SI KWELI PreGE2025 Roma Mkatoliki mbaroni nchini Marekani kwa kosa la madawa ya kulevya

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Roma Mkatoliki mbaroni nchini Marekani kwa kosa la madawa ya kulevya

Taarifa kamili inafuatiliwa kwa kina na Watanzania waishio Marekani, inawezekana inachelewa kwasababu Roma sio msanii maarufu Marekani hivyo basi ili kupata taarifa zake inalazimu Watanzania waishio Marekani wafuatilie kwa undani lakini vilevile ITV waulizwe undani wa habari hii kwasababu Template yao ni ushahidi kuwa walichapisha taarifa hii

Ushahidi: Bei Facebook anmelden

​
 
Tunachokijua
Ibrahim Mussa ambaye amekuwa akifahamika kama Roma Mkatoliki, ni msanii wa muziki aina ya Hiphop ambaye kwa kiasi kikubwa mashairi yake yamekuwa yakigusa maslahi ya wananchi, pia ni mwanaharakati ambaye amekua akikosoa utendaji wa serikali pamoja na kupigania haki za binadamu.

Madai

Kumekuwapo na machapisho yanayosambazwa mtandaoni yakidaiwa kuchapishwa na ITV pamoja na Jambo TV yakiwa na madai ya kukamatwa kwa Roma mkatoliki akihusishwa na madawa ya kulevya.

Uhalisia

Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia utafutaji wa maneno muhimu (Key Word Search) umebaini kuwa madai hayo Si ya Kweli, kwani hayajachapishwa kwenye kurasa rasmi za ITV na Jambo TV.

Aidha yamebainika mapungufu kadhaa katika chapisho hilo yanayodhihirishwa kuwa ni la kutengenezwa na wapotoshaji. Sehemu ya nyuma palipoandikwa tarehe muonekano wake haufanani na machapisho rasmi ya ITV, pia mwandiko (font) uliotumika kwenye tarehe pia ni tofauti na ule unaotumiwa na machapisho rasmi.

Hata hivyo kupitia kupitia ukurasa wake wa Instagram Roma Mkatoliki amewataka wafuasi wake kuiipuza taarifa hiyo kwani si ya kweli.​

Attachments

  • snapins-ai_3627810332489176093.jpg
    137.5 KB · Views: 51
Hawa ndiyo wanaotuchafulia jina watanzania!
 
Moderator fungieni huyu. Anaharibu hadhi ya jukwaa kwa ku-post uongo wa kutunga.
 
Hawa ndiyo wanaotuchafulia jina watanzania!
Inafikirisha sana kijana yeyote yule anapofanya majaribio ya kuvunja Sheria za Marekani, jambo la kushangaza sio madawa bali ni uthubutu wa kufanya jaribio hilo
 
Akili kama hizi bonyeza......kwa vichekesho zaidi.

Roma sio mjinga
 
Nimegoma kuamini.

Mbona hiyo ni headline tu. Habari haijakamilika tunaomba habari kamili.
Mange Kimambi anafuatilia kwa undani zaidi ili aje na taarifa kamili, taarifa kamili inachelewa kwasababu Roma sio msanii mkubwa nayejulikana Marekani kwahiyo ili kupata taarifa kwa undani ni pale Watanzania watakapofanya uchunguzi zaidi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…