Coaster2015
JF-Expert Member
- Aug 21, 2018
- 2,607
- 2,730
HopelessDegree nne sio mchezo tuache utani,sio kila moja anaweza kusoma hivyo
Mwacheni mwakyembe ajidai
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
HopelessDegree nne sio mchezo tuache utani,sio kila moja anaweza kusoma hivyo
Mwacheni mwakyembe ajidai
Mtu anaweza kuwa na digrii hata 10 lakini akawa wa hovyo kuliko hata wa darasa la saba. Kwani si kuna mtu ana Phd lakini ukimsikiliza utazani anaongea kibajaji? Hizi sumu zimewathiri sana hawa ma Phd wetu hawako vizuri kabisa maana tulikuwa tunajiuliza kunani kumbe mlipigwa sumu na siri mmeitoa wenyewe.Kwani kufundisha vyuo vikuu ndo kuwa na akili? aliyesema kaokotwa jalalani hakuwa professor wa chuo kikuu kabla ya kuokotwa? Huyu ahurumiwe tu.
1Kwa hiyo tuseme Mwakyembe:
1. ana elimu lakini hana akili!
2. Au ana vyote elimu na akili au
3. ana akili hana elimu!
chagua moja tu!
Tulimumu, zamani wasomi walikuwa wanogopeka na kuheshimika saana, leo msomi hana toauti na ambaye hakusoma kwani hata ongea yao inajidhihirisha, wanaweza hata kusoma magazeti ya Udaku, zamani walikuwa wanabeba Daily News, Sunday News, The Citizen na mengineyo ndio yalikuwa magazeti yaoMtu anaweza kuwa na digrii hata 10 lakini akawa wa hovyo kuliko hata wa darasa la saba. Kwani si kuna mtu ana Phd lakini ukimsikiliza utazani anaongea kibajaji? Hizi sumu zimewathiri sana hawa ma Phd wetu hawako vizuri kabisa maana tulikuwa tunajiuliza kunani kumbe mlipigwa sumu na siri mmeitoa wenyewe.
Naomba hii atumiwe moja kwa moja Dr Mwakyembe na Dr wa Korosho pale juu.Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni kile kinachobakia baada ya kuondoa yote uliyofundishwa darasani.
Kwa mujibu wa Einstein kuna watu wakiondoa yale waliyofundishwa darasani, vichwa vyao vinabaki vitupu. Kitu pekee walichojaza kichwani ni walichofundishwa darasani. Hawa ndio hujisifia vyeti, au idadi ya "digrii" walizonazo. Hawana akili, japo wana elimu.
Einstein alisema hakuna uhusiano kati ya elimu na akili. Kuna watu wana elimu lakini hawana akili, na wengine wana akili lakini hawana elimu. Ni bora uwe na akili ukose elimu, kuliko uwe na elimu ukose akili.
Icons wa Sayansi kama Isaac Newton, Galileo Galilei na Archimedes of Syracuse hawakuwa na elimu yoyote ya cheti, diploma wala degree, lakini walikua na AKILI. Ugunduzi wao mpaka leo unaiongoza dunia.
Akili siku zote ni "superior" kuliko elimu kwa sababu akili ndio ilibuni elimu. Yani watu wenye akili walikaa wakaweka utaratibu wa mtu kukaa darasani na kujifunza kwa kipindi fulani, kisha apimwe kwa mitihani na atunukiwe cheti. Ubunifu huo ulifanywa na wenye akili. Kama huamini jiulize mtu wa kwanza kutunukiwa degree duniani alifundishwa na nani?
So mtu mwenye akili lakini akakosa elimu, ni msaada kwa jamii kuliko mtu mwenye elimu lakini akakosa akili. Mark Zukerberg hakumaliza shule lakini kwa kutumia akili amebuni mifumo rahisi ya mawasiliano kupitia mtandao.
Yeye ndiye mmiliki wa Facebook, Whatsapp na Instagram. Wale maprofesa waliomuona "kilaza" darasani leo wanatumia ubunifu wake kuendesha maisha yao. Kama sio FB basi wanatumia Instagram au Whatsapp. Maprofesa wenye elimu kubwa wamezidiwa ujanja na "kilaza" mwenye Akili.
Usijidharau kwa uchache wa madarasa ulionayo, unaweza kuwa na akili nyingi kuliko mwenye degree 4.
Kumbuka Einstein alisema akili ni kile kinachobakia baada ya kuondoa yote uliyofundishwa darasani. Jiulize ukiondoa yale uliyofundishwa darasani unabaki na nini? Yani ukiondoa hiyo diploma, degree au PhD unayojivunia, kichwa chako kinabaki na nini?
Kama kuna kitu kinabakia basi hicho kinachobakia kinaitwa "AKILI". Na kama hamna kinachobakia basi hilo bichwa halina tofauti na mtungi wa gesi.
#SinaAkili
#NinaDegree4
Malisa GJ
Mwambieni Mwakyembe atulie sindano imuingie vizuri hadi mwisho.
Hapo ndiyo utajua tofauti ya mtu aliyeelimika na aliyehudhuria darasani"Kama msanii unang'ang'ana kuimba siasa na kukosoa serikali basi amua kuachana na muziki uanzishe chama cha siasa. Lakini kama unataka kupata maslahi kwenye muziki, basi nyimbo hizo hazilipi. Haiingii akilini nina shahada nne halafu msanii ambaye hajaenda hata shule anatunga nyimbo za kunikosoa. Wewe na darasa la nne lako sijui la 7 utanionya mimi mwenye degree nne na nimefundisha vyuo vikuu mbalimbali?"
Dr.Harisson Mwakyembe (PhD), Waziri wa Habari, Sanaa na Michezo.!

