SI KWELI PreGE2025 Roma Mkatoliki mbaroni nchini Marekani kwa kosa la madawa ya kulevya

SI KWELI PreGE2025 Roma Mkatoliki mbaroni nchini Marekani kwa kosa la madawa ya kulevya

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Roma Mkatoliki mbaroni nchini Marekani kwa kosa la madawa ya kulevya

Taarifa kamili inafuatiliwa kwa kina na Watanzania waishio Marekani, inawezekana inachelewa kwasababu Roma sio msanii maarufu Marekani hivyo basi ili kupata taarifa zake inalazimu Watanzania waishio Marekani wafuatilie kwa undani lakini vilevile ITV waulizwe undani wa habari hii kwasababu Template yao ni ushahidi kuwa walichapisha taarifa hii

Ushahidi: Bei Facebook anmelden

SIKWELI_8MEI25.jpg
SIKWELI_8MEI25B.jpg
 
Tunachokijua
Ibrahim Mussa ambaye amekuwa akifahamika kama Roma Mkatoliki, ni msanii wa muziki aina ya Hiphop ambaye kwa kiasi kikubwa mashairi yake yamekuwa yakigusa maslahi ya wananchi, pia ni mwanaharakati ambaye amekua akikosoa utendaji wa serikali pamoja na kupigania haki za binadamu.

Madai

Kumekuwapo na machapisho yanayosambazwa mtandaoni yakidaiwa kuchapishwa na ITV pamoja na Jambo TV yakiwa na madai ya kukamatwa kwa Roma mkatoliki akihusishwa na madawa ya kulevya.

Uhalisia

Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia utafutaji wa maneno muhimu (Key Word Search) umebaini kuwa madai hayo Si ya Kweli, kwani hayajachapishwa kwenye kurasa rasmi za ITV na Jambo TV.

Aidha yamebainika mapungufu kadhaa katika chapisho hilo yanayodhihirishwa kuwa ni la kutengenezwa na wapotoshaji. Sehemu ya nyuma palipoandikwa tarehe muonekano wake haufanani na machapisho rasmi ya ITV, pia mwandiko (font) uliotumika kwenye tarehe pia ni tofauti na ule unaotumiwa na machapisho rasmi.

Hata hivyo kupitia kupitia ukurasa wake wa Instagram Roma Mkatoliki amewataka wafuasi wake kuiipuza taarifa hiyo kwani si ya kweli.​

Attachments

  • snapins-ai_3627810332489176093.jpg
    snapins-ai_3627810332489176093.jpg
    137.5 KB · Views: 51
Inafikirisha sana kijana yeyote yule anapofanya majaribio ya kuvunja Sheria za bara la Ulaya, jambo la kushangaza sio madawa bali ni uthubutu wa kufanya jaribio hilo
Marekani sio ulaya
 
Kwamba huyu naye alikimbia "uovu" wa Magufuli! Taratibu ya gizani yatawekwa mezani mchana kweupe...

G55 ambao nao walikuwa wanalalamika kuwa Magufuli anataka "kuiamgamiza" Chadema kumbe aliziba mirija yao ndani ya CCM.

Ukweli huwa unachelewa kufika, na bado jogoo hajawika mara ya tatu, waliompiga risasi Tundu Lissu "kwa ramani walizopewa na akina Mrema" na wenzako watafahamika Tu!
 
Post umeweka photo ya itvdigital

Nategemea source itoke itv mkuu___ facebook page ya mtu binafsi mkuu?
Hiyo ni original ITV Template, hivyobasi waulizwe ITV
 
  • Thanks
Reactions: Lax
Mbona kule X yupo anajib comment
au marekani ukiwa mbaroni hunyang'anywi simu?
Tafadhali ITV waulizwe kwasababu hii ni original Template yao au maswali hayo tuyapeleke kwenye source hii kwasababu sisi sote tunatafuta ukweli wa habari hii Bei Facebook anmelden
 
Amekamatwa na madawa ya kulevya ama akiwa anataka kujitoa muhanga, mbona mnaandika visivyoeleweka?
 
Back
Top Bottom