tpaul
JF-Expert Member
- Feb 3, 2008
- 24,225
- 22,632
Ashukuriwe Mungu wa mbinguni Mwenyezi kwa kumpa madam Rose mume mwema na handsome. Ama kweli Mungu hamtupi mja wake! Amesubiri muda mrefu baada ya kutoswa na watanzania akalazimika kukimbilia Kenya kama ilivyowekwa bayana kwenye uzi huu hapa chini:ROSE MUHANDO ACHUMBIWA NA KUTAMBULISHWA UKWENI KAHAMA.
View attachment 2774077
Wiki hii imekuwa wiki ya baraka kwa Malkia wa nyimbo za Injili Tanzania, Rose Muhando baada ya kwenda kutambulishwa ukweni Kahama kwa ndugu wa mchumba wake. Kama wanavyoonekana pichani Rose Muhando akiwa na mawifi zake na mwanaume wa pembeni yake aliyevaa t-shirt rangi nyekundu ndiye mume wake mtarajiwa.
Kama atafanikiwa kuolewa na ndoa ikapita salama basi hii itakuwa ndoa yake ya kwanza kwa mwanamama huyo mwenye watoto watatu ambao amezaa na wanaume tofauti.
Mungu awaongoze na ikawe ndoa ya kheri🙏
Watanzania wamemtupa Rose Muhando porini, ameokotwa na Wakenya
Hakuna shaka kwamba msanii nguli wa nyimbo za injili, Rose Muhando, ndiye malkia na gwiji wa nyimbo za injili Afrika Mashariki na Kati. Msaanii huyu alianza kuvuma kwa muda mrefu sana na kiwango chake kimebakia juu pamoja na kwamba umri wake kwa sasa umesogea. Album kali kabisa ya Rose Muhando...