elimu zao ni juu ya darasa la saba. Kwamba watu wenye elimu chini ya darasa la saba, hawana haki na uwezo wa kujua ugumu wa maisha, kupanda kwa gharama za mahitaji muhimu. Haya ndio mawazo ya mtu mwenye phd.
Kwa kuhitimisha, ni sawa na kusema, kwenue uchaguzi mkuu ujao, Mwakyembe na wasomi wenzie wanaoamini kayika hilo na wasiotaka kukosolewa na watu walio na elimu ya darasa la saba, baasi wajiandae kuwatafuta wasomi wenzao watakao wapigia kura.
Nikisema ni heri ROMA MKAYOLIKI kijana mwenye hekima kuliko mzee pumbavu mwenye digrii 4 nitakuwa nimekosea. Hakika Viongozi hawana maarifa, hawataki kukosolewa.
 
NINA DEGREE NNE ZA HOVYO HOVYO!
Na. Robert Heriel.
Mimi ni mjinga sana. Tena mimi ni mpuuzi nisiyevumilika. Yaani ati kisa nina Vishahada vyangu sijui nimevipatia pale UDSM. Au sijui nimevipatia nje ya nchi ndio nisikosolewe. Mimi ni mpuuzi sana.
Tena watoto wangu wa niliowazaa nioneni kuwa Baba yenu nilikuwa Baba Jinga lisilo na akili. Baba lenu lilienda kusomea shahada za ujinga ujinga ndio maana nipo hivi nilivyo.

Kisa ninadegree nne ndio nisikosolewe. Hivi Mimi Baba yenu kama sio chizi nitakuwa mwendawazimu tuu.
Nisikosolewe kwa lipi la maana nililolifanya hapa duniani. Lipi la kujisifu mpaka ati nisikosolewe. Au ni hivi vishahada uchwara vya kukariri madesa ya watu walioandika zamani. Kukariri madesa ati ndio nisikosolewe na wasiokariri madesa. Kweli nina degree nne za hovyo kichwani.

Mtu sina la maana nililolifanya. Zaidi ya kuvaa joho na kofia zisizo na maana yoyote kwa jamii yangu. Zaidi ya kujifanya naongea maandishi ya wengine sina la maana nililolifanya. Alafu natishia watu na degree nne.
Degree nne nashindwa kukemee maovu yanayofanywa kwenye jamii. Ati kisa nina degree nne ndio maana siwezi kukemee mauaji yaliyotokea. Siwezi kemea utekaji. Siwezi kemea ukandamizaji wa haki za watu. Ati kisa nina degree nne. Mimi ni mwendawazimu.

Degree nne zote ninashindwa kutoa mawazo chanya kuhusu kutatua tatizo la ajira. Mimi kazi yangu kujifaraguza tuu. Sina la maana zaidi ya maneno matupu na mikwala tuu ya kipuuzi. Ninawapiga mikwala wasiokuwa na degree kama mimi. Wanangu Mungu asiwalaani ikiwa mtaniona Baba yenu ni mjinga. Tena mnicheke na kunitukana. Na Mungu asiwahesabie dhambi.

Degree nne ninashindwa hata na Diamond Platnum ambaye hajui hata chuo ni nini. Diamond kanishinda na Shahada zangu nne kutengeneza ajira kwa vijana nchini. Lakini mimi nimebaki na degree kabatini. Degree nyingine mdomoni nazitapika kwenye vyombo vya habari nikiwatisha wasiosoma.
Ambao hawajasoma wanawasaidia Watanzania makundi kwa makundi. Maelfu kwa maelfu. Lakini Mimi degree nne nashindwa hata kuwasaidia Watanzania zaidi ya kudai posho na pesa zao.
Sitaki kukosolewa kwa lipi hasa nililo nalo la maana. Ni hizo degree za hovyo ambazo haziisaidii jamii. Au ni hiki cheo changu nilichopewa.

Nina degree nne za hovyo ndio maana najisikia aibu kukosolewa na Vijana wa darasa la saba wanaokemea maovu katika jamii. Yaani Haki za kisiasa zinakandamizwa alafu mimi nakalia degree nne zangu za kipuuzi puuzi tuu.
Unajua Taikon ni kweli shule nimeenda. Nimesoma madesa na kukariri maneno na alama zote za uandishi. Nimekariri mpaka picha na michoro yote ya kisomi. Nimekariri namba na Wataalamuna wote.

