SI KWELI PreGE2025 Roma Mkatoliki mbaroni nchini Marekani kwa kosa la madawa ya kulevya

SI KWELI PreGE2025 Roma Mkatoliki mbaroni nchini Marekani kwa kosa la madawa ya kulevya

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Roma Mkatoliki mbaroni nchini Marekani kwa kosa la madawa ya kulevya

Taarifa kamili inafuatiliwa kwa kina na Watanzania waishio Marekani, inawezekana inachelewa kwasababu Roma sio msanii maarufu Marekani hivyo basi ili kupata taarifa zake inalazimu Watanzania waishio Marekani wafuatilie kwa undani lakini vilevile ITV waulizwe undani wa habari hii kwasababu Template yao ni ushahidi kuwa walichapisha taarifa hii

Ushahidi: Bei Facebook anmelden

SIKWELI_8MEI25.jpg
SIKWELI_8MEI25B.jpg
 
Tunachokijua
Ibrahim Mussa ambaye amekuwa akifahamika kama Roma Mkatoliki, ni msanii wa muziki aina ya Hiphop ambaye kwa kiasi kikubwa mashairi yake yamekuwa yakigusa maslahi ya wananchi, pia ni mwanaharakati ambaye amekua akikosoa utendaji wa serikali pamoja na kupigania haki za binadamu.

Madai

Kumekuwapo na machapisho yanayosambazwa mtandaoni yakidaiwa kuchapishwa na ITV pamoja na Jambo TV yakiwa na madai ya kukamatwa kwa Roma mkatoliki akihusishwa na madawa ya kulevya.

Uhalisia

Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia utafutaji wa maneno muhimu (Key Word Search) umebaini kuwa madai hayo Si ya Kweli, kwani hayajachapishwa kwenye kurasa rasmi za ITV na Jambo TV.

Aidha yamebainika mapungufu kadhaa katika chapisho hilo yanayodhihirishwa kuwa ni la kutengenezwa na wapotoshaji. Sehemu ya nyuma palipoandikwa tarehe muonekano wake haufanani na machapisho rasmi ya ITV, pia mwandiko (font) uliotumika kwenye tarehe pia ni tofauti na ule unaotumiwa na machapisho rasmi.

Hata hivyo kupitia kupitia ukurasa wake wa Instagram Roma Mkatoliki amewataka wafuasi wake kuiipuza taarifa hiyo kwani si ya kweli.​

Attachments

  • snapins-ai_3627810332489176093.jpg
    snapins-ai_3627810332489176093.jpg
    137.5 KB · Views: 51
Moderator fungieni huyu. Anaharibu hadhi ya jukwaa kwa ku-post uongo wa kutunga.
Sisi sote tupo hapa kutafuta ukweli wa habari hii tukishirikiana na Watanzania waishio nchini Marekani kwasababu chapisho hili lilirushwa na ITV kama template yao inavyothibitisha
 
Mods piga ban mpuuzi huyu. No reforms, No election 2025.
Wakupigwa ban ni ITV na sio mimi kwasababu Template yao ni ushahidi tosha kuwa wanahaki ya kutupiwa lawama wao na sio watazamaji wao
 
Roma Mkatoliki mbaroni nchini Marekani kwa kosa la madawa ya kulevya

Roma Mkatoliki aingia mdomo wa chatu kwa jaribio la kuvunja Sheria za Marekani

Inawezekana jaribio hili lilikuwa la kujitoa mhanga kwasababu intelligence ya Marekani ni kubwa sana kiasi kwamba ni hatari kufanya majaribio ya kuvunja Sheria

Taarifa kamili inafuatiliwa kwa kina na Watanzania waishio Marekani, inawezekana inachelewa kwasababu Roma sio msanii maarufu Marekani hivyo basi ili kupata taarifa zake inalazimu Watanzania waishio Marekani wafuatilie kwa undani

Ushahidi: Bei Facebook anmelden

View attachment 3327021
Roma ni msanii maarufu marekani? You got bullshiting me😂😂
 
Roma ni msanii maarufu marekani? You got bullshiting me😂😂
Tunadhani undani wa habari hii unachelewa pengine kwasababu Roma sio msanii maarufu Marekani, Watanzania waishio Marekani wanafuatilia kwa kina ili wapate majibu kamili
 
Duh?!
Roma vipi tena dogo?! Rudi home kama yamekuwa hayo!
 
Ufisadi, wizi, uongo, utekaji, utesaji na mauaji...masikini Tanzania! Adui namba wani wa taifa hili ni CCM!
 
Kwahiyo wewe umeamini hiyo habari?
Inaweza kuaminiwa kwasababu ilichapishwa na chombo kikubwa cha habari cha ITV na template yao ni ushahidi kuwa walichapisha hivyo basi ni rahisi kuaminika, pengine ITV waulizwe
 
Inaweza kuaminiwa kwasababu ilichapishwa na chombo kikubwa cha habari cha ITV na template yao ni ushahidi kuwa walichapisha hivyo basi ni rahisi kuaminika, pengine ITV waulizwe
Yawezekana hizo ni Editing tu mkuu,
Technology imekuwa bila shaka unajua.

Juzi kuna waraka wa wakatoliki umetoka na Muhuri kabisa ila ulikuwa fake.

Sasa ww kuona nembo ya ITV ndio ukaamini ni kweli na kurusha huku?
Kwann usingesubiri hao watu wa marekan wadhibitishe kwanza
 
Ushauri wako ni sahihi
 
Wakupigwa ban ni ITV na sio mimi kwasababu Template yao ni ushahidi tosha kuwa wanahaki ya kutupiwa lawama wao na sio watazamaji wao
Una uhakika ni ITV wamepost hii au ni wajinga wametengeneza? Weka hiyo link inayotupeleka kwenye hii habari. Kwanza hiyo profile picture ya Mange haipo kwenye account zake zote.
 
Wale waliozaliwa USA wenyewe wasipokua na michongo ya maana wanaishia kuwa ma Homeless yeye kaenda huko kazi yake kupost twitter alaf anaishi maisha safi kumbe mtu ya dili
 
Wale waliozaliwa USA wenyewe wasipokua na michongo ya maana wanaishia kuwa ma Homeless yeye kaenda huko kazi yake kupost twitter alaf anaishi maisha safi kumbe mtu ya dili
Wabongo mmezoea ''michongo'' mnadhani kila sehemu watu wanaishi kwa michongo. Halafu jaribu kuwa na subra kwa sababu huna uhakika kama hili ni jambo la kweli.
 
Watanzania gani mnaowasemea nyie ilihali asubuhi tuu alikuwa ofisini kwake?

Hizo propaganda za kijinga sijui mnafundishiwa wapi? Mnamdhalilisha mpaka mnaempambania
 
Back
Top Bottom