Exactly anajificha kwenye kivuli cha usomi uchwaraMtu anae jisifu kasoma ujue kashindwa hoja hapo unakuwa anatafuta pa kutokea
Mi huwa na mdarau yeyote anae hisi kasoma haihitaji ushauri wa wenzake
Wale walokuwa wanamsifia sana Mwakyembe miaka flani ya nyuma waje wamsifie na hili."Kama msanii unang'ang'ana kuimba siasa na kukosoa serikali basi amua kuachana na muziki uanzishe chama cha siasa. Lakini kama unataka kupata maslahi kwenye muziki, basi nyimbo hizo hazilipi. Haiingii akilini nina shahada nne halafu msanii ambaye hajaenda hata shule anatunga nyimbo za kunikosoa. Wewe na darasa la nne lako sijui la 7 utanionya mimi mwenye degree nne na nimefundisha vyuo vikuu mbalimbali?"
Dr.Harisson Mwakyembe (PhD), Waziri wa Habari, Sanaa na Michezo.!
Wasomi kibongobongo unafiki tu angekuwa hivyo angelikata chapisho lake la serikari tatu za muungano?Roma arudi shule jamani
Mtu anaefundisha au aliwahi kufundisha chuo sio wa kumfananisha na alieishia darasa la saba jamani huo ni ukweli usiopingika
Mwakyembe alipasua GPA kubwa Bachelor akabakizwa kuwa mwanataaluma UDSM huwezi fananisha na Msanii yeyote hapa nchini
Huko mbali sana. Anzia hapa hapa Mbagala kwa Diamond Platinumz.Muziki na digrii wapi na wapi mbona Michael Jackson hakusoma na alikuwa anajulikana Dunia nzima.
"Kama msanii unang'ang'ana kuimba siasa na kukosoa serikali basi amua kuachana na muziki uanzishe chama cha siasa. Lakini kama unataka kupata maslahi kwenye muziki, basi nyimbo hizo hazilipi. Haiingii akilini nina shahada nne halafu msanii ambaye hajaenda hata shule anatunga nyimbo za kunikosoa. Wewe na darasa la nne lako sijui la 7 utanionya mimi mwenye degree nne na nimefundisha vyuo vikuu mbalimbali?"
Dr.Harisson Mwakyembe (PhD), Waziri wa Habari, Sanaa na Michezo.!
Aiseeee, these guys hawazi encourage kabisa kwenda kutafuta degree nyingine, ni kama kwenda kuongeza ujinga kwenye ujinga nilionao.maajabu msomi wa shahada nne hajui kazi za fasihi katika jamii
imefanya kushare tu wazee
Na Anderson Ndambo
HERI KIJANA MWENYE HEKIMA KULIKO MZEE MPUMBAVU.
Waziri wa habari na michezo ametamka maneno ambayo ni kichefuchefu kuweza kutamkwa na mtu wa elimu na umri wake mbele za jamii.
Amesema, Mtu mwenye elimu ya darasa la saba hawezi kuwa nasifa ya kumkosoa mtu mwenye elimu ya digrii 4. Kwamba Roma mkatoliki aliewasilisha ukosoaji wake dhidi ya serikali kupitia kipaji chake anakosa sifa ya kuikosoa serikali kwasababu elimu yake ni darasa la saba na wakati serikalini ni watu wenye digrii nyingi, upumbavu mtupu.
Kwa tafsiri ya jumla kutoka kwenye maoni ya msomi huyu mwenye PHD ya sheria ni kwamba.
1. Wanzania wote wenye elimu chini ya darasa la saba, hawana sifa za kuhoji au kukosoa jambo lolote lile tu kama mkosolewaji ana Elimu kubwa. Kwahiyo kukifanyika mauwaji kama ya Kibiti, Kigoma, Lindi na kwingineko, watanzania hawapaswi kuhoji au kukosoa kama hawana elimu zaidi ya darasa la saba.
2. Kukifanyika ufisadi na wizi wa mali za umma, kama kupotea fedha za umma za Trilioni 2.5, watanzania wote wenye elimu chini ya darasa la saba, wanakosa sifa ya kuikosoa serikali na kuhoji kwasababu watekelezaji wa wizi huo ni wenye elimu kubwa kama ya waziri.
3. Msingi wa kuikosoa serikali na watendaji wake ni elimu, kwamba wasio na elimu zaidi ya darasa la saba, hawana sifa na haki ya kuikosoa serikali ya Tanzania na watendaji wake kwenye makosa yoyote yale.
4. Waziri ameamua kuwaondolea watanzania wote wenye elimu chini ya darasa la saba haki ya kikatiba ya kutoa maoni, kuikosoa serikali.
5. Kwa uelewa wa msomi huyu mwenye PHD ni kwamba, ufahamu wa kupanda kwa gharama za maisha, umuhimu wa bima za afya, umuhimu wa kilimo kwa wakulima na wafanyabiashara unapatikana tu kwa watu ambao elimu zao ni juu ya darasa la saba. Kwamba watu wenye elimu chini ya darasa la saba, hawana haki na uwezo wa kujua ugumu wa maisha, kupanda kwa gharama za mahitaji muhimu. Haya ndio mawazo ya mtu mwenye phd.
Kwa kuhitimisha, ni sawa na kusema, kwenue uchaguzi mkuu ujao, Mwakyembe na wasomi wenzie wanaoamini kayika hilo na wasiotaka kukosolewa na watu walio na elimu ya darasa la saba, baasi wajiandae kuwatafuta wasomi wenzao watakao wapigia kura.
Nikisema ni heri ROMA MKAYOLIKI kijana mwenye hekima kuliko mzee pumbavu mwenye digrii 4 nitakuwa nimekosea. Hakika Viongozi hawana maarifa, hawataki kukosolewa.