SI KWELI PreGE2025 Roma Mkatoliki mbaroni nchini Marekani kwa kosa la madawa ya kulevya

SI KWELI PreGE2025 Roma Mkatoliki mbaroni nchini Marekani kwa kosa la madawa ya kulevya

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Roma Mkatoliki mbaroni nchini Marekani kwa kosa la madawa ya kulevya

Taarifa kamili inafuatiliwa kwa kina na Watanzania waishio Marekani, inawezekana inachelewa kwasababu Roma sio msanii maarufu Marekani hivyo basi ili kupata taarifa zake inalazimu Watanzania waishio Marekani wafuatilie kwa undani lakini vilevile ITV waulizwe undani wa habari hii kwasababu Template yao ni ushahidi kuwa walichapisha taarifa hii

Ushahidi: Bei Facebook anmelden

SIKWELI_8MEI25.jpg
SIKWELI_8MEI25B.jpg
 
Tunachokijua
Ibrahim Mussa ambaye amekuwa akifahamika kama Roma Mkatoliki, ni msanii wa muziki aina ya Hiphop ambaye kwa kiasi kikubwa mashairi yake yamekuwa yakigusa maslahi ya wananchi, pia ni mwanaharakati ambaye amekua akikosoa utendaji wa serikali pamoja na kupigania haki za binadamu.

Madai

Kumekuwapo na machapisho yanayosambazwa mtandaoni yakidaiwa kuchapishwa na ITV pamoja na Jambo TV yakiwa na madai ya kukamatwa kwa Roma mkatoliki akihusishwa na madawa ya kulevya.

Uhalisia

Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia utafutaji wa maneno muhimu (Key Word Search) umebaini kuwa madai hayo Si ya Kweli, kwani hayajachapishwa kwenye kurasa rasmi za ITV na Jambo TV.

Aidha yamebainika mapungufu kadhaa katika chapisho hilo yanayodhihirishwa kuwa ni la kutengenezwa na wapotoshaji. Sehemu ya nyuma palipoandikwa tarehe muonekano wake haufanani na machapisho rasmi ya ITV, pia mwandiko (font) uliotumika kwenye tarehe pia ni tofauti na ule unaotumiwa na machapisho rasmi.

Hata hivyo kupitia kupitia ukurasa wake wa Instagram Roma Mkatoliki amewataka wafuasi wake kuiipuza taarifa hiyo kwani si ya kweli.​

Attachments

  • snapins-ai_3627810332489176093.jpg
    snapins-ai_3627810332489176093.jpg
    137.5 KB · Views: 51
Screenshot_20250508-091344.jpg
Kwa hiyo hizo mahabusu za magharibi watuhumiwa wanatumia simu kama wapo uraiani?
 
Ni ngumu sana kukanusha kuwa taarifa hii haikuchapishwa na ITV kwasababu Template yao ni original

Njia ya kufanya ni kuwasiliana na ITV watupe uhakika wa habari yao lakini vilevile Diaspora watusaidie kufuatilia, anayetakiwa kukanusha habari hii ni ITV na sio sisi walaji

Pia tukumbuke ITV ni chombo kikubwa cha habari na sifa hiyo ndiyo inayotusukuma kuamini habari zinazochapishwa katika kurasa zao za mitandao ya kijamii

Ikiwa habari hii haina ukweli basi ITV wakanushe na ikiwa ni fake basi wamtafute mchapishaji huyo aliyeweka Facebook na ndiyo maana nimeambatanisha screenshot ili itumike kama ushahidi wa chanzo chake
Naona ndiyo umeanza kutumia Internet mwaka huu. Wewe kila kitu ni ''original''. Hjui hata kuwa hiyo watu wame-copy na kuandika watakacho.
 
Back
Top Bottom