Habibu B. Anga,
Kwa akili ya haraka haraka tu suala kama hili haliwezekani likafanyika kwenye nchi za magharibi au hata hapa Afrika leo hii. Lakini hivyo ndivyo mambo yalivyoendeshwa kihuni nchini Rusia miaka ya tisini na mwanzo mwa 2000. Hiyo ndio maana hasa ya 'Wild Wild East.!""
Mwandishi, hapo penye kivuli (bolded paragraph) ''nimepatoa kwenye utunzi wako'' hii inafanyika hata sasa tena kote duniani siyo ulaya, Russia, Asia tena Afrika ndiyo watu wanauana kila sekunde kama kuku.
Nafanya, forensic investigation katika financial institutions na crime scenes wengi wao ni mambo hayo yanaendelea tena dunia nzima labda nikusaidie tu kuwa matukio hayo bado yanatokea lakini yamepungua.
Kama unajinadi kuwa una vyanzo vya intelijensia hapo Tanzania na Afrika ya mashariki usingeweza kushindwa kuelewa kuwa mambo hayo yapo kila sekunde.
Kajielimishe tena kuhusu mauaji ya hapo Tanzania na Afrika Mashariki hata Afrika nzima.
Mfano hapo Tanzania ; unaelewa ni kwa nini wahindi wanaishi maisha wanayoishi ?
Mfano, hapo hapo Tanzania, unadhani kuwa distributor /wholesaler wa bidhaa fulani fulani hivi ambazo baadhi ya watu wanajiona kuwa ni haki yao ; unadhania ni watu wangapi wamekufa? Mfano SODA, Vituo vya Mafuta, kumiliki hotels (humu JF tu kuna uzi wa mmiliki mmoja wa hotel hapo Jiji la Makonda alipigwa risasi kisa umiliki wa eneo na hotel, wanajukwaa ndiyo wameandika humu JF ) n.k.
Je, unajua ni watu wangapi wamekufa kwa sababu ya kutaka kuuza bidhaa hizo hapo tu Tanzania?.
Twende Kenya , kwao ni biashara na siasa wanauana kila wakati; mfano miaka 2 tu iliyopita Kenya walimzingira kigogo (biashara na siasa chanzo cha kifo chake) wakamtoa roho yake mbele ya familia yake (mke na watoto wakishuhudia).
Rwanda ndiyo usiseme kwa jinsi palivyochafuka. (Rwanda mwezi hauishi), sasa Uganda nako hali tete.
Afrika ya Kusini, Nigeria, kote tunaelewa.
Nchi za Magharibi hasa huko USA, wanamuziki wanauana kama kuku kwa risasi, sumu, ajali za barabarani za kutengenezwa.
Hivyo, ukiandika kuwa Ulaya, USA hata Afrika hakuna hayo sijui unazungumzia dunia nyingine yenye majina haya au ni hii tuijuayo wote?
Kama nawe u mtu wa intelijensia huko uliko yaani utakuwa ni mzigo kwa hiyo taasisi.
Boy, you got wrong information from your secret service compatriots.