Roma Mkatoliki mbaroni nchini Marekani kwa kosa la madawa ya kulevya
Taarifa kamili inafuatiliwa kwa kina na Watanzania waishio Marekani, inawezekana inachelewa kwasababu Roma sio msanii maarufu Marekani hivyo basi ili kupata taarifa zake inalazimu Watanzania waishio Marekani wafuatilie kwa undani lakini vilevile ITV waulizwe undani wa habari hii kwasababu Template yao ni ushahidi kuwa walichapisha taarifa hii
Ushahidi: Bei Facebook anmelden

- Tunachokijua
- Ibrahim Mussa ambaye amekuwa akifahamika kama Roma Mkatoliki, ni msanii wa muziki aina ya Hiphop ambaye kwa kiasi kikubwa mashairi yake yamekuwa yakigusa maslahi ya wananchi, pia ni mwanaharakati ambaye amekua akikosoa utendaji wa serikali pamoja na kupigania haki za binadamu.
Madai
Kumekuwapo na machapisho yanayosambazwa mtandaoni yakidaiwa kuchapishwa na ITV pamoja na Jambo TV yakiwa na madai ya kukamatwa kwa Roma mkatoliki akihusishwa na madawa ya kulevya.
Uhalisia
Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia utafutaji wa maneno muhimu (Key Word Search) umebaini kuwa madai hayo Si ya Kweli, kwani hayajachapishwa kwenye kurasa rasmi za ITV na Jambo TV.
Aidha yamebainika mapungufu kadhaa katika chapisho hilo yanayodhihirishwa kuwa ni la kutengenezwa na wapotoshaji. Sehemu ya nyuma palipoandikwa tarehe muonekano wake haufanani na machapisho rasmi ya ITV, pia mwandiko (font) uliotumika kwenye tarehe pia ni tofauti na ule unaotumiwa na machapisho rasmi.
Hata hivyo kupitia kupitia ukurasa wake wa Instagram Roma Mkatoliki amewataka wafuasi wake kuiipuza taarifa hiyo kwani si ya kweli.