Nina degree nne lakini nashindwa kubuni mbinu nne za kuwasaidia Wasanii wafanye sanaa itakayolibadili taifa hili. Nimeshindwa kuzuia waimbaji wa matusi lakini waimbaji wanaokemea maovu ninawakemea. Mungu nilaani ikiwa nitamkemea anayekemea maovu. Mungu ni laani hizi degree zangu ziwe upumbavu niwe aibu kwa watu ikiwa nitashindwa kukemea maovu. Ikiwa nitawazuia wanaotetea wanyonge na kukemea maovu wasiwakemee watendao maovu. Ni laani Ewe Mungu na Degree zangu hizo nne.

Nina degree nne lakini nashindwa kupandisha thamani ya shilingi dhidi ya dola. Alafu mtu anione wa maana. La maana kwangu ni lipi hasa. Ninatangaza rasmi degree zangu nne ni za hovyo ikiwa ninashindwa kupandisha thamani ya dola.
Nina Degree nne lakini nashindwa kutoa mbinu kila mwanachuo apewe mkopo bila kujali anatoka familia bora au masikini. Bila kujali mwanafunzi amesoma Mchepuo wa sanaa au ya sayansi au biashara. Mimi nina maana ipi hasa na hizi degree zangu.

Nina degree nne lakini ninashindwa kumkabili Rais na kumshauri hata kwenye sakata la Korosho mpaka taifa linaingia hasara na Wakulima wanasota. Bado niheshimike. Nina heshimika kwa lipi zaidi ya kuonekana mhuni tuu niliyeliibia taifa kodi na kupoteza pesa za watu wa taifa langu. Nina Degree nne lakini nimeshindwa kuinua Sekta ya Kilimo. Soko la Pamba, Kahawa na mahindi linayumba kama unyoya. Alafu mtu anione wa maana. Ati Nisikosolewe kisa na mkasa nina vidigrii vyangu vinne uchwara.

Nina degree nne za nini kama sio za hovyo. Kama sikusomea ujinga embu aje mtu aniambie nilisomea nini.
Nawezaje kuwa na degree nne lakini nashindwa kuwapa waandishi uhuru katika kazi zao. Mpaka utekaji unafanyika. Watu wanapigwa risasi waandishi wanashindwa kufanya uchunguzi na kutoa habari nzito kuhusiana na matukio tata yanayoeakabili wananchi wenzangu alafu mtu akinikosoa bado nimuite Darasa la Saba. Sijui Darasa la tatu B. Taikon kweli nimechanganyikiwa walahi.

Nina Degree nne lakini mpaka sasa sijaona umuhimu wa Katiba Mpya. Wala sijafanya jitihada za upatikanaji wake. Bado nisikosolewe na kuonekana kama wengine. Kwa kipi hasa cha maana. Ati najiongelesha kwa mbwembwe ati nina degree nne. Hahahah!.
Labda degree za centigredi kama sio fahrent sijui nini huko. Wataalamu wa Fizikia ndio watatuambia ni degree za joto au za pembe. Hahaha!

Nina Degree nne lakini mpaka sasa sijabuni jambo lolote linaloendana na degree zangu nilizozisomea. Sijui huko chuo nilienda kusoma magazeti au fema. Degree nne sio lelemama. Yaani nashindwa kubuni hata jambo dogo linaloendana na fani yangu. Atu ubunifu wangu ni kuzuia watetezi wa haki na wanaopinga uovu. Hivi mimi kama sijasomea degree ya hovyo si nitakuwa kichaa mimi.

Jamani Nina degree nne sitaki mtu atoe maoni yake kwenye posti yangu kwa maana ninyi hamjasoma kama mimi. Hamna elimu ya kukomenti katika mada hii. Ninyi ni vilaza.
Ngoja nipumzike.

Eeh Mungu wangu. Naomba unilaani ikiwa nitafikia hatua nitawapinga wale wote wanapigania haki. Wale wanaopinga maovu. Hiyo itakuwa dalili ya kukupinga wewe. Tafsiri yake ni kuwa siku nikiwa nafanya maovu watu wataniacha bila ya kunikosoa ili nikurudie ewe Mungu wangu.

Na alaaniwe mtu yeyote awapingao na kuwakemea wanaotetea haki. Tena alaaniwe mtu awapingao wapingao maovu. Mtu huyo awe kituko hata kizazi cha sita na saba cha watakaorithi tabia zake.
Jumbe hii isomwe na wenye degree nne kama mimi.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
 
Aione Mheshi-miwa Mwakinembe
IMG-20191116-WA0028.jpeg
 
Back
Top Bottom